#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 502
Mhe. Lissu anaendelea
Anasema uamuzi huu wa kunikuta na hatia na kosa ambalo sikushtakiwa nalo, sikujitetea ni kosa la kutengeneza, effect yake ni kwamba unatoa kinga ya kisiasa kwa wale ambao walihusika mauaji amkubwa ya kisiasa, watatoka na kusema wauaji walishapataikana.
Serikali ya Samia imeua watu wengi zaidi ukiachilia historia ya vita vya majimaji, hawa mass murderers watashangilia sana na uamuzi huu kwasababu mmewapa sababu ya kusema aliyesababisha mauaji ya Oktoba 2025 amepatikana na hatia lakini hii haitafunika ukweli.
Serikali ya Mwalimu Nyerere iliuwa watu 37 mwaka 1977 na iliwajibika, Peter Kisumo alikuwa Mkuu wa Mkoa w Shinyanga alijiuzulu, na wengine akiwemo Mwinyi.
Leo watu 518 walioripotiwa kwa uchache hakuna aliyewajibishwa, uamuzi wenu hautaficha hiyo kashfa.
Kwenye sentences guidelines za Mahakama hii, inasema lazima adhabu ya faini itolewe isipokuwa kama ni grave offence, kosa nililoshtakiwa nalo sio grave.
Waheshimiwa Majaji hukumu mnayo, ambayo mmeagizwa muitoe, itoeni nawashukuruni sana.
Jaji Ndunguru anawasha mic anasema tumesikiliza hoja za pande zote na katika kutoa adhabu tumezingatia sababu kadha wa kadha.
Kwanza mshtakiwa umeomba dhamana ili ukate rufaa, tumeangalia hoja ya ugonjwa na kuwa wewe ni mkosaji wa kwanza, hoja ya adhabu ya faini au kifungo.
Kifungu cha 390 hakijatoa adhabu na ukisoma kanuni ya adhabu kifungu cha 35 kinahusika pale ambapo hakuna adhabu.
Adhabu ni kifungo kisichozidi miaka 5 au fani au vyote viwili na hakijaelekeza faini ni kiasi gani.
Tunajua kuwa pale ambapo fani na kifungo vinakuwa vinatolewa first option ni faini.
Tumesoma na maamuzi mbalimbali na mengine ambayo tumeshayasema mfano kuzuia uchaguzi ni kukiuka katiba, ukisoma Ibara ya 30(1) imeeleza kuwa hutakiwa kuingilia haki za mtu mwingine.
Mahakama inatoa adhabu kwa mshitakiwa kutumikia kifungo cha muda wa miaka 4 na una haki ya kukata rufaa.
Majaji wanatoka.
Naomba Repost yako.
@HildaNewton21 Kwa maana hiyo atakabiliwa na kesi ya uchochezi lakini sio leo na uchochezi unadhaminika hivyo basi Kwa namna yoyote mzee wetu leo atapata wasaa wa kula cha jioni na familia yake
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 498
Jaji Ndunguru anasema katika kutafisiri hicho kifungu cha 319(1-2) cha CPA Mahakama ya Rufani ilielezea kwa marefu na mapana kwenye kesi ya DPP vs Zombe kuhusu kifungu hicho kuwa sio automatic.
Kwakuwa mshtakiwa hakushtakiwa na kosa dogo, Mahakama pia haiwezi kutumia kifungu hicho bila kumpa mshtakiwa haki ya kusikilizwa au kumpa notice.
Kwa mujibu wa ushahidi uliopo kuwa maneno hayo yalirushwa live ili kuuhabarisha umma na video hizo video hazikutolewa mahakamani na kwa vile hajakanusha kutamka maneno hayo na upande wa jamhuri umesema kuwa alilenga kuchochea umma na mashahidi wa upande wa utetezi nao hawajakataa kuhusu mshtakiwa kutamka maneno hayo.
Tumeridhika kwamba mshtakiwa kutamka maneno hayo hadharani mbele ya umma alilenga kuchochea umma ili kuvuruga uchaguzi wa 2025 kwa njia isiyo ya amani kutokana na maneno yake hivyo basi tukiongozwa na maamuzi mbalimbali na kwa muktadha wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu kosa lililotengenezwa na kifungu cha 390 ni kosa dogo la uhaini, kifungu cha 390 kinalengo la kuzuia crime katika hatua ya mwanzo before public harm.
Kwa tafsiri yetu tunasema kifungu hiki kina prevent nia na present danger.
Upande wa mashtaka wanapaswa kuthibitisha kuwa maneno ambayo mshtakiwa aliyatamka kufanya instigation yalikuwa communicated, pia mshtakiwa alilenga kuwa mtu au watu watende kosa.
Tunaelewa kwamba kifungu cha 390 kinatumika kwenye kosa lolote hakijataja kosa lolote pale, tunaamini kwamba kufanya kosa la uchochezi kunaweza kupelekea present danger, tunaamini ni minor offence na ni cognate offence kwa mujibu wa 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.
Ni kwa mtazamo wetu sasa kwamba ni common sense kwamba incitement ni component ya offence ya treason hivyo sio lazima mtu awe charged independently.
Kulingana na ushahidi uliotolewa mshtakiwa alichochea umma kuvuruga uchaguzi, kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi na kukinukisha vibaya sana.
Upande wa utetezi haujaonyesha ni kwa namna gani walipanga kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi, na mashahidi wa upande wa Jamhuri walieleza namna ambavyo walishawishika na maneno ya mshtakiwa mfano shahidi wa 4, 5,8 ,11, 13, 14 walishawishika na kujiunga na wale ambao walishawishika ili waweze kuvuruga uchaguzi.
Part 499 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Hoja ya pili, kwamba Lissu alitengeneza 'nia ya kuzuia uchaguzi kwa lengo ya kuitisha serikali' - imepigwa chini.
It goes without saying that this flickering case was dead on arrival.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 496
Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la!
Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa.
Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu.
Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha
Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live.
Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali.
Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.
Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini.
Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa.
Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini.
Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa.
Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.