TAANZANIA NAMBA 11 KWA IDADI YA WALINDA AMANI
Tanzania imefanikisha ushiriki wake katika juhudi za amani na operesheni za kulinda amani kimataifa.
Kufikia Mei 2025, Tanzania ilikuwa na walinda amani 1,890 na kushika nafasi ya 11 kati ya nchi 119 zinazochangia walinda amani katika misheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.
Haya ni Mafanikio ya Bajeti ya serikali kwa mwaka 2024/25 kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Bangi ni dawa ya kulevya inayotokana na mmea uitwao Cannabis sativa. Majani na maua ya mmea huu hukauka na kuvutwa kama sigara au kuchanganywa na dawa nyingine. Bangi huathiri bongo na huweza kubadilisha namna mtu anavyotafsiri uhalisia wa mambo.
#NiulizeNikujibu_DCEA
Idadi ya utumiaji wa Intaneti imeongezeka kwa asilimia 69.4 kutoka milioni 29.1 machi 2021 hadi Milioni 49.3 Machi 2025.
Takwimu zinaonesha kuwa, idadi ya watumiaji wa intaneti nchini imeongezeka kwa asilimia 69.4% kutoka watu milioni 29.1 Machi 2021 hadi kufikia watu milioni 49.3 Machi 2025.
Hili ni ongezeko kubwa na la kujivunia, linaloashiria kasi ya mageuzi ya kidigitali katika jamii yetu.
Ongezeko linaimarisha mawasiliano kati ya watu na kuongeza kasi ya upatikanaji wa taarifa muhimu. Pili, linafungua fursa nyingi za ajira, hasa kwa vijana, kupitia biashara mtandaoni na huduma za kidijitali
Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa
Dodoma, Mei 30, 2025
Siku ya pili ya mkutano wetu jijini Dodoma ambapo kwa pamoja tumezindua Ilani ya CCM 2025-2030. Ilani hii imeandaliwa kwa weledi mkubwa kwa manufaa ya Taifa letu, ikilenga zaidi katika kuchochea mapinduzi ya kiuchumi, kuzalisha ajira na kuboresha maisha ya wananchi.
Vipaumbele vingine ni kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, kukuza matumizi ya sayansi na teknolojia, kudumisha amani, utulivu na usalama, kudumisha utamaduni, na kukuza sanaa na michezo na kuongeza kasi ya maendeleo vijijini.
Aidha, tukielekea kwenye uchaguzi mkuu, nimezielekeza kamati za kuteua wagombea kutenda haki ili tupate viongozi watakaotekeleza ilani kikamilifu. Pia, nimewaasa wanachama wa CCM kuimarisha umoja na mshikamano, tuingie kwenye uchaguzi tukiwa wamoja, ili chama chetu kipate ushindi mkubwa na turudi kuendeleza kazi ya kuwatumikia wananchi wote.
Utiaji saini umefanyika Tokyo, Japan ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni na Serikali ya Japan ikiongozwa na Waziri wa Mazingira, Mhe. Asao Keiichiro(Kei)
Mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na washiriki zaidi ya 80 ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Same, Madiwani, watumishi wa Halmashauri, Watendaji ngazi ya Kata, Vijiji na Vitongoji ambapo mgeni rasmi katika mafunzo hayo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Prof. Tumaini Joseph Nagu kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Afya kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.