#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 502
Mhe. Lissu anaendelea
Anasema uamuzi huu wa kunikuta na hatia na kosa ambalo sikushtakiwa nalo, sikujitetea ni kosa la kutengeneza, effect yake ni kwamba unatoa kinga ya kisiasa kwa wale ambao walihusika mauaji amkubwa ya kisiasa, watatoka na kusema wauaji walishapataikana.
Serikali ya Samia imeua watu wengi zaidi ukiachilia historia ya vita vya majimaji, hawa mass murderers watashangilia sana na uamuzi huu kwasababu mmewapa sababu ya kusema aliyesababisha mauaji ya Oktoba 2025 amepatikana na hatia lakini hii haitafunika ukweli.
Serikali ya Mwalimu Nyerere iliuwa watu 37 mwaka 1977 na iliwajibika, Peter Kisumo alikuwa Mkuu wa Mkoa w Shinyanga alijiuzulu, na wengine akiwemo Mwinyi.
Leo watu 518 walioripotiwa kwa uchache hakuna aliyewajibishwa, uamuzi wenu hautaficha hiyo kashfa.
Kwenye sentences guidelines za Mahakama hii, inasema lazima adhabu ya faini itolewe isipokuwa kama ni grave offence, kosa nililoshtakiwa nalo sio grave.
Waheshimiwa Majaji hukumu mnayo, ambayo mmeagizwa muitoe, itoeni nawashukuruni sana.
Jaji Ndunguru anawasha mic anasema tumesikiliza hoja za pande zote na katika kutoa adhabu tumezingatia sababu kadha wa kadha.
Kwanza mshtakiwa umeomba dhamana ili ukate rufaa, tumeangalia hoja ya ugonjwa na kuwa wewe ni mkosaji wa kwanza, hoja ya adhabu ya faini au kifungo.
Kifungu cha 390 hakijatoa adhabu na ukisoma kanuni ya adhabu kifungu cha 35 kinahusika pale ambapo hakuna adhabu.
Adhabu ni kifungo kisichozidi miaka 5 au fani au vyote viwili na hakijaelekeza faini ni kiasi gani.
Tunajua kuwa pale ambapo fani na kifungo vinakuwa vinatolewa first option ni faini.
Tumesoma na maamuzi mbalimbali na mengine ambayo tumeshayasema mfano kuzuia uchaguzi ni kukiuka katiba, ukisoma Ibara ya 30(1) imeeleza kuwa hutakiwa kuingilia haki za mtu mwingine.
Mahakama inatoa adhabu kwa mshitakiwa kutumikia kifungo cha muda wa miaka 4 na una haki ya kukata rufaa.
Majaji wanatoka.
Naomba Repost yako.