#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 9
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa hoja ni je yanayozungumzwa kwenye hivyo vifungu yanazungumzia confession peke yake?
S. 263(3) of CPA inasema you may say anything that relevant to charge against you and will be written and may be used in evidence at your trial.
Sasa kwenye kifungu hiki kuna admission yoyote?
Kesi ya Dodoli Kapufi mahakama ya kabidhi hairuhusiwi kufanya maamuzi ya maswala ya kisheria 266(6)
Anasoma hapa hiki kifungu....
Anaanza kuelezea hapa kwamba Hakimu alipaswa kuandika maelezo ya Lissu kama yalivyo na sheria imeandika kabisa kuwa inampasa na kumlazimu kuandika maelezo hayo ila mahakama ya kabidhi ilizuia maelezo hayo kuandikwa.
Kwahiyo Waheshimiwa Majaji haya maneno niliotakiwa kusema yalikuwa ushahidi wangu unaopaswa kutumika kwenye mahakama hii.
Wakili Katuga anasema bila kusomewa hayo maelezo Lissu kaathirika vip?Lissu anajibu kuwa maelezo yangu ambayo ni ushahidi hayakuchukuliwa hio ilikuwa kinyume na sheria na kinyume na haki.
Anaendelea hapa anasema twende kwenye mashahidi wangu mtakumbuka mashahidi aliowataja walikuwa Rais, Waziri Mkuu, Makamu Rais.
Ukisema Shahidi yangu Yesu basi atakuuliza nipe anuani yake hiyo ndio gist ya 264 ya CPA.๐
Sio kusema sitaki kuandika.
Presidential affairs Act imesemwa jana na imerudiwa leo hii mahakama hii imeambiwa kuwa hawa wana kinga za kupewa summons za mahakama kuja kitoa ushahidi mahakamani.
Mmesomewa kifungu cha 10 jana kilitajwa cha 9 leo wamerekebisha.
Anasoma kifungu cha 10 cha Presidential Affairs Act. .....
Kwahiyo Rais hawezi pelekewa Summons ya Mahakama kwa maneno hayo niliyosema.
Sheria inasema unatakiwa umuone Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu wa Rais au Katibu Mkuu baada ya kuombwa na mahakama wa kuomba msaada wa kumserve Rais huyo Katibu wa Rais au Katibu Mkuu kiongozi watatoa utaratibu.
Sasa haya ndio yanayotoa zuio? Au wanasoma sheria kwa namna gani?
Walisema kifungu hiki kinawahusu Waziri Mkuu na Makamu wa Rais sasa katika kifungu hiki wapi wamesemwa hawa aliowataja Mrema leo?
Sasa Mheshimiwa Jaji kuna kitu hakisemwi naomba nikiseme mimi.
Sect. 9 ya sheria hiyo ya Sasa. Presidential Affairs Act.
Kinasema immunity of Arrest au kumlazimisha aje mahakamani.
Sasa mimi nimeomba Rais akamatwe? Hakuna nilipoomba.
Kifungu cha 9 kinasema kama yupo mtu atahitaji Rais awe shahidi Mahakama itamnotify Rais kuhusu nia ya mtu huyo.
The court is required to notified the President. Ana kinga ya kutokushitakiwa tu na sio kinga ya kuja kutoa ushahidi.
Mahakama inapaswa kumpelekea Katibu Mkuu kiongozi au katibu wa Rais na hao wanapaswa kuisaidia mahakama kumfikishia Rais sio kwa mujibu wa sheria kuwa jambo hilo limekatazwa. Sio kweli.
Hiyo hoja ni ya bure. ๐๐๐
Naomba sasa nijielekeze kwenda kusoma haya maamuzi waliyonipa ili tuweze kurudi kesho nije kujibu kuhusu hayo.
Jaji anasema Katuga unasemaje.
Katuga anajibu kuwa mimi sina shida. Akasomeee tukutane kesho.
Majaji wanateta hapa kidogo.
Wanaandika wakiwa wameinama chini. Tusubiri maelekezo. Kuna dalili tutakutana kesho hapa.
Jaji anasema kutokana hakuna pingamizi lolote tunaahirisha shauri hili saa tatu asubuhi kesho tutakuja kukusikiliza umalizie
Shauri limeahirishwa hadi kesho asubuhi saa tatu.
