Waswahili hunena;
Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu. Lakini ukweli ni kwamba, ukifunzwa ama usifunzwe ulimwengu unakusubiri utakufunza tena.
@Profmaganga1
Kwanini useme siwezi? Neno siwezi ni kikwazo kwako, na utashindwa kufikia mafanikio ikiwa unatanguliza neno SIWEZI. Inapokuja fursa usiiache kwa kisingizio cha mimi siwezi, bali ichukue na tafuta mtu anayeweza muifanye pamoja.@Profmaganga1
Inawezekana umeomba kitu, ama umehitaji huduma lakini ukapata jibu la HAPANA AU SITAKI. Hili neno lisiwe chanzo cha kukata TAMAA kamwe, bali liwe ni fursa kwako kwani linakufunza kufanya upembuzi yakinifu na kuchagua kilichobora zaidi ya cha awali. HAPANA NI FURSA! @Profmaganga1
Fursa si kupata mafanikio tu bali hata kupata changamoto ni moja ya fursa, ukizitumia vizuri changamoto zako zitakupa fursa zaidi ya unavyofikiria. @Profmaganga1#lifequotes#lifecoach