Government official page
all LGA's in Arusha Region well managed for sustainable development aimed at poverty reduction and promotion of economic growth.
RC Mkonda sasa ni mpiga kura rasmi wa Mkoa wa Arusha, Jimbo la Arusha Mjini Kata ya Sekei mara baada ya kuhuisha taarifa zake kwenye daftari la kudumu la wapiga kura leo 20 Mei, 2025.
Mkoa wa Arusha una jumla ya vituo 331 kwaajili ya kuhuisha taarifa za wapiga kura ili kusaidia kuondoa usumbufu wakati wa kupiga kura na zoezi hilo litahitimishwa kwa mara ya pili tarehe 22 Mei, 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumanne Mei 20, 2025 ameungana na Watanzania wengine kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwenye kituo cha Hospitali ya AICC, Mtaa wa Mahakama Kata ya Sekei Jijini Arusha.
Amesema Mhe. Makonda. Katika hatua nyingine Mhe. Makonda amewataka waajiri wote katika Mkoa huo kutoa ruhusa kwa watumishi wa Umma, Mashirika na Taasisi mbalimbali kwenda kuhuisha taarifa zao kwa kuwa zoezi hilo halichukui muda mrefu kukamilisha taarifa za mpiga kura.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, leo asubuhi amefanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa madaraja mawili ya King’ori yanayojengwa katika barabara kuu ya Arusha – Moshi na kuridhishwa na kasi na ubora wa ujenzi wa madaraja hayo.
Kijana Joshua Obama (14), ambaye ni kati ya Vijana 29, waliobahatika kuwa wanufaika wa Ufadhili wa masomo ya ufundi stadi yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda amemshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa kuwa sehemu ya kutimiza ndoto zake akiwa anaendelea na masomo
ni kulea sekta binafsi na kujenga miundombinu, alichofanya awamu ya tano ni kujenga miundombinu ya uchumi na anachofanya Rais Samia ni kuifungua Nchi." Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo
"Kazi iliyofanyika na awamu ya kwanza ya Mwl. Nyerere ni kujenga Taifa, alichofanya Mzee Mwinyi kwa awamu ya pili ni kufungua sekta binafsi, alichofanya Mzee Mkapa, ni kujenga taasisi za kuratibu sekta binafsi na kuanza ujenzi wa miundombinu muhimu, alichofanya Kikwete
"tupo kwenye zama ambazo maendeleo hayategemei maamuzi ya viongozi wa kitaifa pekee, bali yanategemea uwezo wa maeneo yetu, mikoa yetu, halmashauri zetu kuongoza dira na maamuzi ya kimkakati kama Taifa"
"Ni wajibu kila Mkoa sasa kuanisha fursa zilizopo kwenye mikoa yao, kufanya makongamano kama hili ili wananchi waweze kujua fursa zinazopatikana kwenye maeneo yao." Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Mohamed Mchengerwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda, wakipiga ngoma na kufurahia wakati utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati Jijini Arusha.
WAZIRI MCHENGERWA APONGEZA RC MAKONDA KWA UZALENDO NA UBUNIFU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kwa uzalendo wake kwa wananchi na ubunifu mkubwa wa kuwaletea maendeleo Watanzania.