Former secretary for mobilization and pioneers CCM youth league-UDSM|Muuza mchele wa Mbeya| Marketing Manager |@udsmalumni |Editor|Writter|Translator|B.A.K|IKS|
Mbishi hafundishiki wala haambiliki. Ukijaribu kumfafanulia hasikilizi japo anasikia kwasababu anamajibu yake tayari anayoamini kuwa ni sahihi. Kinachoweza kubadilisha msimamo wa mbishi ni kile anachokiamini kikimgeuka. Vinginevyo utakuwa unasaga mawe kwa meno.
-Mollel
"Kuwa makini na watu utakaokutana nao wenye simulizi za kuonewa na msururu wa watu. Si kawaida kwa maisha kumuadhibu mtu bila sababu za msingi. Wahanga wengine wanatumikia malipo ya ubaya wao. Ukiwakumbatia unaweza kuzama nao." ~Togolani Mavura.
"Maisha ya binadamu hayakamiliki bila lile shaka moja, jambo moja au tatizo moja linalomuumiza kichwa na ambalo hana majawabu yake ya moja kwa moja au ujasiri wa kulikabili kwa wakati huo na kuamua kuliweka katika mabano ama kuliahirisha. Kila binadamu ana lake. Hauko peke yako!"
"Sote ama ni wahanga au wahanga watarajiwa wa magonjwa ya afya ya akili. Maisha yetu yamezungukwa na sababu nyingi za kutukatisha tamaa na kutupa msongo wa mawazo. Daima jitahidi kutopoteza mambo mawili, kwanza, tumaini, na pili, watu sahihi katika mduara wako (support system)."
"Furaha yako wakati mwingine inategemea na kutokujua taarifa au ukweli fulani. Kwepa kutafuta taarifa na kuujua ukweli ambao ama haukuhusu au moyo wako hauko tayari kuupokea na kuhimili. Huwezi kuumizwa na usilolijua." ~Togolani Mavura.
Maisha ni kama mfululizo wa kutatua matatizo.
Unapokuwa unamalizana na moja, jingine tayari linafanya warm up😃
Tofauti si kukosa matatizo, bali kujifunza kuyakabili kwa hekima, uvumilivu na moyo wa kusonga mbele.🤛🏼
Sawa kabisa mnaosema Marekani wasitunyanyase! Sawa! Na sisi tusidai kutonyanyaswa bali tudai kutotekwa, kutotekwa na kutouwawa bila sababu. Hivi hilo nalo ni gumu, wajameni?! Punguzeni povu midomoni, ongezeni fikra vichwani. Huo ni mkwamo mlikokwama na dawa yake si kasi ya midomo.
2026 jifunze kusema;
1. Sina
2. Sitaki
3. Siwezi
4. Sipendi
5. Imeisha
6. Haitoshi
7. Sipo/Siendi
8. Haiwezekani
9. Lipo nje ya uwezo wangu
10. Mpaka nimalize hili jambo