@Adventure_36 Mngekua mmesoma sheria kitu kinaitwa invitations to treaty msinge hata lalamika ni kitu cha kawaida. Iyo ina muinvite mteja aweze kuleta offer yake na iyo bei sio kwamba ndo bei ya bidhaaa. Mfano mwingine ishu za minada unakuta bidhaa inatangazwa itautwa ivi lakini inakuja badlik
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 167
Tumerudi tayari.
Majaji wameingia, na Mhe. Lissu nae karudi.
Kwa dalili zilivyo naona ni kama Mhe. Lissu hajapatiwa Chakula, sijui lakini ngoja tusikie.
Majaji wanaandika kidogo pale.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude anasema uwakilishi wetu kama ulivyokuwa awali, tuko tayari kama ameshakula labda tumsikilize.
Mhe. Lissu: Mhe. Jaji sijala lakini naomba tuendelee tu ivo ivo maana issue ya mimi kupewa chakula imeshindikana.
Magereza wamekataa kunipatia Chakula. wamesema nitaenda kula Gerezani.
Majaji ni kama wamekasirika au wamechanganyikiwa hapa.
Renatus Mkude amemuita askari Magereza wanaongea ongea hapa sijui wanaongea nini?
Jaji Ndunguru anasema Chakula ni haki ya msingi kabisa na haitakuwa sahihi kuendelea na shauri hili bila mshitakiwa kupatiwa Chakula.
Wenzetu wa Magereza mzingatie kuleta Chakula, itakuwa ni kinyume cha haki za binadamu kumnyima mshitakiwa chakula.
Tunaomba kuahirisha hadi kesho saa tatu asubuhi na mtakumbuka tulisema shauri litasikilizwa hadi saa 11 jioni.
Kuanzia kesho hakikisheni anapata Chakula Mchana.
Nahairisha kesi hii hadi kesho saa tatu kamili asubuhi. 13/02/2026.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 13, 2026
Jana tuliishia Part 167 so leo tunaendelea na-;
Part 168
Mahakama imeanza muda huu saa tatu na nusu.
Mhe. Lissu anaingia akiwa amevaa kombati nyeusi.
Sauti ya High Courttt inapigwa kila mtu anasimama na kelele za kumsalimia Mwenyekiti zinasimama kidogo.
Majaji wanaandika kidogo pale mbele.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude anasema yupo na Ajuaye, Katuga, Ignas, Cathbert na Winiwa na wote tunawakilisha Jamhuri na Mshitakiwa yupo.
Sisi tuko tayari kuendelea na leo tumekuja na P6 yuko tayari, endapo Mshitakiwa atakuwa tayari.
Mhe. Lissu anaulizwa na yeye anasema yuko tayari.
Jaji Ndunguru: Naomba shahidi aje sasa.
Shahidi analetwa kama Bangi kule mbele kwenye kibox hatumuoni chochote tunaona milango tu inafunguliwa sijui amevalishwa baibui.π
Mlango wa kizimba umefunguliwa muda huu.
Shahidi anaulizwa umri wake anasema miaka 24 na ni Mkristo so anaapishwa muda huu.
Jaji anauliza nani atamuongoza? Anajibiwa ni Cathbert Mbiringe Wakili wa Serikali ndio atamuongoza.
Anamuuliza unanisikia.
Haya mkazi wa wapi?
Mimi natokea Ruvuma Songea na kazi yangu ni Afisa Usafirishaji Bodaboda, nafanyia huko huko Songea shughuli zangu.
Mwezi October 2024 ni mwaka ambao nilianza kushirikisha siasa za Chama cha Chadema.
Wakili: Ulishiriki kivipi?
Shahidi wa kificho P6: Nilianza kushiriki kwenye mikutano ya hadhara na kuwafuatilia viongozi mbalimbali wa Chadema na nikafanikiwa kuwafahamu Mhe. Lissu na baadhi ya Viongozi waliokuwepo Songea.
Wakili: wakiwepo akina nani?
Shahidi wa kificho P6: nilimfahamu Katibu wa Vijana Songea.
Wakili: Alikuwa anaitwa nani?
Shahidi wa kificho P6: alikuwa anaitwa Chiza au Mwamba wa Kigoma maarufu kwa jina hilo.
Wakili: January 2025 unakumbuka nini?
Shahidi wa kificho P6: Nilianza kuwa nimeshiriki siasa za Chadema na kuvutiwa kuwa mwanachama wa Chama hicho.
Nikaanza jitihada za kutafuta viongozi waliopo Songea, nikamfuata kiongozi wa Vijana Chiza na kumueleza nia yangu ya kutaka kuwa mwanaChama.
Wakili: Nini kiliendelea baada ya hapo?
Shahidi wa kificho P6: Alinipokea na kunisifia kwa uamuzi mzuri. Akasema napaswa kuwa na kadi ya Chama, nilifuatilia hiyo kadi na nikaambiwa nisubiri mashine bado ni mbovu na ataendelea kunishirikisha kwenye shughuli za Chama.
Wakili: Zipi hizo shughuli za Chama?
Shahidi wa kificho P6: Sisi bodaboda huwa tunakuwa kwenye misafara ya Chama na bendera.
Wakili: Tar. 04/04/2025 kilitokea nini?
Shahidi wa kificho P6: Hiyo tarehe nikiwa sehemu yangu ya kazi pia nikiwa na simu yangu ya mkononi aina ya infinix smart 8 nikiwa naangalia mtandao wa Youtube.
Wakili: Youtube ni nini?
Shahidi wa kificho P6: ni mtandao wa kijamii ambao unamuwezesha mtu kutuma video, audio na maudhui mengine.
Huyu Bodaboda wa miaka 24 anavyoelezea mambo unashangaaa ni kama anajibu essay huyu atapata tabu kwenye maswali. π
Anaendelea kuwa simu yake ilikuwa na internet na aliingia google kumuwezesha kuingia youtube.
Shahidi wa kificho P6: Niliingia kwenye account ya Jambo TV nilifanikiwa kuona na kusikiliza hotuba aliyokuwa anatoa Mwenyekiti wa Chama cha Chadema ambapo alionekana akihutubia watu akisema bila mabadiliko hakuna uchaguzi hivyo tunaenda kukinukisha.
Tunakwenda kuvuruga Uchaguzi pia nilisikia na kuona akisema tunakwenda kukinukisha na yeyote atakayekuwa pamoja nasi tutakwenda nae na ambae hatataka tutamuacha pia alisema kama kuna mtu yeyote anatarajia kugombea asahau jambo hilo.
Wakili: Pia akasemaje?
Shahidi wa kificho P6: Pia hata mimi kugombea uenyekiti msahau pia akasema bila mabadiliko hakuna Uchaguzi.
Wakili: Kingine kipi?
Shahidi wa kificho P6: Pia akasema watasema tunafanya uasi ni kweli utakuwa ni uasi kwasababu bila mabadiliko hakuna uchaguzi.
Part 169 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 169
Mazingira aliyokuwa anayatolea ilikuwa ni kama sehemu ya Ukumbini, ndo nilimuona hapo.
Muda huu ameingia Mtaalamu, Wakili Msomi Peter Kibatala wakati kesi inaendelea.
Amekaa pale karibu na Kizimba cha Mhe. Tundu Lissu, nimeona wanasalimiana kimya kimya Mhe. Lissu anacheka anamuonyeshea kidole cha Upendo ni kama anamwambia wewe kijana wangu wewe.π
Wakili wa Serikali: Muonekano wa Lissu ulikuwaje?
Shahidi wa kificho P6: Alivaa Kombati ya Kaki.
Namfahamu Tundu Lissu kama mwanasiasa mkongwe na mwanasiasa maarufu.
Wakili: Baada ya kuona hiyo hotuba wewe ulifanya nini?
