Kama unamdai mtu, usipoteze muda na pesa kuwapa Polisi ili WAKUSAIDIE!! Suala la madai, ni kati ya wahusika tu, it's a civil matter! Lkn, pia inategemea na mazingira mnayodaiana. Sehemu pekee ya kupeleka lalamiko la madai ni mahakamani – hapo utapata MSAADA. Wakati pekee ambapo
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 198
Anaingia jamaa mmoja mrefu, kavaa kaundasuti nyeusi anakitambi ila sio mnene wala mwembamba anaingia hapa.
Jaji anauliza Shahidi unaitwa nani?
H937 Detective Vincent
36 umri,
Mkristo,
Anapewa biblia kwa ajili ya kuapa anasema atasema Ukweli, Ukweli mtupu. 😂
Ataongozwa na wakili wa Serikali hapa.
Wakili: anauliza jina na anapoishi?
Coplo Vincent.: Anajitambilisha na anasema anaishi Mbeya.
Wakili: Sehemu gani?
Coplo Vincent : Anasema Mbeya mjini.
Wakili: Unafanya kazi gani?
Coplo Vincent : Police Wilaya ya Mbeya
Tangu mwaka 2012.
Wakili: Umejiunga mwaka gani?
Coplo Vincent.: Anajibu 2012
Mafunzo ya awali ya upolice kule Moshi 30/3/2012 baada ya kuhitimu nilipangiwa Mkoa wa Rukwa.
Wakili: Majukumu yako ya kila siku ni yapi?
Coplo Vincent: kupeleleza kesi kukamata na kutoa ushahidi Mahakamani katika kitengo cha upelelezi nina miaka Miaka 6.
Wakili: Sasa ieleze Mahakama mnamo Tarehe 5/4/2025 ulikua wapi?
Coplo Vincent : Nilikua kituoni Mwanjelwa naendelea na majukumu yangu.
Wakili: Unakumbuka Nini?
Coplo Vincent : Niliitwa na Mkuu wa kituo na kupewa maelelekezo ya kumtafuta P9.
Wakili: Alikua anakabiliwa na nini mpaka uende kumtafuta?
Coplo Vincent : P9 alikua anahamasisha vijiweni uchaguzi 2025 usifanyike hivyo nikaenda kumkamata.
Wakili: Baada ya kupewa maelekezo hayo ulifanyaje?
Coplo Vincent : Mkuu wa kituo alinipatia namba ya simu ya P9, Mkuu wa kituo hizo namba alizipata kupitia msiri wake ambaye alimletea.
Wakili: nini kiliendelea baada ya kupata mawasiliano ya mtu unayetakiwa kumkamata.
Coplo Vincent: baada ya kufuatilia shughuli zake nikagundua kuwa ni fundi umeme, hivyo nikatumia njia ya kujifanya kama mteja ili niweze kumkamata.
Wakili: nini kilifata?
Coplo Vincent: tulikubaliana kukutana maeneo ya kabwe ili niweze kumpeleka eneo la kazi.
Wakili: nini kilifuatia?
Coplo Vincent : baada ya hapo nikawa nimefika Kabwe kwani hapakuwa mbali, kweli nikakutana nae.
Wakili: baada ya kukutana nae nini kilifuatia.
Coplo Vincent : Nilimwambia mimi shida yangu siyo umeme, nikajitambulisha kuwa mimi ni Askari police nikamuonesha kitambulisho changu.
Wakili: baada ya kuonesha kitambulisho nini kilifuata?
Coplo Vincent : Nilimwambia nimekuja kumkamata anakabiliwa na tuhuma za kufanya uchochezi pamoja na kuhamasisha vurugu za kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025.
Wakili: Mwisho wake ulikuwaje.
Coplo Vincent: bahati nzuri alikuwa muelewa, sikutumia nguvu nyingi hakuwa mtu wa vurugu niliongozana nae hadi kituo cha police kati Mbeya then nikaendelea na majukumu yangu.
Wakili wa Serikali Ignas Mwinuka anasema Waheshimiwa Majaji ni hayo tu kwa shahidi huyu.
Jaji anasema karibu Mshitakiwa kwa ajili ya maswali ya Dodoso.
Mhe. Lissu: umesema unaitwa Coplo Vicent ni sawa?
Coplo Vincent : Mimi naitwa coplo H937 vicent.
Mhe. Lissu; ukienda kwa baba yako na mama yako utawaambia unaitwa coplo H937 Coplo Vicent.? 😂
Coplo Vincent: Hapana.
Mhe. Lissu: nasikia wewe ni homeboy wangu.
Coplo Vincent: Ni kweli.