Naomba repost kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 9
Anaendelea Mhe. Lissu
Kwenye ukurasa wa 61 wa hii niliyopewa leo kuna taarifa kwamba kunashauri yamefunguliwa mahakama kuu kuhusu kuficha mashahidi na mkiangalia.
Pia font ya nyaraka niliyoletewa awali na font niliyoletewa leo. Ombi langu hatuwezi kuendelea leo naomba tuahirishe mnipe muda. Usiku wa leo utanitosha kesho turudi nije kuwaonyesha uchafu uliofanyika hapa.
Documents zimekuwa falsefied naomba tuahirishe turudi kesho ili nije kuendelea.
Kwa kifupi ni kwamba wahuni walitengeneza nyaraka mbili tofauti wakampelekea nyaraka tofauti.
Anasimama Katuga hapa, anaomba azungumzie hiyo criminality.
Jaji anasema ukitaka ku respond kwenye hilo utatuvuruga subiri basi akimaliza na wewe utapata muda wa kujibia huko mbele.
Lissu anasema Wakili atakuwa na hoja asitupotezee muda hapa.
Wananchi wanacheka. ๐๐๐
Majaji wanaandika hapo tusubiri maelekezo yao. Wameanza kuteta kidogo.
Jaji anasema tunaomba utunze maoni yako. Utapata muda wa kujibu maana hajamaliza na linaweza kuibuka lingine utapata muda wa kujibu uwe na utulivu tu Wakili.
Mheshimiwa Lissu amesema yeye usiku wa leo unamtosha ataenda kusoma kila kitu. Tukutane kesho asubuhi.
Tunawasubiri majaji sijui wanasema nini?
Maana ilitakiwa Mtuhumiwa apewe proceedings zote zimekamilika ametokea muhuni mmoja huko ameandika summary tena nyingine kwa mkono vi page kama 20 hivi halafu wakagonga mihuri ya mahakama.
Jaji anasema tukutane kesho saa nne asubuhi.
Mahakama imeahirishwa.
So kutane hapa kesho saa 4 asubuhi.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Elimu ni mbegu,
Maarifa ni maji,
Uelewa ni jua,
Ndoto ni udongo,
Maono ni hewa,
Bidii ni jembe,
Utendaji ni mche,
Uzoefu ni mbolea,
Uvumilivu ni matunda,
Mafanikio ni mavuno.
Hata kesho nikipotea JESHI LA POLISI TANZANIA LINAHUSIKA. @tanpol
Hawa ndio walioniteka mara ya kwanza 23/6/2024, walitaka waniue kwa kunipiga RISASI YA KICHWA MBUGA KUBWA YA HUKO MKOANI KATAVI IKASHINDIKANA.
HII TWEET MUITUMIE KUWASHTAKI HATA NISIPOKUWEPO.๐ค
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Tangazo la kwamba waandishi hawaruhusiwi kurekodi na watu wasitumie simu zao limetolewa karibu mara 10 humu Mahakamani.
Uoga kuhusu kesi hii kuwa wazi kwa umma ni mkubwa sana.
Sijui kinachopangwa kufichwa ni kitu gani? Maandalizi ni makubwa sana hapa.
Toka nianze kufika mahakamani sijawahi kuona kesi imekuwa na maandalizi makubwa kuzidi hii ya leo.
Mara walete maji, Mara walete vitabu, Mara makaratasi, Mara vipaza sauti vikaguliwe.
Aisee yapo maigizo mengi sana.
Acha tuendelee kusubiri.
Mawakili waliitwa kwa Judge na wameshatoka wa pande zote mbili. Jamhuri na utetezi wote wapo hapa ndani mahakamani.
Aliingia msaidizi wa Judge ametoka tena.
Askari wa Magereza kama kawaida yao kwa harakaharaka nimewahesabu wako zaidi ya 200 kwenye hili jengo la mahakama tena ni wale KMKM Kikosi maalumu na kofia zao za kijani.
Kama kawaida yao wamejifunga sura zao kininja hawaonekani kabisa.
Msajili wa Mahakama anaitwa LYAKINANA leo amehangaika sana yupo anazunguka muda wote kuweka mambo sawa.
Ingawa sijui ni mambo gani? ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Upande wa Utetezi ameongezeka Wakili Emmanuel Ukashu ambae ni Mwneyekiti wa Umoja wa Mawakili Vijana Tanganyika.