Shahidi wa kificho P6: Nilivyoona hiyo video maneno yake yaliniingia moyoni na kunishawishi.
Hiyo agenda ya kukinukisha ni kufanya vurugu au kuharibu miundombinu.
Wakili: huo uchaguzi ni upi?
Ukisikiliza majibu ya huyu Shahidi wa kificho ni wazi kaingia na desa anasoma majibu.
Anajibu hapa ni Uchaguzi Mkuu wa 2025 unaohusisha wabunge na Rais na Madiwani.
Wakili: Ikawaje baada ya kushawishika?
Shahidi wa kificho P6: Nikamfuata Mwenyekiti wa Vijana wa Songea alikuwa anaitwa Chiza maarufu kama Mwamba wa Kigoma.
Wakili: ikaendelea nini?
Shahidi wa kificho P6: Nikamueleza nilivyoshawishika na maneno ya Mwenyekiti na kutaka kuwa miongoni mwa watu tutakaokinukisha.
Wakili: Kikaendelea nini?
Shahidi wa kificho P6: Alinisifia sana kwa uamuzi mzuri na wakishujaa na akanipongeza na kuniambia Vijana kama nyie ndio vijana mnaotakiwa kulikomboa Taifa.
Wakili: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Aliniambia ataniunganisha kwenye magroup yanayojadili mipango ya kuzuia Uchaguzi, akaniunga Group la SIASA YETU.
Group lilikuwa linaitwa SIASA YETU UPDATES.
Wakili: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Niliendelea na shughuli zangu na yeye akaendelea.
Tarehe 06/04/2025 nilipata taarifa kuwa Mwenyekiti wa Chadema atakuwa ziarani mkoani Ruvuma.
Wakili: Mwenyekiti ni nani?
Shahidi wa kificho P6: Ni Mh. Tundu Lissu, hiyo taarifa nilipata kutoka kwa ndugu Chiza.
Wakili: Ikakutaka ufanye nini?
Shahidi wa kificho P6: Ilitutaka tufanye maandalizi na tarehe 10/04 atakuwepo Songea.
Wakili: Mlipanga nini kuhusu mkutano?
Shahidi wa kificho P6 ; Tulipanga mkutano ufanyike uwanja wa matalawe. Tarehe 09/04/2025 nilipata taarifa kuwa Mwenyekiti amekamatwa Wilaya ya Mbinga akiwa kwenye ziara ya Mikuta.
Watu wanashangaa mikuta ndio nini? Mashahidi wa siri wanasoma.. πππ
Shahidi wa kificho P6: Nilimtafuta Chiza kumuuliza kuhusu taarifa za Mwenyekiti kukamatwa Wilaya ya Mbinga.
Wakili: ikawaje?
Shahidi wa kificho P6: Akanijibu ni kweli amekamatwa lakini ratiba ya Mkutano wa Tarehe 10/04/2025 itakuwepo palepale. Kwahiyo jiandae kuwepo eneo la Mkutano Tarehe 10.
Wakili: hiyo Tarehe 10 sasa nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Tulikusanyika uwanja wa Matalawe kusubiri viongozi walioambatana na Mwenyekiti kuhutubia mkutano.
Alikuwepo Godbless Lema na Dr. Wilbroad Slaa pia alikuwepo Mh. Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Mh. Heche.
Wakili: nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Wakati tunasubiria likatokea gari ya Polisi na kusema kwa siku hiyo hakuna mkutano utakaofanyika eneo hilo. Na haruhusiwi mtu kukaa eneo hilo.
Wakili: nini kikaendelea?
P6: Ikabidi tutawanyike na kuelekea ofisi za Chama ili tufahamu kwa siku hiyo nini kitaendelea?
Wakili: Ziko wapi hizo ofisi?
P6: Ziko Songea sehemu inaitwa Mfaranyaki.
Wakili: kikaendelea nini?
P6: tuliwakuta viongozi ambao ni Adel Mayala ambae kwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini.
Wakili: Nini kiliendelea?
P6: Wakaja Polisi wakapiga mabomu ya machozi na kusema watu wote watawanyike.
Wakili: Saa saba mchana nini kiliendelea?
P6: Alikuja kiongozi Makamu Mwenyekiti na kusema kwamba amepokea barua kutoka Polisi kwamba kwa siku hiyo usifanyike Mkutano wa aina yoyote katika eneo hilo.
Wakili: Akasema nini kingine?
Part 170 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 170
Shahidi wa kificho P6: Akasema tutawanyike na atapanga tarehe nyingine ya mkutano huo.
Wakili: Huyo Makamu Mwenyekiti ni nani?
Shahidi wa kificho P6: Ni Mh. Heche.
Wakili: Tar. 18/04/2025 nini kilitokea?
Shahidi wa kificho P6: Nilipokea taarifa kuwa tarehe 20/04/2025 siku ya pasaka kutakuwa na matembezi ya hiyari ambapo katika matembezi hayo yataambatana na kuvalia tshirt zilizoandikwa agenda ya No Reforms: No Election ili kuendeleza agenda ya Chama.
Wakili: Kingine kilichoendelea?
Shahidi wa kificho P6: Ukafanyika utaratibu wa kuzipata tshrit na tunachangia elfu 10 ndipo zitasafirishwa hadi kutufikia.
Tukaambiwa hadi kufikia tarehe 20 basi tutakutana kwa ajili ya matembezi hayo ya hiari.
Wakili: Tar. 20/04/2025 kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Tulijikusanya kwa ajili ya matembezi ya hiari kila mmoja alipata tisheti yake na tukakubaliana jioni majira ya saa 10 ndio matembezi ya hiari yatafanyika.
Wakili: Ulipata wapi hizo taarifa:
P6: Group la Siasa Yetu.
Wakili: Matembezi mlikubaliana mkutane wapi?
Shahidi wa kificho P6: Songea Mjini kwa Disi Kitimoto na ilipofika majira ya saa 10 huku tukiwa na bodaboda huku tukisubiri wengine. Mimi nilikuwa kwenye muonekano wa kuvaa tshirt iliyoandikwa agenda ya No Reforms: No Election.
Wakili: Nini kilitokea?
Shahidi wa kificho P6: Wakaja Polisi wakajitambulisha kwa ghafla kuwa wanatokea kituo cha Polisi Songea na wakatuambia tunahitajika kituo cha Polisi Songea kwa ajili ya mahojiano.
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P6: Walitukamata na kutupeleka kituo cha Polisi Songea na wakatuhoji kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali.
Wakili: nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Wakasema tutatoka kwa dhamana lakini tulihitajika kwenda kuripoti ofisi ya RCO.
Wakili: Tarehe 25/04 nini kiliendleea?
Shahidi wa kificho P6: Tuliripoti Ofisi ya RCO tumuelezee kilichotokea hadi kufika sehemu hiyo.
Wakili: Mhe. Jaji ndio hayo kwa shahidi huyo.
Watu wanashangaa sasa huyu shahidi sijui alikuwa anazungumza nini na kinasaidia nini kwenye Uhaini ni Maajabu, ngoja Tunasubiri aanze kuulizwa maswali hapa.
Jaji Ndunguru: Vipi mshitakiwa tukupe nafasi ujikusanye vizuri?
Mhe. Lissu: Mh. Jaji huyu shahidi nilishajiandaa nae toka juzi.
Sasa shahidi sijui wewe ni Kaka au Dada lakini naomba ujibu maswali yangu sawa?
Shahidi wa kificho P6: sawa.
Mhe. Lissu: Uliandika maelezo Polisi?
Shahidi wa kificho P6: Sijaelewa swali.
Mhe. Lissu: Kitaeleweka tu. Jibu swali langu Bwana.
Shahidi wa kificho P6: niliandika
Mhe. Lissu: Ukionyeshwa hayo maelezo yako utayatambua?
Shahidi wa kificho P6: ndio.
Mhe. Lissu: Ulisaini?
