🚨🔵🔴 Raphinha has signed new contract at Barcelona until June 2030!
All approved, closed with his camp and lawyers. New deal done and sealed.
Official announcement and ceremony can take place this week; on Friday, if all goes to plan with documents.
🚨 Pep Guardiola: “Enjoy the moment but… the reality is: who is top of the league? We are not. Goal difference, who is better? They are”.
“Step by step. But, of course, we got hope to still extend our chances to fight until the end...”.
Wizara ya Uchukuzi imetoa tahadhari kwa Wananchi wanaotarajia kusafiri kutumia usafiri wa reli ambazo ni Reli ya SGR na MGR ambapo imesema kuwa kufuatia kuwepo kwa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zimesababisha uharibifu wa miundombinu ya reli katika njia zake katika maeneo mbalimbali.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo hii leo Disemba 28, 2025 imeeleza kuwa mvua zilizonyesha zimeanza kusababisha uharibifu katika madaraja ya reli ya zamani (MGR), hususa ni katika eneo la Kidete, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, pamoja na eneo la Gulwe, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma na kwa upande wa miundombunu ya SGR kumeshuhudiwa hitilafu za umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na umeme wa reli ya kisasa (SGR), hali iliyoathiri uendeshaji wa huduma za reli katika baadhi ya maeneo.
Kutokana na hali hiyo, Wizara imewataka wananchi “kuepuka kusafiri katika maeneo yaliyoathiriwa pale inapowezekana, kufuatilia taarifa rasmi kutoka Serikalini na vyombo husika, pamoja na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na vyombo vya ulinzi na usalama na mamlaka za usafiri na pia kuepuka kusogea karibu na miundombinu ya reli na barabara zilizoathiriwa ili kujikinga na ajali.”
#MillardAyoUPDATES
"Takwimu, zinaonesha kuwa wabunge 223 kati ya wabunge 393 sawa na asilimia 56.7 ni wabunge wapya kabisa. Aidha, asilimia 45 ya wabunge wote ni wanawake." - Rais Samia Suluhu akihutubia na kufungua Bungea la 13
"Nisisitize kuwa zama zile za taasisi kuendelea kuchuma serikalini bila yenyewe kurudisha faida zimepitwa na wakati na hazipo tena. Kila shirika lijitahidi kuzalisha ili litoe. Tunataka mashirika yawajibike, yajibebe na yaibeba Serikali pia." - Rais Samia Suluhu akipokea Gawio na Michango kutoka kwa Taasisi na Mashirika ya Umma
Mbunge wa Mwera Zahor Mohamed Haji amesema Tanzania na kenya ni nchi zinazotegemeana ambapo ametaka wakenya na watanzania wasameheane kwa niaba ya Bunge na Taifa na amesisitiza urafiki na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili uendelee kuimarika zaidi.
Mbunge Haji ameyasema hayo wakati akichangia hoja Bungeni Leo Mei 28, 2025, katika mawasilisho ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje ambapo amesema amesoma na kuona namna ambavyo Rais wa Kenya William Ruto akiomba radhi kwa watanzania ambapo amesema watanzania tumepokea na kutaka pale ambapo bunge na taifa limejikwaa basi wakenya waweze kusamehe kwani mataifa haya mawili bado yanahitajiana.
“Naomba nitumia nafasii hii kupongeza kwa haraka haraka nimesoma na kuona Rafiki yetu na kaka yetu Rais William Ruto akituomba radhi wananchi sisi lakini naomba sana na sisi tunapokea kwa sababu hakuna mwanadamu aliye mkamilifu sasa inawezekana na sisi tunalo tatizo lakini sisi ndio binadamu tusameheane ili maisha yasonge kwa hiyo ningeomba sana kwamba pale ambapo na sisi kama Taifa kama Bunge tumejikwaa ndio maisha lakini ukweli kwamba tunahitajiana kama mataifa rafiki nikimaanisha tunahitajiana kama Tanzania na Kenya lakini pia tunahitajiana kama mataifa yaliyo pamoja.” Amesema Mbunge wa Mwera, Zahor Mohamed Haji.
