#HABARI Mahakama ya Damascus imemhukumu kifungo cha maisha Mufti Mkuu wa zamani wa Syria, Ahmad Badreddine Hassoun, kwa kuchochea ghasia za kidini, kuhalalisha mauaji na kutumia vibaya wadhifa wake wakati wa utawala wa Bashar al-Assad.
Jaji Fakhreddine al-Aryan alisema taasisi za kidini wakati wa Assad zilihalalisha matumizi ya mabomu ya mapipa katika maeneo ya raia. Mashambulizi hayo yalisababisha uharibifu mkubwa.
Mahakama pia imeamuru kutaifishwa kwa mali za Hassoun zinazoweza kuhamishwa. Tofauti na baadhi ya maafisa wengine, Hassoun alihudhuria wakati hukumu yake ikitolewa.
Hassoun alikuwa Mufti Mkuu wa Syria kuanzia 2005 hadi 2021. Alijulikana kwa ukaribu wake na Assad na kumuunga mkono wakati wa maandamano ya mwaka 2011.
Hassoun alikamatwa Machi 2025 katika Uwanja wa Ndege wa Damascus akijaribu kusafiri kwenda Amman, Jordan. Kesi yake ilianza Juni 2026, huku waendesha mashtaka wakiomba apewe adhabu ya kifo.
#EastAfricaRadio #TogetherTunawakilisha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Umakamu wa Rais kuanzia tarehe 4 Septemba 2026, huku akitangaza pia kustaafu rasmi siasa na utumishi wa umma
Uamuzi huo umewekwa wazi kupitia taarifa yake kwa umma aliyoitoa leo tarehe 25 Agosti 2026 kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo amebainisha kuwa tayari amemwandikia barua ya kujiuzulu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Vyanzo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais vimeithibitishia Jambo TV juu ya taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Dkt. Nchimbi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Nchimbi, kujiuzulu kwake kumezingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa kwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Balozi Nchimbi amefunguka sababu iliyomfanya kuchukua hatua hiyo akirejea ahadi aliyompa Rais Samia tarehe 27 Agosti 2025. Katika ahadi hiyo, Nchimbi alimhakikishia Rais kuwa angemtumikia kwa uaminifu na uwezo wake wote, lakini pia akamwahidi kuwa siku yoyote ambayo Rais ataona anahitaji Makamu mwingine wa Rais, yeye angeachia nafasi hiyo bila kusita.
Dkt. Nchimbi amebainisha kuwa amechukua uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa Rais anatamani kufanya mabadiliko katika safu yake ya uongozi.
“Nimejiridhisha pasipo shaka kuwa Mhe. Rais anatamani mabadiliko, hivyo nimeamua kutimiza ahadi yangu,” imeeleza sehemu ya barua hiyo ya kujiuzulu
Kupitia taarifa hiyo, Balozi Nchimbi ametoa shukrani za pekee kwa Rais Samia na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa imani kubwa waliyoonesha kwake wakati wa utumishi wake. Kadhalika, amewashukuru Watanzania wote kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kipindi chote cha utumishi wake wa umma na kuwahakikishia kuwa ataendelea kuwa raia mwema wa Tanzania.
#BreakingNews Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kutafakari kwa kina. Ameeleza kuwa uamuzi huo ni wake binafsi.
Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo, Agosti 25, 2026, ikitumwa pia kwenye ukurasa wake wa Instagram Dkt. Nchimbi amesema ataacha nafasi ya Makamu wa Rais pamoja na utumishi wa umma kuanzia Septemba 4, 2026.
Dkt. Nchimbi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kumsaidia katika uongozi wa nchi. Amesema amejifunza mengi kutokana na kufanya kazi na watu mbalimbali katika kipindi chake cha utumishi.
Amesisitiza kuwa uamuzi wake wa kujiuzulu hauhusiani na mabadiliko yoyote katika uhusiano wake na Rais Samia. Pia amemshukuru Mwenyekiti wa CCM kwa imani aliyokuwa nayo kwake.
Dkt. Nchimbi amesema ataendelea kuwa mwanachama wa CCM na kuitumikia Tanzania kwa nafasi nyingine atakayopewa.
#EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
BREAKING NEWS Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 25 Agosti, 2026, amepokea barua ya ombi la kujiuzulu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi kuanzia tarehe 04 Septemba, 2026 na Mheshimiwa Rais ameridhia ombi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, taratibu za kikatiba za kumpata Makamu wa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania mwingine zitachukuliwa.
#EastAfricaRadio #TogetherTunawakilisha
Wakili wa Mahakama Kuu, Ferdinand Makore amesema kwa mujibu wa Katiba baada ya Makamu wa Rais kujiuluzu, Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan atamteua Mtu mwingine mwenye sifa ndani ya siku 14 tangu kujiuzulu kwa Makamu wa Rais kisha jina hilo litapaswa kuthibitishwa na Bunge la Tanzania ili aapishwe kuwa Makamu wa Rais wa Nchi.
Akizungumza na Ayo TV, leo 25,2026 Makore amesema “baada ya kiti cha Makamu wa Rais ndani ya siku 14 Rais atateua Mtu na Mtu huyo itabidi athibitishwe na Bunge, kwahiyo muda ambao tunao ni siku 14 tangu kujiuzulu kwa Makamu wa Rais, kwahiyo kama Nchimbi amejiuzulu kwa mujibu wa Ibara ya 149 ibara ndogo ya pili basi siku 14 zitahesabiwa kuanzia Septemba 04,2026 hilo ndio jukumu la Rais kutafuta Mtu wa kuziba nafasi ambaye atathibitishwa na Bunge”
“Mtu huyo ambaye atapelekwa Bungeni kuthibitishwa anatakiwa awe na sifa za Kiongozi anayefaa kuwa Makamu wa Rais ambazo zinaainishwa kwenye ibara ya 47 ibara ndogo ya nne, ambapo anatakiwa kuwa Raia wa Tanzania, atimize umri wa miaka 40 na kuendelea, awe Mwanachama wa Chama cha Siasa ambacho Mgombea Urais anatumikia, na anayeweza kuwa na sifa za kugombea ubunge, katika kipindi cha miaka mitano kabla ya kuteuliwa anatakiwa asiwe ameshtakiwa au kutiwa hatiani katika makosa ya ukwepaji wa kodi au kudaiwa na Serikali”
“Rais anaweza kumteua Mbunge kushika madaraka ya Makamu wa Rais kama kiti cha Makamu wa Rais kipo wazi kisha Mbunge huyo atathibitishwa na Wabunge wenzake na Jimbo lake litakuwa wazi kwa ajili ya uchaguzi mdogo kufanyika”
#MillardAyoUPDATES
Kutoka kua na Squadi yenye mateka kama
-kagere
-John boko
-Mugalu
Hadi kua na
-Doumbia na
-Ismail mgunda
Hili ni anguko
Na hata kufika tena robo Fainali CAF itakua ni uongo
🚨 Mechi ya kesho ya NBC PL 🇹🇿 kati ya wenyeji Namungo Fc dhidi ya Mabingwa watetezi Yanga Sc itapigwa saa tatu usiku katika uwanja wa Majaliwa
Wananchi 🔰 wataanza na sherehe za utambulisho wa mchezaji wao mpya katika uwanja wa KMC kisha wataangalia mechi hiyo kwenye BIG SCREEN
🚨Kutoka kuwa na Moussa Camara, hadi Tanja Kassali kwenye nguzo za Simba SC🤦🏽♂️
Anazungumzwa Yusuph Kagoma kama udhaifu wa Simba wakiwa na mpira; Lakini ujue kila shambulizi dhidi ya Simba ni mashaka sana pale golini
Kassali ni udhaifu mwingine wa Simba kwenye kila mchezo
🚨𝐄𝐗𝐂𝐋: Seleman Mwalimu hataweza kutumika kwenye mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga V Simba
⚠️Yanga bado hajafunguliwa kusajili, lakini pia bado Simba SC hawajamtoa kwenye usajili wao Seleman Mwalimu ‘Gomez’ 2026/27
❌Yanga pia bado hawajatuma request ya kumuomba Simba SC