Ameongozana na Mawakili wengine vijana wasiopungua 10 ambao sijajua majina yao hawa sijui watakaaa wapi maana Mahakama imetapika hapa hata pa kukanyaga hakuna.
Tukipata majina yao tutawaletea.
Naona Kalani wa Judge anatoa Tangazo la simu tena ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Watu wamechoka kusikia hata hilo tangazo lake maana kila baada ya dakika kadhaa anakuja hapa kusema simu haziruhusiwi mara waandishi hawaruhusiwi kurekodi.
Amekuja askari kutoa Tangazo tena la watu kuzima simu.
Amezomewa na raia ๐คฃ๐คฃ๐คฃ leo sijui nini kinaendelea.
Toka saa 3 asububi tangazo la kuzimwa simu linatolewa.
Hii kitu inatafakarisha sana.
Pengine kesi imechelewa kuanza kwasababu hiyo ๐คฃ kila anaekuja anazungumza watu kuzima simu.
Kilichobaki wanaweza kuanza kukusanya simu zetu.
Leo kitanuka hapa.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 1
Mh. Lissu ameingia tayari akiwa na vibe kubwa sana.
Majaji pia wameingia.
Kesi hii itasikilizwa na majaji watatu wa Mahakama Kuu na wao pia wameshaingia.
Nitawapa majina ya hawa majaji watatu.
Wakatikati yuko bize kuandika hawa wawili wengine tunaangaliana nao uso kwa macho.
Kesi haijaitwa bado.
Jaji anateta kidogo na mwenzake. Anawasha kipauza sauti.
Anasimama kalani anasema Criminal case No. 19605/2025 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.
Anasimama Nassoro Katuga wakili wa serikali tupo pamoja na
Job Mrema, Thawabu Issa, Mossie Kahima, Harrison Lukosi, Cathbert Mbiringi na Winiwa Kasala.
Hao ndio Mawakili saba wanaoiwakilisha Jamhuri mbele ya mahakama hii.
Mshitakiwa yupo naomba upande wa utetezi waweze kujitambulisha.
Anasimama mwanadada.
Anasema naitwa Neema Saruni ni Wakili. Mdada mrefu ananywele nyinginyingi.
Namuwakilisha mtuhumiwa aliyepo mbele ya mahakama hii tukufu.
Na kwa uwakilishi huo kwa mujibu wa PROBONO na nilipata wasaaa wa kuonana mteja wangu nikakutana nae.
Naomba mahakama impatie nafasi aweze kuelezea.
Watu wameshangaa ngoja tuone sasa.
Jaji anaandika kidogo.
Naambiwa kiutaratibu kesi kubwa watuhumiwa hupewa mawakili na mahakama.
Ngoja tuone.
Jaji anasema ngoja kwanza upande wa mshitaka waseme kesi imekuja kwa hatua gani.
Katuga anasema kesi ilikuja kwa ajili ya Preliminary hearing na sisi tuko tayari.
Kabla ya kuendelea na shauri hili Katuga anasema upande wa Jamhuri ulikuwa na Concern kadhaa kama tutapewa nafasi kuelezea.
Tuko tayari na plea taking na preliminary hearing.
Jaji anamwambia subiri kwanza.
Anaandika kidogo.
Amesimama Neema Saruni anasema tumemsikia Wakili wa Serikali Katuga lakini lipo suala la Uwakilishi wangu ikipendeza mteja apewe nafasi.
Jaji amesema sema wewe kwanza, niliwasiliana na mteja akasema atajiwakilisha mwenyewe, hayuko tayari nimuwakilishe.
Tulianza kushangaaa mbona anasimama wakili ambae hatumfahamu wakati Akina Mzee Mpoki wapo.
Anaanza Mh. Lissu kusema anasema nawashukuru Majaji kwa kunipatia Mawakili.
Pamoja na kwamba mimi sikumuomba na simfahamu wakili Neema Saruni alikuja mwenyewe kuniona kwenye gereza la Ukonga alijitambulisha na kuniambia yeye ndio amepewa hilo jukumu.
Nilifurahi kwa yeye kufanya hivyo. Walifanya vizuri sana.
Sasa Mh. Jaji alivyokuja na kunieleza nilimjulisha kuwa kwenye kesi kubwa kama hii ambayo ni kosa kubwa kuliko yote kwa mujibu wa ibara ya 28.
