Kutazama televisheni & kutumia vifaa vingine vya kielektroniki kwa muda mrefu kunaweza kuwa na athari mbaya kwa uwezo wa akili wa watoto. Matumizi ya muda mrefu ya vifaa hivi yanaweza kusababisha changamoto katika maeneo ya ukuaji wa ubongo, kama vile uwezo wa lugha & kumbukumbu.
Watu wenye mkazo (stressed-out people) mara kwa mara wanakuwa na ubongo mdogo. Viwango vikubwa vya homoni cortisol (homoni ya mkazo) hupunguza ujazo wa ubongo na uwezo wa ubongo kufanya kazi.
Baada ya kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza unaweza kuhisi mwili umechangamka kwa sababu mapigo ya moyo huongezeka kitu kinachomaanisha ongezeko la mzunguko mkubwa wa damu na oksijeni kwenye ubongo.