Mhe. Lissu: bila shaka uliandika maelezo yako ya shahidi na ukionyeshwa utayatambua?
Coplo Vincent: ndio.
‘Mhe. Lissu: waheshimiwa majaji naomba shahidi aonyeshwe maelezo yake.
Mkude: waheshimiwa hatuna pingamizi.
Shahidi Coplo Vincent anaonyeshwa maelezo yake.
Mhe. Lissu: waeleze waheshimiwa majaji kama hayo maelezo ni yako.
Coplo Vincent: ni sahihi ni yangu.
Mhe. Lissu: waheshimiwa nataka ku-impeach credit ya huyu shahidi nataka kuhoji sifa au uaminifu wake, namsoea maelezo yake kisha nitasoma maeneo nayotaka kum-contradict na nitaomba akubali yapokelewe kama kielelezo.
Part 199 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 202
Mhe. Lissu ameanza kumfanyia Cross examination Shahidi wa kificho P3.
Mhe. Lissu: shahidi hapo ulipo unaweza kuniona?
Shahidi wa kificho P3 : hapana
Mhe. Lissu: kwa taarifa yako hata mm siwezi kukuona kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P3 : sahihi.
Mhe. Lissu: nataka nikuhoji kutokana na ushahidi wako na nashukuru umesema wewe ni mfuasi wa CHADEMA, sasa naomba uwaeleze majaji, mfuasi wa CHADEMA anakua na kutambulisho gani?
Shahidi wa kificho P3 ; anakua hana kitambulisho kwasababu anakua bado hajawa mwanachama.
Mhe. Lissu: mimi kiongozi wa CHADEMA na mtu yoyote aliyeopo hapa mahakamani atajuaje kama wewe ni mfuasi wa CHADEMA, huna kitambulisho na pia sikuoni?
Shahidi wa kificho P3 : hilo ni suala la imani
Mhe. Lissu: twende taratibu kaka, waeleze majaji kama wafuasi wa chadema huwa wanaorodheshwa mahali ili kuwatambua.
Shahidi wa kificho P3 : binafsi sijajua huwa wanaorodheshwa wapi?
Mhe. Lissu: kwahiyo hujaorodheshwa?
Shahidi wa kificho P3 : sahihi.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama wafuasi wa CHADEMA kuna mahali huwa wanaenda kujitambulisha ili wajulikane
Shahidi wa kificho P3 : hakuna.
Mhe. Lissu: hapo ulipo kwenye kiboksi na mimi hapa nilipo kama kuna namna mimi naweza nikaelewa au kujua kama wewe ni mfuasi wa CCM na sio CHADEMA?
Shahidi wa kificho P3 : sijui utajuaje ila mm ni mfuasi wa CHADEMA
Mhe. Lissu: na nitajua kama ww sio pandikizi la Polisi kwasababu hujajiandikisha popote wala huna chochote cha kukutambulisha kuwa ni mfuasi wa CHADEMA?
Shahidi wa kificho P3 : itabidi uamini tu na uiamini mahakama tukufu kwasababu mimi sijui kwa kweli utawezaje kunitambua.
Mhe. Lissu: mfusi wa CHADEMA huwa anaalama usoni au kifuani kuwa yeye ni mfuasi wa CHADEMA?
Shahidi wa kificho P3: sijui
Mhe. Lissu : waeleze majaji kama uliandika maelezo Polisi tarehe 17 april 2025?
Shahidi wa kificho P3 : ndio
Mhe. Lissu: ukionyeshwa hayo maelezo yako utayatambua?
Shahidi wa kificho P3 : ndio
Mhe. Lissu: naomba shahidi apewe maelezo yake ya tarehe 17 april 2025.
Mkude: Hatuna pingamizi.
SHAHIDI ANAPEWA MAELEZO YAKE.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama hayo ndio maelezo uliyoyaandika tarehe 17 april 2025?
Shahidi wa kificho P3 : ngoja kidogo nayapitia.
Mhe. Lissu: waeleze waheshimiwa majaji kama hayo ni maelezo yako?
Shahidi wa kificho P3 : ndio yenyewe
Mhe. Lissu: waheshimiwa majaji nataka ku-impeach credit ya shahidi huyu, nitamsomea maelezo yake, nitaonyesha maeneo ambayo nataka kumhoji halafu nikimaliza nitakuomba uyawasilishe kama kielelezo.
Shahidi wa kificho P3 : sawasawa.
Mhe.Lissu: anamsomea shahidi maelezo yake.
Mhe.Lissu: waeleze waheshimiwa Majaji kama nilichokisoma ndicho kilichoko kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P3 : ndiyo ulichokisoma ndicho kilichoko kwenye maelezo yangu.
Mhe.Lissu: Sasa shahidi nataka nikuhoji kwenye eneo unalosema wewe ni mfuasi wa CHADEMA na maeneo mengine kadri nitakavyokuhoji kutokana na ushahidi wako.
Mheshimiwa Lissu anamsomea shahidi maeneo yote anayotaka kumhoji.
Maeneo 8.
Mhe.Lissu: Sasa hili nikuhoji sawasawa naomba uwaeleze waheshimiwa Majaji kama ungependa maelezo yako yapokelewe kama kielelezo mahakamani.
Shahidi wa kificho P3: ndiyo napendelea iwe hivyo.
Mhe.Jaji: itakuwa D12
Mhe.Lissu: ahsante waheshimiwa Majaji, naomba shahidi apewe kielelezo D12
Mhe.Lissu: Sasa swali langu la kwanza ni kwamba kwenye ushahidi wako leo umeieleza mahakama kuwa wewe ni mfuasi wa CHADEMA tangu mwaka 2021, ni kweli au si kweli.
Shahidi wa kificho P3 : ni kweli.
Mhe.Lissu: kwenye kielelezo D12 wasomee waheshimiwa Majaji pale unapoanzia mimi pia ni........ endelea hadi nitakapokwambia inatosha.
Shahidi wa kificho P3 : mimi pia ni mfuasi wa chama hicho.....
Shahidi anasitasita katika kusoma.
Mhe.Lissu: naomba pia nipewe kielelezo hicho naona kama shahidi anatupoteza.
Part 203 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 201
Anasimama Wakili wa Serikali Mkude anasema tunashahidi mwingie wa kulindwa ni P3,
Mpaka sasa huyu ni shahidi wa 13.
Shahidi ameingia kwenye kijumba cha mbao tayari.
Sasa anajitambulisha.
Shahidi wa kificho P3 : Nina miaka 35
Shahidi wa kificho P3: dini yangu muislamu
Shahidi wa kificho P3: naishi halmashauri ya Mbeya mjini, mtaa wa Mwamtengule kata ya Syesye
Shahidi wa kificho P3: najishughulisha na kazi ya dereva boda boda
Shahidi wa kificho P3: shughuli zangu nafanyia katika halmashauri ya jiji la Mbeya.
Shahidi wa kificho P3: nina miaka nane tangu naendesha boda boda
Shahidi wa kificho P3: mimi ni mfuasi wa CHADEMA
Shahidi wa kificho P3: nimekua mfuasi tangu 2021 mpaka sasa bado ni mfuasi
Shahidi wa kificho P3: nimewahi kushiriki matukio baadhi kama kongamano la kutoka Mbalizi mpaka Kabwe tulipoenda kumpokea Mhe. Mbowe mwaka 2024.
Tukio lingine ni kongamano la vijana lakin bahati mbaya au nzuri hatukufanikiwa kwasababu serikali ilizuia.
Shahidi wa kificho P5: tarehe 4 april 2025 nakumbuka kijiweni kwangu kwenye boda boda nilikua nachezea simu yangu nikapata kuona hotuba fupi ambayo Mhe. Tundu Lissu akizungumzia uchaguzi uliopangwa kufanyika 2025.
Shahidi wa kificho P3 : hotuba niliiona youtube.
Shahidi wa kificho P3 : namfahamu Tundu Lissu kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuwa nafatilia sana chama cha CHADEMA tangu mwaka 2021.
Katika chama Tundu Lissu ni mwenyekiti wa CHADEMA, baada ya kusikiliza ile hotuba pale kijiweni nikaanza kuwashirikisha wanachama wenzangu wa boda boda na kuanza kuwashawishi wengine wenye mapenzi na CHADEMA kufanya yale mh. Tundu Lissu ameyasema.
Niliwashawishi tuwe kitu kimoja kupambana kuzuia uchaguzi 2025, tulipanga kuzuia uchaguzi kwa namna ya kwamba watu watakaoenda kupiga kura kuwafanyia fujo ikiwepo kupigwa mawe, ushawishi nilikua naufanyia katika kijiwe changu cha pikipiki, baada ya kushawishi wenzangu kuna baadhi waliliridhika na ushawishi wangu na baadhi hawakuridhika.
Shahidi wa kificho P3 : baada ya hapo alitokea mtu mmoja akanipoint kwenye kijiwe na akaniomba tuongee mara moja, nikaenda kumsikiliza na akajitambulisha kuwa. Yeye ni ofisa wa polisi, akaniambia nahitajika twende kituo cha polisi kwa mahojiano yangu mimi na yeye nilivyofika kituo cha polisi wakaniambia nitoe viatu na mkanda na wakaniweka mahabusu.