Shahidi wa kificho P6: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Mh. Jaji naomba aonyeshwe maelezo yake.
Shahidi wa kificho P6: Nimeyapata na ndio maelezo yangu niliyoandika Polisi Songea.
Mhe. Lissu: Je yana sahihi yako?
Shahidi wa kificho P6: sahihi yangu ipo ndio.
Mhe. Lissu: Ni maelezo ya Tar. 25/04/2025.
Shahidi wa kificho P6: Sioni hiyo Tarehe.
Mhe. Lissu: Angalia juu mwanzoni, anamsomea hilo eneo.
Shahidi wa kificho P6: Sijayaona hayo maelezo.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji nataka ku impeach huyu shahidi, nitamsomea maelezo yake, anamsomea hapa.
Mimi ni mkazi wa Bombambili, kazi yangu Bodaboda na kituo changu ni miembeni.
Ilipofika mwaka 2025 nilimfuata Katibu wa Vijana Essau Chiza alinikaribisha kwenye Chama na kunifanyia mpango wa kadi ya Chama.
Nakumbuka tarehe 04/04/2025 niliona mtandao wa youtube hotuba ya Lissu iliyokua inahusu uchaguzi 2025 iliyokuwa ikihamaisha uasi. Ilinipa moyo wa kijasiri wa kutaka kuvuruga uchaguzi.
Nikamtafuta Essau Chiza ambae ni Katibu kunipa mipango mingine ikiwemo ziara ya Mwenyekiti Taifa.
Anaendelea kumsomea maelezo yake yote hapa.
Part 171 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 171
Mhe. Lissu anaendelea kumsomea Shahidi maelezo yake.
Amemaliza kusoma maelezo anamuonesha maeneo aliyodanganya au kuleta mkanganyiko.
1. Dini
2. Umri
3. Shughuli za Chama alizoambiwa atakuwa anataka kuzifanya
4. Tar. 04/04/2025 ulikuwa na simu infinix smart 8.
5. Hiyo simu yako lilikuwa na bando la Internet
6. Uliingia kwenye mtandao wa youtube wa Jambo Tv
7. Mimi mtuhumiwa nilisema yoyote atakayekuwa nasi tutaenda nae ambae hatataka tutamuacha.
8. Nilisema anayetaka kugombea udiwani au ubunge asahau na mimi niliyetaka kugombea urais nisahau
9. No Reforms: No Election.
10. Wanasema tutafanya uasi ni kweli tutafanya.
11. Niliitoa hotuba yangu ndani ya ukumbi na kulikuwa na bendera ya taifa na ya Chadema
12. Nilivaa kombati za kaki nayo nataka unioneshe.
13. Kwamba tutazuia uchaguzi kwa kufanya vurugu
14. Nataka niyaone maneno ya Mwamba wa Kigoma.
15. Kwamba Mwamba wa Kigoma alikusifia kwa uamuzi wa kishujaa na wewe ni mojawapo ya vijana mnaotakiwa kulikomboa Taifa.
16. Tar. 06/04/2025 ulipata taarifa kuwa Mh. Tundu Lissu atatembelea Mkoa wa Ruvuma.
17. Ulipewa taarifa ya kumpokea Mwenyekiti wa Chama Taifa.
Mhe. Lissu anamsomea maeneo ambayo shahidi amedanganya au ameyasema leo lakini kwenye maelezo yake ya Polisi hajasema.
Anaweza msomea maeneo hata 50.
Kwa kifupi anachokifanya kuyataja hayo maeneo ni kama anamuandaa au kumlainisha shahidi kabla ya kuanza kumsokota, kuonyesha uongo wa shahidi.
Ameonyesha maeneo 20.
Mhe. Lissu Lissu: Anamuuliza je ungependa maelezo yako yapokelewe kama sehemu ya ushahidi na mimi nikuhoji sawasawa?
Shahidi wa kificho P6: Amenyamaza hasemi chochote, hapo haya ndo maelezo yangu na kama kuna kitu hakipo mimi ni binadamu siwezi kukumbuka kila kitu na kama kuna kitu nimekizungumza mahakamani siwezi kukumbuka kila kitu.
Mhe. Lissu: Shahidi Kaka yangu ungependa hayo maelezo yako yapokelewe kama kielelezo?
Shahidi wa kificho P6: Maelezo yangu niloyoyaandika Polisi au niliyozungumza hapa Mahakamani ndio nimetakiwa nizungumze mbele ya Mahakama.
Mhe. Lissu: wambie ungependa yawe sehemu ya ushahidi mahakamani.
Shahidi wa kificho P6: Maelezo yangu yawe ushahidi Mahakamani.
Hatimaye amekubali.
Majaji wanaandika sasa.
Huyu Shahidi amesumbua sana kuyakubali maelezo yake ili yapokelewe hapa Mahakamani.
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka?
Renatus Mkude anasema No Objection.
Jaji Nduguru: Basi maelezo haya yatakuwa ni D4.
Mhe. Lissu: Anasema ahsante sana, sasa anaendelea.
Kabla hujaapishwa hapa Mahakamani uliulizwa dini yako ukasema wewe ni Mkristo?
Shahidi wa kificho P6: Kweli
Mhe.Lissu: waeleze majaji kwenye hayo maelezo yako eneo la dini yako umeweka nini?
Shahidi wa kificho P6: Sijaona hapo.
Anasimama Katuga anaweka pingamizi watu wanamzomea.
Jaji anasema tuendelee
Shahidi wa kificho P6: Hapa Dini imeandikwa sioni vizuri.
Mhe. Lissu: Dini imeandikwa Muislamu?
Shahidi wa kificho P6: hapa sioni vizuri.
Mhe. Lissu: Umri wako je?
Shahidi wa kificho P6: Miaka 23 imeandikwa hapa.
Mhe. Lissu: Ulisema shughuli za Chama ulizopewa ni kuongoza misafara ya Chama ukiwa na bendera na pikipiki?
Shahidi wa kificho P6: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Sasa hayo maneno yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Maelezo yanaonesha nitashiriki kwenye mikutano ni vitu ambavyo sikuviandika.
Mhe. Lissu: Kwahiyo hayo yameandikwa au hayajaandikwa?
Shahidi wa kificho P6: Maelezo yameandikwa kushiriki mikutano.
Mhe. Lissu: We Chadema wa Mapolisi usitupotezee muda, tuambie yapo kama yapo.
Shahidi wa kificho P6: sijui
Mhe. Lissu: Tarehe 04/04 umesema ulikuwa na simu yako infinix smart 8 tuambie kama hayo yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: sifahamu.
Mhe. Lissu: Sijakuuliza unayafahamu au huyafahamu, nimekuuliza yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Part 172, itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 172
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa kificho P6.
Mhe. Lissu: Mhe. Jaji naomba shahidi ajibu maswali yangu.
Jaji: Hebu muulize tena.
Mhe. Lissu: Hayo maneno ya simu infinix smart 8 yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P6: sifahamu.
Jaji: Nafikiri lengo lako mshitakiwa ni ku empeach credibility ya shahidi kwahiyo akisema hafahamu wakati kielelezo kipo na sisi Mahakama tutakipitia. Basi acha aendelee kusema hafahamu.
Mhe. Lissu: Maneno kwamba ulikuwa na bando la kuingia youtube hebu tuoneshe kwenye maelezo yako hapo?
Shahidi wa kificho P6: Yapo.
Mhe. Lissu: Tuonyeshe.
Shahidi wa kificho P6: Majira ya saa nne niliona mtandao wa youtube hotuba ya Tundu Lissu.
Mhe. Lissu: Swali langu ni ulikuwa na bando la internet.
P6: Hayo hayapo.
Lissu: Kumbe una akili unaelewa. Tukienda hivi itakuwa vizuri. Haya tuendeleee.
Ulisema uliingia katika mtandao ya Jambo TV?
