@Eric__Bernard Kuwa mtendaji mkuu hai verify kuwa msemaji. Hizi ni taaluma mbili tofauti.though boss akitaka kuongea mwenyewe hakuna shida.
Kuwa msemaji WA jambo kuna approach yake tofauti kabisa .kuna mtu anaeza kuwa mtendaji mzuri but akawa hana representing skills nzuri
RAIS SAMIA: POLISI WAACHE KUMTAFUTA DKT. GWAJIMA
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameliagiza Jeshi la Polisi liache kumtafuta Askofu Dkt. Josephat Gwajima kama walivyokuwa wametangaza awali ili aweze kuendelea shughuli zake.
Amesema baada ya kutoa msamaha kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima, waumini wanahitaji wamuone kiongozi wao, hivyo anatakiwa ajitokeze hadharani aendelee na kazi yake. “Mwacheni ajitokekeze tujenge umoja wa kitaifa, tushikamane kurudisha umoja wa kitaifa. Tumekutana na TEC, viongozi wa dini, wa mila na viongozi mbalimbali; twendeni sote kwenye jambo hili, tujitokeze tuhamasishe Tanzania yenye amani, huu ndio wito wa kiongozi wetu wa nchi”
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Novemba 30, 2025) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Arumeru katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Magufuli Leganga, kata ya Usa River, wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Waziri Mkuu amewataka Watanzania wakatae kushawishiwa na wanaharakati wanaochochea vurugu kwani zinarudisha nyuma maendeleo ya nchi. "Nimekuja kuwapa pole wananchi wenzangu, kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Anatambua mambo yanayoendelea. Anatambua kazi kubwa ya kujenga Taifa mnayoifanya," amesema.
Kabla ya mkutano huo, Waziri Mkuu alikagua uharibifu uliofanywa wakati wa vurugu za Oktoba 29, mwaka huu kwenye kituo cha polisi cha Kikatiti (mita 500 kutoka barabara kuu ya Arusha - Moshi); Mahakama ya Mwanzo ya Maji ya Chai (km. 3 kutoka barabara hiyo kuu); kituo cha mafuta Total Energies kilichopo Maji ya Chai (kipo barabarani) ambavyo vyote vilichomwa moto ikiwemo kuiba mali kwenye supermarket na kubomoa sefu ya kutunzia fedha.
Waziri Mkuu amesema masuala ya maendeleo ya wilaya ya hiyo kama vile maji na barabara yamo kwenye Ilani ya CCM na kwenye ahadi za Mheshimiwa Rais lakini yatafanyika endapo tu nchi itakuwa na amani. “Tukichagua vurugu tutakuwa tumechagua kufukuza maendeleo, tukichagua vurugu tutakuwa tumechagua kuongeza umaskini kwa mtu mmoja mmoja," ameonya.
"Kila Mtanzania akatae haya yaliyotokea juzijuzi. Tumechochewa, tumechonganishwa lakini wao wako nje, wanalipwa ili kutuvuruga tu. Wengi wanaochochea vurugu ni wanaharakati, wako nje ya nchi. Hakuna kiongozi wa chama cha siasa anasema wananchi wafanye vurugu. Au mmemuona?" alihoji.
Amesema baadhi ya vijana walioko nje ya nchi wamebainika kupokea dola za Marekani milioni mbili (sawa na sh. bilioni 4.5) ili wachochee vurugu. “Hawa wanaowalipa, wana maslahi gani na nchi yetu? Wana ajenda gani na nchi yetu? Tunajua watazirudishaje hizo fedha?”
“Hawa watu wanalenga tugombane ili wachukue madini adimu (rare earth minerals). Sasa hivi Tanzania imegundua uranium ambapo inakuwa nchi ya tisa duniani na ya kwanza barani Afrika. Ina tani za ujazo 890,000. Hii ni karibu tani milioni moja."
Waziri Mkuu ameonya dhidi ya mchezo unaotumika kuanzisha chokochoko ili kusambaratisha nchi pindi inapobainika kuwa na rasilimali. Amesema ziko baadhi ya nchi barani Afrika ziliathirika kutoka na chokochoko hizo. “Wanaanzisha chokochoko, wanaacha mnavurugana, rasilmali zikiisha, wao wanaondoka,” amesisitiza.
"Watanzania tuamkeni, tuchukue tahadhari. Kuna kamchezo kanachezwa. Wanajua Tanzania ina gesi asilia nyingi na inakaribia kuanza. Wanajua ikianza miradi hii, Tanzania itakuwa ya kwanza katika Afrika Mashariki na wala hatutahitaji kutoa mikopo ya wanafunzi."
