Unajua unaweza kupoteza thamani ya TSh MILIONI 1.8 kwa mwaka bila hata kutumia pesa zako? 😳🇹🇿
Mfano: Mshahara wako ni TSh 2,000,000 kwa mwezi = TSh MILIONI 24 kwa mwaka.
Januari 2026:
💵 $1 = TSh 2,470
💰 Milioni 24 = $9,717
Novemba 2026:
💵 $1 = TSh 2,654
💰 Milioni 24 = $9,043
Yaani mshahara wako wa mwaka, ukipimwa kwa dola, umepungua thamani kwa $674 (takriban TSh milioni 1.8)!
Hujapunguziwa mshahara, lakini uwezo wa pesa zako kununua vitu vinavyouzwa kwa USD umepungua.
Sasa badala ya kulalamika, tufanye nini? 👇
- 🇹🇿 Wekeza kwenye hisa za DSE
- 🏦 Angalia Treasury Bills na Bonds za Serikali
- 💵 Hifadhi sehemu ya akiba kwa USD
- 📈 Wekeza kwenye mifuko ya pamoja kama UTT AMIS
- 💼 Jenga chanzo kingine cha kipato
Usifanye kazi kwa ajili ya pesa tu. Hakikisha pesa zako pia zinafanya kazi kwa ajili yako.
Pamoja na kuwa Tanzania ina haki ya kuwa na mahusiano ya kirafiki na nchi yoyote duniani kwa kadri inavyowezekana, kwa maoni yangu safari ya kuelekea Moscow imefanyika katika wakati ambao si muafaka kisiasa na kidiplomasia.
Katika kipindi ambacho Marekani na Umoja wa Ulaya tayari wameonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa kisiasa nchini Tanzania, hususan baada ya matukio ya Oktoba 2025, malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu, na kuendelea kushikiliwa kwa viongozi wa upinzani, jambo la mwisho ambalo Tanzania ilihitaji ni kutuma ujumbe unaoweza kutafsiriwa kama kuhamisha mwelekeo wake wa kimkakati kutoka kwa washirika wake wakuu wa maendeleo kwenda Moscow.
Tatizo si kwenda Moscow.
Tatizo ni kwenda Moscow wakati Washington na Brussels wanaanza kuhoji mwelekeo wa kisiasa wa Tanzania.
Diplomasia sio suala la hisia; ni suala la muda, mazingira na maslahi ya taifa.
Ukweli ambao hatupaswi kuuficha ni kwamba kwa sasa Russia haiwezi kuchukua nafasi ya Marekani na Umoja wa Ulaya katika maendeleo ya Tanzania.
Takwimu zinaonyesha wazi:
Marekani imechangia zaidi ya dola bilioni 3 katika kipindi cha 2020–2025.
Umoja wa Ulaya umechangia takribani dola bilioni 3.2.
Russia imechangia karibu sifuri katika Official Development Assistance (ODA).
Haya si maoni. Hizi ni takwimu.
Wakati mwingine katika siasa tunajidanganya kwamba washirika wanaweza kubadilishwa kwa urahisi. Historia inaonyesha sivyo.
Marekani na Umoja wa Ulaya hawatoi fedha pekee.
Wamekuwa nguzo muhimu katika:
mapambano dhidi ya UKIMWI na malaria,
chanjo na mifumo ya afya,
elimu,
maji safi,
kilimo,
uwekezaji wa sekta binafsi,
teknolojia,
mafunzo ya wataalamu,
na upatikanaji wa masoko ya kimataifa.
Pengo litakalotokana na kupungua kwa ushirikiano huo haliwezi kuzibwa kwa picha za viongozi kukutana au mikataba michache ya kisiasa.
Mataifa hayajengwi kwa alama za kidiplomasia; yanajengwa kwa maslahi halisi ya wananchi.
Swali ambalo viongozi wanapaswa kujiuliza si kama tunaweza kuwa marafiki wa Russia.
Swali ni:
Je, Russia inaweza kuchukua mzigo wa afya, elimu, uwekezaji, biashara na maendeleo ambao Marekani na Umoja wa Ulaya wameubeba kwa miongo kadhaa?
Mpaka sasa, jibu la ukweli ni hapana.
