Ukiachana na huo utani wa “Millennials” na “Gen Z”, kuna eneo moja nakubaliana na Gen Z 100%. Ni ukweli kwamba Millennials tumelifikisha Taifa letu matopeni. Hatuwezi kuiwajibisha Serikali hata inapokosea.
Millennials ndiyo uti wa mgongo wa utumishi wa umma kwa sasa; sisi ndiyo injini ya nchi. Lakini injini hii ikikubali kufanya kazi kwenye matope bila kuhoji kwanini barabara haitengenezwi, nchi inabaki palepale.
Kizazi chetu kwa sehemu kubwa ndiyo watumishi wa umma, hata tusipoongezwa mshahara na marupurupu kwa miaka 10, tunaona ni sawa tu. Tunaona ni kawaida na ndiyo kitu ambacho kama watumishi, tunastahili.
Kizazi cha wasomi wengi kimegeuka kuwa kizazi cha “ndiyo mzee.” Millennials wamekuwa watulizaji (stabilizers) wa mfumo hata kama ni mbovu. Gen Z ni wavurugaji (disruptors) wa mfumo ili ukae sawa.
Hofu ya kupoteza mshahara inayoweza kusababisha watoto wakose ada/familia ikose chakula imewafanya Millennials kuwa waoga (risk-averse). Hii imetengeneza kizazi kinachopendelea diplomasia ya unyenyekevu.
Kwa sababu ya familia, tumekuwa kizazi cha viumbe wabinafsi sana. Hatujui kudai haki zetu, na tumezalisha machawa na wapambe wengi. Kizazi chetu kimeasisi mfumo wa kusifu na kuabudu (sycophancy).
Tazama, hata machawa wakubwa na wazito (pro-max) wanaosifu na kuabudu Serikali hii ni kizazi cha Millennials. Wasanii wakubwa wa muziki wa kizazi kipya ambao ni wafuasi wa watawala ni Millennials.
Gen Z wengi bado hawajazama kwenye majukumu mazito ya kifamilia, hivyo wana ujasiri wa kupaza sauti bila kuwaza “kesho nitalishaje watoto.” Hawalazimiki kuwa machawa ili waweze kuendesha maisha yao.
Gen Z wanakuja na utamaduni tofauti: wako ‘connected’ na wanatumia teknolojia ipasavyo. Wanaona wenzao duniani wanavyowajibisha serikali zao, hawaamini katika uvumilivu wa miaka 10 bila ongezeko la maslahi.
Hawahitaji mikutano ya siri; wanatumia simu kuanzisha mijadala, kuumbua ubadhirifu, na kuungana kwa kasi ya ajabu. Hii imepunguza nguvu ya machawa ambao walizoea kutawala simulizi za mtandaoni. Safi sana.
Wakati Millennials walifundishwa kuwa na shukrani hata kwa kidogo (ile dhana ya bora mkono uende kinywani), Gen Z wanauliza: “Kwanini iwe kidogo wakati rasilimali zipo?” Hapa ndipo sasa nawakubali madogo hawa.
Hawa Gen Z wana uwezo wa kuungana kama kizazi bila kujali itikadi za vyama, kitu ambacho Millennials wengi wameshindwa kwa sababu ya kuweka mbele maslahi ya ajira zao. Wamekataa mambo ya “Status Quo.”
Gen Z wamevunja mwiko. Millennials wamefungwa na nidhamu ya uoga au hofu ya kupoteza walichonacho, sasa wanatazamana na kizazi kinachoongozwa na kanuni moja kuu: “Haki haiombwi, haki inadaiwa.”
Labda shinikizo hili la Gen Z litatumika kama kioo cha kuwafanya Millennials wajione walivyojipoteza. Binafsi, wananikosha sana. Gen Z wanaupiga mwingi. Mimi nawatia moyo, wasiogope. Kaka zao tupo pamoja nao.
Gen Z, take a bow, fellas.
Mimi langu ni hivi : kama unaskiliza wale wasanii wanaliolipwa kushangilia damu za watu na kama bado wewe ni shabiki wa zile timu maarufu hapa Venezuela,ripoti hii ikufurahishe tu.
Wewe sio mtu
WaTanzania itufike tuache kujilaza kisiasa kwa mambo ya “sishiriki/sina chama”. Upinzani ndio njia pekee yakuleta ahueni kwahio ukiweza wezesha chama pinzani uwezavyo. Napendekeza CHADEMA✌🏾
Media, dini, asasi, taasisi za serikali na binafsi, vyama mchongo n.k vyote vimepokwa na ccm-serikali.
Chama/taasisi pekee ccm-dola inahujumu kwa hali na mali ni CHADEMA kwasababu unyonge wa chadema ndio ustawi wa dhulma za ccm.
Katika maswaibu tunayopitia anayetutetea tunaomizwa tunamuona na anayetetea anayetuumiza tunamuona. Wao walishachagua upande na wanaufanyia kazi haswa ila wewe unasusua ukilalama ukitarajia muujiza ya haki au “wajionee aibu”.