WAGOMBEA wetu karibu wote jijini Dar es Salaam, wameondolewa kwa madai ya kuandika DSM kwenye viapo vyao, badala ya Dar es Salaam. Makosa hayo hayakufanywa na wagombea, yamefanywa na Mahakama. Msimamizi wa Uchaguzi anawezaje kutambua kosa, kuliko Hakimu?
MPAKA sasa, wagombea wa Ubunge 57 kutoka Chadema na 48 wa ACT - Wazalendo, wameshaenguliwa katika mbio za ubunge. UMOJA ni MUHIMU. Viongozi wetu, CHONDE CHONDE, wekeni maslahi ya umma mbele.
NIMEPOKEA ujumbe kutoka kwa baadhi ya wazee wangu wa Ubungo, wakiniomba nirejee tena jimboni humo kuwakilisha. Naendelea kutafakari. Lakini sitawaangusha.
HATIME nimemaliza miaka yangu 5 ya ubunge kwa heshima kubwa. Asante Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema. Asanteni sana wananchi wa Ubungo kwa heshima mlionipa.
NIMEKUTANA na hili andishi. Siyo langu. Naomba lipuuzwe. Siwezi kuwa mkosefu wa ubinadamu. Nimelelewa na kukuzwa na wazazi na marafiki wanaoelewa na kuheshimu thamani ya utu na uongozi. Pole sana Mhe. Mbowe. Poleni sana wanademokrasia wote.
Lipumba naye anataka kuungana na au kushirikiana na anaosema, "wanataka kuiondoa CCM madarakani."
Anayetaka kuiondoa CCM madarakani, ndiye huyo huyo anayefanyia mikutano yake kwenye kumbi za wale anaowataka waondolewe madarakani.
KIPYENGA kimepulizwa cha uchaguzi wa urais ndani ya chama changu. Ni jambo jema. Lakini ni vema kila mtu akatendewa haki. Tusiruhusu umangimeza wala ukengeushi.
Zimebakia siku 104 kabla ya Tume ya Uchaguzi (NEC), kupuliza kipyenga cha uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020. Lakini Tume Huru ya Uchaguzi ambayo ni kilo cha wengi, bado haijapatikana. Na sasa, sioni tena dalili za kupatikana kwa kuwa tumehamia kwenye Corona.
Siyo wote wanaohama wamenunuliwa, ingawa ni kweli kuwa wapo baadhi ya waliohama wamenunuliwa.
Kuna wengine wamehama kutokana na kuwapo migogoro, chuki na ubaguzi katika maeneo waliyokuwapo.
Makao makuu ya nchi na chama kilichopo Ikulu, yako Dodoma. Lakini chuo cha chama hicho, kinajengwa Kibaha.
Hapa ndipo unapoweza kuthibitisha kuwa hakuna dhamira wala nia thabiti ya kuhamia Dodoma. Ni usanii.
Tofauti kati ya Rais John Magufuli na wengine kwenye suala la Demokrasia ni ndogo sana. Kwamba, yeye ananena na kutenda.
Lakini wengine hawaneni, bali wanatenda.