Wakili: Shahidi P3 baada ya kukaa mahabusu nini kilifuata
Shahidi wa kificho P3 : baada ya muda mchache nikapelekwa kwenye chumba kingine wakaanza kunihoji kwamba nilikuwa naongea nini pale kijiweni, kwanini nilikuwa nahamasisha kufanya uasi.
Wakili: walikuuliza kwa nini unahamasisha uasi gani kama unakumbuka.
Shahidi wa kificho P3: kwanini nahamasisha uasi wa kuzuia uchaguzi wa 2025.
Wakili: Sasa shahidi baada ya maelezo hayo nini kilifuatia.
Shahidi wa kificho P3: waliniambia nitafute mtu wa kunidhamini ili niweze kuendelea na taratibu nyingine.
Wakili: ikawaje.
Shahidi wa kificho P3: nilimpata ndugu yangu akaja kunidhamini.
Wakili: nini kilifuata
Shahidi wa kificho P3: nilipata ndugu yangu akaja kunidhamini. Nikaambiwa niwe naripoti Kila baada ya siku tatu.
Wakili: ulikuwa unaripoti wapi.
Shahidi wa kificho P: nilienda kuripoti Kituo cha Polisi Ilonga.
Wakili: ulivoenda kuripoti ikawaje.
Shahidi wa kificho P3: nikaingia ndani kituoni na kukutana na huyo askari aliyeniandika maelezo toka mwanzo.
Wakili: huyo Askari aliyekuandika maelezo kutoka Mwanzo anaitwa nani kama unakumbuka.
Shahidi wa kificho P3 : namkumbuka kwa jina moja anaitwa Amani.
Wakili: baada ya kukutana na Amani mlifanya nini.
Shahidi wa kificho P3: aliniandika maelezo tena na kuniambia naendelee na utaratibu wa kuripoti.
Wakili: waheshimiwa Majaji wa Mahakama kuu kwa Shahidi huyu ni hayo tu
Part 202 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 19, 2026
Jana tuliishia Part 195 so leo tunaendelea na-;
Part 196
Majaji na mtuhumiwa ndio wanaingia ndani ya Chumba cha Mahakama almaarufu Ukumbi Na. 1 hapa Mahakama Kuu.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara, John Heche alifika mapema sana hapa Mahakamani majira ya saa 3 asubuhi.
Jaji anamuita kalani asome namba ya shauri anasoma hapa.
Jaji anasema Wakili wa Serikali unasemaje?
Anasimama Renatus Mkude anatambulisha kikundi chake cha kila siku anachoshirikiana nacho kuiwakilisha Jamhuri.
Mshitakiwa anasema yuko tayari pia.
Jamhuri wanadai wanamambo mawili.
1. Notice of additional substance of Evidence chini ya kifungu cha 308 (1) Taarifa ya ushahidi wa ziada.
2. Jambo la pili
Mwenendo wa shauri linaloendelea na kauli zinazotolewa kuhusu mashahidi wanaotoa ushahidi Mahakamani.
Anasima Mh. Tundu Lissu kurespond kwenye hayo Mambo mawili yaliyosemwa na Mawakili wa Serikali.
Kuhusu hiyo Notice yao
utaratibu wa kisheria hauruhusu.
Anasimama Katuga anasema mtuhumiwa afate utaratibu kwamba mawakili wa Serikali wameregister Notice
Hivyo jukumu lake ni kujibu kuwa mtuhumiwa yupo tayari kusikiliza?
Mhe. Lissu anasema kama wameleta notice basi wafahamu kwamba nitakua na lakusema baada ya submission yao.
Waendelee tu sitaacha kitu, wajue hilo.
Majaji wanashauriana kwa muda mrefu kidogo hapa, tunasubiri nini kitakachoendelea.
Mhe.Jaji: tunajaribu kuangalia kama hii notice iko ndani ya mfumo na tumeona ni kweli iko ndani ya mfumo.
Katuga: tunaomba tuisubmite kwanza ili tuweze kumuombea shahidi tuliyenaye leo kwa sababu shahidi tuliyenaye leo si miongoni kati ya mashahidi tuliowaombea.
Mhe.Lissu : kiutaratibu ili waweze kusubmit notice ni lazima wafate utaratibu kwa sababu hawajafuata utaratibu tuendelee na mashahidi waliopo.
