VIDEO:
Mfanyabiashara na mwalimu kutoka mkoani Arusha, Sabina John (40), ameiomba serikali kutoa tamko kuhusu mali zake, ikiwemo magari manne aina ya Scania, ambayo amedai kuwa yameharibiwa vibaya kiasi cha kushindwa kutazamika.
Akizungumza na waandishi wa habari, Sabina amesema: "Kwa miaka yote hii ambayo gari ziko hapa, zimechinjwa kiasi hiki, na sina chochote ninachoweza kufanya. Ndo gari nambiwa niichukue."
Sabina ameeleza kuwa alikwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, kuomba msaada, ambapo magari hayo yalikuwa bado katika hali nzuri wakati huo. Hata hivyo, amedai kuwa baada ya amri ya magari hayo kupelekwa polisi, suala hilo limekuwa likipigwa danadana kati ya mahakama na polisi.
"Mkuu wa mkoa alitoa amri magari yaende polisi, lakini huyu anasema ni kazi ya mahakama, mwingine polisi. Kwa kweli nimechoka," ameongeza.
Sabina pia amesema kuwa ameshinda kesi kadhaa mahakamani lakini bado hajapata msaada wowote, huku akidai kwamba wadaiwa wake, ambao ni mpenzi wake wa zamani Julius na fundi aliyeachiwa magari hayo, hawana uwezo wa kumlipa fidia.
Katika moja ya gereji ambalo gari moja liko, Jambo TV imekuta gari hilo limeharibiwa vibaya, likiwa halina viungo muhimu kama matairi, injini, chesesi, na vifaa vingine vya msingi. Inadaiwa gari hilo lililetwa gereji likiwa bado linatembea, lakini hali yake sasa inasikitisha.
Mfanyabiashara huyo amesema yupo njia panda, akishindwa kuelewa nani atawajibika kwa hasara hiyo kubwa ambayo ameipata. Ameiomba serikali kuingilia kati ili kuhakikisha haki inatendeka na kupata fidia ya mali zake.
Hi @elonmusk, I need your attention pls
The acc @ComradeKawaida has been spreading hate against ๐น๐ฟ youth and inciting fear, urging the Tanzanian gov to close @x
This person is anti-free speech, promotes censorship, and misrepresents @X. Pls permanently block this acc. Thank you