VIDEO:
Makada, wanachama na viongozi 16 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mwanza wamejitosa kwenye kinyang'anyiro cha uongozi kuziba pengo ya nafasi zilizoachwa wazi ngazi ya mkoa na viongozi waliokihama chama hicho kwenda vyama vingine.
Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake, Katibu wa CHADEMA Kanda ya Victoria, Zakaria Obad amesema nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wametia 4, Katibu Mkoa 4, Katibu Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Mkoa 2, Mwenyekiti Baraza la Wazee Chadema (BAZECHA) Mkoa 3, nafasi ya Katibu BAZECHA 2 na nafasi ya uwekahazina BAZECHA mmoja.
"Tukishamaliza usaili leo hatua ambayo itafuata ni uteuzi kwa maana kamati ya uchunguzi itafanya uteuzi leo na wale ambao watakuwa wameteuliwa wataanza moja kwa moja kampeni na wale ambao hawatateuliwa watajulishwa sababu za kutokuteuliwa," amesema.
Hata hivyo Obad ametoa onyo kali kwa wagombea watakaopitishwa na wajumbe wa uchaguzi kuepukana na vitendo vya rushwa, na vitendo vinavyokiuka maadili ya chama hicho huku akidai kuwa hawatasita kuwachukulia hatua watakaobainika.
"Uchaguzi huu ni uchaguzi wa chama ambacho kipo na misimamo wazi ambayo inajulikana, chama kinachopinga rushwa hadharani, chama kinachotaka haki itendeke sio tu kuonekana na sisi kama viongozi wa Kanda tunaosimamia uchaguzi huu tutahakikisha tunasimamia kwa kutenda haki," amesema Obad
Mchekeshaji Eric Omondi ameachiwa huru leo na Mahakama ya Kilimani nchini Kenya baada ya kushikiliwa kwa siku mbili kutokana kudaiwa kuhusika moja kwa moja katika maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta yaliyofanyika majuma mawili yayopita nchini humo.
Wakili wa Omondi ambae ni mbunge wa Jimbo la Embakasi Mashariki Dkt. Babu Owino amesema mteja wake sasa yupo huru na ni mwananchi anayefuata sheria kwa uadilifu.
"Eric sasa yupo huru, ni mwananchi anayefuata sheria za nchi na amekuwa akisaidia Wakenya wa hali ya chini kwa mfululizo na ameachiwa bila masharti"
VIDEO:
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amelihutubia taifa na kupiga marufuku makundi ya raia kujichukulia sheria mkononi kwa kuwasimamisha wageni barabarani na kudai vitambulisho, huku akisisitiza kuwa wananchi wa nchi hiyo hawana tabia ya kuchukia wageni.
Katika hotuba yake ya dharura iliyotolewa kufuatia kuongezeka kwa vitisho dhidi ya wahamiaji nchini humo, Rais Ramaphosa ameonya kuwa serikali haitavumilia makundi yanayotumia changamoto za ndani, ikiwemo ukosefu wa ajira, kama kisingizio cha kuchochea uvunjifu wa sheria, vurugu na kuvuruga usalama wa nchi.
Taharuki hii inakuja wakati makundi yanayopinga wageni nchini humo yakiwa yameweka msimamo wa mwisho wa tarehe 30 Juni, 2026, kwa wahamiaji wote wasio na nyaraka halali kufunganya virago na kuondoka nchini humo.
Rais Ramaphosa ameweka wazi kuwa hakuna raia au kikundi cha kijamii chenye mamlaka ya kisheria ya kuhoji uhalali wa mgeni mtaani.
Ninajua kuwa Waafrika Kusini si watu wanaochukia wageni. Kama jamii, hatupaswi kushawishiwa kujiunga na wale wanaotaka tuwageuke watu ambao hawakuzaliwa katika nchi hii," amesisitiza Rais Ramaphosa.
Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya David Maraga(75) amekamatwa asubuhi ya leo Juni 8, 2026 alipokuwa akishiriki maandamano ya amani ya kulinda Hifadhi ya Taifa ya Nairobi dhidi ya pendekezo la ujenzi wa maegesho ya magari yenye uwezo wa kuhifadhi magari 1,300.
David Maraga ambaye ni mtia nia wa Urais kupitia chama cha United Green Movement Party alitangaza kuwa leo atafanya maandamano hayo akiwaalika wakenya huku wakiwa wamepangwa kuvaa mavazi ya kijani.
