Leo ni kumbukizi ya kuzaliwa ya gwiji wetu wa zamani Jersyon Tegete. Tegete alisajiliwa na Yanga akitokea katika kikosi cha Stars, tofauti na wachezaji wengine ambao husajiliwa kutokea katika vilabu vya ligi kuu.
Leo tumecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania katika viwanja vya Gymkhana, Dar Es Salaam na kupata ushindi wa Magoli 2-1
1. Clement Mzize โฝ๏ธ
2. Cheikh Toure โฝ๏ธ
#TimuYaWananchi#DaimaMbeleNyumaMwiko
Rais wa Young Africans Sports Club Eng. Hersi Said na Rais wa Barcelona, Joan Laporte wamekubaliana kuwa ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐.. ๐๐คฉ
#TimuYaWananchi#DaimaMbeleNyumaMwiko
Leo tumefanya semina kwa vijana ikihusisha mada mbalimbali muhimu, ikiwemo usalama na ulinzi wa watoto (Safeguarding & Child Protection), uzoefu wa safari za kimataifa pamoja na maarifa na misingi ya ufundishaji wa soka kwa vijana.
Kupitia makubaliano yetu na Dulla Sports Centre ya Zanzibar katika kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana, moja ya maeneo muhimu tuliyokubaliana ni kubadilishana uzoefu, maarifa na utaalamu kwa lengo la kuwajengea vijana mazingira bora ya kukuza vipaji vyao ndani na nje ya uwanja.
Tunaamini uwekezaji katika maarifa, malezi na maendeleo ya vijana ni sehemu muhimu ya kujenga kizazi cha wachezaji wenye uwezo, nidhamu na uelewa mpana wa soka.
#TimuYaWananchi
#DaimaMbeleNyumaMwiko
Idara ya Wanachama na Masoko leo imetembelea Ofisi za Vodacom Tanzania kwa ajili ya zoezi la usajili wa wanachama sambamba na kuimarisha Tawi la Yanga Vodacom.
Zoezi hili ni sehemu ya mkakati wa Klabu wa kuwafikia Wananchi katika taasisi, makampuni na maeneo mbalimbali ya kazi ili kuwawezesha kujiunga na familia ya Yanga na kuendelea kuwa sehemu ya safari ya Klabu popote walipo.
Tunawashukuru uongozi pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa mapokezi mazuri na ushirikiano wao katika kufanikisha zoezi hili.
#TimuYaWananchi
#DaimaMbeleNyumaMwiko
Mdhamini na Mfadhili wa Klabu yetu, Ghalib Said Mohamed, Rais wa Klabu yetu, Eng. Hersi Said, pamoja na viongozi na wadau mbalimbali wa Klabu, wameungana na familia, viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika mazishi ya Mama yetu mpendwa Fatma Karume, yaliyofanyika leo Zanzibar.
Tunatoa pole za dhati kwa familia, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu. Tunawaombea nguvu, faraja na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
Pumzika kwa Amani, Mama yetu Fatma Karume. ๐๏ธ
#TimuYaWananchi
#DaimaMbeleNyumaMwiko