Kwenye kosa linaloshitakiwa kwa kusema maneno.
Kosa la aina hii nitajitetea Mwenyewe.
Kwasababu inabidi tuambiwe na nchi hii ukisema maneno yasiyowapendeza watu fulani fulani unaweza kuhukumiwa kifo.
Kwasababu hiyo nikasema nitajitetea mwenyewe.
Part 2 itaendele kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 2
Anaendele kuzungumza Mhe. Lissu
Mimi niliyesema hayo maneno nitajitetea na niwasikilize hao wanaosema nimefanya uhaini kuwa nimetenda makosa hayo.
Naomba pia mfahamu kabla mahakama hii haijaniteulia mawakili toka tukiwa kisutu sijawahi kuwa na upungufu wa mawakili zaidi ya 50 na baadhi yao wapo hapa leo.
Niliwaambia ambayo nimesema haya kwenye kesi kama hii sitataka mtu anizungumzie nilisema hivyo toka Kisutu na tulielewana.
Nafahamu uzito wa kesi kama hii Waheshimiwa Majaji, anayeshtakiwa ana haki ya kuwakilishwa na mawakili hata kama hana uwezo mahakama itamtafutia Wakili wa kumsaidia.
Mimi uwezo ninao na suala la kwamba sina uwezo hilo halipo. Mimi uwezo ninao.
Pili watu wanaostahili kuwekewa mawakili ni wale ambao wanakabiliwa na makosa makubwa na hawawezi kujitetea wenyewe.
Mimi nina uwezo wa kujitetea mwenyewe. Mimi ni Wakili wa Mahakama hii kwa miaka 23 hadi leo kama Wakili.
Nimefanya kazi ya uanasheria huu ni mwaka wangu wa 31, There is no question whatsoever to defend my self.
Najitetea mwenyewe kwasababu this is ultimate test, huu ndio mtihani mkubwa kwa mfumo wetu wa kisheria.
On this one, kwa heshima zote I will take full responsibility for myself.
Nitaweza to the best of my ability..
This is about my life. I will defend myself to the fullest.
Naomba niseme jambo kuhusu hili jopo la Mawakili toka Kisutu naomba katika kesi hii waendelee kuwepo wanisaidie kwenye research maana gerezani hakuna mtandao hakuna library kule.
Waendelee kuwepo ili wanisaidie nijiteteee kwa ukamilifu.
Na kama hilo litawapendeza nitafurahi kama watatambulishwa na pia hata huyu Wakili Neema Saruni atakubali na yeye awe sehemu ya jopo hilo la Mawakili wataonisaidia kufanya research.
Majaji wanaandika kidogo hapa.
KATUGA anasema tumefuatilia wenzetu mshitakiwa pamoja na Wakili wake.
Kwa mujibu wa kifungu cha 329 cha sheria ya mwenendo wa jinai kinatoa haki kwa mshitakiwa kuwa na uwakilishi kwneye kesi inayomkabili.
Ingawa haki hii sio ya lazima, busara ya mahakama ilimpa Wakili kwa ridhaa yake anaiambia Mahakama hii kujitetea mwenyewe.
Kwenye hiyo hoja ya kujitetea mwenyewe kwakuwa amesema ni mbobezi wa sheria hatuna pingamizi kwenye hilo.
Lakini upande wa jamhuri unasita kukubaliana kwenye hoja ya kuwa ana mawakili ambao watamsaidia kufanya research na watambulishwe.
Hatupingi wao kumfanyia research lakini tunapinga wao kuingia kwenye rekodi. ๐คฃ๐คฃhuyu Baba ana wivu hata watu kutambulishwa, utadhan wakitambulishwa kuna kitu kitapungua kwenye mwili wake.
Anaendelea pale kunapokuwa na kesi ya pande mbili. Lazima Wakili apate nafasi ya kuwa na mtu anayemuwakilisha, hawa wasitambulishwe kabisa.
Jaji anaeongoza jopo la Majaji ni Mh. Dunstan Ndunguru
Huyu Katuga anaongea watu wana hasira nae ni kama wanataka kupasuka hivi sijui hata huyu ndugu anatafuta nini kuna mambo watu wanashangaa kwanini amekuwa na akili kama za mkaanga sumu.
Wanateta jambo mawakili wa Serikali.
