Mwenye uhitataji wakiwanja kwa matumizi yoyote uwekezaji, iwe makazi afike hili eneo atapapenda hasa kwa mtu anayeweza kujenga shule eneo lina uhaba wa shule wanafunzi wanatembea zaidi ya kilometa 10 kwenda shule kibiashara pia ni pazuri kuishi ndo usiseme namba:0744965608
@Jambotv_ Bob Marley ashawahi kusema ukiwa politics huwezi kumjua mungu! Kwa sababu mwanasiasa anaamini siasa inaweza kufanya chochote lakini biblia inaamini mungu ndo kila kitu very huge difference!!
A Tanzanian mother saw her son in this scene from our investigation.
She has not been able to find him since 29th October and doesn't know if he's alive or dead
IWE KIFUNGO AU KIFO.
1.Msimamo wangu kuhusu Muungano uko Bayana. Tuwe na Serikali Moja au la Tuwe na Serikali Tatu.Hatuwezi kuwa na Muungano ambao Taifa moja linabaki na mambo yake yote halafu mambo yote ya Taifa lingine yanageuzwa kuwa ndiyo mambo ya Muungano .Kama hatuwezi kuwa na Serikali Moja kama ilivyokuwa kusudio la awali la waasisi wa Muungano lazima tuwe na serikali tatu.Tanganyika,Zanzibar na Mungano.Tuache hoja za kipropaganda kwenye mambo serious.
2.Msimao wangu kwamba kila raia ana haki ya kuwa na maoni huru na kuwa na mtazamo huru au kushawishi mtizamo wake ukubalike na kwamba kufanya hivyo siyo Uhalifu wala uhaini.Kufanya Maandamano,Midahalo au Maongezi kuhusu hali fulani ya kiutawala,demokrasia,sheria au uwajibikaji siyo uhalifu na watu wote wanao kamatwa na kushtakiwa kwa makosa makubwa wana haki ya kuwakilishwa na wakili mwenye uzoefu na Wakili kuwawakilisha watu wa namna hii anakuwa hajafanya kosa lolote.
3.Uchaguzi wa Tarehe 29 Oktoba hauna sifa ya kuwa uchaguzi huru na Wazi na haukukidhi vigezo vya kuitwa Uchaguzi huru na Haki.Rejea Ripoti za wasimamizi wa Uchaguzi SADC,AU na wengine.Ukitawaliwa na vificho,mauwaji,kuwekwa kizuizini kwa chama kikuu cha Upinzani na kuzuiwa kushiriki uchaguzi, uchaguzi kufanyika gizani na Kukosekana kwa Tume Huru ya Uchaguzi.
4.Namna ya Kutoka hapa tulipo ni kuhakikisha kusitishwa mara moja kwa ukamataji hovyo wa vijana na kuwabambikia kesi,Kufutwa kwa kesi zote za uwongo dhidi ya chama kikuu cha Upinzani na uwepo wa Tume huru ya Kiuchunguzi ya Kimataifa ambayo Ichunguze Mauwaji na upotezwaji wa watu kuanzia kabla,wakati na baada ya Uchaguzi na iangazie uhalisia wa Takwimu za uchaguzi na matokeo yake. Na ndiyo ije na mapendekezo ya hatua za kuchukua.
5. SERIKALI itoke hadharani Ikiri kwamba yenyewe ndiyo chanzo cha kusababisha Vijana waandamane kwa ujeuri wa viongozi wake na kutopenda kusikiliza ushauri na kwamba vijana wale hawakuwa na njia nyingine ya kueleza hisia zao kwani Mahakama ilikwisha onekana kutokuwa sehemu sahihi kitoka na aina ya utitiri wa Maamuzi hususan kupotzwa kwa watu na Bunge lilikataa kata kata kujadili matatizo ya wananchi na kujigeuza kikaragosi cha serikali na hawakuwa na njia nyingine isipokuwa hiyo na kuwa kwa Makusudi au Uzembe iliruhusu vyombo vyake vya ulinzi kutumia sila za moto dhidi ya waandamanaji na wasio waandamanaji na kuuwa wananchi hata wale ambao hawakuwepo kabisa katika maandamano ikiwemo watoti wadogo na akina mama walioshambuliwa katika nyumba zao.
