Wewe unatamani kuniona unavyotaka wewe, alafu Mimi natamani kujiona ninavyotaka Mimi. Kubwa zaidi MUNGU anatamani kuniona anavyotaka yeye. Somo hapa ni kwamba Mimi na wewe tumuachie MUNGU kuhusu Mimi.
Fanya kinachokupa pesa kwa ajili ya maisha yako, lakini pia fanya kinachokupa furaha kwa ajili ya uhai wako. Kama kinachokupa pesa ndicho kinachokupa furaha, basi mshukuru Mungu.
Kuna nguvu tatu zinazombeba mwanadamu. Nguvu ya mwili, nguvu ya akili na nguvu ya imani. Nguvu ya mwili huchoka, nguvu ya akili hutikiswa, lakini nguvu ya imani huinuka hata pale kila kitu kinapoanguka. Ndiyo maana, kati ya nguvu zote, nguvu ya kuizingatia zaidi ni nguvu ya imani
Mtu aliyezaliwa kufanya kitu fulani na aliyesomea kufanya kitu kama hicho, utofauti wao huwa kwenye performance. Aliyesomea hawezi ku-perfom vizuri kama aliyezaliwa na hicho kipawa. Pia aliyesomea hawezi kufanya bila mshahara, ila aliyezaliwa na kipawa hufanya hata bila mshahara.
Kama umezaliwa enzi za Nyerere, wewe ni Babu au Bibi; enzi za Mwinyi, wewe ni Baba au Mama; enzi za Mkapa, wewe ni Kaka au Dada; enzi za Kikwete, wewe ni Dogo; enzi za Magufuli, wewe ni Mtoto; na enzi za Samia, wewe ni Kinda. Huu ndio mzunguko wa vizazi vya Watanzania.
Simba na Yanga zingepaswa kuwa na after match parties kila wanapocheza kwenye ligi kuu ya NBC, ambapo kiingilio kingekuwa jezi za mwaka husika. Hii ni njia bora ya kuongeza mshikamano kati ya klabu na mashabiki.
Mashabiki wa Tanzania hawapendi mpira, wanazipenda Simba na Yanga; hawapendi muziki, wanawapenda Diamond na Alikiba; hawapendi ngumi, wanawapenda Mwakinyo na Kiduku. Hawakuwa wanapenda filamu, waliwapenda Late Kanumba na Ray.
Wazungu walitutengeneza kufurahia kuwa watumwa. Mfanyakazi wa taasisi/kampuni akivimba au kuonyesha dharau, hicho ni kiburi cha ufahari wa kuwa mtumwa. Wakoloni walipanda mbegu hii kwa kutengeneza mfumo unaomfanya mtu kujivunia kuwa mfanyakazi, huku akipoteza uhuru wake wa kweli.
Mfumo wa vyama vingi si zawadi ya uhuru, bali ni chombo cha mataifa yenye nguvu cha kutawala. Chama tawala kinapokataa matakwa yao, hukata misaada na huduma kisha hukinyanyua chama pinzani na kukiweka madarakani ili waendelee kututawala. Mfumo wa vyama vingi ni mpango wa mabepari
Nafikiri kuna haja ya kiongozi wa Dini kuandikiwa speech ambayo ataitumia wakati wa kuzungumza madhabahuni, ili kuendelea kutunza Imani kwa wanaoamini.