"Sisi ni Tanzania" dhamira ya Watanzania kuwa pamoja kudumisha umoja, urafiki,utaifa, kuthamini utamaduni wetu na kujenga taifa lenye maendeleo na umoja
Ndoto, Mtaji na Mabadiliko: Jinsi Kilimo Kilivyogeuka Biashara Kubwa Kahama. Kila Punje Ina Hadithi: Jinsi Elizabeth Mzulingi anavyobadilisha Sekta ya Mpunga @MsigwaGerson @Mzulingicompany @ikulumawasliano@SuluhuSamia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Taifa mara baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa silaha za jadi Mkuki kutoka kwa Mzee Ndijina Ndilanza Ndilito, mwakilishi wa wazee wa Tanzania Bara pamoja na ngao kutoka kwa Bi. Ubwa Hamis Ally mwakilishi wa Wazee wa Zanzibar kama ishara ya kulinda na kuitetea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kuapishwa katika uwanja wa Gwaride, Chamwino Ikulu mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Dkt. Samia Suluhu Hassan akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, George Mcheche Masaju kuwa Rais wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo.