Haki inapopimwa kwa jina la mtu anayeshtakiwa badala ya ukweli wa jambo lenyewe, haki huwa imepoteza maana.
Muachieni Tundu Lissu, si kwa sababu ni Tundu Lissu, bali kwa sababu Tanzania haiwezi kujenga amani ya kudumu juu ya msingi wa dhuluma.
Serikali haionyeshi nguvu kwa kumshikilia mkosoaji wake, inaonyesha nguvu kwa kuwa na ujasiri wa kuiruhusu haki itawale.
@MariaSTsehai wanajua umuhimu wa kesi hii kitaifa na kimataifa.WATATUMIKA KAMA REFERENCE YA HUKUMU KATIKA "AINA HII PEKEE YA KESI YA UHAINI uliofanywa na mtu mmoja tu, mgombea urais, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini, kwa kuhutubia PRESS waandishi wa habari, kuelezea msimamo wa CDM",
Tanzania ya Mwalimu Nyerere iliyotoa watu na mali kupigania uhuru wa Afrika.
Tanzania iliyotoa ardhi yake kuweka vituo vya mafunzo wa wapigania Uhuru kwenye bara la Afrika.
Tanzania iliyosifika kwa kupigania haki za binadamu.
Leo Tanzania ndio inatajwa kwa kutoa mercenary kwenda kuvuruga chaguzi kwenye Nchi za watu wengine!!!
What a shame!!
“Mbali na mauaji ya Vita vya Maji Maji chini ya utawala wa Kijerumani, mauaji yaliyotokea 29 Oktoba 2025 ndiyo makubwa zaidi katika historia ya nchi yetu. Hakuna awamu yoyote ya utawala kuanzia Waingereza waliodumu miaka 42, hadi marais wa awali kama Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, na Magufuli iliyowahi kushuhudia maafa ya kiwango hiki. Katika wiki moja pekee ya utawala wa sasa, angalau watu 518 wamepoteza maisha kwa kuuwawa na risasi za moto, jambo linalofanya tukio hili kuwa mauaji mabaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu.” - Tundu A.M Lissu, 12 August 2026
HII SIYO YA KUKOSA: Kesi ya TUNDU LISSU ni KESHO, 10/8/2026 na kuendelea. FIKENI KWA WINGI MAHAKAMANI kumpa KAMPANI Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, Chama Kikuu cha Upinzani Nchini Tanzania.
TEGEMEO LA WANANCHI. TANZANIA YA KESHO. Tanzania ya VIJANA.
Nchi hii karibu kila kiongozi ana motorcade! Huu sasa siyo tena utaratibu wa kawaida, ni uhuni wa hali ya juu katika uvunjaji wa sheria za nchi. Barabara za wananchi zinageuzwa njia za misafara binafsi, sheria zinawekwa pembeni, na mamlaka zinaonekana kushangilia.
Kama kila mtu anahitaji motorcade ili ajione muhimu, basi tunahitaji kuuliza, nani anailinda sheria dhidi ya wanaoivunja kwa jina la mamlaka?
#TANZANIA: TUNATAKA LISSU ATOKE GEREZANI, WATEKAJI, WAUWAJI WAWAJIBISHWE, WAJE WASULUHISHI HURU - HECHE
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche ameendelea kusisitiza kuwa kwa sasa hawawezi kushiriki kwenye mjadala wowote unaohusu mapatano au maridhiano bila Mwenyekiti wao wa Taifa, Tundu Lissu kuachiwa huru na kwamba kama kutakuwa na mazungumzo ya aina yoyote yanayohusu masuala hayo Lissu ndiye atakayekuwa kinara wa kuongoza chama hicho.
Aidha, Heche amesema wanataka wasuluhishi huru toka nje ya nchi ambao hawatakuwa na upande katika usuluhishi huo.
Zaidi: https://t.co/3saDF3yo23
Tanganyika AMKA 🔥👊🏽
Vijana usiku huu wako bize wanasambaza vipeperushi kuamsha watanganyiks tupambane!
Kila mtu apambane anavyoweza! Hakuna kuwapa muda wa kupumua hawa wauaji mafedhuli!
Hadi tupate Haki 💪🏽🔥
#TutaelewanaTu#JusticeForMO29
Nchimbi on record kagoma kujiuzulu - kawa preempt wasije wakaleta barua kama ya Ndugai bure 👊🏽😁
Kaa humuhumu @nchimbie pambana hadi mwisho hakuna kujiuzulu wala kujitoa 💥
Bi Msumi presha inapanda ama inashuka? Na watanganyika ndani ya CCM amkeni! Mnaendeshwaje na akili za Kizimkazi?
#TutaelewanaTu
Magaidi tuendelee kupeleka moto, mwaga Moto ALAFU comment muamala hapo chini.
CHANGIA BARAZA KUU LA UMMA.
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba: 22606600140
Jina: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Breastfeeding doesn't happen because a mother tries harder. It succeeds because families, employers, healthcare workers and communities make room for it. Breastfeeding is everyone's business. #WBW2026#AfyaYaWatotoWetu
Maarifa ya lishe kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo ni nyenzo muhimu kwa madaktari na wauguzi wanaowahudumia wagonjwa.
Madaktari na wauguzi wanaalikwa katika mafunzo maalumu ya lishe kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo.
Bwana Kitila Mkumbo!!
