Entrepreneurs to Take Action
It’s the first Friday of 2026, a powerful reminder that the future belongs to those who dare to begin. There is nothing to lose and everything to gain—now is the time to move with clarity, courage, and purpose. #entrepreneurial#journey
Nadhani taifa lina bahati sana ya kuwa na viongozi wa chama kikuu cha upinzani wanaoongozwa na UCHU WA MABADILIKO badala ya UCHU WA MADARAKA.
Wakati wenzao wanawaza ubunge na ruzuku, @TunduALissu na @HecheJohn wanawaza mabadiliko ya kweli yanayogusa maslahi mapana ya umma.
Viongozi ambao kupitia dhati ya kauli zao na matendo yao, unaweza kuongea kwa confidence kwamba hawana price tag.
Kwa wale tuliopata bahati ya kusoma falsafa kama Metaphysics of Morals ya Kant, tunaweza kusema hawa ni viongozi ambao wameelewa vizuri kuwa taifa linaweza kuwa na sheria na miongozo inayopaswa kufuatwa, sheria na miongozo hiyo ikivunjwa na kusiginwa na wenye mamlaka, basi umma una MORAL DUTY ya kufanya CIVIL DISOBEDIENCE.
Inaonekana ni viongozi walioelewa kuwa unapofika hatua ya kutekeleza MORAL DUTY, matakwa ya umma yanakuwa paramount above matakwa binafsi.
Na katika hatua hii ambapo kiongozi anapaswa kuwaza kupanda mti na kuumwagilia kwa wivu mkubwa huku akijua wazi kuwa hatokaa chini ya kivuli cha mti huo.
Ni hatua inayomtaka kiongozi ajikane nafsi yake kwa kuyatoa sadaka mafanikio yote ya muda mfupi (immediate gratification) huku akiwa na imani kubwa kwamba anachokifanya kitaleta matokeo makubwa baadae.
Lakini la muhimu zaidi ni kwamba Tundu Lissu na John Heche wanatutia moyo kwa kutuonesha wazi kuwa wanafahamu vizuri chochoro za madaraka na namna ambavyo watawala wamekuwa wakiwatumia kama ngazi.
Inaonekana wamesoma vizuri ile Second Treatise of the Government ya John Locke na kutambua kuwa msingi wa mamlaka ya dola ni consent ya umma.
Wameelewa kuwa kadiri umma unavyoendelea kubend over kila mtawala anapofanya ushenzi wake ndivyo mtawala anavyoendelea kupata uhalali wa kufanya hivyo.
Kwa mantiki hiyo, njia pekee na muhimu kuzuia huu urudifishaji wa matumizi haramu ya mamlaka ni kuondoa consent.
Wameelewa vizuri pia kuwa hauwezi kuondoa consent kwa kuchubua matawi tu kwani kufanya hivyo ni sawa na kujaribu kumpaka nguruwe lipstick ili abadilike kuwa ng’ombe, unahitaji kung’oa mizizi.
Now, wakati wanalisimamia hili kutakuwa na milio mingi sana.
Kama mnakumbuka wakati tunakua kulikuwa na wale wadudu wanaitwa funza.
Vilikuwa ni vidudu hatari ambavyo kama haupo makini vinaweza kushambulia vidole na visigino mpaka mguu ukaenda upande.
Namna pekee ya kudeal navyo ilikuwa kuchukua pini au mwiba na kuviondoa kwenye kidole.
Hata hivyo vilikuwa na sifa moja nzuri sana, vikikuingia vilikuwa vinawasha halafu ukivisugua unasikia raha hatari, matokeo yake unajikuta wewe ndio unakatunza kuanzia kwakuwa kakiroboto mpaka limekuwa likubwa.
Wakati mama anakukamata kukatoa tulikuwa tunalia kweli kwa sababu ni lazima akufanyie operation ndogo. Hata hivyo ulitolewa hivyo hivyo na kilio chako na mwishowe ulibaki huru.
Wazazi waliozembea kwa kuogopa mtoto atalia, ndio wale ambao watoto wao miguu ilienda upande.
So, kaka wakubwa @HecheJohn na @TunduALissu , tunafurahi kuwa mnaendelea kumtoa huyu funza bila kutishwa na kilio cha mtoto.
Itakuwa rahisi? Jawabu ni hapana, ingekuwa rahisi kila mtu angefanya.
Tundu ni intelligent, natural orator na ni natural Mwalimu. He didn’t die baada ya kupigwa risasi 16. Huyu jamaa doesn’t give up! Hizi ni Powerful combination.
Hili WAZO lake #NoReformsNoElection ni changa lakini wananchi wanaanza kulielewa na kulikariri.
A man to watch,