Mhe.Jaji: tutaendelea na mashahidi waliopo lakini hatuwezi kuacha notice hii bila kuizungumzia ili iweze kuingia kwenye utaratibu wa Mahakama, wakati tukiendelea na mashahidi waliopo kesho tuweze kuanza na hii notice.
Mhe.Lissu: siku ya jana tuliambiwa Shahidi aliyepaswa kuendelea ambaye ni mpelelezi Mkuu alipata msiba hivyo ataendelea leo, sasa wanatwambia kuwa huyu shahidi wanayemuombea notice anayo maelezo ya ziada ni kwa nini tusiendelee na mashahidi waliopo kwanza wakati wakifuata utaratibu.
Katuga: wameshimiwa Majaji naomba tuendelee na submission ya hii notice kwanza kabla ya kuendelea kusikiliza mashahidi wengine ili tujue kama tutaruhusiwa kumleta huyu Shahidi.
Majaji wanaendelea kujadiliana hapa.
Mhe.Jaji: kwa sababu tayari tunao mashahidi wengine hii issue ya notice ibaki reserve isubirie kwanza tutaizungumzia baada ya kumaliza mashahidi waliopo, hivyo tuendelee na mashahidi waliopo kwanza.
Mkude: Mhe.Jaji tunaomba tuadress mambo yanayoendelea katika premise ya mahakama kuhusu mashahidi kabla hatujaendelea.
Mhe.Jaji: mshitakiwa ameomba kujua ni mambo gani hayo, yasijekuwa mambo ya kutupotezea muda yanayohitaji tuanze kuandika rulling kwanza na kutuzuia kuendelea.
Wakili Mkude: mheshimiwa Jaji kuna mambo yamekuwa yakiendelea na mshitakiwa amekuwa akiadress baadhi ya mambo. Tangu kesi ianze kuna mambo yamekuwa yakijadiliwa kuhusu mashahidi wanavotoa ushahidi wao, katika mitandao ya kijamii mambo yamekuwa yakizungumzwa namna mashahidi wanavotoa ushahidi wao, wengine wakiitwa waongo, hatukatazi kureport muenendo wa kesi lakini usiathiri proceedings. Kifungu 114 cha Penal Code.
Kwa kifupi hawa jamaa hawataki mashahidi na ushahidi wao uzungumzwe nje ya Mahakama. Hawataki habari za kwamba mashahidi ni waongo. 😂😂 yaleyale ya kutaka kesi iwe gizani kwa kila kitu.
Hata hii kuripoti tu wanaona wananchi mnafaidi sana, wanataka Mahakama izuie.
Part 197 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 193
Wakili wa Serikali; ikawaje?
Shahidi wa kificho : Nikaandika maelezo haya niliyoyatoa Mahakamani.
Wakili wa Serikali anasema Mheshimiwa Jaji Mwisho wa Mahojiano na Shahidi. Tuko tayari kwa Maswali ya Dodoso.
Anasimama Mhe. Tundu Lissu.
Mhe. Lissu: Unanisikia?
Shahidi wa kificho P7 : Vizuri sana.
Mhe. Lissu: we ni mzaliwa wa kiranyi?
Shahidi wa kificho P7: Ndio
Mhe. Lissu: Unapandia Sakina juu kama unaenda kwa Mzee Disouza Wakili?
Shahidi wa kificho P7: kimya
Mhe. Lissu: Unanisikia shahidi?
Shahidi wa kificho P7 : siwezi kuwa nawajua watu wote
Mhe. Lissu: Ila unapandia Sakina pale?
Shahidi wa kificho P7 : Ndio
Mhe. Lissu: Sasa sitakufuata huko ila nilivyoona kiranyi nikakumbuka nimefanya kazi na Mzee Disouza huko.
Shahidi wa kificho P7 : Sawa.
Mhe. Lissu: Sina shida na wewe unajua hilo? Sipigi watu.
Shahidi wa kificho P7 : Hata mimi sikuogopi.
Mhe. Lissu: Mbona umejificha huko kwenye kibox kama huniogopi?
Shahidi wa kificho P7: Ndio hivyo sasa
Mhe. Lissu: Sasa tuanze na ushahidi ambao uliandika maelezo kuhusu tuhuma za wewe kufanya kosa la kutaka kufanya fujo?
Shahidi wa kificho P7 : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Hayo maelezo ya kosa hilo yako wapi?
Shahidi wa kificho P7 : maelezo niliyoandika tarehe 03/04 ndio hayo hayo niliandika tarehe 17/04.
Mhe. Lissu: Uliandika au hukuandika tarehe 03/04
Shahidi wa kificho P7 : niliandika kweli
Mhe. Lissu: yako wapi?
