Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi katika muendelezo wa Kampeni, mkoani Katavi tarehe 18 Oktoba, 2025.
#HaijapataKutokea#KaziNaUtu2025#DiraYaSamia#SamiaHadi2030
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe. Dkt. Samia @SuluhuSamia akiendelea na kampeni za CCM leo tarehe 18 Oktoba 2025 katika mji wa Mpanda, mkoani Katavi, amewahakikishia wananchi kuwa serikali itaendelea kusikiliza na kushughulikia changamoto zao.
Mhe. Dkt. Samia amekiri kupokea taarifa za kuwapo kwa wananchi 243 wanaodai fidia baada ya kupisha ujenzi wa Barabara ya Mpanda–Vikonge iliyokamilika mwaka 2021, pamoja na wananchi 830 wanaodai fidia kufuatia ujenzi wa Barabara ya Mpanda–Sitalike uliofanyika mwaka 2012–2013.
“Ninawaahidi kwamba nitaiagiza Wizara ya Ujenzi kufanya upekuzi wa madai haya, kuyathibitisha na kuhakikisha waliostahili kulipwa fidia wanapatiwa haki zao,” amesema Mhe. Dkt. Samia.
Aidha, ameeleza kuwa serikali imeendelea kuimarisha huduma za usafiri wa anga mkoani Katavi kwa kuboresha Uwanja wa Ndege wa Mpanda, ikiwemo ujenzi wa jengo jipya la abiria.
Uboreshaji huo umeimarisha kwa kiwango kikubwa huduma za usafiri wa anga kati ya Mpanda na Dar es Salaam, na kuchochea zaidi shughuli za kiuchumi na uwekezaji mkoani humo.
#HaijapataKutokea #DiraYaSamia #KaziNaUtu2025 #SamiaHadi2030
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia , akiendelea na kampeni za CCM leo tarehe 18 Oktoba 2025 katika mji wa Mpanda, mkoani Katavi, ameeleza dhamira ya serikali kuimarisha zaidi miundombinu ya usafiri na usafirishaji nchini.
Ameeleza kuwa serikali imekamilisha ujenzi wa Bandari ya Kalema katika mwambao wa Ziwa Tanganyika mradi mkubwa uliogharimu shilingi bilioni 47.9 ambao utarahisisha usafiri wa abiria na mizigo kati ya Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi na Zambia.
Aidha ameeleza kuwa ujenzi wa bandari hiyo unaenda sambamba na ujenzi wa meli nne za mizigo katika Ziwa Tanganyika, hatua itakayoongeza ufanisi wa usafirishaji wa majini na kukuza biashara za kimataifa.
Dkt Samia amebainisha pia kuwa kuelekea mwaka 2030 serikali inalenga kuhakikisha biashara kubwa kati ya Tanzania na DRC inapita kupitia Bandari ya Kalema. Ili kufanikisha azma hiyo, usanifu wa maboresho ya reli ya Kaliua–Mpanda yenye urefu wa kilomita 210 tayari umefanyika.
Maboresho hayo yatapunguza muda wa safari kutoka zaidi ya masaa 7 hadi kufikia masaa 2–3 pekee, hivyo kuongeza kasi ya usafirishaji na tija katika sekta ya uchumi.
#HaijapataKutokea #DiraYaSamia #KaziNaUtu2025 #SamiaHadi2030