P6: Nilisema niliingia kwenye account.
Lissu: Hivyo hivyo account eheee yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Hayapo.
Mhe. Lissu: Umeeleza kwamba wakati nahutubia huo Mkutano nilisema maneno kwamba yeyote atakayekuwa nasi tutaenda nae na asiyetaka tutamuacha, yapo kwenye maelezo?
Shahidi wa kificho P6: Hayapo.
Mhe.Lissu: Ulisema nilisema kuwa kama kuna anayetaka kugombea udiwani asahau na anayetaka kugombea ubunge asahau, hayo nayo yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Polisi nilitoa ila hapa kwenye maandishi sioni.
Mhe. Lissu: Ahsante, Polisi ni waongo wamekuibia maneno yako, tuendelee.
Haya umesema nilisema maneno No Reforms, No Election, haya ni maneno yangu kweli nimeyasema sana.
Shahidi wa kificho P6: hayo sikusema. nilisema bila mabadiliko hakuna uchaguzi.
Mhe. Lissu: Basi twende na hayo hayo, yapo kwenye maelezo au hayapo?
Shahidi wa kificho P6: Hayo maneno siyaoni kwenye maelezo.
Mhe. Lissu: Turudi kwenye simu kwenye maelezo yako yote Polisi nataka uniambie ulisema kama ulikuwa na simu popote pale? Nataka unioneshe humo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: nilisema nimejiunga na magroup ya whatsapp kwahiyo maana yake ni simu.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama maneno ya bendera za taifa na Chadema yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Hayapo.
Mhe.Lissu: Kwamba nilivaa kombati za Kaki nayo pia yapo humo kwenye maelezo?
Shahidi wa kificho P6: Maelezo siyaoni.
Mhe. Lissu: Umemuelezea mtu anaitwa Essau Chiza pia anaitwa Mwamba wa Kigoma sasa tuoneshe Mwamba wa Kigoma kama yapo?
Shahidi wa kificho P6: Hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema Essau ni Katibu sehemu nyingine ni Mwenyekiti kipi ni kipi?
Shahidi wa kificho P6: Mimi sijasema hivyo.
Mhe. Lissu: Sasa wewe leta hayo maelezo nikuoneshe, anamsomea aliposema Mwenyekiti na aliposema ni Katibu.
Shahidi wa kificho P6: Mimi sikusema hivyo watakuwa mapolisi ndio walikosea.
Mhe. Lissu: Pole kwa kuingizwa chaka na mapolisi.
Shahidi wa kificho P6: Ahsante sana.
Watu wanacheka.πππ
Mhe. Lissu: Ulisema ulivyohamasika kufanya vurugu tuoneshe hizo habari nazo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: anasoma mambo tofauti kabisa.
Mhe. Lissu: Wewe ulihamasika kwamba utazuia uchaguzi kwa kukinukisha ndio nayataka yapo?
Shahidi wa kificho P6: Mimi binafsi maneno ya Mwenyekiti wa Chama yalinihamasisha na kupata moyo wa kijasiri na kunipa hamasa ya kuvuruga uchaguzi mkuu 2025 kwa kukinukisha.
Mhe. Lissu: Ohoo Hongera sana kumbe wewe na mimi letu lilikuwa moja ila Mwenzangu uko kizimba cha shahidi nashangaaa. Haya tuendelee lakini.
Part 173 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 173
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa kificho P6.
Mhe. Lissu: Pameandikwa tarehe 06/04 kutakuwa na ziara ya Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Songea, umeona vizuri hapo.
Shahidi wa kificho P6: Naweza kurudia pia wilaya ya songea anaisoma. π
Shahidi ni kama Futuhi kwakweli.
Mhe. Lissu: Twende Tarehe 10/04 umesema hivi ukiwa umekusanyika uwanja wa shule ya Msingi Matalawe na kuwataja viongozi ghafla gari ya polisi ilifika na kuwatawanya. Waeleze majaji kama hayo maneno gari la polisi lilifika na mkatawanywa.
Shahidi wa kificho P6: Hayapo hayo.
Mhe. Lissu: kuhusu kwenda ofisi za Chama Mfaranyaki mlikoenda na viongozi wakataka kuzungumza na waandishi wa Habari kuwa polisi walifika na kuwapiga mabomu?
Shahidi wa kificho P6: Kutupiga mabomu hayapo kwenye maelezo.
Mhe. Lissu: Je wapi kuna maneno kuwa polisi waliwatawanya ofisi za Chama.
Shahidi wa kificho P6: Hayapo kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu: Sasa ngoja nikuulize mengine baada ya kumaliza kukutembeza kwenye maelezo yako.
Mhe. Lissu: Kwa ufahamu wako Kiongozi wa Chama kama mimi kuitisha mkutano na kusema bila mabadiliko hakuna uchaguzi ni kosa la jinai?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu mimi.
Mhe. Lissu: Kusema tutazuia uchaguzi nalo ni kosa la jinai?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu pia.
Mhe. Lissu: unafahamu hakuna sheria yoyote nchi hii inayokataza kuzuia uchaguzi?
Shahidi wa kificho P6: Huko kwenye sheria mimi sifahamu.
Mhe. Lissu: Polisi hawakukwambia kuwa sio kosa? Hao waliokuwa wanakufundisha kuja kusema hapa.
Shahidi wa kificho P6: amenyamaza
Mhe. Lissu: Ulisema mikutano ya Songea ilizuiwa kufanya mikutano na kupigwa mabomu. Je hiyo ni sawa na ni haki ya kisheria kwa Chama?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Mhe. Lissu: unafahamu polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kukataza mikutano?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Unajua Mikutano hiyo ilitolewa taarifa siku mbili nyuma?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Kwani wewe si ndio umesema ulikuwa umehamasika na Chadema?
Shahidi wa kificho P6: Ndio hivyo sasa sifahamu.
Mhe. Lissu: Ulivaa tshirt imeandikwa No Reforms, No Election ni kosa?
Shahidi wa kificho P6: sifahamu.
Mhe. Lissu: Ulikamatwa Tar. 20/04/2025 mkiwa katika eneo la DS Kitimoto mkakamatwa kwa tuhuma za kufanya maandamano yasiyo ha hiari ni kweli?
Shahidi wa kificho P6: kweli
Mhe. Lissu: maelezo ya hayo mahojiano yako wapi?
Shahidi wa kificho P6: sifahamu.
Mhe. Lissu: Hizo tuhuma ziliishia wapi za kutaka kufanya maandamano na kuhojiwa?
Shahidi wa kificho P6: ndio tulipelekwa Mahakamani ila kaka angu alikuwa ananiwakilisha.
Mhe. Lissu: Kwahiyo Kaka yako alishtakiwa badala yako?
Shahidi wa kificho P6: ndio yeye alikuwa anaisimamia
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji ilikuwaje ukabadilika kuwa mtuhumiwa wa kupanga njama za kufanya maandamano na leo ukawa shahidi?
Shahidi wa kificho P6: Hata mimi sijui nini kilitokea.
Mhe. Lissu: Polisi walikwambia ukiwa shahidi kwenye kesi hii watakufutia mashitaka yako si ndio?
Shahidi wa kificho P6: Hapana Mheshimiwa we acha tu.
Mhe. Lissu: Wewe ni Mwanachama wa Chadema?
Shahidi wa kificho P6: Ndio.
Mhe. Lissu: Umeingia lini? Niambie tarehe na mwezi.
Katuga amesema hilo swali akijibu ataweza kujulikana maana kwenye mfumo wanajulikana watu waliosajiliwa ni akina nani siku fulani.
Majaji wamejadili kama dakika tano. Tunasubiri watasema nini?
Part 174 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 174
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Mhe. Jaji hawako serious hawa kwanza ukisoma D4 kila kitu chake kipo hata jina lake hawajaficha lipo na taarifa zake zote zipo, hawajielewi hawa.