#MillardAyoUPDATES
Mbunge wa Viti Maalum na mmoja kati ya wabunge 19 wa CHADEMA, Salome Makamba amesema hawezi kuhamasisha kupinga uchaguzi nchini kwani ni kutokuwa na shukrani baada ya mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda leo Jumatano January 08, 2025 amekutana na kuongea na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa ambapo Waziri Mbarawa ameridhia ombi la Makonda la kuboresha reli ya Kaskazini (Tanga-Arusha) katika kuboresha huduma za Utalii Mkoani Arusha kwa kupunguza foleni.
Katika mazungumzo yao, Makonda mbali ya kusema kuwa sekta ya uchukuzi ni muhimu kwenye kukuza na kuimarisha Utalii Mkoani Arusha, amesema kuboreshwa kwa reli hiyo pamoja na kujengwa kwa bandari kavu Mkoani Arusha kutaondoa wingi wa malori ya mizigo barabarani pamoja na kusaidia katika matunzo ya barabara katika kuzisaidia kudumu muda mrefu zaidi.
Mbarawa amesema Arusha ni Mkoa muhimu kwa Utalii na uchukuzi ukiwa wa tatu kwa miruko ya ndege nchini Tanzania, akiahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mkoa katika kufanikisha utekelezaji wa ilani ya CCM ikiwemo kusimamia maboresho ya uwanja wa ndege wa Arusha, unaotarajiwa kuanza kufungwa taa hivi karibuni ambapo Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari imeshatenga Tsh. bilioni 11 za kufunga taa kwenye uwanja huo wa ndege Arusha.
#MillardAyoUPDATES
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni za GSM, Benson Mahenya amesema Serikali imemsahau mtoto wa kiume na badala yake kuweka mkazo zaidi kwa mtoto wa kike jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya Taifa.
🚨 Arne Slot: “Federico Chiesa is feeling sick, unfortunately for him because he had some minutes against Southampton”.
“He was sick in the last two days and today as well so we couldn’t bring him to the game”.
Rais wa Marekani, Joe Biden ametoa msamaha usio na masharti kwa mtoto wake, Hunter Biden, ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi za uhalifu, akidai kuwa hakutendewa haki.
Hunter alikiri mashtaka ya kukwepa kulipa ushuru, na kupatikana na hatia ya utumiaji haramu wa dawa za kulevya na kumiliki bunduki mwezi Juni, ambapo alikuwa akingoja kujua ni hukumu gani atapokea katika kila moja ya kesi hizo.
Kwa mara nyingine tena, Tanzania imeibuka Mshindi kwa kujinyakulia tuzo nne katika Tuzo za Utalii zinazotolewa na World Travel Awards ya Nchini Marekani.
Tuzo hizo ni pamoja na Eneo Bora la Utalii Afrika (Tanzania), Bodi Bora ya Utalii Afrika (TTB), Hifadhi Bora ya Afrika (Serengeti), na Kivutio Bora cha Utalii Afrika (Mlima Kilimanjaro).
Tuzo hizi zimetolewa katika hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia leo October 19, 2024, Mjini Mombasa, Kenya, na kupokelewa na Viongozi wa Wizara ya Utalii, TTB, na TANAPA, wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii Nkoba Mabula, Mjumbe wa Bodi ya TANAPA CPA Hadija Mohamed, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii, Ephraim Mafuru, Mkuu wa Kanda ya Kaskazini, Betrita Lyimo na Mkuu wa Hifadhi ya Serengeti, Stephano Msumi.
Ushindi huu unaifanya Serengeti kuendelea kuwa Hifadhi Bora ya Afrika kwa miaka sita mfululizo (2019, 2020, 2021, 2022, 2023, na 2024), pia Bodi ya Utalii Tanzania imekuwa Bora Afrika kwa miaka mitatu mfululizo (2022, 2023, na 2024) ambapo Nkoba amesema ushindi umechagizwa na sera za Rais Dkt. Samia kuvutia Watalii na kukuza utalii kwa ujumla kupitia Royal Tour.