Maraga amekuwa Jaji Mkuu wa Kenya kwa miaka mitano (2016-2021) ambapo baada ya kustaafu miaka ya karibuni amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali jambo lililopelekea mwaka jana 2025 kunyang'anywa walinzi ambao alipatiwa kwa mujibu wa sheria za wastaafu nchini humo.
Mkoa wa Morogoro leo Juni 8, 2026 umepokea Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 ambazo zinatarajiwa kukimbizwa katika Halmashauri tisa za Mkoa huo kwa lengo la kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.
Jumla ya miradi 63 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 50.9 itatembelewa na Mwenge huo Uhuru katika kipindi cha mbio hizo.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Kighoma Malima, katika tukio liliofanyika mkoani humo baada ya kuwasili ukitokea Mkoa wa Dodoma.
Mapokezi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo wa Morogoro.
Akiupokea Mwenge huo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amesema Mwenge wa Uhuru ni chombo muhimu cha kuhamasisha maendeleo, uwajibikaji na ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo hapa nchini.
Aidha, amewataka wananchi wa Morogoro kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio za Mwenge na kulinda mafanikio ya miradi inayotekelezwa kwa manufaa ya jamii.
Ukiwa Mkoani humo mwenge wa uhuru utakimbizwa umbali wa Km 1898 na utakabidhiwa Mkoa wa Tanga tar.17 Juni, 2026
VIDEO:
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, Masaga Kaloli, ameingilia kati mjadala mzito wa kisiasa uliozuka bungeni hivi karibuni baada ya Mbunge wa Tunguu (Zanzibar), Simai Mohammed Said, kambatiza kiongozifulani serikali jina la "Yuda Iskariote."
Akizungumza na wananchi mkoani Mbeya jana Jumapili, Juni 7, 2026, Kaloli amesema kuwa CHADEMA haitaki kuingilia migogoro ya ndani ya chama tawala, lakini akatoa ofa kwa kiongozi huyo anayeitwa Yuda kwamba kama ana nia njema na nchi basi anakaribishwa kujiunga na upinzani.
Kaloli ametumia sakata hilo kukosoa mfumo wa uwakilishi wa wabunge wa chama tawala bungeni, akidai kuwa wameacha wajibu wao wa kikatiba wa kuisimamia serikali na kutetea wananchi, na badala yake wamebaki kumsifu na kumlinda mkuu wa nchi pekee.
Karibu kupitia kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za baadhi ya magazeti ya Tanzania yaliyochapisha Habari za Siasa, Jamii, Uchumi, Michezo, Sanaa na Burudani leo, Jumatatu Juni 08.2026
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema kuwa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Urusi ni ziara ambayo imeleta mtikisiko chanya wa kidunia.
Balozi Kombo ameyasema hayo leo Juni 7, 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa mtikisiko huo unatokana na sababu kadhaa ikiwemo nchi idadi ya watu duniani ambao Urusi inahusiana nao wakikadiriwa zaidi ya bilioni sita.
"Nimekwenda ziara kadhaa na Mheshimiwa Rais lakini naomba nithibitishe ziara ambayo imeleta mtikisiko wa kidunia ni ziara hii ya Urusi. Mtikisiko chanya sababu ya kwanza imefanyika wakati ambapo Urusi inapanua uchumi wake kwenye bara la Afrika"
Wakati Serikali ikiendelea kuhimiza utekelezaji wa miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), imeelezwa kuwa mtazamo hasi wa baadhi ya wananchi kuhusu mfumo huo bado ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha mafanikio ya miradi hiyo nchini.
Akizungumza katika Muhadhara wa Umma uliofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), mtoa mada wa tatu, Dkt. Amani David kutoka Idara ya Usimamizi wa Biashara na Menejimenti, amesema historia ya Tanzania katika mfumo wa ujamaa imechangia kuwepo kwa hisia kwamba baadhi ya miradi ya PPP inaweza kuwa na sura ya unyonyaji.
Amesema katika kipindi ambacho nchi inaendelea kufanya mageuzi ya kiuchumi kuelekea uchumi wa soko, bado kuna wananchi wanaoutazama ushiriki wa sekta binafsi kwa tahadhari, jambo linaloathiri namna wanavyoupokea na kuunga mkono utekelezaji wa miradi ya ubia.