Katuga: Anasimama anasema Mh. Sisi ni maafisa wa mahakama aonywe mshitakiwa kwanini anasema hatuko serious.
Mhe. Lissu: Mh. Jaji ni kweli hayupo serious ila nataka niliondoe neno hilo lakini kama anasema nionywe siko tayari kuonywa naomba nifanye submission ya kuonesha ni kwa namna gani hawako serious?
Jaji Ndunguru: Basi Mshitakiwa tuishie hapo kama umesema umeliondoa.
Watu wanacheka sana. πππ
Mhe. Lissu: je umesema kokote kuwa uliwahi kutishiwa maisha?
Shahidi wa kificho P6: Sijawahi kutishiwa maisha mimi.
Mhe. Lissu: Kuna mwanachadema au kiongozi amewahi kukutishia kukupiga au kukudhuru kwa wewe kwenda kutoa maelezo haya Polisi?
Shahidi wa kificho P6: Hayupo kabisa.
Mhe. Lissu: Je kuna ndugu yako ametishiwa pia?
Shahidi wa kificho P6: Hayupo hata mmoja.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji sina swali lingine kwa shahidi huyu.
Majaji wanaandika kidogo pale mbele.
Kwa sasa ni saa 7 na dakika 15 mchana, huu ni huwa ni muda wa kwenda Break, ngoja tusubiri Kitakachoendelea muda mfupi ujao.
Jaji: Re Examination Jamhuri?
Wakili Cathbert: Hatuna swali lolote Waheshimiwa Majaji.
Jaji Ndunguru Kiogozi wa Jopo la Majaji watatu anateta tena ma wenzake kabla hajasema nini kiendelee.
Anawasha kipaza sauti.
Shahidi umemaliza sasa unaweza kwenda.
Renatus Mkude tunaomba ahirisho tukawaandae mashahidi, lisaa limoja.
Mhe. Lissu: Sawa sina pingamizi.
Jaji Ndunguru: Basi tukutane baada ya lisaa limoja.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 175
Mahakama imerejea.
Anasimama Renatus Mkude na kusema tuko tayari kuendelea na tuko na shahidi wa wazi.
Muda huu tunaendelea na shahidi ambae ni H3923 Detective Coplo Michael, Mimi ni askari Polisi. Mimi ni Mristo.
Huyu Polisi mwingine ni shahidi ambae atakuwa ni PW6 Anaongozwa na Ignas Mwinuka, Wakili wa Serikali.
Shahidi ni mwemba mrefu kidogo, mweusi na amevaa miwani.
D. Koplo Michael anasema anaishi Kiusa Street, Moshi Kilimanjaro.
Ninafanya kazi Askari Polisi, naifanyia kazi yangu ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro, nimekuwa katika ofisi hiyo tangu mwaka 2015.
Nimejiunga Jeshi la Polisi mwaka 2012 na kuhitimu mwaka 2013, nilipata mafunzo ya awali katika shule ya Polisi Tanzania TPS kwa maana ya Shule ya Polisi iliyopo Moshi.
Majukumu yangu ni upelelezi wa makosa ya jinai, ukamataji wa wahalifu, kuzuia uhalifu pamoja na majukumu mengine mbalimbali ya jeshi la Polisi.
Tarehe 08/04/2025 nakumbuka majira ya asubuhi nilikuwa doria na askari wenzangu tulikuwa tunazungukia maeneo mbalimbali ya Moshi mjini.
Anaendelea Detective Koplo Michael anasema lengo ni kufanya doria, kukamata wahalifu na kulinda raia na mali zao.
Tukiwa tumefika maeneo ya Njoro hapo wilayani Moshi, tulipata taarifa za kiintelijensia kuwa kuna kijana mmoja anahamasisha wenzake kuhusiana na kufanyika na Uchaguzi Mkuu uliokuwa unatarajiwa kufanyika mwaka 2025.
Baada ya kupata hizo taarifa kutoka kwa P8 ambae analindwa na Mahakama, tulimkamata mtuhumiwa na kumpeleka ofisi ya RCO kilimanjaro.
Tukampeleka ACP Abichi alinielekeza nifungue jalada la uchunguzi na nilifungua jalada lenye Kumb. No. KR/CID/PE/18/2025 ambalo ni jalada la Uchunguzi.
Afande alisema kijana huyo apigiwe simu na ahojiwe na D. Koplo Rashid na awekwe mahabusu kwanza na atatoa maelekezo baadae.
Wakili Ignas Mwinuka, anaendelea kumuhoji.
D. Koplo Michael anasema kijana huyo alitolewa kwa masharti awe anaripoti kila jumatatu hapo Polisi.
Ilipofika Tarehe 22/04/2025 Afande RCO aliniambia nimtafute yule kijana anayekuja kuripoti, nimuandike maelezo upya.
Na hayo yalikuwa ni maelezo ya shahidi aeleze ni kitu gani kilichompelekea yeye kuhamasisha wenzake kufanya vurugu katika uchaguzi uliotarajiwa kufanyika.
Nilipofuatilia kumbukumbu nikagundua siku hiyo hiyo ndio alikuwa amepangiwa aje kuripoti, alipofika nilionana nae na nikamuandika maelezo ya shahidi.
Kwenye maelezo yake aliniambia yeye ni MwanaChadema alidai alikuwa Mwanachama toka akiwa anasoma Sekondari.
Alisema yeye ni mkereketwa wa Chadema na alikuwa anaunga mkono kauli ya Mwenyekiti wake wa Chama Tundu Lissu ndio maana alikuwa anahamasisha fuko na kukinukisha.
Alidhamiria kufanya uasi kwa serikali inayoongozwa na CCM na aliongeza kwa kusema kuwa Mwenyekiti wao alisema hawatakubali uchaguzi kufanyika.
Na wako tayari kukinukisha hadi Serikali watakapofanya marekebisho ya tume huru ya Uchaguzi pamoja na Katiba Mpya.
Baada ya kumuandika maelezo nilimpa ayasaini kila page na akakubali kuwa ni malezo yake.
Waheshimiwa Majaji kwa shahidi huyu ni hayo tu. Amemaliza Ignas Mwinuka.
Part 176 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 176
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa una maswali ya Dodoso?
Mhe. Lissu: Ninayo mengi sana.
Mhe: Lissu: Na Nyie ambao mna watoto mnawapeleka kuwa askari polisi mnawapeleka kwenda kutenda Dhambi za kusema uongo, mjue hivyo.
Mhe. Lissu: Sasa D. Koplo Michael unakumbuka ulitoa maelezo yako na unaweza kuyatambua ukiyaona?
Koplo Michael : Ndio naweza.
Anapatiwa maelezo yake hapa.
Koplo Michael : Haya maelezo ni ya tarehe 22/04 nimeyatambua yana sahihi yangu.
Mhe. Lissu: Naomba nikusomee maelezo yako na pia nitakuonesha maeneo ninayotaka ku impeach na baadae nitamuomba yapokelewe kama kielelezo.
Anaanza kumsomea hayo maelezo yake huyu afande Michael.
Mhe. Lissu: Je hayo yote niloyosoma ni maelezo yako.
Koplo Michael: Ndio ni yangu.
Mhe. Lissu: Sasa nakusomea maeneo ninayotaka kuku contradict ikiwemo kilichotokea tarehe 22/04, maneno aliyosema wakati unamuhoji, kuhusu wanataka kufanya uasi dhidi ya serikali ya CCM.
Anamsomea hayo maeneo amefika eneo la 10 kwa sasa.
Mhe. Lissu: Je uko tayari yapokelewe kuwa ushahidi Mahakamani?
Koplo Michael: Maelezo haya niliandika kwa kifupi tu.
Mhe. Lissu: Wewe Polisi jibu swali langu usilete Story za Line Polisi hapa. Uko tayari yapokelewe? Jibu ndio au hapana?