Shahidi wa kificho P7 : Waulize maaskari
Mhe. Lissu: Wewe ni mjanja nenda kawaulize hao maaskari wako, Leo nitashinda hapa na wewe.
Tarehe 17/04 ukioneshwa hayo maelezo utayatambua?
Shahidi wa kificho P7 : Nitayatambua.
Mhe. Lissu: Naomba aonyeshwe maelezo yake tafadhali. Wanamtafutia na kumpatia.
Shahidi wa kificho P7 : Ndio haya maelezo yangu.
Mhe. Lissu: Umeyapata?
Shahidi wa kificho P7 : nayapitia
Mhe. Lissu: Yapitie halafu wambie majaji kama ndio yako?
Shahidi wa kificho P7 : ndio yenyewe.
Mhe. Lissu: Naomba nimsomeee maneno yake na nitamuonesha maeneo ninayotaka kumkanusha na baadae kuomba ayatoe kama ushahidi.
Anaanza kumsomea hapa.
Amemaliza anamuuliza je maelezo haya yako sawa na uliyonayo?
Shahidi wa kificho P7 : Ndio yako sawa
Mhe. Lissu: Sasa nakuoensha maeneo nitakayokukanusha.
1. Kuhusu kwa Morombo kuwa na watu wengi
2. Tar. 03/04 kuna mtu mmoja alianza
kusema habari za Lissu na Chadema.
3. Watakinukisha Mbaya
4. Polisi wanaiba kura hata ukienda
Mahakamani hutapata haki.
5. Kuhusu wewe kupata hamasa.
6. Uliingia kwa kutumia simu.
Anamsomea hayo maeneo mengi kidogo atakayomuhoji.
Mhe. Lissu: Je ungependa maelezo yako yapokelewe kama kielelezo cha ushahidi?
Shahidi wa kificho P7 : Ndio.
Jaji upande wa Mashitaka mnasemaje?
Wakili Renatus: Hatuna pingamizi.
Jaji Ndunguru: Basi kitakuwa kielelezo D10 kwa Upande wa Mshitakiwa.
Mhe. Lissu: Naomba sasa shahidi apatiwe kielelezo D10.
Mhe. Lissu: Umeieleza Mahakama kuwa pale kijiweni kuna watu wengi ikiwemo madereva bajaji na wenye maduka ya vitu vya nyumbani
Shahidi wa kificho P7 : Kweli
Mhe. Lissu: Sasa tuoneshe kwenye hicho kielelezo hayo maneno yapo?
Shahidi wa kificho P7 : Hayapo.
Mhe. Lissu: tar. 03/04 mlikuwa mnazungumza mazungumzo ya kawaida na kuna mtu akaibua mazungumzo mengine kuhusu Chadema kuzuia Uchaguzi.
Shahidi wa kificho P7 : ndio
Mhe. Lissu: haya nioneshe yapo wapi?
Shahidi wa kificho P7 : hapa imesema alianzisha lakini mtu yani
Mhe. Lissu: Maneno yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P7 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Tena watakinukisha mbaya. Yapo au hayapo kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P7 : Watakinukisha.
Mhe. Lissu: swali langu umesema hayo maneno yalisemwa na mtu mmoja?
Shahidi wa kificho P7 : Hapana.
Mhe. Lissu: Ahsante. Sasa umesema pia huyo mtu mmoja akasema Polisi wanaiba kura hata ukienda mahakamani majaji ni vibaraka wa CCM.
Part 194 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 18, 2026
Jana tuliishia Part 191 so leo tunaendelea na-;
Part 192
Kesi inaanza muda huu Majaji na Mshitakiwa wamefika.
Mawakili wa Serikali pia wapo tayari.
Hali ya hewa ilikuwa ya mvua kwahiyo mahudhurio sio makubwa ya watu hapa Mahakamani.
Tupo hapa kuwaletea updates kama kawaida.
Anasimama Renatus Mkude anasema wanae shahidi mmoja lakini shahidi mwingine anayefuata amefiwa na Mkwe wake kwahiyo leo tunae shahidi mmoja.
Anasimama Lissu anasema kama amepata msiba ni wazi hawezi akaja.
Mimi niko tayari kuendelea na shahidi aliyepo lakini tulikubaliana angalau waje mashahidi watatu kwa siku.
Nasema hayo sio kwasababu sitaki watu waende msibani ila nasema ili tujue ni muhimu tukatumia muda vizuri ili wasio kwenda msibani tubaki nao kufanya kesi.
Anasimama Renatus Mkude anasema hili ni jambo la kibinadamu tunaomba na sisi mawakili wa serikali twende pale kumcomfort mwenzetu.