6.Wahanga wote na Familia zilizoathirika serikali iwajibike kuonesha wapi waliko waliotekwa na kupotezwa na pia ioneshe miili ya wale wote waliouwawa katika sakata la Oktoba 29 na kuhakikisha kuwa wale waliohusika kutekekeza mauaji haya wote wanachukuliwa hatua za kisheria.
7. Msimamo wangu kuhusu sakata linalohusiana na uchaguzi ni kwamba Taifa linahitaji UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI.Baada ya hapo ndipo tuone namna bora ya kuwa na uongozi jumuishi unaowasilisha ridhaa ya wananchi kwani hawa waliopo sasa japo dejure ni viongozi de facto wanakosa uhalali wa Kijamii kupitia mazingira ya namna zoezi la uchaguzi lilivyo endeshwa.
8.Kwamba Maandamano ya Gen.Z kupinga dhuluma za kidemokrasia siyo uhalifu ...bali ni matokeo ya ukaidi na kutopenda mashauriano kwa baadhi ya viongozi wajuu wa serikali jambo linalopelekea vijana kukata tamaa na kukosa matumaini. Tusipo jifunza kutatua mambo yetu kwa kuzungumza asili itatufunza kutatatua mambo hayo hayo kwa kupigana.
TUSIWINDWE ILI KUUWAWA AU KUBAMBIKWA KESI KWASABABU YA MISIMAMO YETU ..HOJA HAZIPIGWI RUNGU.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 147
Anaendelea Mhe. Lissu
Waheshimiwa Majaji,
Hoja yangu ya pili ni kwamba, huyo shahidi ni shahidi wa namna gani?
Kwa mujibu wa kanuni ya 3 lazima awe yuko chini ya amri ya ulinzi.
Sasa Mahakama hii inawezaje kujua shahidi kama yuko chini ya amri ya ulinzi?
Naomba kuwarejesha kwenye Kanuni ya 5(1) ambayo inasema mtu huyo lazima awe amebainishwa katika maombi.
Maana ya haya maneno ni nini?
Maana yake rahisi ni kwamba mtu ambaye jina lake lilipelekwa kwa jaji likaombewa ulinzi.
Jaji awe anamfahamu kwa jina na kuwa maisha yake yako hatarini.
Naomba niwarejeshe kwenye hati ya maombi ya tarehe 14 Julai 2025, hiyo application ina viapo viwili, ina kiapo cha SSA Mose Kaima na ACP Amini Mahamba.
Waheshimiwa majaji kwenye hiyo hati ya maombi, hivyo viapo viwili hakuna kiapo hata kimoja chenye jina la shahidi hata mmoja.
Katika orodha ya mashahidi wanaoitwa wamepewa ulinzi, hakuna hata jina moja la shahidi ambalo lilipelekwa kwa Jaji Mtembwa.
Hiyo amri ilitolewa on insufficient ground na ilitolewa kwa concealment (kwa kuficha Ushahidi kwa mahakama) na mawakili wa serikali.
Walipaswa kupeleka majina kwa jaji lakini hawakufanya hivyo, hivyo Jaji Mtembwa hawafahamu na nyie waheshimiwa majaji hamuwafahamu, wanajulikana tu na waliowaleta, hivyo sitaki kusema kuwa amri ya ulinzi ilipatikana kwa fraud but by concealment by the State Attorneys.
Waheshimiwa majaji kama hiyo ni haki then tunahitaji tafsiri mpya ya haki huku Duniani.
