Leo nimesikiliza interview ya humu mchambuzi wa siasa, sikuweza kuongelea lolote
Ila kaongea mambo mengi na yakutisha mpaka mawingu wameshusha baadhi ya clip zake
Hii ni moja ya kauli amezungumza pale kwenye media ya mawinguni
Anyway acha tusubiri kamati kuu ya ccm, Deo karibu
👉Tangu Tanganyika ipate Uhuru mwaka 1961 na baadaye kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964, historia ya siasa za Tanzania imewahi kushuhudia viongozi mbalimbali wakijiuzulu kutokana na sababu za kisiasa, kiutawala, uwajibikaji,...
Rais Samia tayari amefanya kazi na Makamu wa Rais wawili huku pia akihudumu na Mawaziri Wakuu wawili tangu alipoingia madarakani kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2021.
Makamu wa Rais Philip Mpango alianza naye kazi baada ya kushika hatamu za uongozi kufuatia kifo cha mtangulizi
Hakika hili limeniumiza sana, sikutegemea kabisa.
Stay safe mzee wangu utakumbukwa kwa misimamo yako yenye uhalali.
Binafsi naamini ipo siku utakuwa sehemu kubwa yenye hadhi.
Be strong baba mungu akusimamie kwenye hali na mali.
Taifa ni letu hakika maamuzi makubwa umechukua🫡
Picha hii inaeleza mengi na kumbukumbu hii ilipigwa pale Rufiji mkoani Pwani, tarehe 22 Agosti 2026.
Dkt Balozi Emmanuel Nchimbi alitumia usafiri wa Ndege, aina ya folker 50 iliyomshusha pale mwl Nyerere airport.
Picha ilipigwa ikimuonyesha Balozi akiwa na utulivu sana.
Jana kikao cha maadili walikuwa na mahojiano na makamu ila mzito alikuwa na misimamo yake.
Kwenye kikao cha hivi karibu ndio kilikuwa kinatoa hatima ya mzito ilikuwa ni kumuondoa.
So, akaona isiwe shida kaamua kutema nyongo kwa mtindo wa kustafu siasa kabisa.
Biteko welcome
Ukweli ni kwamba hatuwezi kurudisha roho za waliyokufa Oktoba 29.
Ila tunaweza kuyapigania yale walikuwa wakiyapigania ile siku.
Tuliyobaki tunaitaji kuitaka katiba mpya na mifumo imara nchini.
Kuitaka serikali iombe radhi bado haitasaidia kurudisha nafsi za wapendwa wetu
HUU NDIO UKWELI UNAUMIZA WANAHARAKATI
Tunapambana ili kuijenga Tanzania na kumaliza migogoro iliyotokea Baada ya uchaguzi, nchi ilikumbwa na maandamano na vurugu zilinazozua mjadala mkubwa kuhusu uchaguzi, matumizi ya nguvu, nafas ya upinzani na mustakabali wa demokrasia nchini.
🚨KAMA UNA DINI NA UNAAMINI KATIKA YESU KRISTO ALIYE HAI BASI TUNAKUSIHI NA KUKUOMBA...👇🏾
💡Ombea sana hii nchi inaitwa Tanzania asubuhi mchana na jioni bila kuchoka na kukoma kwenye zamu yako ya kufanya hivyo..
💡Tanzania inakwenda kupita kwenye mtihani mzito,sehemu ngumu sana na mtikisiko mkubwa sana utatokea katika historia yake tangia kuumbwa kwa ulimwengu huu.
💡Ndani ya miezi 2-3 kuanzia sasa itakuwa migumu sana kwa taifa hili na jambo hili linalokuja lisipopita salama basi hakutakuwa na Tanzania tena.
KWA KUJUA haya sisi wenye imani katika Yesu Kristo aliye hai acha twende mlimani na madhabahuni pa BWANA YESU kwa ajili kumlilia MUNGU na kumuomba asije kutuacha maana gharama yake ni kubwa sana..
NYIE ENDELEENI KUNYWA POMBE NA KULA KULA VITUMBUA ,SISI ACHA TUTAWAOMBEE TOBA KWA MUNGU JUU YA NCHI HII NA UWEPO WAKE... TUTARUDI PALE BWANA WETU YESU KRISTO AKITUSEMESHA NA NENO LAKE KUTIMIA..🙏
KAENI KWA AMANI...NA BWANA AWATAZAME KWA USO WAKE WA FADHILI NA AWAHURUMIE SANA MAANA HAMSIKII..📌
#KigogoMediaUpdates
Hakuna MUNGU kama MUNGU wa Isaka na Yakobo..
Sifa na utukufu ni vya kwako wewe uketiye mahali pa juu sana ,juu ya falme zote na mamlaka zote na kila jina liitwalo jina katika ulimwengu huu na ule ujao..
SIKU YA JANA TAREHE 13/08/2026 ,MIMI NIMEKUONA MUNGU KWA MATENDO YAKO MAKUU SANA NA MAGUVU YAKO YANAYOOGOFYA SANA..
Utabakia kuitwa MUNGU..🙏
Chadema imefanikiwa sana kupata vijana wajinga na wapumbavu, kwamba Mbowe kwenda kwenye shuhuli za serikali ndio limekua kosa na kuanza kutoa matusi
Tafuteni shughuli za kufanya vijana haya mambo anayofanya Mbowe ni ya kawaida mnoo ukiwa na kazi ya kufanya, kama kazi yako ni kubet na kusubiri chadema waje wakomboe maisha yako ndio huwezi kumuelewa Mbowe
Huku mtaani kwetu hoja huwa aziishi kabisa na kila siku hawa wazee sijui muda wa kuingia online wanautoa wapi.