Jaji Mshitakiwa unasemaje?
Mhe. Tundu Lissu sijawahi kuwa na roho mbaya kiwango hicho kukataza watu wasiende msibani, kama wao wameona kuna umuhimu huo wa kwenda.
Jaji anasema basi tuendelee.
Renatus anasema shahidi tuliyenae ni P7 na ataongozwa na Thawabu Issa Wakili wa Serikali.
Shahidi analetwa anaingizwa kwenye kibox chenye joto. 😂
Jaji anauliza una miaka mingapi?
26 ninayo.
Dini yako?
Mkristo.
Anaapishwa hapa Shahidi.
Wakili wa Serikali Thawabu Issa anaanza kumuhoji shahidi hapa.
Wakili: unajishughulisha na nini?
Shahidi wa kificho P7 : Dereva bajaji nafanyia kwa Morombo kule Arusha toka 2023 nafanya kazi hiyo.
Wakili: Hapo kwa morombo pakoje?
Shahidi wa kificho : Kuna watu wengi sana. Kuna maduka na watu wanafanya biashara hapo. Ikiwemo maduka ya mahitaji ya nyumbani.
Wakili: Tarehe 03/04/2025 kuna nini kilitokea?
Shahidi wa kificho : hiyo tarehe majira ya jioni nilikuwa kijiwe cha kwa morombo Arusha. Tulikuwa hapo kijiweni na tunafanya mazungumzo ya kawaida.
Wakili: Ikawaje?
Shahidi wa kificho : Kuna mwenzetu akasema hamjasikia Chadema wamesema watazuia Uchaguzi wa Mwaka huu. Wamesema watakinukisha mbaya. Alikuwa anatuelezea huyo mtu.
Wakili: kingine ni nini?
Shahidi wa kificho : Akasema kuwa Polisi wanaiba kura hata ukienda Mahakamani hautapata haki.
Wakili: Kikaendelea baada ya mtu huyo kusema?
Shahidi wa kificho : Akasema pia Majaji ni vibaraka wa CCM, akasema pia mwaka 2024 tume ya Uchaguzi ilipewa maelekezo ya kukata wajumbe wa Chadema. Tukiwa tunaendelea na hayo mazungumzo nilipata hamasa kupitia hayo maneno niliyosikia akisema yule Bajaji mwenzangu.
Wakili: Sasa weka vizuri, wewe ulifanya nini?
Shahidi wa kificho : Niliingia kwenye mtandao wa youtube na mimi niweze kujionea hayo maneno. Nilitumia simu yangu na kuingia channel inaitwa Jambo. Simu ya janja.
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho : Nikafungua channel ya Jambo na kukuta yale maneno kama nilivyoambiwa hapo kijiweni.
Wakili: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho : Baada ya dakika chache kuna watu wakaja wakajitambulisha kama wao ni maaskari na baadae watu walikimbia tukakamatwa mimi na P4.
Wakili: kilichoendelea hapo?
Shahidi wa kificho : Tukapelekwa kituo cha Polisi Murieti. Tulikaa kama Dakika 45 tukapelekwa kituo cha Polisi Central Mjini.
Wakili: baada ya kuwa umepelekwa Central ikawaje?
Shahidi wa kificho : Tukaingizwa Ofisi ya RCO nikaambiwa nashitakiwa kwa kosa la kutaka kufanya fujo, niliandikwa maelezo na kuingizwa Mahabusu na asubuhi yake ndugu zangu walinifuata nikazaminiwa na kupewa tarehe za kuwa naenda kuripoti kwenye hicho kituo cha Polisi.
Wakili: Nini kilifuata?
Shahidi wa kificho : Nikawa naripoti kwa mujibu mpangilio wa hiyo ratiba na ilipofika Tar. 17/04 2025 baada ya kufika kuripoti kama kawaida, nikaambiwa naandikwa maelezo upya.
Part 193 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 17, 2026
Jana tuliishia Part 182 so leo tunaendelea na-;
Part 183
Mhe. Tundu Lissu ameingia muda huu leo makamanda wanaimba Shujaaa Shujaaa Shujaa.
Amepiga Tshirt yake nyeusi hapa.
Majaji nao wanaingia kama kawaida yupo
1. Jaji Dunstan Ndunguru Kiongozi wa Jopo.
2. Jaji James Karayemaha
3. Jaji Ferdinand Kiwonde
Wote watatu wapo wakiwa kwenye majoho yao mekundu na Beib nyeupe.
Renatus Mkude anasimama, yupo na ajuaye, Thawabu Issa, Ignas, Winiwa Kasawa pia.
