Ninaipongeza Klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo. Mafanikio haya ni ushahidi wa juhudi, nidhamu na kujituma kwa wachezaji, benchi la ufundi, uongozi pamoja na mashabiki.
Aidha, ninazipongeza klabu zote zilizoshiriki Ligi Kuu msimu huu kwa ushindani mzuri uliofanya mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania kuendelea kukua, kuvutia na kuongeza hamasa kwa mashabiki pamoja na wadau wa mchezo huu.
Kati ya ulipo leo na unapotaka kufika kesho ni kujiwekea malengo makubwa, na kuwa tayari kujituma kuyafikia bila kukata tamaa.
Maisha si mashindano ya kuwa na zaidi. Ni safari ya kuwa bora zaidi.