#Neno..LAKINI NAKUMBUKA JAMBO HILI MOJA.
Maombolezo 3:15-22.
Katika mapito haya ya kila siku, ni vyema kuwa na jambo moja unalokumbuka na linakupa matumaini. Mwandishi anasema anakumbuka kwamba Mungu ni wa huruma. Wewe unakumbuka jambo lipi? Tukutane Galilaya! #nurunaevahmwalili
#Neno.....ONJA UONE BWANA NI MWEMA. Zaburi 34:1-8..Hakika Bwana ni mwema, ni wa huruma, yeye hututia nuru na kufanya nyuso zetu zing'ae, ukimwita anaitika na kushughulika.. Onja uone Kwamba yeye ni mwema na ni vyema kumwamini. Tukutane Galilaya! #NuruNaEvahMwalili
#Neno...VAA SILAHA ZA MUNGU. Waefeso 6:10-13..Huwezi ukaushinda ulimwengu kwa kuishi maisha ya kawaida, lazima uvalie silaha za Mungu. Ulimwengu umejawa na nguvu za giza ambazo hupigani kikawaida, hapa unapambana kwa silaha za Mungu. Zivae!! Tukutane Galilaya! #NuruNaEvahMwalili
#Neno....BWANA YU KARIBU NAWE. Zaburi 145:18,19..
Unapomwita Mungu kwa uaminifu hatakubwaga atakuja! Atakupa matamanio ya moyo wako. Nakuombea katika Jina la Yesu, katika hali hii, Mungu akujibu na akupe matamanio ya moyo wako. Tukutane Galilaya! #NuruNaEvahMwalili
#Neno....OMBA BILA SHAKA MOYONI. Marko 11:20-24
...Yesu alipouambia mtini usizae kamwe, maneno yake hayakua na shaka na yalitimia. Nasi pia tukitamkia hali zetu, tukiomba bila shaka tutaona majibu ya ajabu. Believe and you will have it! Tukutane Galilaya! #NuruNaEvahMwalili
#Neno...WAKATI UNAPOWADIA, FULL TIME! Luka 1:24-25, 57-58....Wakati wako ukiwadia, Mungu atafanya watu wasikie, waone na washukuru Kwa Kile kimefanyika, maana kitakuwa cha kupendeza. Tulia, Mungu atarembesha ushuhuda wako kabisa! Tukutane Galilaya! #NuruNaEvahMwalili