“Katika uchumi kama wetu ambao umetoka kwenye mfumo wa ujamaa na sasa unaelekea zaidi kwenye uchumi wa soko, wakati mwingine kunakuwa na mtazamo kwamba miradi ya PPP inaweza kuleta unyonyaji,” alisema Dkt. Amani.
Kwa mujibu wake, hali hiyo inaonyesha umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa umma ili kubadili fikra na mtazamo kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika kuchochea maendeleo ya taifa kupitia ushirikiano na Serikali.
Zaidi ya vikundi 43 vya wajasiriamali vimesajiliwa kufuatia mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Fadhil Ngajilo, yaliyofanyika kwa siku sita katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Ruaha, Manispaa ya Iringa.
Akifunga mafunzo hayo leo Juni 2026, Mwenyekiti wa UWT Iringa Mjini, Christina Makweyi, amepongeza hatua hiyo na kuwataka wajasiriamali kuwa wabunifu, kuzalisha bidhaa zenye soko na kutumia maeneo rasmi ya biashara yaliyotengwa na serikali.
Kwa upande wake, Mbunge Fadhil Ngajilo amesema mafunzo hayo yamekuwa chachu ya maendeleo kwa wajasiriamali, huku akibainisha kuwa tayari vikundi 43 vimeshasajiliwa ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo kutoka halmashauri na taasisi za kifedha.
Aidha amesema mafunzo hayo yataendelea kutolewa kwa mfumo wa kanda ikiwemo Kihesa na Ruaha ili kuwafikia wajasiriamali wengi zaidi.
Baadhi ya washiriki wameishukuru ofisi ya Mbunge kwa kuwapatia elimu ya vitendo kuhusu biashara, matumizi sahihi ya fedha pamoja na kuwajengea ushirikiano kupitia mafunzo hayo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe ametoa wito kwa walimu wote nchini wa shule za awali, msingi na sekondari kufundisha kwa umahiri ili taifa liwe imara na rasilimali watu yenye kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii.
Prof. Shemdoe ametoa wito huo kwa walimu hao Juni 06, 2026 katika Ukumbi wa Maktaba mpya wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano la taifa la stadi za ufundishaji kwa walimu wa awali, msingi na sekondari nchini.
“Kaulimbiu hii inayosema Ufundishaji Bora, Taifa Imara ina mashiko, hivyo ninatoa wito kwa walimu mfundisheni vizuri, na wito huu si kwa walimu mlioshinda tu bali ni kwa walimu wote nchi nzima kwani mnapaswa kuzingatia kuwa ufundishaji bora utatupatia taifa imara,” amesisitiza Prof. Shemdoe.
Ili kuwapatia motisha walimu 35 walioshinda katika shindano la taifa la stadi za ufundishaji, Prof. Shemdoe amewaelekeza wakurugenzi wa halmashauri zote ambazo walimu hao wanafundisha kuhakikisha wanawapatia kiwanja ili waendelee kubaki katika vituo vyao vya kazi na kulitumikia taifa, huku viwanja hivyo vikibaki kuwa ni kumbukumbu ya kudumu ya namna Serikali inavyothamini utendaji kazi wao.
Sanjari na hilo, Prof. Shemdoe amewataka walimu wengi zaidi kujitokeza kushiriki katika shindalo hilo mwakani ili kuibuka washindi na kutambulika kitaifa kutokana na umahiri wao katika stadi za ufundishaji.
