Siku hizi watu hawaamini kwenye kujituma na kutafuta kwao imekuwa Kila anayefanikiwa ni fremason.tufanye kazi Kwa juhudi huku tukiendelea kuomba na kuwa na subra nawe ipo siku utafanikiwa na itakusaidia kufuta dhana kuwa Kila mwenye mafanikio ni freemason.
Marafiki wanaweza wakawa chanzo Cha wewe kushuka kimaendeleo, pia marafiki wanaweza wakawa chanzo Cha wewe kufanikiwa kutokana na support mbalimbali. Hivyo inategemea wewe umeamua kuwa na marafiki wa aina ipi ?
Jaribu kuwafundisha watoto wako namna Bora yakuishi na watu, usiwajaze chuki juu ya mtu fulani ila wafundishe kuishi Kwa upendo na Kila mtu. Kumbuka hautaishi nao milele