Mh. Lissu ameulizwa unasemaje anasema mimi sina shida hata tusipowatambulisha. Tuendelee kwenye mambo ya msingi.
Nilidhani ni jambo dogo lisingekuwa na nongwa kama wenzetu wameona ni nongwa basi tuendelee na kazi ya leo, Mimi sina shida.
Part 3 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 3
Jaji anasema Wakili Neema anakuwa discharged na mahakama ila kama ataendelea au kubaki na hiyo timu sisi hatuna shida mtamalizana nae.
Pia kuhusu hiyo timu tunakuachia uendelee nayo kama ulivyoomba wakusaidie research.
Anasimama Katuga sasa.
Tulikuwa tumejiandaa na jukumu la leo. Lakini asubuhi ya leo tumepokea Notice of Motion kwa mujibu wa kifungu cha 294(1) na 295 cha CPA ikionekana imesajiliwa na Mshitakiwa mwenyewe na imepitishwa na Mkuu wa Gereza la Ukonga.
Kama imeshafika hapa mahakamani tulikuwa na concern hiyo na ipo kwenye mfumo.
Jaji anamjibu.
Kwenye hii Notice Wah. Majaji lipo ombi la pili kuwa ambalo ameleta maombi mawili ameweka nia ya kuleta pingamizi kwenye hati ya mashitaka lakini pia ana question mamlaka ya mahakama hii kwa maana ya jurisdiction ambae yeye anaona lipo hapa kinyume cha Sheria.
Ameeleza mengi, concern yetu sisi ni kwamba linapotokea suala la mamlaka ya mahakama (jurisduction) maamuzi mbalimbali yanasema tutaanza kwanza kutatua tatizo hilo kabla yakuendelea na jambo lingine lolote.
Hii ni kwasababu huwezi kuendelea na jambo lolote ambalo huna mamlaka nayo.
Hivyo mshitakiwa anasema lazima tujiridhishe kwa jambo hilo na yamesemwa pia kwenye kesi ya mahakama ya rufaa Thabiti Ramadhani Maziku, Kisuku Salumu Kaptura dhidi ya Amina Hamisi Tyeira and another. Rufaa Madai No. 98/2011 ukurasa wa 4 wa rufaa hiyo majaji wa rufani walisema suala la jurisdiction likiibuliwa lazima liamuliwe kwanza kabla ya kuendelea na mambo mengine.
Katika mazingira haya hatuwezi kuendelea.
Tuliamue jambo hili lililoletwa na mtuhumiwa.
Amemaliza kusema Katuga.
Part 4 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 4
Anakaribishwa Mhe. Tundu Lissu.
Anasema kwamba sina pingamizi na mapendekezo ya wakili wa serikali Mkuu.
Kwanini nimeleta hizo hoja mbili
1. 4/09/2025 nililetewa summons kuwa nitasomewa mashtaka leo na kuyajibu. Sasa kwenye shauri kama hili kifungu Cha 295(1) cha CPA kinasema pale ambapo taarifa information yaani charge sheet haionyeshi kosa na haiwezi kurekebishika kwa mujibu wa kifungu cha 294 basi mahakama ina mamlaka ya kufutiliwa mbali na hiyo ni immediately kabla ya mshitakiwa kujibu mara tu baada ya kusomewa hilo Shitaka.
2. Naelewa concern kwamba kuna suala la mamlaka ya mahakama hii kusikiliza. Suala la jurisdiction linapaswa kuamuliwa mapema. Ninachoweza kusema mimi nilikuwa nimejiandaa kwa hoja zote mbili. Kwamba kuna kesi hapa? Au mahakama hii ina mamlaka? Mimi niko tayari kwa lolote kati ya hayo. Mahakama iamue tuanze na lipi kati ya hayo mawili.
Mtanielekeza.
Haya makosa ya uhaini yanakuja mara moja moja katika maisha ya binadamu.
Kwa mara ya kwanza 1983 ndio kesi ya kwanza ya uhani. Kesi ya R vs Khatibu Gandi na kabla ya hapo ilikuwepo 1970 kesi ya kwanza ya uhaini.
Hii yangu ni kesi ya tatu ya Uhaini ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kesi kama hizi zinaweka misingi ya Kisheria katika sheria.
Kwasababu hiyo Mahakama hii kama itaridhia kujibu swali la hivi HATI YA MASHITAKA ya makosa ya uhaini inatakiwa kuwaje? Itakuwa ni Precedent nzuri na kubwa sana.