Hatari kubwa zaidi si kupoteza misaada.
Hatari kubwa ni kupoteza imani.
Mataifa yanaweza kuishi bila misaada kwa muda fulani.
Lakini ni vigumu kuishi bila imani ya wawekezaji, masoko ya kimataifa, taasisi za kifedha na washirika wa maendeleo.
Fedha za dunia zina tabia moja:
Hukimbilia kwenye utulivu, uwazi wa kisiasa na taasisi zinazoaminika.
Ndiyo maana nchi yenye busara haiharibu madaraja kabla haijajenga mengine.
Na hata kama imeamua kujenga daraja jipya kuelekea Moscow, ni hatari kubomoa madaraja yaliyoiunganisha na Washington na Brussels kwa zaidi ya nusu karne.
Kwa sababu katika siasa za kimataifa, si kila rafiki mpya ana uwezo wa kuchukua nafasi ya rafiki wa zamani.
Na katika wakati ambao Tanzania inahitaji uwekezaji zaidi, ajira zaidi, teknolojia zaidi na masoko zaidi, taifa linapaswa kuwa makini sana lisije likachanganya uhuru wa kidiplomasia na kujitenga kidiplomasia.
Uzalendo wa kweli si kupiga picha na mataifa makubwa; uzalendo wa kweli ni kuhakikisha maamuzi ya leo hayaleti gharama ambazo wananchi wa kawaida watazilipa kesho.
MEDICINAL DRINK !
It gets rid of bad cells formed in the body or inhibits their growth!
Take it for 3 months, health is instantly restored. It's like a miracle.
You need one beetroot, two carrots and one apple..
Check Thread 👇
Mzee ni kweli trillion 97 hajakopa Samia peke yake..
Lakini tumekua na marais 6 tangu uhuru.
Marais wengine watano wamekopa trillion 65 kwa pamoja wastani wa trillion 13 kwa kila mmoja.
Rais Samia peke yake kwa kipindi cha miaka 4 amekopa zaidi ya trillion 31 fikiria itakuwaje hali hii ikiendelea?
Kuna FIKRA unaziona unashangaa sana. Kufikiri NO REFORMS NO ELECTION ni jambo linalohusu UCHAGUZI ni kutokujua maana halisi ya mabadiliko na kusudi tunalo litaka. Mifumo takribani yote ya utawala wa Nchi inaamuliwa na viongozi wanaotokana na UCHAGUZI. Kufanya mzaha na uchaguzi ni kufanya mzaha na biashara, ujasiriamali,afya ,elimu usalama na future ya wajukuu na vitukuu vya Nchi hii.
Utakuwa ni Ubinafsi Mkubwa kujali maslahi ya Urais,Ubunge na Udiwani ktk kuamua dhana hii kuliko mtazamo mpana wa afya na ustawi wa Nchi yetu. Ubunge na Urais sio ajira ni utumishi , hivyo misingi ktk kutafuta kazi hizi lazima uongozwe na ukweli na haki. Ukishiriki uchaguzi unashindwa unaibiwa kura usiposhiriki pia unashindwa , kwa hiyo matokeo yanafanana either way , kwa hiyo kubadilisha matokeo ni kuchukua hatua tofauti. Hivyo basi kila mtu anahusika ktk kufikiri FIKRA hii mpya ya No Reforms no Election . NI wajibu wa wananchi wote.
Nini kinakwenda kutokea baada ya Rais wa Marekani Trump kutia saini agizo la kuiondoa Marekani katika Shirika la Afya Duniani (WHO).
Inafahamika kwamba Vidonge vya ARV nchini Tanzania hutoleowa bure kabsa chini ya WHO Kupitia USA.
Kikawaida Gharama ya Dose mmoja ya ARV ya siku 30 sio chini ya $120+ nikama Tsh Laki 3 iliyo changamka.
Kama Marekani yenye watu takribani 299M Huchangia zaidi ya dollar Milioni $499 kwenye WHO,, Huku China yenye watu takribani Bilioni 1 Huchangia dollar Milioni $39 kwenye WHO..
Swali Je..? Misaada Africa Ikiwa ni pamoja na Tanzania Kupitia WHO itaendelea kutolewa bure...