Taifa halifi kwanza kwa kukosa rasilimali, hufa pale watu wake wanapoanza kuogopa kutumia akili zao.
Kuna tofauti kubwa kati ya elimu na akili. Elimu ni zao la akili. Kabla ya kuwepo shule, vitabu na vyuo, kulikuwepo akili iliyouliza maswali, ikafanya uchunguzi na kuumba maarifa. Ndiyo maana jamii inayoheshimu elimu lakini inaadhibu fikra huru, hujenga wasomi lakini si wenye hekima.
Hatari kubwa ya wakati wetu si ukosefu wa elimu, bali ni pale kufikiri kwa kina kunapoonekana kuwa kosa, na ujinga unapoonekana kuwa salama. Siku ambayo watu wataogopa kusema ukweli wanaouona kwa sababu ya hofu, siku hiyo taifa litakuwa limeanza kupoteza uhuru wake wa ndani, hata kama bendera yake bado inapepea.
Na taifa haliishi peke yake. Heshima ya taifa mbele ya mataifa mengine ni mtaji usioonekana, lakini wenye thamani kubwa kuliko mali nyingi zinazoonekana. Ndiyo maana mataifa huwekeza katika diplomasia, hujenga uaminifu na hulinda taswira yao kwa uangalifu mkubwa. Ni rahisi kubomoa sifa ya taifa kwa kauli moja, lakini inaweza kuchukua miaka mingi kuijenga upya.
Mahusiano ya kimataifa si mali ya serikali pekee, ni urithi wa kila raia. Ndani yake kuna biashara, uwekezaji, elimu, utalii, ajira na ndoto za mamilioni ya watu. Kauli inayodhoofisha hadhi ya taifa haimuumizi mtawala pekee, humuumiza mfanyabiashara, mwanafunzi, mkulima, mwekezaji na kijana anayesubiri nafasi yake duniani.
Pia , tunapaswa kukumbuka kuwa sehemu kubwa ya fedha za kigeni zinazoingia nchini hutegemea imani ya dunia kwa Tanzania. Wageni wengi wanaotembelea nchi yetu wanatoka Marekani, Ulaya na mataifa mengine yanayotuangalia kupitia taswira tunayoiunda kila siku kwa maneno na matendo yetu.
Hekima ya kweli si kusema kila unachoweza kusema, ni kujua athari ya kila neno kabla halijatamkwa. Kwa sababu mwisho wa yote, maneno hujenga historia, na historia ndiyo huamua hatima ya vizazi.
Bwana Kitila , tafadhali usikatishe watu tamaa kusomesha watoto.
Nimemsikia kijana wa ccm anasema mimi kumwambia Mzee wetu Wasira astaafu kwasababu ya umri mkubwa ni matusi .
Pia huyo kijana amesema yeye ni kijana kutoka Mkoa wa Mara.
Je Mzee Warioba ni Mzee kutoka Mkoa gani?
Je anajua kwamba miongoni mwa mawaziri kwenye serikali hii aliwahi kumvuta , kumkaba na kudhalilisha vibaya mzee Warioba kwasababu mzee wetu alitaka katiba mpya na bora?
Huyo kijana kwa kudhalilisha Mzee wetu chama chao kimempa vyeo vingi kama zawadi.
1. Ukuu wa wilaya
2.Ukuu wa Mkoa
3. Uenezi wa ccm
4. Uwaziri na ubunge wa kupewa.
Je kwa huyu kijana anaejiita wa Mkoa wa Mara,
kumwambia mzee kustafu kwasababu huwa anasinzia kwenye vikao na mambo ya msingi yanampita ni matusi kuliko mtu anaepiga Wazee?
Je huyu kijana amewahi kukemea tukio la Mzee Warioba kudhalilishwa?
Je amewahi kukemea watu kutekwa akiwemo katibu Mwenezi wa ccm bwana Polepole?
Je ni vibaya kumwambia mtu astafu na kuachia kizazi kipya ni vibaya kuliko mauaji ya Oktoba 29? Huyu kijana amewahi kusema nini kuhusu mauaji hayo au hajui wapo Wazee pia waliuwawa kwenye yale matukio?
VIDEO:
Wazee wa ambao ni wanachama na wafuasi Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Simiyu wameeleza kuridhishwa na kiongozi wao Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara John Heche huku wakimtaka aendelee kukipigania chama hicho ili kuleta mabadiliko.
Akizungumza kwa niaba ya wazee hao Mjumbe wa Baraza la Wazee CHADEMA(BAZECHA) Mkoa wa Simiyu, Kenedy Onyangi kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA mkoa huo uliohudhuriwa na Heche @HecheJohn amesema pamoja na kusikia shutma mbalimbali ambazo zinaelekezwa kwa kiongozi huyo bado wana imani naye na wapo tayari kuchangia chama.
"Tunayaona yote wanayoyaongea kuhusu kwamba umekula hela sijui umefanya nini yote tunayaona sio kwamba hatuyaoni lakini sisi tunaimani na wewe lakini ukipata nafasi ya kumuona Mandela wa Tanzania, Tundu Lissu mwambie sisi wazee wa Simiyu tupo na yeye," amesema
Mbali na kutoa pongezi hizo, wazee hao pia walimpatia Heche zawadi ya fedha na mbuzi ikiwa ni ishara ya kumtia moyo katika mapambano ya uongozi ndani ya chama hicho.