Leo kwenye maongezi ikaja hii mada ya hii tweet ya heche mzee mmoja anaitwa GANDHI akasema kwa sasa HECHE anaweza kuwa na nguvu sana ya kisiasa sababu ni huruma
Mpaka sasa nimepigiwa simu 10 watu wakiniuliza niko wapi na mbona @jidejaydee hawamuoni.
Nimewaambia dada yetu mpendwa hata kuwepo yuko njee ya nchi tuangalie waliyopo.
Naona hawaamini kabisa nime screen shot hii aisee wameipokea ila kishingo upande.😂
Tunasikiliza music mzuri
Mzee @freemanmbowetz
Wanyama wa porini huua/kupigana kwa sababu zinazohusiana na mahitaji ya kuishi: chakula, kujilinda, kulinda watoto au eneo. Simba anawinda kwa ajili ya chakula siyo mateso, chuki, kisasi
Binadamu ni viumbe katili zaidi ya wanyama. Binadamu anaweza kumdhuru mwingine kwa sababu ya chuki, ubaguzi, tamaa, kulipiza kisasi, madaraka au kwa sababu anaona mwingine hafai kuishi
Kutoka Mikocheni kwenda ilipo Mahakama Kuu ya Tanzania ni umbali usiozidi 5KM. Kutoka Mikocheni kwenda Rufiji ulipo mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni umbali wa 260KM
Unaweza kusafiri kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya saa tano kuhudhuria shughuli za Serikali katili ya CCM lakini huwezi kutumia dakika 10 kutoka kwako kwenda Mahakama Kuu katika kesi ya TAL?
Huwezi kwenda safari ya 5KM kumuona Mwenyekiti wako wa chama, aliyerithi kiti chako katika uchaguzi HURU na HAKI lakini unaweza kwenda 260KM kuungana na watesi wa Mwenyekiti wako?
Nini muhimu zaidi kwako? Ni wewe ulitueleza miradi ya maendeleo haiwezi kuwa mbadala wa haki za binadamu. Leo kuna watu wanatekwa na kupotezwa, wanashtakiwa kwa ugaidi na uhaini. Hujui?
Lakini umechagua nini? Nimekusikiliza ukisema “mradi wa JNHPP usichukuliwe kisiasa kwa kuwa ni mradi unaokwenda kusaidia uchumi”. Umesahau ulitueleza nini kuhusu miradi ya MAGUFULI?
Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kwa sasa ni ‘mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya CHADEMA - ni kutokana na hiki kinachoitwa ‘ustaafu’ wa uenyekiti wa CHADEMA Taifa
Kwa maana kwamba, Freeman Mbowe yupo katika kundi sogozi la WhatsApp na mengine (kama yapo) ambayo wajumbe wa kamati kuu wanajadili kwa hisia zao tofauti masuala mbalimbali ya chama
Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu CHADEMA huwezi kwenda Mahakamani katika kesi ya kiongozi wa chama, lakini unaweza kwenda katika shughuli zinazoongozwa na mwenyekiti wa CCM
Freeman Mbowe umesahau, wakati ukishtakiwa kwa makosa ya uongo ya UGAIDI, Tundu Lissu alikuwa Belgium akijiuguza majera ya risasi. Aliomba kukutana na Rais alipokuwa Brussels
Pamoja na mambo mengine waliyokubaliana, alisema Mwenyekiti Freeman Mbowe aachiwe ndiyo tufungue ukurasa mpya. Tundu Lissu alitujulisha mwenyewe hayo alipozungumza na umma.
Tundu Lissu akiwa na siku 500 gerezani. Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe hujawahi kukanyaga Mahakamani kuanzia Kisutu hadi Mahakama Kuu hata kwa bahati mbaya.
Saa 24 baada ya Mahakama Kuu kusema Tundu Lissu ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya UHAINI ya uongo na uzandiki, Freeman Mbowe unaibuka katika shughuli za Serikali ukiwa na MAWAZIRI.
Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CHADEMA umekataa kabisa kuhudhuria shughuli zozote za CHADEMA lakini unaweza kuhudhuria shughuli unazoalikwa na WATAWALA KATILI wa CCM.
Unahudhuria shughuli za Serikali umeongozana na mawaziri wa Serikali katili ya CCM wakati ambao wanachama na wafuasi wa CHADEMA kwa mamia wamekamatwa na kushtakiwa kwa UGAIDI?
Mzee Freeman Mbowe umesahau haraka. Kuna watu walifungwa gerezani, wengine sasa ni walemavu, wengine sasa ni marehemu kwa sababu ya kupigania jina lako ukiwa kiongozi wa chama chetu.
Umesahau, wakati unakamatwa na Serikali katili ya CCM, 2021, wanachama wa CHADEMA walikwenda kuonyesha ‘solidarity’ na wewe pale KISUTU. Walikamatwa, wakashtakiwa, wakafungwa
Najutia zile siku nilisimama nawe, kukutetea na kunadi jina lako kwa nia njema kabisa nikifikiri unapambania uhuru, haki na mabadiliko ya kweli. Haikuwa hivyo. Ulitudanganya tukishindwa.
Nasema kwa kuwa kwa hiari yangu, niliamua kusimama nawe, kukunadi katika mazingira ambayo ilionekana ni kama kuuza kitimoto Mecca. Lakini sikutarajia tukishindwa, tuisaliti CHADEMA
Wengine sasa tumeelewa kwa kuchelewa sana. Hii chuki haiwezi kuwa ya kushindwa uchaguzi. Lazima kuna mafekeche mengine. Kuna kingine kimeujaza chuki moyo wako. Je, kuna mrija, umekatwa?
Najutia kumpa mtoto wangu jina lako, Freeman.