HISTORIA YA SAED KUBENEA — MWANDISHI WA HABARI ALIYEPIGWA RISASI, AKANUSURIKA KIFO KISHA AKAWA MBUNGE KUPITIA CHADEMA
Katika historia ya Tanzania ya kisasa majina machache yameacha alama kubwa katika tasnia ya habari na siasa miongoni mwao ni Saed Kubenea
Kwa zaidi ya miongo miwili kubenea amejulikana kama mmoja wa waandishi wa habari za uchunguzi waliokuwa tayari kuandika habari ngumu na nyeti bila kujali presha au hatari zinazoweza kujitokeza. Ujasiri wake ulimjengea heshima kubwa miongoni mwa wanahabari, wanaharakati na wananchi wengi waliokuwa wakifuatilia masuala ya uwajibikaji na utawala bora
Wengi wanamkumbuka kama mmoja wa waandishi waliokuwa mstari wa mbele kuamini kuwa kalamu inaweza kuwa silaha ya kuleta mabadiliko katika jamii. Kupitia kazi zake alijenga sifa ya mtu asiyeogopa kuhoji mamlaka, kufuatilia ukweli na kusimamia kile alichoamini kuwa maslahi ya umma
Umaarufu wake uliongezeka kupitia gazeti la MwanaHALISI ambalo kwa kipindi chake lilikuwa miongoni mwa magazeti yenye ushawishi mkubwa zaidi nchini Tanzania
Gazeti hilo lilisifika kwa uchunguzi wake wa kina kuhusu siasa, ufisadi, matumizi ya madaraka na masuala mbalimbali ya kitaifa. Kwa wasomaji wengi, MwanaHALISI halikuwa gazeti la kawaida bali jukwaa la kupata taarifa ambazo mara nyingi hazikupatikana kirahisi sehemu nyingine
Kutokana na kazi hizo, Kubenea alijijengea taswira ya mwandishi jasiri, mwenye uthubutu na asiyeogopa kusimamia anachoamini hasa ukweli, Haki na uwajibikaji
Mwaka 2008, Tanzania ilishtushwa na habari za kushambuliwa kwa risasi kwa Saed Kubenea na watu wasiojulikana alijeruhiwa vibaya lakini alinusurika na kifo
Kwa wengi, tukio hilo lilikuwa ishara ya gharama ambazo wakati mwingine waandishi wa habari hulazimika kulipa wanaposhughulikia masuala nyeti ya umma
Kunusurika kwake kuliongeza zaidi taswira yake kama mtu aliyepitia changamoto kubwa lakini akaendelea kusimama na kuendelea na kazi na misimamo yake
Baada ya miaka mingi ya kutumia kalamu kuhoji mamlaka Kubenea aliamua kuingia moja kwa moja kwenye siasa kupitia CHADEMA
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, alichaguliwa kuwa Mbunge wa Ubungo.
Kwa wafuasi wake, ushindi huo ulikuwa matokeo ya imani kubwa ambayo wananchi walikuwa wameijenga kwake kutokana na kazi zake za muda mrefu katika uandishi wa habari
Akiwa bungeni aliendelea kujulikana kwa hoja zake, uchambuzi wake na msimamo wake kuhusu demokrasia, uwajibikaji wa viongozi na uhuru wa habari
Leo hii, Saed Kubenea anatajwa miongoni mwa waandishi wa habari waliofanikiwa kuhamia kwenye siasa huku wakibaki kuwa sehemu muhimu ya mjadala wa kitaifa
Kwa wengi, simulizi yake ni ya mtu aliyepambana na vikwazo vingi, akafungiwa gazeti, akanusurika risasi, akaendelea kusimama na hatimaye akapata nafasi ya kuwawakilisha wananchi bungeni
Jina lake limebaki kuwa sehemu ya historia ya vyombo vya habari na siasa za Tanzania na kwa wengi ni mfano wa uthubutu, uvumilivu na msimamo katika kusimamia kile unachoamini
Siku ya leo nmepigiwa simu asubuhi kuwa Mama yangu kafariki,
Nilikuwa siamini mpaka pale ambapo nimeambiwa nipande gari kwaajili ya kurudi nyumbani kumzika Mama yangu..
Eeh Mwenyezi Mungu naomba unipe uvumilivu,kila nikijikaza nashindwa kujizuia..😭😭😭😭
KATORO – GEITA. Viwanja vya SATELİTE. CHADEMA tumekusanya #ToneTone kiasi cha TZS 2,071,000. MSAJILI USITUTISHE. Huwezi kamwe kutupangia namna gani tushughulike na MaCCM. RUZUKU ya kiwaki HATUTAKI. Angusha TONE lako hapo kupitia 0744446969; Jina - CHADEMA HQ. #PeoplesPower. 👊🏾
Speed haina maana kama umepotea njia .
kuongeza mwendo wakati wakati umepotea ni kupotea zaidi.
1. Kuendelea kuteka watu, kuua watu, na kutishia maisha ya watu ni kupotea njia zaidi.
2. Matishio dhidi ya taasisi ambazo zipo kisheria na zinazotakiwa kufanya wajibu wake, ni kupotea zaidi
3.kuendelea kumshikilia Lissu na kutaka kukamata viongozi wenzake ni kuongeza tatizo ni kupotea zaidi.
4.kujaribu kufunika mabaya ambayo yalifanywa na dola bila kutambua na kujirekebisha ni kupotea zaidi.
Rudi nyuma soma Ramani shika njia sahihi.
KATORO – GEITA. Mamma Mia! 🙆🏾
Watu ni wengi kama mchanga.
Kilio cha SHOSTI na wenzake tunakielewa.
Kwa huu mtiti, lazima watoe mlio.
Kazi ni moja. Kuyapelekea moto MaCCM.
Hii inaitwa ‘IGA UFE AU JARIBU UFILISIKE’
#PeoplesPower#StrongerTogether ✌🏾
Safi kabisa hatuna muda wa kujadili ushenzi wa Takataka inaitwa "SISTA NYAHOZA".
KuFungia chadema, kuifuta Chadema ni kucheza na UTULIVU wa nchi uliopo.
Sote tunajua nchi haina AMANI-hiki ni kisiwa cha UVUMILIVU, afu wewe ulete ushinzi wako.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