๐งต ARiS NI KAMPUNI GANI? HISTORIA YAKE, HUDUMA ZAKE NA NAFASI YAKE TANZANIA
ARiS Risk & Insurance Solutions Limited ni kampuni inayojihusisha na udalali wa bima na usimamizi wa hatari za kifedha na kibiashara. Ilianza shughuli zake mwaka 1998 ikiwa ni wakala mdogo wa bima jijini Dar es Salaam https://t.co/jzmsNCwnmA
Kampuni hii ilianzishwa na Sanjay Suchak. Mwaka 2002, Alexander Forbes, kampuni ya huduma za kifedha iliyokuwa na makao yake Afrika Kusini ilinunua hisa nyingi za ARiS ili kusaidia upanuzi wa biashara yake na huduma kwa kampuni za kimataifa
Mwaka 2013, kundi la Marekani lilinunua Alexander Forbes. Baadaye uongozi wa kampuni nchini Tanzania uliamua kuinunua na kuendelea na shughuli zake chini ya jina ARiS. Mwaka 2021, jina lake lilibadilishwa rasmi kutoka African Risk & Insurance Services Limited kwenda ARiS Risk & Insurance Solutions Limited
ARiS hufanya kazi gani hasa?
โข Husaidia wateja kupata bima inayolingana na mahitaji yao
โข Huchambua hatari zinazoweza kuathiri biashara na mali
โข Husaidia katika taratibu za kuwasilisha na kufuatilia madai ya bima
โข Hutoa huduma za bima ya afya na mafunzo kwa wateja
Huduma zake zingine ni bima za majengo, miradi ya ujenzi, mitambo, ajali, moto na anga. Kwa biashara zinazohitaji kulipa gharama za bima kwa awamu, kampuni pia inaeleza kutoa mipango ya ufadhili wa malipo ya bima kupitia ushirikiano na benki
ARiS ina shughuli nchini Tanzania, Kenya na Uganda pamoja na uwepo wa kampuni nchini Uingereza. Makao yake Tanzania yapo ARiS House, Plot No. 152, Haile Selassie Road, Oysterbay, Dar es Salaam
Kampuni hiyo ina cheti cha ISO 9001:2015 na utambuzi wa International Professional Partner Firm kutoka Chartered Insurance Institute ya Uingereza
Nani ni Charles Zanny, na ana nafasi gani ARiS?
Kwa mujibu wa wasifu rasmi wa kampuni, @CharlesZanny ni Group Technical Director wa ARiS Risk & Insurance Solutions
Ana shahada ya Takwimu (Statistics) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na uzoefu wa zaidi ya miaka 18 katika sekta ya bima, akiwa amewahi kufanya kazi katika upande wa kampuni za bima (insurers) na udalali wa bima (brokers)
Katika nafasi yake ya uongozi majukumu yake ni kusimamia masuala ya kiufundi ya bima, kusaidia kuhakikisha ubora wa huduma na kutoa mwongozo wa kitaalamu katika shughuli za bima
Wasifu wake pia unaeleza uzoefu wa miaka 20 na ushiriki katika mafunzo mbalimbali ya kiufundi ndani na nje ya nchi
Kwa nini kampuni kama ARiS ni muhimu?
Katika uchumi, bima husaidia watu na taasisi kupunguza athari za hasara zinazoweza kusababishwa na ajali, moto, uharibifu wa mali na majanga mengine. Dalali wa bima humsaidia mteja kuchagua kinga inayofaa na kufuatilia mchakato wa madai kwa mujibu wa masharti ya mkataba
#ElimuYaFedha #Insurance
Soma bila stress, daka Boom mapema!
Fungua Scholar Account ya CRDB ufurahie Boom, Boom Advance, zawadi na Bima ya Maisha hadi TSh 2M.
๐ Tembelea tawi la CRDB!
#LetsKonekt#CRDBBank#Tunakusikiliza
Leo ni Siku Mpya. Vaa Matumaini, Beba Ujasiri, Heshimu Watu, Tafuta Fursa Na Usisahau Kuwa Kila Mwanzo Mdogo Unaweza Kuwa Mwanzo Wa Hadithi Kubwa. ๐ฏ๐ฅ
Udugu wangu, samba zile za kamba zimekaa kiume sana.
Kwa sasa trend ipo humu
Samba za kuchana, specifically kwa wanawake. Hata si bei kubwa ya kukushinda udugu wangu. 60k tu badala ya 65,000.
Mc MSAE.
๐ค MC wa shughuli zone- Harusi, Sendoff, Kitchen Party n.k
๐ Bookings: +255754211024
โก Let's make your event unforgettable ๐ฅ๐ฅ
๐ https://t.co/mHyBG08jx9...
Happy birthday to me ๐๐.
Today, I celebrate myself, my growth, my strength, and the person I am becoming. ๐๐ฝโจ I thank God for the gift of life, the lessons learned, the battles Iโve overcome, and the blessings yet to come.