Anasema leo wako na mashahidi watatu na tuko tayari kuendelea.
Jaji anamuuliza Mshitakiwa nae anamjibu niko tayari.
Majaji wanaandika kidogo.
Ukimfuatilia Mwenyekiti wa Jopo la Majaji, Jaji Ndunguru amekuwa anaonekana ni mtu mstaarabu.
PF 1864 ASP Geofrey Lutufye
Anaingia hapa kizimbani huyu ni askari huyu ni PW 9 ni shahidi ambae muonekano wake yupo kama amekesha hajanyoa nywele, ameshika kipaza sauti anatetemeka.
Naitwa PF18544 ASP Geofrey Aggrey Lutufye
Umri wa miaka 47.
Naishi Arusha.
Mkristu.
Huyu shahidi leo atadondoka kizimbani maana kwa anavotetemeka wote tunamuona hapa, Ukikutana nae barabarani huwezi sema ni Polisi maana amidevu na minywele yupo rafu sana.
Anaongozwa na Renatus Mkude.
Anaanza Renatus Mkude kumuuliza Maswali.
Wakili: Ikumbushe mahakama majina yako.
ASP Geofrey Lutufye: Anataja majina yake hapa
Wakili: Kazi yako?
ASP Geofrey Lutufye: upelelezi, niko ofisi ya mkuu wa upelelezi Arusha na mimi ni kiongozi wa kikosi cha Anti Robbery
Wakili: Anti Robbery ni nini?
ASP Geofrey Lutufye: Kikosi cha kuzuia uhalifu kama vile uporaji.
Kumbe ndio maana ana hali hii huyu askari. maana kiukweli amekaa hovyo sana kumbe anadeal na mambo ya kupora.
Wakili : Umepata mafunzo gani?
ASP Geofrey Lutufye: Nilipata tarehe 28/04/2003 Chuo cha Polisi Moshi.
Nilijifunza upelelezi na mafunzo mengine mbalimbali, nilimaliza mwezi wa 11, 2003.
Mafunzo mengine nilipata ya nyota ya kwanza, nilisomea Chuo cha Polisi Moshi ilikuwa ni Mwaka 2013 na baadae mafunzo ya cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi. Nililipata chuo Dar es salaam Polisi Academy hapa Dar es salaam nilimaliza mwezi wa 11 mwaka 2023.
Wakili: kingine ni nini?
ASP Geofrey Lutufye: Mengine ni on job trainning yaani mafunzo kazini.
Wakili: Una uzoefu kazini wa mwaka gani?
ASP Geofrey Lutufye: Miaka 15 ya upelelezi ninayo.
Wakili: Arusha uko tangu lini ofisi ya upelelezi.
ASP Geofrey Lutufye: Tangu mwaka 2023.
Wakili: kabla ya hapo ulikuwa wapi?
ASP Geofrey Lutufye: Nilianzia Polisi Oysterbay Dar es salaam, nilianza kama General Duty na baadae nikapelekwa Geita Ofisi ya Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Geita ndo nikahamia mkoa wa Arusha baada ya huko.
Wakili: Majukumu yako hapo ofisi ya Upelelezi Arusha ni yapi?
ASP Geofrey Lutufye: Kufanya doria mbalimbali, kukamata watuhumiwa, kufanya upelelezi na kuwafikishia watuhumiwa Mahakamani.
Wakili: Tarehe 03/04/2025 kilitokea nini?
ASP Geofrey Lutufye: Nilikuwa na wenzangu tukiwa na section 1 ambayo ni askari 9 hadi na dereva tukiwa kwenye doria.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Tulikuwa tunafanya doria tukiwa tunatumia gari la Polisi aina ya Toyota Landcruiser na nikapata maelekezo kutoka kwa kaimu mkuu wa upelelekezi ASP Bonny Mgogo.
Wakili: kwa njia ulipata maelekezo?
ASP Geofrey Lutufye: Nilipata kwa njia ya radio call ambayo ni kifaa cha mawasiliano. Maelekezo kuwa amepata taarifa kutoka kwa msiri kuwa kwa Mromboo kijiwe cha Bajaji kuna vijana wanahamasishana kuzuia uchaguzi wa mwaka 2025.
Wakili: Baada ya kufika huko kwa Mromboo nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Nilikuta vijana wakila njama za kuzuia uchaguzi Mkuu 2025.
Jaji anasema umesema Walikuwa wanakula nini?
ASP Geofrey Lutufye: Walikuwa wanazungumzia uchaguzi mkuu wa 2025.
Jaji: Kumbe walikuwa wanazungumzia sio kula tena?
Watu wanacheka.😂😂😂
Part 184 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.