It will be unfortunately kama mahakama haitajipa fursa ya kuangalia jambo hili kuhusu makosa ya uhaini na ombi langu ni hilo.
Ishu ya Jurisdiction na inshu ya hati ya mashitaka kama iko kihalali.
Tufanye hiyo kazi ili tuweke kumbukumbu sawa na rekodi hiyo itakumbukwa na dunia nzima wamba mahakama kuu iliamua nini kuhusu mambo haya makubwa mawili hata siku ambapo mimi na nyinyi hatutakuwepo mambo haya yatakumbukwa na vizazi vyote. Ahsanteni.
Majaji wanaandika na kuteta kwa pamoja.
Leo Mh. Lissu amekuja na style kama anabembeleza hivi lakini nasikia radha ya hii misumari.
Anatumia style moja inaitwa SIMBA MWENDA POLE ndio mla nyama.
Anainuka KATUGA anasema anaomba rejoinder, amepewa nafasi anasema alichomuelewa mshitakiwa ni kuwa anakubaliana na maelezo yetu.
Wao wanachoamini mashitaka yanapingwa kwenye mahakama yenye mamlaka. Kwenye anasisitiza liamuliwe suala la jurisdiction halafu ndio tuanze kujadili suala la uhalali wa mashitaka.
Majaji wanaandika na bila shaka Kiongozi wa Jopo la Majaji watatu ambae ni Jaji Dunstan Ndunguru atatoa mwelekeo kuwa tuendaje mbele.
Mahakama imetulia sana wananchi waliopo sehemu ya chini na sehemu ya juu kule gorofani wote wako makini sana kufuatilia hili shauri. Kesi ina mvuto sana.
Kuna namna watizamaji wakimuona KATUGA anazungumza ni kama wanavurugwa sana ๐คฃ๐คฃ
Ngoja tuwasikilize majaji watasemaje. Amemaliza Katuga.
Jaji Ndunguru anasema suala la jurisdiction ni suala la kisheria.
Kwahiyo tuanze na suala la jurisdiction halafu baadae ndio tuendelee na suala la uhalali wa hati ya mashitaka.
Part 5 itaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 5
Anasimama Mhe. Lissu kuanza na suala la jurisdiction kwanza.
Ameleta pingamizi kuwa mahakama hii haina mamlaka kivipi kusikiliza kesi hii.
Mh. Lissu anaanza kwa kusema taarifa hii niliyoitoa nilishaitoa mapema huko nyuma hasahasa mahakama ya Kisutu.
Naomba niibadilishe hiyo hoja kidogo sana.
Hoja yangu isomeke mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi hii kwasababu ya makosa mengi na makubwa yanayoonekana kwenye uso wa rekodi ya mahakama ya ukabidhi (committal Court) yaani ile mahakama ya kisutu.
Makosa hayo yameuharamisha utaratibu wote wa committal Court.
Anasema kingereza chake cha haya niliyoyasema ni hiki. Anatema ung'eng'e kwamba under section 184 of CPA on the face of record the committal proceedings includes irregularities.
Jaji anauliza tunaachana nayo kivipi? Anamjibu kuwa nilichokwambia kwa sasa ndio iwe record yako na nitazungumzia kwa namna nilivyoliweka hili pingamizi kwa sasa. Tuendelee kwa utaratibu huo tafadhali. Wanakubaliana hapa.
Mh. Lissu anaendelea anasema naomba nianze kuweka msingi wa kisheria.
What is the law on committal proceedings? Hii sheria inasemaje na ikoje?
Kif. cha 261cha CPA kinasema pale ambapo shitaka limepelekwa mahakamani dhidi ya mtu yeyote kwa kosa ambalo haliwezi kusikilizwa na mahakama ya chini basi mashauri ya ukabidhi (committal case) itafanyika katika mahakama ya huko chini.
Anasoma hapa hicho kifungu cha sheria kilivyoandikwa.
Kwahiyo committal proceedings ilipaswa kufanyika kwenye hiyo mahakama ya chini.
Kifungu cha 184 of CPA kilipaswa kusomwa pamoja na kifungu cha 261 nilichosema awali.
Ambapo kinasema hakuna kesi ya namna hii itaendelea hapa bila ya mtuhumiwa kuwa committed kwenye mahakama hii ili iweze kusikilizwa.