Aidha, Prof. Shemdoe amemshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele kikubwa cha kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu hususani katika eneo la ujifunzaji na ufundishaji, hatua ambayo imeongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba amesema kuwa shindano hilo limejumuisha halmashauri zote 184 za Tanzania Bara na linaratibiwa na Serikali kupitia TET chini ya Programu ya kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) na Mradi wa kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
Washindi wa shindano hilo la taifa la stadi za ufundishaji kwa walimu wa awali, msingi na sekondari wamepatiwa zawadi ya fedha tasilimu, kompyuta, kompyuta mpakato, vibao vya kidijitali na projekta kwa ajili ya shule zao ili kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pemba leo, Jumapili Juni 07.2026 kimetoa taarifa kwa umma kuwa Kamati Tendaji ya Chama hicho ngazi ya Kanda ilikutana katika kikao chake cha dharula kilichoongozwa na Mwenyekiti wake Omar Nassor
Katika kikao hicho kilichofanyika Juni 06.2026, agenda ya kikao chake ilikuwa ni kujadili suala la nidhamu linalomhusu aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohammed, ambapo Kamati hiyo ilipokea na kujadili taarifa iliyowasilishwa mbele yake na kufanya tathmini kwa kuzingatia masharti ya Katiba, Kanuni na Miongozo ya chama hicho
Taarifa hiyo kwa umma ilizosainiwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Pemba Abdulla Hassan, imesema baada ya kujiridhisha kuwa Said Issa Mohammed amekiuka Katiba, Kanuni na Miongozo ya chama hicho, hivyo kwa pamoja Kamati hiyo imeazimia kumfukuza uanachama kuanzia Juni 06.2026
"Kutokana na uamuzi huo, CHADEMA Kanda ya Pemba kinautaarifu umma na wanachama wote kuwa kuanzia tarehe tajwa, Ndugu Said Issa Mohammed si mwanachama wa CHADEMA na hatambuliki tena kama kiongozi au mwakilishi wa chama katika ngazi yoyote, hivyo kauli, matendo au shughuli zozote atakazozifanya baada ya tarehe hiyo zitakuwa ni za kwake binafsi na hazitahusishwa na chama" -imeeleza taarifa hiyo.
Watetezi wa haki za binadamu wawili, Jackson Martine Kabalo na Joseph Chaviruka Mrindoko, maarufu kama “Wachokonozi”, wameachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Arumeru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuendelea na ushahidi katika Shauri la Jinai Na. 000017735/2025.
Taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) imeeleza kuwa shauri hilo lilipangwa kusikilizwa tarehe 26, 27 na 28 Mei 2026 pamoja na tarehe 4 na 5 Juni 2026. Katika tarehe hizo, upande wa Jamhuri uliwasilisha shahidi mmoja pekee mnamo tarehe 26 Mei 2026 ambaye alikuwa shahidi wa saba (7). Hata hivyo, katika tarehe zilizofuata upande wa mashtaka haukuwa na mashahidi wala kutoa sababu za msingi za
kutokuwepo kwao.
Mahakama ilieleza kuwa tayari ilikuwa imetoa maelekezo kutokana na shauri hilo kuchukua muda mrefu na kwa kuzingatia umuhimu wa kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati bila ucheleweshaji usio wa lazima. Kutokana na kushindwa kwa upande wa mashtaka kuendelea na ushahidi, Mahakama iliamuru washitakiwa waachiwe huru chini ya Kifungu cha 242(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20, Marejeo
ya Mwaka 2023.
Ikumbukwe kuwa shauri hili lilianzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kama Shauri la Jinai Na. 15727/2025 ambapo tarehe 27 Julai 2025 upande wa Jamhuri uliomba kuondolewa kwa shauri hilo kwakuwa haukuwa tayari kuendelea nalo (nolle prosequi), na Mahakama ikaamuru washitakiwa waachiwe huru. Hata hivyo, siku hiyo hiyo walikamatwa tena na kufikishwa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kwa mashtaka yale yale bila maelezo ya msingi kutolewa kuhusu hatua hiyo.
Mashtaka yaliyokuwa yanawakabili ni mawili ambayo ni: Kutoa taarifa za uongo mtandaoni; na Kufanya shughuli za utoaji wa maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni.
Katika kipindi chote cha mwenendo wa shauri hili, washitakiwa walikuwa wanatetewa na mawakili kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), ambao ni Wakili Simon Mbwambo na Wakili Ally Mhyellah wa mkoani Arusha.
Karibu kupitia kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za baadhi ya magazeti ya Tanzania yaliyochapisha habari za Siasa, Jamii, Uchumi, Michezo, Sanaa na Burudani leo, Jumapili Juni 07.2026
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa, Stephen Wasira, amesema ujamaa bado ni msingi mkuu unaoendesha sera na mipango ya maendeleo nchini.
Akizungumza na wanachama wa CCM mjini Moshi, leo Juni 6 2026, Wasira alisema alikana madai kuwa mfumo huo umepitwa na wakati.
"Wale wanaojidanganya hawaujui. Misingi inayoendesha nchi sasa ni ileile ya ujamaa. Tuanzie na elimu bila malipo, tuendelee na jitihada za kuanzisha Bima ya Afya kwa wote. Haya yote ni mafanikio ya ujamaa," alisema.