Koplo Michael: Kama Jamhuri wataridhia sina pingamizi.
Jaji Ndunguru: Yatakuwa ni D5. Yaani ushahidi wa utetezi namba 5.
Mhe. Lissu: Naomba apewe D5.
Anapatiwa hapa.
Mhe. Lissu: Kwamba ni askari Polisi toka mwaka 2015 yapo kwenye maelezo yako?
Koplo Michael: huo mwaka hakuna kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu: Ulijiunga 2012 na 2013 ukafuzu jeshi la polisi
Koplo Michael: Sikuyaandika hayo.
Mhe.Lissu: Sema kwa sauti we polisi.
Koplo Michael: Nimesema kwa sauti mbona.
Ana kasauti fulani hivi kidogodogo amevaa miwani macho ni mekundu sana.
Mhe. Lissu: Kuhusu Shule ya Polisi Tanzania iliyopo Moshi
Koplo Michael : Hayo hayapo kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu: Hivi kwanini hujibu ki askari? Nataka ujibu kama askari.
Koplo Michael: Anachekacheka kama anataka kulia.
Mhe. Lissu: Tarehe 08/04/2025 ulimpeleka ofisi ya RCO na kukuelekeza ufungue faili la Uchunguzi. Ulisema ahojiwe na awekwe mahabusu hadi mtakapopata maelekezo mengine? Yapo kwenye maelezo
Koplo Michael: maneno kuwa awekwe mahabusu hadi yatakapotolewa maelekezo mengine sikuliandika.
Mhe. Lissu: Ulisema sharti la mtuhumiwa kuripoti kila jumatatu. Yapo hayo kwenye maelezo yako?
Koplo Michael: Hakuna.
Mhe. Lissu: kuhusu kumtafuta P8 na kumuhoji maelezo kama shahidi.
Koplo Michael: Kuna mambo hayapo hapo.
Mhe. Lissu: Hivi ulisema alikuwa anaripoti jumatatu?
Koplo Michael: ndio.
Mhe.Lissu: Tarehe 22 ilikuwa jumangapi?
Koplo Michael: Ilikuwa jumanne lakini alikuja kuripoti jumanne kwasbaabu
Mhe. Lissu: Hiyo kwasababu mpelekeee RCO wako Kule Kilimanjaro mimi jibu langu limetosha kuwa ilikuwa jumanne.
Mhe. Lissu: maelezo ya kuunga mkono kauli ya Chama uliandika?
Koplo Michael: Sikuandika lakini
Mhe. Lissu: Nimekwambia lakini zako utawaeleza waandishi wa habari baadae au mapolisi wenzako sio hapa.
Watu wanacheka. ππππ
Mhe. Lissu: Wewe askari mimi nimefundishwa kukamata waongo.
Koplo Michael : Mimi pia ni mtaalamu mheshimiwa.
Mhe. Lissu: Wewe sio mtaalamu wa Chochote ndio maana ni Koplo wa polisi. Ungekuwa mtaalamu usingekuwa Koplo.
Kicheko kidogo kwa mashabiki hapa, lakini tunaendelea.πππ
Mhe. Lissu: hivi umeeleza sababu ya maelezo yako polisi na uliyosema mahakamani.
Koplo Michael: Sijaeleza sababu kwasababu hakuna utofauti.
Mhe. Lissu: Unasema ulimkamata P8 na kumpeleka kituoni. Halafu RCO akakwambia ufungue shauri.
Koplo Michael: hata sikuelewi yani.
Mhe. Lissu: kwahiyo ulimkamata ukiwa tayari una faili la Uchunguzi?
Koplo Michael: Sio kweli nilifungua baada ya kuwa nimeshamkamata.
Mhe. Lissu: Kupanga kufanya vurugu ni kosa?
Koplo Michael: Sahihi.
Part 177 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 177
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Koplo Michael.
Mhe. Lissu: Kwahiyi P8 alikuwa amefanya kosa?
Koplo Michael: ni kweli alikuwa amefanya makosa
Mhe. Lissu: Kwahiyo maelezo yake hayapo?
Koplo Michael: Sijayaleta
Mhe. Lissu: Je mlifungua kesi?
Koplo Michael: Hatukufungua kesi.
Mhe. Lissu: hadi leo hamjafungua?
Koplo Michael: Sijui kwakweli.
Lissu: RCO ndio alikwambia chukua maelezo ya shahidi kwenye kesi ya Lissu.
Shahidi: Hapana sio hivyo.
Mhe. Lissu: anamsomea alipoandika kuwa shahidi kwenye kesi ya lissu.
Koplo Michael: Ni kweli nilisema kumbe.
Mhe. Lissu: Kwahiyo mlikuwa mnaandaa kesi ya Lissu?
Koplo Michael: Sio kweli.
Mhe. Lissu: Kwahiyo mlikuwa mnaandaa nini?
Koplo Michael: Ushahidi wa kesi.
Mhe. Lissu: Kesi gani?
Koplo Michael: hii ya kwako.
Mhe. Lissu: Kumbe ni yangu umebana umeachia.
Watu; ππππ
Sasa tuendelee na swali lingine.
Mhe. Lissu: Nilitishia Serikali kwasababu nilisema tutazuia Uchaguzi, wambie Majaji ni wapi umesema neno lolote juu ya maneno niliyosema?
Koplo Michael : mimi nilisema aliyoniambia shahidi.
Mhe. Lissu: Umeelewa swali we polisi?
Koplo Michael: Hapana sijasema lolote kuhusu maneno gani ulisema.
Mhe. Lissu: naambiwa nilichapisha maneno mitandaoni sasa sema kama kwenye kielelezo D5 kama ulisema chochote kuhusu maneno yangu niliyochapisha.
Koplo Michael: Hapana sikuandika lolote kwenye hayo.
Mhe. Lissu: Kutaka mabadiliko ya Katiba, Tume Huru ya Uchaguzi ni kosa la jinai?
Koplo Michael: Sio kosa la jinai.
Mhe. Lissu: Kuhamasisha wananchi nchi nzima kupatikana Katiba Mpya na kuzuia uchaguzi ni kosa?
Koplo Michael: ni kosa
Mhe. Lissu: Kosa gani?
Koplo Michael: Mimi sio mtaalamu wa sheria, wanasheria watasema.
Mhe. Lissu: Huna unalojua wewe ni Koplo tu, umetaja Katiba tutajie ibara sasa?
Koplo Michael: Sijui kosa ambalo umeshitakiwa nalo.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa sina swali lingine kwa shahidi huyu.
Jaji Ndunguru: Re Examination.
Ignas Anasimama anasema nina maswali mawili.
Je uliposema hakuna utofauti ulimaanisha nini?
Koplo Michael: Nilimaanisha hakuna tu tofauti maana ni ile ile.
Wakili wa Serikali: Je ulisema hujui anashitakiwa na kosa gani? Ulimaanisha nini?
Koplo Michael: Najua ni uhaini lakini uhaini ni mpana unajumuisha uchochezi na kuharibu mali.
Wakili wa Serikali ni hayo tu Mheshimiwa.
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka mnasemaje?
Renatus Mkude: Tunaomba tuendelee Jumatatu.
Jaji Ndunguru: Kwanini msiendelee na shahidi mwingine atakapoishia ikifika saa 11 tunaacha.
Mkude: Mh. Jaji naomba tuendelee jumatatu tafadhali muda umeenda.
Jaji: Basi jumatatu saa tatu kamili asubuhi tukutane.
Inapigwaa Courttttttt tunatoka.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 16, 2026
Jana tuliishia Part 177 so leo tunaendelea na-;
Part 178.
Majaji wanaingia wakati huo sauti ya Courtttt imepigwa kwa sauti kubwa.
Kelele za Rais Rais Rais kama ilivyo ada pia zinapigwa zikianzia kule juu.