Sasa sheria inasema utaratibu wa Committal lazima ufuatwe ili tuendeleee vizuri hapa leo.
Mahakama ya rufani ya Tz ineweka msimamo wake kwneye nasuala haya kesi ya Jamhuri vs Dodoli Kapufi na wenzake. Criminal Rev. CAT At Mbeya.
Ninayo nakala moja niko gerezani, ukurasa wa 25 sect. 178 of the CPA creates a bar against a taking of cognizance unless the same has been investigated and the accused have been committed duly committed for trial.
Kwanza lazima iwe properly investigated na pia iwe duly yaani properly ina accordance of the law.
Hayo masharti kwa namna ya kuifanya hiyo kesi ifike hapa jwenye mahakama hii. Je masharti hayo ni yapi? Masharti gani hayo?
Kif. Cha 262(1) cha CPA kinaweka sharti la kwanza la committal processes.
Kinasema kwamba pamoja na mambo mengine sharti la kwanza unapelekewa kwenye mahakama ya eneo ulilokamatiwa.
Mimi nilikamatiwa Mbinga, mkoa wa Ruvuma. Committal proceedings zimefanyikia Kisutu Dar es salaam. KM nyingi kutoka Mbinga. Sheria ilisema nipelekwe nilipokamatiwa.
Sharti la Pili ni la kusomewa shtaka kif. 262(2) cha CPA na hatatakiwa asijibu.
Sharti la tatu, liko kwneye kifungu cha 262(3) of CPA baada ya charges kusomwa mtuhumiwa aambiwe kuwa hatapaswa kujibu na atapelekwa gerezani.
Sharti la nne ni kwamba liko 262(6) of CPA baada ya upelelezi kukamilika ataandaa information (mashtaka) kwa mujibu wa sheria na kuyafungua mahakama kuu.
Sasa waheshimiwa ma jaji sharti muhimu kwa ajili ya hoja yangu ya leo lipo kwneye section 265(1) ya CPA.
Kifungu hicho kinasema kuahirishwa kwa kesi wakati wa committal. Nitakielezea pia.
Part 6 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 6
Anaendelea kuongea Mhe. Lissu
Kifungu kinasema hicho cha 265(1) of CPA kinasema kama kuna haja ya kuahirishwa kwa shauri basi mahakama itaamuru mtuhumiwa apelekwe gerezani kwa siku 14.
Mahakama inapaswa kusema kwanini kesi imeahirishwa? Kila siku lazima iandike hivyo.
Naomba niwapeleke sasa kwenye hizi records za kutoka Kisutu.
Mimi nilikamatwa tar. 09/04/2025 usiku Mbinga hadi Dar es salaam usiku kwa usiku nakufika Dar es salaam niisafirishwa.
Niliwekwa pale Shimoni police central.
Tar. 10 hiyohiyo nilipelekwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu kusomewa hili shtaka la uhaini.
The treason charge was read on 10/04/2025 pale Kisutu.
Nikapelekwa gereza la Keko hiyo tar. 10/04/2025.
Ilisema kesi itakuja tar. 24/04 tena.
Hawa majaji hawamuingilii kabisa Mhe. Lissu tofauti na kule Kisutu labda wabadilike kwenye eneo hilo huko mbele.
Ta. 24/04 wakati naenda Kisutu nilikuwa natokea Ukonga sio Keko tena.
Waliahirisha kesi siku hiyo hadi 19/05/2025 kwamba upelelezi bado.
Walisema pia upelelezi bado ikaahirishwa 02/06 na mara zote nimerudishwa gerezani na leo ni 153 siku niko gerezani.
Tar. 16/06 ikaahirishwa tena, upelelezi bado ndio sababu yao.
Tar. 01/07 nikapelekwa ikaahirishwa tena na mahakama ikasema tar. 15/07 ikaahirishwa tena walikuwa hawajajiandaaa ndio walichosema mahakamani.
Tukarudi tar. 30/07 ikaahirishwa tena na muda wote napelekwa gerezani na ninakaa na wafungwa waliohukumiwa kifo.
Tar. 13/08 tukarudi tena Kisutu ndio upande wa mashitaka wakasema wako tayari.
Ikaahirihswa tena lakini mpaka tarehe 18/08 ndio mahakama ikafanya kile kinachoitwa Commitall hearing.