Waheshimiwa majaji sio tu kuwa hakuna majina ya mashahidi ila hakuna hata majina ya wanaowatishia ni maneno tu, maneno matupu kabisa.
Hata nature ya vitisho haijaelezwa kwamba wanatishiwaje, kivipi na nani anawatisha? Haipo kabisa.
Waheshimiwa majaji, sasa niende kwenye hoja yangu ya tatu ambayo ni kuhusu amri ya Mahakama Kuu;
Mahakama kuu ilitoa ulinzi upi? Ili kujibu hilo swali sawasawa naomba nitangulize kanuni ya 7(1) ya Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi.
Kanuni inasema kwamba hatua za ulinzi wa shahidi zitadumu kwa kipindi cha usikilizwaji wa kesi isipokuwa kama amri husika itaashiria vinginevyo.
Kwenye uamuzi wa Jaji Mtembwa maombi ya Jamhuri yalikuwa kutokuonyesha utambulisho wa mashahidi wanaotarajiwa kwa kutokuweka wazi nyaraka zinazoweza kupelekea shahidi kujulikana, matumizi ya majina bandia, amri nyingine yoyote kwaajili ya usalama wa mashahidi wa Jamhuri wakati wa mwenendo wa ukabidhi au wakati wa kesi kusikilizwa.
Naomba waheshimiwa majaji pia muangalie kanuni ya 6(1) ili muone ni maombi gani mengine ambayo kama upande wa mashtaka wangetaka wangeyaomba.
Kanuni hii imetaja orodha ya amri zinazoweza kuombwa na kutolewa na mahakama. Zimeelezwa kwa uwazi kabisa kwenye kanuni husika hii itatusaidia kuelewa ninachotaka kukisema.
Waheshimiwa majaji, katika kanuni hiyo ya 6 kuna amri 16 ambazo zinaweza kuombwa na hiyo ya kutumia kizimba maalumu hawakuomba mawakili wa serikali.
Katika dunia hii waheshimiwa majaji, usipoomba hupewi, hili sio takwa la kisheria tu ni takwa pia la kibiblia kuwa ombeni nanyi mtapewa.
Jamhuri walipewa amri nne walizoomba lakini amri ya kutumia kizimba maalum hawakuomba, hivyo hawawezi kupewa kitu ambacho hawakuomba katika lugha ya kisheria, they are estopped.
Waheshimiwa majaji kwa maoni yangu kanuni hizi zilitungwa kuwafurahisha waendesha mashtaka na watu wao. They are totally one sided.
Waheshimiwa majaji kwa mujibu pia wa kanuni ya 8 kama Jamhuri wangeona amri za Jaji Mtembwa haikulinda mashahidi sawa sawa walikuwa na fursa ya kuleta maombi mbele yenu kwa mfano kuwa tunaomba kutumia kizimba maalum, hawajaleta maombi hayo.
Now it is late in the day to sneek in today kuleta hao mashahidi. Wameleta wakijua kanuni hizi hamtazisoma au mshtakiwa atanyamaza. Wamelalia haki yao, waachwe waendelee kuilalia.
Part 148 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
@HildaNewton21 Kesi ishakuwa ngumu haya mashambilizi ni hatari Kwa kifupi lissu ameizidi akili hadi AI sio kwa hoja hizii hata majaji wanashangaa hata mimi nashangaa kwamba lissu naye anaongozwa Rais Samia me nadhani akili kama hii inahitajika sana pale ikulu.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 148
Anaendelea Mhe. Lissu
Hoja yangu ya nne Waheshimiwa Majaji ipo kwenye kanuni ya 6(2) ambapo Mahakama inaweza kutoa amri bila kuathiri haki ya kusikilizwa kwa usawa.
Waheshimiwa majaji naomba hiyo kanuni isomwe pamoja na kanuni ya 5(2)(f) ambayo inasisitiza kutohatarisha maslahi ya haki na kuhakikisha kwamba kuna effective cross examination.
