Punguza kujitoa kupita kiasi. Kizazi hiki hakina kumbukumbu watu wanasahau haraka sana. Ukifeli kidogo tu, wale uliowasaidia Jana wanaweza kuwa wa kwanza leo kukudharau, kukucheka na kukusengenya.
Umri wa miaka 25–30 kwa mwanaume ni kipindi kigumu zaidi,
kwa sababu ndipo unagundua makosa uliyoyarudia kwa muda mrefu, kisha unaanza kuyarekebisha hatua kwa hatua.
Huu ndio umri wa kutuliza akili,
kutawala hisia na kujijenga upya bila presha ya dunia.