Mh. Lissu amepiga Tshirt yake ya No Reforms, No Election.
Majaji wanaandika kidogo.
Kama kawaida Mawakili wa Serikali wapo karibia 10 siku zote huwa wanajitahidi kuwa wengi sana. π
Mhe. Lissu pia anateta kwa mbali na vijana wake pale wapo Mawakili Ikoti Lissu, Deogratias Mahinyila, Michael Lugina na Sisty Aloyce.
Anasimama Renatus Mkude anawatambulisha wenzake na kusema wana mashahidi wawili wanaolindwa na wako tayari.
Shahidi amesubiriwa kwa muda mrefu sana.
Jaji anauliza mmeenda kumatafutia wapi?
Yupo Mheshimiwa anajibiwa.
Jaji huyo shahidi ni nani?
Renatus mkude: Ni P2 huyu.
Jaji: Shahidi una miaka mingapi?
Shahidi wa kificho P2: 38
Jaji: Dini yako?
Shahidi wa kificho P2: Mkristu.
Shahidi wa kificho P2 amefika na anajibu hivyo.
Jaji: Haya tuendelee. Muapisheni.
Anasimama Renatus Mkude anasema huyu Shahidi ataongozwa na Wakili Ignas Mwinuka.
Anasimama Ignas kuendelea.
Ignas Wakili wa Serikali: Shahidi nitakuuliza maswali na hutakiwi kutoa utambulisho wako.
Unaitwa nani?
Shahidi wa kificho P2: Mimi naitwa P2 mkazi wa matalawe, Songea Ruvuma.
Wakili: Kazi gani unafanya?
Shahidi wa kificho P2: Mimi ni fundi umeme.
Wakili: Wewe ni mfuasi wa Chama gani?
Shahidi wa kificho P2: mimi ni mfuasi wa Chadema toka 2021.
Wakili Ignas: unajishughulishaje ukiwa mfuasi wa Chama hicho?
Shahidi wa kificho P2: Huwa najishughulisha na mikutano na kulipa michango.
Wakili: tukumbushe tar. 04/04/2025 ulikuwa wapi?
Shahidi wa kificho P2: Nilikuwa manispaa ya songea kwenye shughuli zangu, nakumbuka nikiwa napitia mitandao ya kijamii nilikutana na ujumbe wa Antipass Tundu Lissu akiwa katika mkutano na wanahabari.
Wakili: Mtandao gani:
Shahidi wa kificho P2: Youtube nilikuaa naangalia.
Wakili: ukabaini nini?
Shahidi wa kificho P2: Nilikutana na ujumbe wa mwenyekiti wa Chama akisema hakutakuwa na uchaguzi, wanaotaka kugombea wasahau mwaka huu. Alisisitiza namna ya kuzuia uchaguzi ni njia ya kuleta mabadiliko na alihamasisha kila mmoja awe jasiri.
Wakili: ulifanya nini wewe?
Shahidi wa kificho P2: Nilivyopata ujumbe huo nikapata hamasa na kuanza kuwatafuta viongozi walioko songea ili tujue linatekelezeka vipi hilo.
Wakili: Kingine kilichoendelea?
Shahidi wa kificho P2: Nilimtafuta Essau Said Mwenyekiti wa Vijana Songea kwa ufafanuzi zaidi.
Alinielekeza atafanya mawasiliano na viongozi wengine na ilipofika tarehe 07/04/2025 kwahiyo alituambia tutoe michango ya hiari na mimi nilichangia elfu 10 hiyo michango ya hiari inaitwa Tonetone.
Wakili: Mwendelezo wa ziara ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa?
Shahidi wa kificho P2: Niliendelea na shughuli zangu nikawa nasubiri tarehe 10/04/2025 ambayo itakuwa ndio siku ya Mkutano na tuliambiwa hivyo sisi.
Tarehe 09/04 nilipata taarifa kuwa amekamatwa Mwenyekiti Lissu na kwa vile siku na taarifa za kutosha.
Wakili: Ikawaje?
Shahidi wa kificho P2: Nilijiandaa tar. 10/04 ile asubuhi ili niende kwenye mkutano na kupata ufafanuzi wa nini kimeendelea hadi Mwenyekiti kukamatwa.
Nilipofika mjini nikakutana na polisi wengi na wakawa wanatuambia hakuna mkutano siku hiyo.
Wakili: Ikawaje?
Shahidi wa kificho P2: Nikaona nielekee ofisi za Chama maana tuliambiwa Makamu Mwenyekiti wa Chama atakuwa anazungumza na wanachama pale Ofisini.
Wakili: Makamu Mwenyekiti anaitwa nani?
Shahidi wa kificho P2: John Heche.
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P2: Tukiwa pale Ofisi za Chama wakati tunasubiri Mh. Heche azungumze wakaja polisi na mimi nilikamatwa katika tukio hilo na kupelekwa kituo cha Polisi.
Part 178 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 178
Wakili wa Serikali anaendelea kumuongoza Shahidi wa kificho ambae kapewa jina la P2
Wakili: Nini kiliendelea kituoni?
Shahidi wa kificho P2: Niliwekwa mahabusu na baadae nikahojiwa kwa tuhuma za kufanya fujo na uchochezi.
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P2: Waliniachia kwa Dhamana na nilitakiwa kuwa naripoti kila jumatatu.
Tarehe 14/04 niliripoti na tare21/04 nilipaswa kuripoti tena, I kawa sikukuu nikarudi tarehe 22/04 ambapo nilipofika nikapelekwa Central kuchukuliwa maelezo kwa mara ya pili.
Wakili: Maelezo gani?
Shahidi wa kificho P2: Akaniambia nieleze Mwanzo mwisho hadi nilipokamatwa. Nikamueleza kuwa mimi ni mwanaChama na akayachukua hayo maelezo afande Juma Batazary.
Wakili: Mh. Tundu Lissu umemtaja sana unamfahamuje?
Shahidi wa kificho P2: Nikiwa Songea nimemfahamu Mh. Tundu Lissu anafahamika karibu na kila mtu toka akiwa Bungeni na alikuwa Makamu Mwenyekiti na baadae akawa Mwenyekiti.
Wakili: huo uchaguzi ungezuiwaje? Kwa mujibu wa Lissu.
Shahidi wa kificho P2: Sijui ungezuiwaje lakini yeye alisema kwa uasi, Mwenyekiti wa Chama alikuwa anakuja Ruvuma na tukajua angekuja kutupatia mbinu hizo maana alisema wanaotaka kwenda nae ataenda nao na mimi nilikuwa kwenye kundi hilo.
Jaji: Shahidi unaongea mfululizo, hatujui unaelekea wapi wala unaongea nini? Sasa Wakili muongozeni shahidi tujue ameanzia wapi na anaelekea wapi?
Wakili: Ulikuwa unajua uchaguzi utazuiwaje?
Shahidi wa kificho P2: Nilikuwa sijui. π
Wakili: Kwa shahidi huyu ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.
Jaji Ndunguru: Wakili unasema nini nini sikuelewi.
Wakili Ignas: Mh. Jaji nimesema ni hayo kwa shahidi huyu.
Jaji Ndunguru ohoo kumbe mmemaliza. Haya sawa.
Watu wanacheka sana πππ
Jaji: Naombeni utulivu tafadhali.
Majaji wanaandika kidogo na wanasema maswali ya Dodoso tafadhali Mshitakiwa. Anasimana Lissu.
Mhe.Lissu: Shahidi unanisikia sawasawa?
Shahidi wa kificho P2: Sikusikiii.
Jaji: humsikii kweli?
Shahidi wa kificho P2: Namsikia Jaji.
Mhe.Lissu: Habari ya Matarawe?
Shahidi wa kificho P2: Nzuri tu.
Mhe. Lissu: Uliandika maelezo Polis?