Waheshimiwa Majaji naomba mtafakari hayo maneno ya mahitaji ya fair trial, kutohatarisha maslahi ya haki na kuhakikisha kuna effective cross examination.
Waheshimiwa majaji kwenye kesi ambayo adhabu yake ni kifo, shahidi akatoa Ushahidi ambaye Mahakama haimfahamu, mshtakiwa hamfahamu isipokuwa tu mawakili wa serikali.
Shahidi akitoa Ushahidi bila mahakama kumuona, majaji hawamfahamu, mtuhumiwa atafanyaje effective cross examination? Shahidi asiyejulikana na Mahakama, haonekani kwa mtuhumiwa itatoaje uamuzi ambao hauhatarishi maslahi ya haki?
Waheshimiwa majaji kuruhusu Ushahidi wa namna hii itakuwa ni a mockery of justice and just adjudication of cases by the court, hakutakuwa na haki kabisa.
Waheshimiwa Majaji katika mazingira haya shahidi akiruhusiwa kutoa kinachoitwa Ushahidi wake:
Mahakama itajuaje demeanour of the witness?
Hii haitakuwa fair hearing, hakutakuwa na usawa mbele ya sheria, mtahakikishaje waheshimiwa majaji kuwa kutakuwa na usawa mbele ya sheria kama ambavyo Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya JMT inasema.
Tunapozungumzia usawa mbele ya Sheria hatuzungumzii kanuni zilizotungwa na Jaji Mkuu tu peke yake, tunazungumzia kanuni za kikatiba pamoja na Ibara ya 107A ambayo inaweka sharti kwamba Mahakama lazima itende haki sawa kwa wote.
Waheshimiwa majaji hili litawezaje kutekelezwa kama mtaruhusu mashahidi msiowajua na msiowaona kutoa Ushahidi? Waheshimiwa majaji nawaomba msije mkakubali kutumika kuharibu utendaji haki katika mahakama zetu, don’t ever allow.
Labda nichomekee jambo hapa kidogo. Ukiachana na Mh. Lissu anaongea Sheria lakini lolote analosema linamuingia kila mtu akilini na moyoni. Ukiwaangalia hata Majaji ni kama wanasema unachokisema tunakuelewa kabisa na ndio ukweli wa Mungu lakini tutafanyaje sasa? Hiyo ndio impression tunayoiona hapa Mahakamani tukiwa tunawatazama majaji na hata mawakili wa Serikali. Ukiwaangalia hata mapolisi waliopo humu nao sura zao zinasema ni kweli hatujui sheria sisi kama mapolisi ila anayosema Lissu yanaeleweka na ni sahihi.😂
Waheshimiwa majaji haya niliyoyasema ya misingi ya haki yamewekwa pia katika mikataba mbalimbali ambayo nchi yetu imeridhia.
Naomba niwape mifano, Ibara ya 2 , 7, 10 and 11 za Tangazo la Haki za Binadamu of UDHR 1948, Ibara ya 14(1) , 14(3) (e ) na 26 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kirai na Kisiasa wa Mwaka 1966 (ICCPR) zote zinazungumzia usawa mbele ya Sheria, ulinzi sawa mbele ya sheria.
Waheshimiwa majaji naomba kuwasomea Ibara ya 14(3)(e) of ICCPR inasisitiza kuhusu in full equality, mkiruhusu shahidi ambaye hamumjui, hamumfahamu, mimi simuoni na wala simfahamu, hiyo in full equality itatoka wapi?
Vilevile Ibara ya 3 na 7 ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu, ibara ya 6(d) na 7(2) ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rules of Procedure International Residual Criminal Procedure Mechanisms hizi zimeweka gold standard na best practices za umoja wa Mataifa hivyo mahakama zetu zinaweza zikazitumia hasa kanuni ya 75A, 75C, 86A na 86B.