Maana ukiachama na ARV kuna hizi chanjo zinazo tolewa bure kwa watoto, Ni Gharama sana....🤔🤔
UKIAMKA...!
1. Kunywa Glass 1-2 za Maji Asubuhi hii, Fanya hivyo Kwa Ajili ya Vital organs zako 🫀!
2. Pata Angalau dk 15-30 za Mazoezi ya Asubuhi, KEGEL ni MUHIMU zaidi Kwa Mwanaume!
3. Oga Maji Baridi (Zingatia mazingira na sehemu iliyopo).
4. "Kaa Mbalii" na Sukari Nyingi.
5. Kula Angalau yai 🥚 1 Leo Kwa Ajili ya Moyo na Ubongo 🧠.
6. Pata Muda wa Kuyafurahia Maisha Yako na mafanikio uliyopata, hata kama ni kidogo na Kwa kufanya Hivyo utailinda Afya yako ya Akili 🧠.
7. Hakikisha unapata Mboga za Majani Kwa Ajili ya Kuimarisha Kinga Yako ya Mwili.
8. Usikae sehemu moja kwa Masaa au muda mrefu, inuka jinyooshe, tembea, Utauokoa uti wako wa mgongo!
9. Pata Muda wa Kupumzika, Ni nzuri Kwa Afya yako ya Akili.
10. Like & Repost ili iwafikie na Kuwasaidia Wengine 🙏
Alhamdulillah! My first son has graduated high school. I’m the proudest father in the world. My dear son: may Allah continue to guide you on your path. With all my love - Mo 🎉🙏
1. Kunywa Glass 2 za Maji Asubuhi hii, Fanya hivyo Kwa Ajili ya Vital organs zako🫀🫁 .
2. "Kaa Mbalii" na Sukari Nyingi, na utakua umeuokoa Mwili wako.
3. Usinywe Soda wala Energy Drink Leo, Okoa Moyowako na Kongosho (Pancreas).
4. Kula Angalau yai 🥚 1 Leo Kwa Ajili ya Moyo na Ubongo 🧠.
5. Usiwe Mtu wa Huzuni au Kujinenea Mabaya, Fanya Hivyo ili Kuilinda Afya Yako ya Akili.
6. Hakikisha unapata Mboga za Majani Kwa Ajili ya Kuimarisha Kinga Yako ya Mwili.
7. Usikae sehemu moja Kwa Masaa Kadhaa Kwa Muda Mrefu, Kaa wima, simama jinyooshe, Fanya hivyo kukusaidia Mgongo wako.
8. Pata Muda wa Kupumzika, Ni nzuri Kwa Afya yako ya Akili.
9. Pata Muda wa Mazoezi, Angalau dk 30 TU, Utakuwa umeuweka mwili wako mbali na Magonjwa Nyemelezi Kwa kuwa na Kinga.
10. Like & Repost ili iwafikie na Kuwasaidia Wengine 🙏
"Usijinyime kujiwazia ndoto kubwa na kujiwekea malengo ya muda mrefu. Wajibu wako ni kuanzisha safari ya kuzielekea.Hata usipofanikisha katika uhai wako, utakuwa umejenga msingi kwa watoto na wajukuu wako kuzitimiza na kuziishi. Kabidhi kizazi chako kijiti sio lawama na majuto!"
Japhet Maganga Katibu mkuu wa chama cha walimu (CWT) aliteuliwa mkuu wa wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera. Ndugu Thadei Ole Mushi akasema Maganga atakataa huo uteuzi kwa sababu ana mshahara wa 7.8M kama Katibu mkuu wa CWT, lakini akienda kuwa DC atalipwa 3M.
"Kwa kuwa kila kinachozaliwa hufa, basi hatukuzaliwa ili tufe, tumezaliwa ili tutimize wito wetu katika kipindi tunachojaliwa kuishi duniani." ~Togolani Mavura.
"Kukikucha wanaamka wema na waovu, waadilifu na wahalifu, werevu na wapumbafu, matajiri na maskini. Ili maisha yaende, tunapaswa kuamka wote kwa pamoja ili maisha yaweze kuwa na maana na msawazo. Tungekuwa tunaamshwa kwa zamu ingekuwaje? Tuvumiliane tu maana tunahitajiana."