Naungana na Wanachama wenzangu wa CCM kutoa pole zetu za dhati kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha Mume wake.
Mungu awatie faraja katika wakati huu mgumu.
Asanteni Sana Tabora kwa Mapokezi yenu leo hii, Sikutegemea Mapokezi Makubwa kwa kiwango cha namna hii. Naamini yote ni kuonesha kwamba tulifanya kazi kwa pamoja vizuri, Tuliishi Vizuri na tulisikilizana kwa Uzuri Kabisa.
Tukutane Uwanja wa TBC Tabora Jioni hii🙏🏽
Nachotaka nikiwa Katibu wa NEC Organaizesheni kuhakikisha ukifika wakati Uchaguzi, Kila Mwanachama anapata Haki yake. Sitasimama na watoa Rushwa, na nitahakikisha hakuna Begi lolote la Fedha ambalo litagawiwa kwa Wanachama ili fulani achaguliwe.
Karibu Tuwasiliane.
Nikiwa Katibu wa NEC – Idara ya Organizesheni, CCM Taifa, ni wajibu wangu kuwa karibu na kila mwanachama, popote alipo nchini. Ndiyo maana nimeweka wazi mawasiliano yangu ili kurahisisha mawasiliano, kupokea maoni, ushauri na changamoto za wanachama.