Waheshimiwa Majaji hizi kanuni 4 ndio best standards za kulinda mashahidi, hivyo utaratibu huu upo sio kwamba umegunduliwa na mawakili wa serikali na hazina hii darkness tunayotaka kuletewa hapa (Lissu anaonyesha kizimba alipojificha shahidi wa leo),😂😂
Utaratibu huu hauwezi kuleta fair trial, mkiruhusu huu utaratibu unaotaka kuletwa hapa then we must forget about fair trial.
Part 149 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 149
Waheshimiwa Majaji, naomba niende kwenye hoja ya tano;
Naomba kurejea kesi zifuatazo High hope international group Jiangsu native produce import and export cooporation limited vs JOC Textile (Tanzania Company Limited) Misc. Commercial Application No 48 of 2020, kesi ya Sheer Illusions Ltd vs Christina Ulawe Umiro Civil Appeal 114 of 2014.
Hizi kanuni zimechapishwa Julai 11, 2025 miezi mitatu kabla ya kesi hii. Swali ni je, kanuni hizi zinaweza kutumika katika kesi iliyoanza kabla hazijatungwa? Jibu ni Sheer Illusions kwenye ukurasa wa 11 wa hukumu hiyo kuwa haziwezi kutumika kwenye kesi yangu.
Waheshimiwa Majaji hoja yangu nyingine ni kwamba kifungu cha 194 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa Jinai ambacho ndio msingi wa Kanuni hizi.
Kifungu hiki kililetwa na Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 07 ya 2018. Hii sheria inayoruhusu kuficha mashahidi haijawahi kuchapishwa kwenye gazeti la serikali.
Kifungu cha 14 cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria kinasema ili sheria ianze kutumika lazima iwe published kwenye gazeti.
Sheria yenyewe haisemi itaanza kutumika tarehe ngapi hivyo ilipaswa kuanza kutumika siku ilipotangazwa kwenye gazeti la serikali hadi muda huu niliposimama hapa sheria hii haijawahi kutangazwa kwenye gazeti la serikali.
Waheshimiwa majaji sheria ikitangazwa katika gazette la Serikali inachapishwa kwenye website ya Serikali, official website ya ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Rais Idara ya Utumishi, huku vilevile haipo.
Ndugu zangu Watanzania huyu Lissu nawahakikishia sio binadamu wa kawaida. Haya mapingamizi pia naona kuna dalili yanaweza kuifyatua hii kesi vibaya sana. Hawa watu wafute hii kesi tutaona mengi sana wakiendelea kuiacha.
Haya anaendelea Mhe. Lissu tena.
Waheshimiwa Majaji publication in the Government Gazette ni takwa la Sheria kuwa gazette lazima liwasilishwe Bungeni, halikuwa tabled Bungeni.
Sheria ikitangazwa katika Gazette la Serikali utakuta physical copies katika maktaba ya Mahakama kuu Dar es Salaam kwenye jengo hili, napo haipo.
Vilevile kwenye ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali vilevile haipo na huko.
Mahakama Kuu kitengo cha Biashara pia haipo kwenye Hansard za Bunge pia haipo, kwenye duka la Serikali Dodoma na Dar es Salaam pia haipo kwenye Sheria ya Huduma za Maktaba inasema Sheria ikiwa gazetted and published lazima kuwekwa Maktaba Kuu ya Taifa Dar es Salaam hapo Kisutu pia haipo, kuna Sheria nyingine inaitwa Publications (Compulsory Deposit) Act Cap. 294 ambayo inalazimishwa publication must be deposited central library Dar es Salaam.
Kwenye hiyo sheria kuna Publications (Compulsory Deposit) Order GN 61 of 1964 inayosema all publications must be deposited in the central library, haipo waheshimiwa majaji.
