ARISTODI FURIA (Mdau): Rushwa huwa inaanzia ngazi ya Familia, mara nyingi Vijana wanapokuwa wadogo, wanakua wakiangalia kile kinachofanywa na Wazazi, Walezi au wakubwa wao
Kama tunashindwa kudhibiti Rushwa kuanzia ngazi ya Familia ni ngumu kudhibiti nje ya Familia
#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Mwenda are you proficient in Kiswahili? At this incidence are you aware of what was going on?
Do you want to steer enmity between Tanzania and M23 supporters namely Rwanda?
In this video, Tanzanian soldiers, whom President Tshisekedi invited to DRC to help him fight M23, are surrounded and stranded at Goma airport without anyone to help rescue them. Now Tshisekedi’s rescuers are the ones that need to be rescued.
Six million Jews, one of them my grandfather, and millions of others were murdered by Nazis.
On Holocaust Remembrance Day, we honor the innocent lives taken and families destroyed. Never again means countering any and all antisemitism and hate taking root. The work is not over.
Nimemsikia Mh @TunduALissu @Lissu_2025 mitandaoni akisema kuwa Rais anawahonga viongozi makanisani mabilioni ya mapesa na anahoji hizo pesa zinatoka wapi. Pia amelinganisha tuhuma hiyo na hali ilivyokuwa kwa ma Raisi walio mtangulia. Amewataja. Mimi napenda kujua mambo 2
@SuluhuSamia peke yake?. Miaka ya 1980 Kanisa lilichaposha Kitabu Development and Religion in Tanzania. Nndani ya kitabu kile kuna nyaraka kutoka kwa Rais wa wakati ule (Julius Nyerere) ambaye @Lissu_2025 @TunduALissu anamfagilia. Nyaraka zile zinaahidi upendeleo kwa Kanisa.
Kwa hiyo Bwana Lema tukileta posa nyumbani kwako na tukakukuta uko shamba huondoke ee? Mbona Waafrika sisi kuahirisha kazi kwa ajili ya kumrai mgeni ni kawaida sana? Huko Ulaya naona kunaharibu akili za watu mdogo wangu. Usirudi huko
Baba Mwita, mimi si mwanasheria kama wewe, hivyo nitalieleza jambo hili kwa uelewa wangu wa kawaida kuhusu utaratibu uliotumika kumteua Rais Samia kuwa mgombea wa urais wa CCM. Naomba baada ya maelezo yangu unisaidie kutueleza ni wapi hasa sheria za chama zilivunjwa, kama unavyodai.
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Ibara ya 101(5)(b), Mkutano Mkuu wa Chama ndio chombo chenye mamlaka ya kuchagua jina moja la mwanachama atakayesimama kama mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa maoni yangu, hili ndilo sharti kuu linaloipa Mkutano Mkuu mamlaka ya kuteua mgombea wa chama.
Baada ya baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu, wakiwemo akina Ngw’asi Kenani, kupendekeza jina la Rais Samia kuwa mgombea wa chama, taratibu za kichama zilifuatwa. Hii ilijumuisha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kukutana na kupitisha azimio la kumtaka Rais Samia kuwa mgombea wa chama.
Ibara ya 103(b) ya Katiba ya CCM inaeleza kwamba, wakati wa uchaguzi, Halmashauri Kuu ina mamlaka ya kupendekeza majina yasiyozidi matatu ya wanachama wanaogombea nafasi ya urais. Kwa hiyo, pale Halmashauri Kuu ilipokaa na kupitisha jina la Rais Samia, ilikuwa inatekeleza wajibu wake kikanuni na kisheria.
Baada ya azimio la Halmashauri Kuu, hoja hiyo ilipelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama. Ukirejea tena Ibara ya 101(5)(b), Mkutano Mkuu ndio chombo chenye mamlaka ya kuchagua rasmi jina la mgombea wa urais. Kabla ya kupiga kura ya kuteua mgombea, Mkutano Mkuu ulipiga kura ya kusimamisha kanuni za kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM ili kuruhusu mchakato kuendelea.
Kwa hivyo, hayo ni maelezo yangu ya msingi kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Ningependa sana unieleze ni wapi hasa sheria ya chama ilivunjwa katika mchakato huu. Nitafurahi kujifunza kutoka kwako.
Msajili wa Vyama anaweza ihukumu CCM kwa kutumia Katiba yao tu. Tukumbuke vyama vina sheria zao ila pia zina tamaduni zao. Ila katika kutoa hukumu na adhabu, Msajili anaweza kuangalia sheria na kanuni za chama tu na sio utamaduni.
Ila nipo tayari kujifunza maana haya nilioandika ni kwa uelewa ambao mimi ninao. Huenda unauelewa zaidi ukatusaidia.
ALERT: Kuna hasira na Manung'uniko makubwa sana chamani. Ndani ya CCM watu wanalalamika kitendo cha Rais Samia kulazimisha apitishwe kuwa mgombea pekee. Za chini ya Carpet, kama huu mchakato hautarudiwa, basi viongozi wengi waandamizi wako tayari kuunga mkono Upinzani.
Ni vizuri Mheshimiwa kweli ukatubia
Lakini utakuwa umetutendea haki ikiwa katika kutubu kwako utatuambia @ChademaTz iliwateka watu wangapi na ni akina nani zama za uongozi wako na Slaa akiwa Katibu mkuu.
Mungu akuongoze katika mapito yako na akupe mwisho mwema
Nimesoma neno la leo katika Kalenda ya KKKT kwenye Biblia kutoka Kitabu cha Yakobo 3 : 13 - 18. Limenirutubisha. Natamani nanyi mrutubishwe nalo.
"Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aoneshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima. Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi, msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli. Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani. Maana popote palipo na wivu na ubinafsi, hapo pana fujo na kila aina ya uovu. Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki. Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika amani."