Shahidi wa kificho P2: Ndio
Mhe.Lissu: Ndio haya tar. 24/04?
Shahidi wa kificho P2: Ndio nilisaini pia.
Mhe. Lissu. Mh. Jaji naomba shahidi aonyeshwe maelezo yake ya Polisi hayo ya tarehe 24/04.
Hayo maelezo ni ya kwako?
Shahidi wa kificho P2: Ni maelezo yangu ndio.
Mhe. Lissu: Uzuri umesema mwenyewe kuwa ni mfuasi wangu sasa nikikuuliza jibu haraka ndio au hapana ili tuendelee. Sawa Bwana mkubwa?
Shahidi wa kificho P2: sawa
Mhe. Lissu: Naomba nimsomeee maelezo yake haya.
Anaanza kumsomea hapa.
Anamsomea maelezo yake hapa anasema mimi ni mwanaChama wa Chadema sina kadi lakini pia nilikuwa mfuasi wa Mh. Lissu hata kipindi anagombea uwenyekiti wa Chama, hapa songea niko chini ya kiongozi wa Vijana Essau.
Nimeshiriki pia kuchangisha pesa za Tonetone nikishirikiana na kiongozi wa vijana na pia mimi nimechangia Elfu 10 kutokana na hali yangu ya kiuchumi. Ziara hiyo atakuwepo Gobless Lema, Makamu Mwenyekiti, Twaha Mwaipaya.
Baadae nilipata taarifa Mh. Lissu amekamatwa na nilipomuuliza Essau Chiza nikaambiwa taarifa Rasmi nitapewa kwenye mkutano, nilipofika ofisini niliwakuta viongozi na baadae nikakamatwa.
Leo nimekuja kuripoti nikaletwa kwako na wewe unasema unataka kunihoji.
Amemaliza kumsomea maelezo yake.
Mhe. Lissu: Niliyosoma ndio maelezo yako?
Shahidi wa kificho P2: Yes ni yenyewe na yako sahihi.
Mhe. Lissu: nakuonyesha maeneo ya kukukanusha: yafuatayo:
1. Tarehe 04/04/2025 uliona mkutano wa Lissu na waandishi wa Habari.
2. Video ya mkutano inasema Mwenyekiti alisema hakutakuwa na Uchaguzi na wanaotaka kugombea wasahau.
3. Uliposema unamfahamuje Mh. Lissu.
Anamsomea maeneo kadhaaa hapa. Ambayo atamuuliza maswali.
Mhe. Lissu: Je ungependa maelezo yako yawasilishwe Mahakamani kama ushahiidi?
Shahidi wa kificho P2: Yawasilishwe tu
Part 179 itaendea kwny post inayofuata,
Naomba repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 179
Mhe. Lissu anaendelea na maswali ya dodoso
Jaji Ndunguru: Vipi Jamhuri?
Renatus Mkude: Hatuna pingamizi.
Jaji Ndunguru: Hiyo itakuwa ni D6.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji naomba shahidi apewe D6.
Mhe. Lissu: Shahidi umesema kwamba Tarehe 22/04 ulipelekwa Central Polisi Songea kwenda kuchukuliwa maelezo haya?
Shahidi wa kificho P2: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Sasa angalia hayo maelezo yako na uwaeleze majaji kuwa umesema chochote kuhusu hiyo tarehe?
Mhe. Lissu: Shahidi kuna mahali kokote?
Shahidi wa kificho P2: sijazungumzia chochote isipokuwa saini.
Mhe. Lissu: Kwahiyo hayapo?
Shahidi wa kificho P2: yapo.
Mhe. Lissu: Kuna tarehe 22/04 kokote.
Shahidi wa kificho P2: Haipo hiyo.
Mhe. Lissu: Kuna mahali umetaja Central Polisi Station Songea? Kituo Kikuu cha Polisi.
Shahidi wa kificho P2: sijakitaja.
Mhe. Lissu: Ulisema unamfahamu Lissu kwasababu ni mwanasiasa maarufu na anafahamika na kila mtu. Si ni kweli?
Shahidi wa kificho P2: Ni kweli
Mhe. Lissu: Uliyasema Polisi hayo?
Shahidi wa kificho P2: sijayasema.
Mhe. Lissu: Tar. 04/04/2025 hayo maelezo kuwa uliangalia youtube yapo?
Shahidi wa kificho P2: yapo
Mhe. Lissu: Wafuasi wangu huwa wana akili sasa unaanza kunitia wasiwasi yapo hayapo?
Shahidi wa kificho P2: Hayapo kiukweli.
Mhe. Lissu: wafuasi wa Chadema wana alama usoni?
Shahidi wa kificho P2: Sijui
Mhe. Lissu: Una kadi?
Shahidi wa kificho P2: Sina.
Mhe. Lissu: Majaji watajuaje?
Shahidi wa kificho P2: Sijui
Mhe. Lissu: Tutajuaje wewe kama sio Chawa wa Mama?
Shahidi wa kificho P2: Sijui
Watu wanacheka.πππ
Mhe. Lissu: unajua utaratibu wa kulipia michango ya Chama.
Shahidi wa kificho P2: Sijui.
Mhe. Lissu. Ulimlipa nani hiyo hela?
Shahidi wa kificho P2: Mwamba wa Kigoma Essau Chiza.
Mhe. Lissu: Ushahidi wowote umeleta?
Shahidi wa kificho P2: Hapana.
Mhe. Lissu: Umesema kuhusu video. Je umewaonyesha hiyo video?
Shahidi wa kificho P2: Hapana.
Mhe. Lissu: Umewasilisha hiyo video kama kielelezo.
Shahidi wa kificho P2: Sijui
Mhe. Lissu: Ulisema ulikamatiwa eneo la Ofisi za Chama Mfaranyaki Songea?
Shahidi wa kificho P2: Kweli
Mhe. Lissu: Ulienda Mfaranyaki kupata ufafanuzi?
Shahidi wa kificho P2: Ni kweli
Mhe. Lissu: Sasa kwenda kutafuta ufafanuzi wa kwanini Mwenyekiti amekamatwa ni kosa?
Shahidi wa kificho P2: Sijui sheria.
Mhe. Lissu: Hata kwa akili ya Kujiongeza tu. Ni kosa hilo?
Shahidi wa kificho P2: Sijui
Mhe. Lissu: Wewe huwa unamfuatilia Lissu kwenye nini kama hujui vitu namna hii maana nimekwambia wafuasi wangu wana akili.
Shahidi wa kificho P2: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Mkutano huo wa tarehe 10 unajua ulikuwa umetolewa taarifa Polisi?
Shahidi wa kificho P2: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Ulihojiwa kwa tuhuma za uchochezi?
Shahidi wa kificho P2: Ndio.
Mhe. Lissu: wewe ulienda kufanya uchochezi ofisi za Chama?
Shahidi wa kificho P2: Ndio
Mhe. Lissu: kwahiyo ulikamatwa ukiwa hujafanya kosa lolote?
Shahidi wa kificho P2: Sijui.
Watu wanacheka.πππ
Mhe. Lissu: Kwahiyo ulisema ulichukuliwa maelezo ya Uchochezi?
Shahidi wa kificho P2: Ndio.
Mhe. Lissu: Yako wapi hayo maelezo?
Shahidi wa kificho P2: Sijui.
Mhe. Lissu: Je ulifunguliwa kesi ya Uchochezi au kesi yoyote?
Shahidi wa kificho P2: Sikufunguliwa kesi yangu iliishia tarehe 22/04
Mhe. Lissu: Mkutano wangu wa Tarehe
03/04 wewe ulikuwa kwenye huo mkutano wangu?
Shahidi wa kificho P2: Sikuwepo.
Mhe. Lissu: Umekuja kufanya nini sasa?
Shahidi wa kificho P2: Kusema nilichoona tu.
Part 180 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.