DAR: Wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (#LHRC), William Maduhu amesema hayo Mei 20, 2026 wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Wasafi FM, akidai kwa kauli za Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (#UWT), Mary Chatanda, anategemea Msajili wa Vyama vya Siasa ataiandikia barua CCM kuionya au kuifuta.
Soma https://t.co/ezaQrf9RlW
#JamiiForums #Uwajibikaji #Siasa
#TheInterview | Kitu kimoja kikubwa ambacho Injinia Mapunda Alfred, anaamini ni kuwa Kujenga ni kuamua kwani hata ukiwa na kiasi kidogo unaweza kuanza Ujenzi wa Nyumba ya ndoto yako.
#SupaBreakfast | #HainaKuchoka | #TheInterview
“Sisi wakenya tuko wakali, sisi si nchi rahisi ya kuendeshwa. Hao marais wote mnaowaona wa East Africa hawaezi endesha Kenya, ni ngumu.�� - Hon. Beatrice Elachi.
#JamboKenya
#RadioNumberOne
#HABARI Spika wa Bunge la Uganda Anita Annet Among anayekamilisha muda wake, anakabiliwa na uchunguzi mkali kuhusu madai ya ufisadi na utakatishaji fedha.
Vyombo vya usalama vinaripotiwa kufanya upekuzi katika makazi yake Jijini Kampala na maeneo ya jirani wakichunguza mali zinazodaiwa kupatikana kwa njia isiyo halali.
Katika operesheni hiyo, maafisa walikamata gari lake la kifahari aina ya Rolls-Royce Cullinan linalokadiriwa kuwa na thamani ya dola 440,000 za Marekani (takribani Shilingi bilioni 1.2). Magari mengine ya kifahari pia yalitaifishwa huku uchunguzi ukiendelea kutafuta nyaraka za kifedha na ushahidi mwingine unaohusishwa na kesi hiyo.
Ripoti zinaeleza kuwa uchunguzi huo ni sehemu ya kampeni kubwa dhidi ya ufisadi inayowalenga viongozi waandamizi nchini Uganda.
Among, ambaye aliwekewa vikwazo na Marekani mwaka 2024 kutokana na madai kama hayo ya ufisadi, amesema hatagombea tena uspika wa Bunge jipya na yuko tayari kushirikiana na mamlaka katika uchunguzi unaoendelea.
#EastAfricaTV
“Wakati nakuja hapa nimepigiwa simu na Mdogo wake Lissu aitwaye Vicent ameniambia tangu jana jioni Mwenyekiti wetu anaumwa sana Tumbo, Tumbo linamkata haarishi lakini ana maumivu makali sana tumesema tena na tena na tena Lissu akipata shida haitaeleweka Nchi hii”-; Mhe. @HecheJohn
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaongoza wakazi wa kijiji cha Mabuimerafuru melafuru Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Mkoani Mara katika mazishi aliyekuwa mwandishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Marehemu Boniface Makene ambaye amefariki dunia kwa ugonjwa wa kiharusi.
Akiongoza mazishi hayo Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewataka Watanzania kuweka utamanduni wa kutoa mawazo kwania njema kwa maslahi ya Taifa lao.
"Tukijenga utaratibu wa kuwa wakweli,tukijenga utaratibu wa kutoa mawazo kwania njema tutaweza Kujenga nchi yetu kwa kiwango kikubwa sana,lakini tukijenga utaratibu wa kuwa na mawazo mazuri na kuyaficha tutaishia Kujenga Taifa la wanafiki ambalo haliwezi Kupata Maendeleo" Alisema Dkt. Emmanuel Nchimbi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ulikuwa unajua kuwa Ulimi haupaswi kusafishwa na Brashi za Mswaki?
Msikilize Dkt. Sharon Kendi, Balozi wa afya ya kinywa na meno kutoka Enamel Ellegance Dentist Clinic akielezea swala hili kwa undani kupitia TV47 Kenya
Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje wa bunge la Ulaya mh David McAllister, ametoa ujumbe kwa utawala dhalimu kumuachia mhe Tundu Lissu.. amesema haya leo tarehe 9/4/2026 kama kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kukamatwa kwa Mwenyekiti wetu.
Dunia inajua na Dunia haitanyamaza.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema mradi wa uwanja wa mpira wa Arusha ulikadiriwa kugharimu TZS bilioni 187, lakini ulisainiwa kwa TZS bilioni 338.54, sawa na ongezeko la asilimia 81.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema katika mwaka wa fedha 2024/25 Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilipata hasara ya TZS bilioni 191.19, ikiwa ni ongezeko la asilimia 108, na kufikisha jumla ya hasara ya TZS bilioni 748 tangu ianzishwe.
Katika kuendeleza jitihada za kuondokana na nishati isiyokuwa safi, Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) limejipanga kuwakopesha majiko ya nishati safi kwa wateja wake pale wanapoingiza umeme.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Tanesco, Lazaro Twange wakati akizungumza katika kongamano la wanawake wa lililoandaliwa na shirika hilo kuhamasisha matumizi ya nishati safi.
#mwananchiupdates
#tunawezeshataifa
Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Zanzibar), Said Issa Mohammed na wenzake kupinga Tundu Lissu kuunganishwa katika Kesi ya Mgawanyo wa Mali inayowakabili Katibu Mkuu wa CHADEMA na Bodi ya Wadhamini.
Maombi ya msingi ya Lissu yatasikilizwa Machi 6, 2026 mbele ya Jaji Hamidu Mwanga.
Je, unakubaliana na mtazamo wake?😃
Meya wa Cameroon amezua mjadala kwa kusema Wanaume wanapaswa kuweka 'Password' kwenye simu zao kwa sababu wao wanalinda ndoa, huku Wanawake wakiambiwa kuacha simu zao wazi kwakuwa hawatakiwi kuficha chochote, akiwauliza "Mnaficha nini?"
Tembelea https://t.co/dDd21Ugmlv kushiriki mijadala mbalimabali.
#JamiiForums #DataPrivacy #TaarifaZakoNiZako
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema kuwa moja ya mambo ambayo yanamchukiza ni ugomvi wa baina ya vyama akieleza kuwa sote tunajenga taifa moja hakuna sababu ya kuwepo kwa mambo hayo.
Akizungumza leo Februari 28, 2026 kwenye msiba wa Hayati Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa amekuwa na msimamo wa kutopenda mambo hayo na aliuonyesha hata alipokuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
"Mimi hata mambo ya kugombana kivyama vyama siyapendi ujinga tu, nchi yenu moja mnagombana nini?" amesema Dkt. Nchimbi
Amesisitiza kuwa hata mtu akihama kwenda chama kingine ni hatua tu katika hatua za kwenda kulitumikia taifa.