Mkurugenzi Mtendaji wa AICC Bi. Christine Mwakatobe akimkaribisha Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete-Waziri wa Nchi OWM - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu alipowasili Kituoni hapo leo Julai 10, 2025 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 14 wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasim Majaliwa ampongeza Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) Bi.Christine Mwakatobe kwa kutoa huduma bora za kumbi za mikutano nchini.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akimkabidhi tuzo mbalimbali Bw. Assah Mwambene, Afisa Uhusiano Mkuu wa Wateja kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa AICC kwa kutambua mchango wake katika kukuza Sekta ya Utalii wa Mikutano nchini.
AICC imeshiriki kikamilifu kwenye Uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje Toleo la 2024 ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Uzinduzi huo umefanyika JNICC, jijini Dar es Salaam leo tarehe 19 Mei, 2025
Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 16 Mei 2025 amefungua resmi Mkutano Mkuu wa 30 wa Wanahisa wa CRDB katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) jijini Arusha.
Wafanyakazi wapya wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) wakifuatilia kwa makini mafunzo elekezi ya awali yanayoendeshwa kituoni hapo na Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC).
#webringtheworldtotanzania
Mkufunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Bi. Mariam Kuhenga akiendesha mafunzo kwa wafanyakazi wapya wa AICC yanayolenga kuwajengea uwezo wa kufanyakazi Serikalini kwa kufuata sheria, taratibu, kanuni na miongozo, mafunzo hayo yameanza tarehe 13 Mei, 2025 kituoni hapa jijini Arusha
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) Mha. Steven Samwel Mokare akisisitiza jambo wakati akifungua Mafunzo Elekezi ya Awali (Induction Course) kwa wafanyakazi wapya wa Kituo tarehe 13 Mei, 2025 kituoni hapa, jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Bi. Christine Mwakatobe akisalimiana na viongozi wa Serikali walioshiriki Jukwaa la Uchumi Mkoa wa Arusha, 2025 lililofanyika kwenye Kituo cha AICC leo, tarehe 03 Mei, 2025
#webringtheworldtotanzania
Wafanyakazi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) wameshiriki kikamilifu kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya wafanyakazi duniani 2025 kwa kuonesha shughuli zinazofaywa na Kituo.
#webringtheworldtotanzania
Makamu wa Rais wa JMT Mhe. Dkt. Philip Mpango amefungua Kongamano la Kodi na Uwekezaji la mwaka 2025 lililofanyika leo Aprili, 15 2025 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
#webringtheworldtotanzania