Forgiveness: A deliberate act of Love, Mercy and Grace. In the process, God has to be involved.
It needs you to let go of the anger and bitterness that you harbor towards another person.
-Pastor Matroner George (@theoceanindar)
Matthews 6:15 ๐๐ฝ
UTUMISHI NA UONGOZI KATIKA NYAKATI ZA MWISHO
"Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari"
[2 Timotheo 3:1]
Maandiko yametoa viashiria mara kadhaa juu ya hatari iliyopo katika nyakati za Mwisho. Katika Danieli 12:4 tunaambiwa tu maarifa yataongezeka. Ongezeko la maarifa katika jamii haliji peke yake. Kuna vitu vingi tu linaambatana navyo bila kusahau uasi, kutojali, na dhambi zinazijipenyeza hata pale ulipofunga mlango.
Ukimsoma Yesu kwenye mafundisho yake juu ya nyakati za mwisho utaona kwamba kutakuwa na utapeli mwingi wa imani na mazingaombwe kwenye taasisi za imani. Jiulize kwa nini? Kwa sababu vyuma vitakaza kila kona na watu wataona sehemu ya kukimbilia ni kwenye taasisi za dini. Lakini unadhani adui atawatazama tu watu wakimbie? Anawafuata huko huko na kujifanya na yeye ni mmoja wao! Ndio maana ukisoma Yohana katika Ufunuo 13 anaonesha kuwa mpinga Kristo atajitokeza kama mtumishi wa kanisa na atatenda hata miujiza.
Paulo ambaye alitumika kwenye Ukristo wa Kizazi au tolea la kwanza alipewa neema ya kuona hatari ya siku za Mwisho. Bahati mbaya hakuoneshwa miaka ambayo hatari hizo itatokea. Hili liliachwa wazi kwa kila kizazi kujitathimini. Lakini alichokifanya, alitoa tahadhari na kuelekeza Kijana wake Timotheo anayeachiwa Kanisa afanye nini ili Kanisa na wafuasi wa Mungu wawe salama.
Kuna Kitabu kinakuja kinachotafisiri Nyaraka za Kichungaji โ Timotheo na Tito, humo utaona mwongozo wa utumishi katika nyakati za mwisho. Sio rahisi kuongoza taasisi yoyote ile katika nyakati kama hizi, na sasa inapokuwa ni taasisi ya dini, kuna kuwa na ugumu zaidi.
Washarika waombeeni watumishi wanaotumika katika taasisi zenu. Msipofanya hivyo, mtapotoshwa maana adui namba moja wa shetani ni yule anayebeba kusudi la Mungu. Waombeeni majumbani mwenu na zaidi sana kwenye mikusanyiko yenu ya kiibada.
Watumishi mnaosimama mbele ya wengine bila kujali huwa unasimama mbele ya watu wa ngapi, fahamuni jambo hili: mmewekwa katika mstari wa mbele wa mapambano. Mishale toka kwa adui, kabla haijawafikia washarika mnaowaongoza inatua kwenu! Kama mnakumbuka alichokiona Zekaria, basi kizingatieni. Kama mmesahau, nawaambia tena: Zekaria analeta neno hili: Nitampiga Mchungaji na kondoo watatawanyika. Sasa kabla hamjapigwa, liimarisheni kundi, lilisheni kundi liwe na afya. Ili hata mkipigwa ninyi, kutakuwa na watu wa kuwaombea.
Mkazo haupo tu kwenye kuombewa na watu. Wewe kama kiongozi pia uombe. Sifa #1 uliyo nayo siyo utumishi, bali ni ufuasi. Na ukijua kuwa mfuasi anatakiwa kuomba, basi fanya hivyo. Nilipumzika kwa siku nyingi tu lakini naona jambo hili linakuja kwa nguvu. Najua kuna jambo Mungu analifanya.
Nyakati hizi ni za hatari, jifungeni mikanda. Adui anaweza kupita na yeyote kwa namna yoyote ile. Taasisi za dini, jengeni utamaduni wa kujifunza Neno la Mungu kwa kina. Tukikaa katika Neno tutakuwa salama. Maana katika Neno kuna Mungu na Mungu anasema atakuwa ngao yetu.
Hii ni ahadi muhimu sana kuikumbuka. Mungu akubariki.
Amen
ยฉ 22.9.2026
Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye.
Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe.
Mithali 26:4-5 ๐๐ฝ
Rooted in the soil, driven by purpose,
From cultivating our fields to caring for our livestock, every day is an investment in feeding our nation and growing a better tomorrow. ๐น๐ฟ
Ningekuwa na karama ya unabii na kujua siri zote na maarifa yote, hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu.
1 Wakorintho 13:2 ๐๐ฝ
One chapter closed today. Big up to all the little warriors who just finished their Grade 7 National Exams. One of those warriors happens to be my Son MAHER ๐๐ช๐ฝ
Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana harusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi harusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Isa 61:10 ๐๐พ
Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Mhubiri 9:11 ๐