Wasira alitoa mfano wa Mkoa wa Kilimanjaro, akibainisha kuwa kama sio ujamaa, ardhi na mashamba ya kahawa yangekuwa yamenunuliwa na watu binafsi na wananchi wasingeweza kumiliki.
"Kama hapa Kilimanjaro tungekosa ujamaa, kahawa yote ingenunuliwa. Ni uongo kusema ingekuwa bado mikononi mwa wananchi," alieleza.
Pia, alizungumzia umuhimu wa uwekezaji wa sekta binafsi, akisema ni jambo la kawaida na la lazima kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.
Akimnukuu Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere alisema: "Watu wote hawatakuwa na mapato sawa. Mkulima wa nyanya Kilimanjaro na mchimbaji wa gesi Lindi hawawezi kulingana. Hata wachimbaji madini nao hawalingani na wale wasiochimba."
Kwa mujibu wa Wasira, serikali inaleta haki kwa kuwatoza kodi wenye uwezo na kuwasaidia wasio na uwezo.
"Huwezi kujenga nchi bila mtaji. Wenye mtaji ni watu binafsi na kampuni. Kazi yetu ni kuwatoza kodi na kuwasaidia wanyonge," alisema.
== ==
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-Centre), David Kafulila, amesema kuwa dhana ya ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi katika kutekeleza miradi mikubwa ni sahihi na itaendelea kuwa sahihi daima. Hata hivyo, amekiri kuwa mtihani mkubwa umekuwa kwenye hatua ya utekelezaji wa dhana hiyo.
Kafulila ametoa ufafanuzi huo Juni 6, 2026, wakati akiongoza kongamano la wadau wa sekta ya afya na elimu lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), jijini Dar es Salaam.
Akifafanua utendaji wa mfumo wa PPP, Kafulila alieleza kuwa jukumu kuu la kituo anachokiongoza ni kuweka misingi madhubuti itakayolihakikishia taifa miradi yenye thamani na manufaa kwa wananchi.
Ili kukomesha hisia hasi na mashaka kutoka kwa wananchi, alisisitiza kuwa mfumo huo umejengwa kwenye nguzo ya uwazi na uwajibikaji.
VIDEO:
Ikiwa imebaki siku moja zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ngazi ya Mkoa wa Mwanza zilizoachwa wazi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukihama chama hicho limeendelea kushika kasi kwa makada na wanachama kuendelea kuchukua na kurejesha fomu.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Ofisi ya Katibu wa CHADEMA Kanda ya Victoria nafasi zilizowazi ni Uenyekiti wa Baraza la Uongozi Mkoa, Ukatibu wa Baraza la Uongozi Mkoa, Uenyekiti wa Baraza la Wazee (BAZECHA) Mkoa, Ukatibu wa Baraza la Wazee (BAZECHA) Mkoa na Ukatibu wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) Mkoa.
Wakizungumza na Royal Tv, Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema, Paul Fulano aliyetia nia kugombea nafasi ya Katibu Chadema Mkoa wa Mwanza amesema lengo kubwa ni kutaka kurudisha thamani na heshima ya mkoa wa Mwanza sambamba na thamani ya wanachama.
"Hatuwezi kuwa na Mkoa namba moja harafu ukawa na viongozi ambao wanakaa siku mbili wanakimbilia CCM, CHAUMMA kwahiyo nilazima nirudishe, nikisema kurudisha thamani ni ukweli usiopingika kwamba thamani ya wanachama mkoa huu ni ndogo sana," amesema.
Kwa upande wake Katibu BAWACHA Wilaya ya Sengerema, Olivary John aliyetia nia kugombea nafasi ya Katibu BAWACHA Mkoa wa Mwanza amesema sababu ya kutia nia ni kutaka kukomesha kasumba ya viongozi wa baraza hilo kila mara kuondoka au kuhama na kufanya baraza hilo kuwa yatima.
Itakumbukwa zoezi la uchukua fomu kugombea nafasi hizo lilifunguliwa Juni mosi mwaka huu huku likitarajiwa kufungwa kesho Juni 7 ambapo kwa mujibu wa ratiba zoezi la usaili, uteuzi na kampeni litafanyika Jumatatu Juni 8 huku Juni 9 ikiwa ni siku ya kusikiliza pingamizi na rufaa.
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam Edward Mpogolo ametoa rai kwa viongozi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia Madiwani, Mameya na Wakurugenzi kufikiria namna bora itakayopelekea makampuni yaliyopewa tenda ya kufanya usafi kwenye Barabara za Mkoa huo, kulingana na mikataba waliyopewa waweze kuja na vifaa vya kisasa vya kufanyia usafi
"Mkoa wa Dar es Salaam, ni Mkoa ambao Mheshimiwa Rais ameleta fedha nyingi za ujenzi wa miundombinu, moja ya changamoto ambayo tunaendelea kuipata ni makampuni yetu, mikataba ambayo makampuni yetu inayo kwenye Halmashauri zetu, muda wanaopewa wakati mwingine wanashindwa kununua vifaa vya kisasa vya kufanyia usafi katika maeneo ambayo yamejengwa, mfano leo hii unazungumzia Barabara ambayo Mheshimiwa Rais ameijenga kutoka kazikati ya Jiji la Dar es Salaam kwenda Ubungo, kwenda Kimara, kwenda Mbezi unategemea Mama yangu mwenye fagio afagie zaidi ya Km 40 kwa fagio ya chelewa, haiwezekani..." -Mpogolo
Amesema katika wakati huu ambapo Taifa liko kwenye maandalizi kabambe ya maandalizi ya AFCON 2027, haikubaliki kuona wageni wanaotarajia kufika kutoka maeneo mbalimbali Duniani anakuta Mama anahangaika kufagia Barabarani kwa fagio ya chelewa.
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, ameahidi ofisi yake kutafuta suluhisho la changamoto ya mikopo na madeni chechefu inayowakabili walimu 256 katika Manispaa ya Ilemela ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi bila hofu.
Akizungumza leo kwenye Tamasha la Ilemela Mwalimu Festival lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi na sekondari, Mtanda amesema changamoto ya mikopo chechefu ni kubwa hali inayosababisha baadhi ya walimu kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kutokana na makato makjubwa kwenye mishahara yao.
"Ipo changamoto kubwa ya mikopo na madeni chechefu hivi karibuni tulikutana na baadhi ya walimu kwa wilaya ya Nyamagana walikuja walimu 16 ambao payslip yao inaisha kwa sababu ya mikopo, wanashindwa kufundisha, wanashindwa kuhudhuria kwenye vituo vyao," amesema.
Kuhusu Ilemela RC Mtanda amesema "Nakupongeza Mkuu wa Wilaya umefanyia kazi maelekezo yangu, jumla ya walimu 256 wamesajiriwa kuwa na madeni na mikopo chechefu ambao nataka tufanye nao mkutano maalumu ili na hao wanaokopesha tukutane pamoja na kujadiliana nao tuyamalize ili walimu wapate utulivu,".
Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Alfred Kusaga amemuomba RC Mtanda kufikisha kilio cha upandishaji vyeo kwa walimu changamoto ambayo amedai kusababishwa na mfumo kushughulikiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amir Mkalipa amewapongeza walimu wa shule za msingi na Sekondari kwa kuendelea kuchapa kazi na kuhakikisha wanafunzi wanaofaulu wanaongezeka.
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa Tanzania haitachagua upande katika siasa wala mivutano ya kiitikadi inayovuta mataifa makubwa duniani bali itaendelea kusimamia misingi ya kutofungamana na upande wowote ikichukua fursa za kiuchumi kutoka vitalu vyote kwa maslahi ya taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari alioambatana nao katika ziara yake ya kiserikali jijini Moscow nchini Urusi, Rais Samia amebainisha kuwa nchi itashirikiana na Marekani, Ulaya, China, Urusi na Asia kwa usawa.
Mkuu huyo wa nchi amefafanuzi kuwa diplomasia ya kisasa ya kiuchumi inaitaka serikali kufungua milango kwa kila mwekezaji, huku akichambua kwa kina miradi ya kimkakati inayounganisha Tanzania na mataifa ya Magharibi pamoja na sababu zilizosababisha ukimya wa kiushirikiano na Urusi tangu miaka ya 1980.
Rais Samia ameweka wazi kuwa msimamo wa kufungua milango kwa Urusi haumaanishi nchi inatupa washirika wake wa kihistoria wa Magharibi, ambao uwekezaji wao ni mkubwa nchini.