Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umesema wananchi wameitikia kwa wingi wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu katika matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
USIKOSE KUTAZAMA MAKALA MAALUM YA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI KUPITIA LUNINGA YA ITV
Kila Jumanne na Ijumaa Saa 12:30 Jioni na Marudio ni kila Jumanne na Alhamis Saa 7:30 Mchana.
Jionee namna ambavyo fursa lukuki zilizoibuliwa vijijini baada ya kupelekewa huduma ya umeme
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Nishati Tanzania kutoka Benki ya Dunia, Dkt. Rhonda Antoine ameihakikishia ushirikiano REA katika utekelezaji wa miradi ya Nishati kote nchini kwa ulinzi wa mazingira na ustawi wa Taifa kwa ujumla.
USIKOSE KUTAZAMA MAKALA MAALUM YA YA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI KUPITIA LUNINGA YA CHANNEL 10
Ni leo hii (Ijumaa) Saa 2:00 Usiku na Marudio ni Saa 7:30 Mchana (Jumamosi).
Jionee namna ambavyo Tanzania imepiga hatua katika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
REA inatekeleza mradi wa Shilingi Bilioni 17.39 wa kusambaza umeme katika vitongoji 120 utakaonufaisha Kaya 3,960 Mkoani Singida.
Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu amebainisha hayo Mkoani Singida wakati wa kumtambulisha Mkandarasi anayetekeleza mradi
USIKOSE KUTAZAMA MAKALA MAALUM CHANNEL 10
Ni leo hii (Jumatano) Saa 2:00 Usiku na Marudio ni Saa 7:30 Mchana (Alhamis)
Jionee namna ambavyo fursa lukuki zilizoibuliwa vijijini baada ya kupelekewa huduma ya umeme hasa katika maeneo ambayo ni ngumu kufikiwa na gridi ya taifa.
Baada ya kufikisha umeme migodini; Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imefanikisha kushuka kwa gharama za uendeshaji wa migodi.
Hivi sasa shughuli za uendeshaji wa migodi zimerahisishwa ikilinganishwa na hapo awali.
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) kwa kutoa ruzuku ya asilimia 50 kwenye majiko ya gesi ya kilo sita kote nchini.
Okoa Mazingira na linda afya yako kwa kutumia Nishati Safi ya Kupikia.
Shuhudia namna ambavyo Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inavyoboresha maisha ya wananchi wake maeneo ya vijijini kupitia nishati ya umeme
Wakulima wafurahia maisha, umeme umetengeneza fursa...
Yajayo yanafurahisha...
REA kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu inafanya utafiti wa tatu wa hali ya upatikanaji na matumizi ya nishati katika mikoa yote ya Tanzania Bara ili kubaini hali ya usambazaji na matumizi ya nishati kwa lengo la kuboresha mipango yake katika sekta ya nishati kwa ujumla
Utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizinduliwa rasmi na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei mwaka huu.
Mkakati unaelekeza 'Ifikapo 2034; 80% ya Watanzania wawe wanatumia Nishati Safi ya Kupikia.'
#REAinatekeleza
Wananchi Wilayani Karatu Mkoani Arusha wamejitokeza kwa wingi kujipatia majiko ya gesi ya kilo sita (LPG) yanayotolewa na Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Lake Gas kwa bei ya ruzuku ya 50%. REA inatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034