Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari wamekabidhiwa mifuko yenye msimbo (QR Code) katika kilele cha Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, msimbo wenye taarifa kuhusu programu mbalimbali zinazotolewa na SUA pamoja na taratibu na vigezo vya kujiunga na Chuo.
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na @costechTANZANIA wamekuja na Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Wafugaji Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
COSTECH wamefadhili Mradi huo kwa shilingi milioni 400.
Ushiriki wa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mafiga iliyochini ya SUA imekuwa kivutio kwa viongozi mbalimbali wanaofika katika Banda la SUA kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki 2026.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ametembelea Banda la SUA katika Maonesho ya Nanenane 2026 Kanda ya Mashariki na kupongeza mchango wa Chuo katika kuendeleza kilimo kupitia tafiti, ubunifu na teknolojia, 07 Agosti, 2026.
SUA imezindua programu mpya za Shahada ya Ualimu zenye msisitizo wa mafunzo kwa vitendo, hatua inayolenga kuwaandaa wahitimu wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira na kuwawezesha kujiajiri.
https://t.co/x3oqBUIt3s