Sasa Wah. Majaji imeahirishwa mara 10 kuanzia 10/04 na 18/08 mwaka huu.
Muangalie hiyo record kuanzia tar. 10 hiyo yote yaliyofanyika yako wapi kwenye hii record yako wapi?
Yaliyopo humu ni ya tarehe 18/08 tu ndio yameletwa huku mahakama kuu.
Hayo mengine yote yako wapi?
Kwanini wameficha wanaficha nini?
Kesi imeahirishwa zaidi ya mara 10 lakini kwenye hizi records hayapo kabisa.
S. 265(1) ya CPA ukiahirisha hata mara moja lazima uandike sababu za kuahirisha.
Records ziko kimya tena UKIMYA WA KABURINI.
Hazisemi chochote kuhusu hayo mengine yaliyotokea huko nyuma.
Waheshimiwa Majaji naomba niwapeleke kif. Cha 266(3) cha CPA
Amesimama KATUGA anasema Mh. Tunaona kama mwenzetu amepewa proceeding fupi tofauti na tulizonazo na sisi.
Mh. Lissu amemjibu kuwa nilichopewa ndio hicho na ndio ninachokisema hapa Mahakamani kuwa nimepewa nyaraka zinazoanzia tarehe 18/08.
Mahakama imeibua vicheko. ๐๐๐
Jaji anasema wahudhuriaji wawe watulivu tafadhali. Majaji wanaandika kidogo.
Mh. Lissu amewapa proceedings ambazo amepelekewa ili majaji nao wazipitie na kusoma kama kweli ziko sahihi au haziko sahihi.
Kimya kimetanda hapa. Hali ya hewa imeshachafuka.
Kuna wahuni nafikiri walishafanya kazi yao.
Ngoja tuone. ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Majaji wanateta na kushauriana.
KATUGA yeye anazo proceedings zilizokamilika.
Halafu Mh. Lissu wamempelekea gerezani proceedings ambazo hazijakamilika.
Part 7 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 7
Jaji anasema sisi tukizonazo kama Majaji zinaonesha colum ya kwanza tar. 10/04/2025. Na anasoma waliokuwepo siku hiyo.
Upande wa utetezi pia anawasoma waliokuwepo.
Jaji anasema au tukupe kwanza ili uendeleee. ?
LISSU anakubali.
Wameenda kuzitafuta huko ili wamleteee aweze kuendelea.
Sijui kwanini walizificha.๐
Ili tuwe fair tunaomba uzipate kwanza halafu useme unazionaje.
Lissu anasema mkinipa hizo nyaraka nitahitaji dakika 30 tu nipitie na nitakuwa na cha kusema.
Anasimama KATUGA anasema busara tumpe muda wakutosha
Leo Katuga amekuwa mtetezi wa Lissu kwa mara ya kwanza. ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Eti upande wetu tunaangalia fair hearing. Watu wanacheka. ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Katunga anasema wao wanaiachia mahakama apate.
Jaji anasema hiyo nusu saa kwani kaomba nani? Si yeye wewe una shida gani?
Lissu ameulizwa amejibu anasema kwa kuwa leo Katuga ameamua kunipenda sana naomba nipewe lisaa limoja.
Jaji anauliza tukirudi saa 10 unahisi tunaweza kuendelea?
Lissu anasema niko tayari mimi labda nyie majaji mseme hamko tayari.
Jaji amesema tukupe lisaa limoja halafu turudi hapa.
Anamuuliza Katuga yeye anasemaje watu wanacheka sana. ๐๐๐
Katuga amesimama tunasubiri sijui atajibu nini?
Katuga amesimama haongei.
Watu humu mahakamani wanasema KATUGA piga simu uuloze kwamba LISSU aruhusiwe kukaa humu ndani ya mahakama ya lisaa limoja au akasomee lockup? ๐๐๐
Maana Mh. Lissu amesema akipewa hizo nyaraka azisomeee humu humu ndani na Mawakili wanaomsaidia research asiende kule lockup.
KATUGA amefikisha dakika kadhaa hajasema kitu.๐๐๐
Jaji anasema utapelekwa sehemu unayostahili na mawakili watakuja huko. Na saa 10:10 tutarudi hapa kwa pamoja.
Tukutane hapa saa 10 ndugu zangu.
Naomba Repost yako kwenye tweet.