Tuzo za World Travel zilianzishwa mwaka 1993 kwa lengo la kutambua, kutunza, na kusherehekea ubora katika sekta zote muhimu, ikiwemo usafiri, utalii, na ukarimu, leo hii World Travel Awards inatambulika Kimataifa kama alama ya ubora katika tasnia mbalimbali.
#MillardAyoUPDATES
🔴⚪️ Arteta: "Kai Havertz is fantastic. He's smart and also powerful. How he occupies the spaces, the way he glides everything together...".
"Now when he's around the box and you have the feeling he's going to score a goal!".
“Jumapili tukutane uwanja wa Mkapa tukamkaange Al Ahli Tropoli na ukikaanga ni mambo mawili, kiive au kiungue kabisa sasa lolote litakalokuja muhimu ni kumsambaratisha Al Ahli ili twende makundi”
“Ukitoa Ayoub Lakred, wengine wote ni wazima na wako tayari kuwapeleka hatua ya makundi na sisi kama Viongozi wenu tumeshafanya maandalizi yote na nyie kama Mashabiki mje uwanjani kuishangilia timu yetu ikienda makundi, iwe mvua iwe jua Mnyama anakwenda makundi”
“Wanasimba nyie ndio mmeipeleka timu mara tano hatua ya makundi na sasa kila Mwanasimba atambue ana kazi ya kuipeleka hatua ya makundi mara ya sita, sio kazi ya Mo Dewji, sio kazi ya Mangungu ni kazi ya kila Mwanasimba, muhimu ni Jumapili kuja uwanjani” —— Msemaji wa Club ya Simba Ahmed Ally akiongea Dar es salaam leo
#MillardAyoUPDATES
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesisitiza umuhimu wa utawala bora na Viongozi wanaotokana na Wananchi kuwa msingi mkuu wa Dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 ili kufanikisha utekelezaji sahihi wa mipango na mikakati inayowekwa na Wananchi na Serikali ya Tanzania.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA- Zanzibar, Salim Mwalimu amesema hayo leo August 21,2024 wakati wa kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania Jijini Dar es salaam kilichoitishwa na Ofisi ya Rais Tume ya Mipango kwa ajili ya Wanasiasa kutoa maoni yao kuhusu Dira mpya ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050.
Mwalimu amesema yote yanayoandaliwa sasa yanategemea zaidi suala la utawala bora na Viongozi sahihi katika utekelezaji wake na hivyo kuhimiza Nchu kuwa na Viongozi wanaotokana na maamuzi ya Wananchi.
"Nani tunaenda kumkabidhi dira hii na kuitekeleza, lazima tupate Watu wenye wivu na jambo hili lazima tupate Watu wenye uelewa na utayari wa kukubali kusimamia jambo hiki, lazima tuwe na utawala bora unaotokana na maamuzi ya Watu”
Mwalimu ametaka pia kueleka miaka 25 ijayo msingi mmoja wapo wa utaifa uwe kuheshimiana miongoni mwa Watu huku pia tukiweka msisitizo kwenye uvumbuzi na ubunifu pamoja na kukuza kichocheo cha siasa safi kama mambo yatakayoifanya Nchi kwenda sawa na Nchi nyingine Duniani kote.
#MillardAyoUPDATES
🔴⚪️ Xavi Simons to RB Leipzig will be a loan move, no buy clause included as plan has always been clear.
PSG only considered a loan for Xavi this summer, as reported since April.
The potential sale of Xavi Simons would only take place in summer 2025.
Rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais mwaka 2024.
Chanzo cha kujiuzulu kinatajwa kuwa ni kutokana na wafuasi wake wa chama cha Democratic kupoteza imani juu ya utendaji wake pamoja na uwezo wake wa kiakili.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema ili watoto wa Kitanzania waweze kushindana kwenye soko la ajira la kidunia ni muhimu wafundishwe elimu yenye lugha za kimataifa.