Waheshimiwa majaji nimezungumzia tabling bungeni naomba niwaelekeze kwenye kanuni ya 37(2) Kanuni za Kudumu za Bunge GN 56 of 15/01/2016. Kanuni ya 53(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge GN No. 626 of 2020 hivyo kuchapisha sheria kwenye gazette la serikali ni matakwa ya sheria na kusambaza kwenye hizo sehemu nilizozitaja ni takwa la kisheria, haijafanyika sasa katika kanuni hizi.
Uthibitisho wa kuwa sheria imechapishwa ni sheria yenyewe, mimi na Mawakili wangu wanaonisaidia wamelitafuta hilo gazeti nchi nzima halipo. Vijana wamezunguka kila kona ya nchi hii na kwenye hayo maofisi niliyosema hawajawahi kukutana na hiyo sheria. Haipo.
Namsikiliza Mhe. Lissu halafu natafakari huyu mtu huwa anasoma haya mambo yote saa ngapi na anakumbukaje hivi?
Akili kama hii kuwepo jela badala itoe mchango wa kulisaidia hili taifa ni matumizi mabovu ya rasilimali watu wenye akili. Ipo siku tutashinda na kweli itashinda.
Anaendelea Mhe. Lissu
Hoja hapa ninayojaribu kusema ni kwamba kama hiyo sheria haijawa published kwenye gazeti and there is no proof anywhere na kama imetumika, imetumika kimakosa.
Part 150 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 150
Anaendelea Mhe. Lissu
Hivyo naomba sheria hii kama Jaji Mtembwa aliitumia, naiomba Mahakama hii isiendelee kukosea, isiendelee kuitumia.
Waheshimiwa Majaji mkiangalia sheria namba 7 ya 2018 utaona imeandikwa kwenye header note kuwa sheria hii imetolewa kwenye gazeti maalum la Serikali la tarehe 15 Septemba 2018, waheshimiwa majaji huo ni uongo.
Uthibitisho kuwa ilichapishwa kwenye gazeti la serikali ni kulitoa gazeti lenyewe, proof sio what the law says, bali ni physical existence or electronic existence.
Nawaomba waheshimiwa majaji msiitumie hii sheria, msipoitumia maana yake mashahidi waje watoe Ushahidi hadharani, hii ya kufichaficha mashahidi gizani haitakuwepo kabisa na haitakiwi kabisa kuwepo.
Anasimama Wakili wa Serikali Nassoro Katuga yupo kama amechanganyikiwa au ametoka kubeba gunia la mchanga ni mdogo kama Pilton.
Amesimama akiwa amenywea sana na kusema,
Kwa hoja nyingi zilizoletwa tunaomba muda wa kujiandaa kujibu hoja nyingi sana ambazo mshtakiwa amezisema.
Tunaomba tarehe ambayo tutapangiwa kwaajili ya kuja kujibu.
Lissu hajapinga ila ameomba tarehe ya karibu zaidi wapewe.
Kesi imeahirishwa kwa muda usiojulikana hadi pale ambapo Mahakama itatoa Notisi ya siku ya kusikilizwa kwasababu notisi ya awali ilionyesha mwisho wa kusikiliza kesi hii ni leo Novemba 12, 2025.
Naomba Repost yako.
Leo tarehe 12/11/2025 Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam.
Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo itaendelea hapa.
Leo kuna kila dalili kesi itaendelea. Kwasababu Mhe. Lissu ameshafikishwa asubuhi ya leo na maandalizi yanavyoonekana hapa Ukumbi namba 1 wa Mahakama kuu, shauri litaendelea.
Maandalizi yapo kama ambavyo huwa yanafanyika siku kesi inasikilizwa.
Wafuatiliaji mbalimbali wanaendelea kufika mmoja mmoja na pia amefika Naibu Katibu Mkuu wa Chama, Amani Golugwa, yupo pia Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" na Godbless Lema pia wamefika hapa Mahakamani.
Muda wowote kuanzia sasa shauri linaweza kuanza kusikilizwa.