#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 260
Mhe. Tundu Lissu anaendelea kutoa ushaidi wake
Anasema nilikuwa Msemaji Mkuu wa masuala ya katiba na sheria ya kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Masuala ya Muungano na nilikuwa shadow Attorney General.
Naomba Mahakama irekodi kwamba nilifanya kazi yangu kwa uaminifu mkubwa na umahiri mkubwa sana.
Waheshimiwa majaji katika kipindi cha 2011 hadi 2014 nilikuwa mjumbe maalumu wa Bunge la Katiba kwa kipindi hicho cha 2011 hadi 2015 niliongoza harakati za kupigania Katiba Mpya na mfumo huru wa uchaguzi, niliongoza hayo mapambano bungeni na kwenye Bunge la Katiba kwa uaminifu na umahiri mkubwa sana, hivyo ni ushahidi wangu kwamba kilichotuleta hapa ni mgogoro wa kisiasa, ni vita ya kisiasa na sio Uhaini.
Waheshimiwa Majaji nje ya ubunge nimekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kuanzia Machi hadi Septemba 7, 2017 na huwi Rais wa TLS kama wewe ni mtu wa hovyo hovyo mhaini mhaini.
Nje ya uongozi wa mawakili wenzangu hapa nilipo ni Makamu Mwenyekiti wa Internationa Democrats Union (IDU).
IDU ni muungano au shirikisho linalojumuisha vyama karibu 80 kutoka dunia nzima.
Mimi pia ni mjumbe wa International Executive Committee ya IDU, mimi ni Makamu Mwenyekiti ninayewakilisha bara zima la Afrika
Waheshimiwa majaji ni ushahidi wangu kwamba mimi ni mtu wa heshima ndani ya nchi hii na kimataifa na heshima niliyonayo ni kutokana na msimamo wangu wa kupigania Demokrasia, Haki za binadamu na Utawala wa sheria sio kwasababu nyingine.
Waheshimiwa Majaji mwezi Mei 2011 nilipewa tuzo ya heshima ya kuwa mwenza wa kimataifa wa Chuo Kikuu cha Bridgeport (International Fellow) jimbo la Connectcut lilipo nchini Marekeni, walisema ni kwasababu ya kupigania haki za binadamu, mazingira na demokrasia katika nchi ya Tanzania na Barani Afrika.
Mwezi Desemba 2020 nilitunukiwa heshima nyingine na IDU tuzo inayoitwa Bush Thatcher Award Freedom (kwa jina la Rais wa 41 wa Marekani) sababu yake au citation yake ilisema Tundu Lissu umekuwa ni kielelezo cha msimamo thabiti wa kupigania Haki, Demokrasia na Utawala bora katika nchi za Afrika.
Ni muhimu vilevile iingie kwenye ushahidi kwamba pamoja na kukaa gerezani kwa muda wote, heshima yangu ndani na nje ya nchi haijapungua in fact imeongezeka.
Taasisi nyingi sana za kitaifa, kikanda na kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ulaya, Jumuiya ya Madola zimesema haya mashtaka ni mashtaka ya kisiasa hakuna jinai yoyote na wamedai niachiliwe huru bila masharti yoyote.
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limeeleza sio tu kwamba niachiwa bali nilipwe pia fidia kutokana na usumbufu wote uliojitokeza tangu nilipokamatwa.
Waheshimiwa Majaji naomba iingie kwenye ushahidi kwamba nchi za Jumuiya ya ulaya zimesimamisha misaada kwa Tanzania kwasababu ya mashtaka haya, takribani dola million 700 nchi ya Marekani imesimamisha kwa Serikali ya Tanzania kwa takwimu nilizonazo kwasababu ya mashtaka haya.
Bunge la Marekani linajadili muswaada wa kuiwekea serikali ya Tanzania na Viongozi wake vikwazo kwasababu ya mashtaka haya.
Waheshimiwa majaji dunia haiwezi ikakupigania hivi kama wewe ni mtu wa hovyo hovyo
Watu wanatabasamu sana na kucheka 😂😂😂😂😂😂
Mhe. Lissu anaendelea kusema Dunia inaweza kukupigania hivi kama wewe ni mtu wa heshima.
Part 261 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
Mawingu igeuke tu redio ya matangazo ijulikane...watu wafungue redio kusikiliza tu matangazo siku iishe!
Maana sasa hizi ni dharau kudai wana interview na kiongozi mahojiano dakika 2 matangazo dakika 40!😂
Serikali batili ilikusudia kuleta mashahidi karibu 30 kuonesha Tundu Lissu ni mhaini.
Wamekata moto baada ya mashahidi 17!
Kesi yao imefungwa.
Na vielelezo muhimu vimetupwa.
Lissu anafanya wasilisho la kutokuwa na kesi ya kujibu.
Dear mbogamboga, msiyemtaka anakuja soon!