Amewataka Watanzania waamke na kukataa kurudishwa tena kwenye hali ya vurugu. "Watanzania tuamke, tukatae kurejeshwa kule nyuma. Umaskini utaondolewa nchi ikiwa kwenye amani. Ajira za vijana zitaweza kupatikana nchi ikiwa kwenye amani."
Amesisitiza kuwa vurugu zikiwepo, hata wakulima wa karoti na nyanya wa Ngarenanyuki hazitauzwa na hivyo kuathiri uchumi wa mtu binafsi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameagiza mabasi yote ya Mwendokasi yaanze kutoa huduma katika barabara ya Mbagala kuanzia Novemba 20, 2025.
Leo alasiri nimetangaza uteuzi wa Baraza la Mawaziri pamoja na Naibu Mawaziri. Kwa pamoja, tutafanya kazi ya kutekeleza jukumu la msingi la kuwatumikia wananchi.
Dhamana hii ni wajibu na pia deni ambalo tunapaswa kuwalipa wananchi kwa kuwatumikia kwa ari, bidii na uaminifu mkubwa.
Ninawatakia kila la kheri. Mwenyezi Mungu awasimamie na kuwaongoza.
HABARI PICHA:
Makamu Mkuu wa Chuo cha Kiislamu Morogoro (MUM) na CAG Mstaafu, Professa Mussa Assad, amesema ni muhimu serikali na jamii kuwekeza katika kutoa ujuzi wa ziada kwa vijana hasa waliopo vyuoni ili kuwasaidia kujipambanua kiuchumi na hata kutoa huduma bora katika shughuli wanazofanya huku akisisitiza kuboreshwa kwa kilimo cha umwagiliaji ili kukuza uchumi wa wakulima.
Profesa Assad ameeleza hayo leo Oktoba 22, 2025, alipokuwa akizungumzia nafasi ya Sekta binafsi katika kujenga Uchumi jumuishi, kuelekea dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050, katika mjadala uliofanyika chuo cha MuM kwa kushiriana Sekta ya Ubia Kati ya Sekta binafsi na Sekta ya Umma(PPP)
“Watu wa Sekta binafsi wana ujuzi mkubwa sana kuliko hawa wa Sekta ya Umma si hapa tu hata huko nje ya Nchi hii, kwahiyo mtaji mmoja mkubwa wa Sekta binafsi ni umahiri wa ujuzi na maarifa Hili ni eneo kubwa sana katika uchangiaji wa Uchumi.” Ameeleza Prof Assad
Kuhusu kilimo cha umwagiliaji Prof. Assad ametoa wito kwa serikali kuweka nguvu kubwa kwenye kiimo cha umwagiliaji katika miaka 25 ya kutekeleza Dira ya Taifa 2050.
"tuhakikishe kwamba umwagiliaji unafanyika tuhakikishe miaka inayokuja serikali iingize namna zake za fedha na miundombinu katika kuhakikisha wakulima wetu wana maji ya kutosha"
HABARI:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tarime Rorya limetoa taarifa kwa umma likieleza kuwa hali ya usalama katika mji wa Sirari ni shwari, kufuatia tukio la Oktoba 21, 2025 saa 11:30 jioni, ambapo watu wawili walikamatwa kwa mujibu wa sheria na kupelekwa Kituo cha Polisi Tarime.
Taarifa hiyo imeeleza, baada ya watuhumiwa hao kufikishwa kituoni, kundi la vijana wa bodaboda lililopewa taarifa zisizo sahihi lilienda Sirari na kujaribu kufanya fujo kwa kufunga barabara, lakini Polisi waliwatawanya na kuwakamata watuhumiwa 12 kwaajili ya hatua za kisheria.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa taratibu za kisheria zinaendelea ili watuhumiwa hao wachukuliwe hatua stahiki.
Aidha, kupitia taarifa hiyo Polisi wametoa onyo kali kwa wote wanaopanga au kufikiri kufanya uvunjifu wa sheria, wakisisitiza kuwa watakabiliwa vikali kwa mujibu wa sheria.
"Tanzania kuanzia 2027 itakuwa na umeme wa uhakika. Saa 24 umeme unapatikana kwa uhakika, ukizimwa, lazima itolewe sababu kwanini umeme umezimwa eneo hilo." - Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu kwenye kampeni Sumbawanga mkoani Rukwa
Ninawashukuru wananchi wa Kata ya Kibaoni kwa hamasa na ukarimu, tulipohitimisha kampeni zetu katika Mkoa wa Katavi, kabla ya kuelekea Mkoa wa Rukwa. Ahsanteni sana.
Ahsante Mwalimu.
Miaka 26 tangu ulipotutoka bado tumebaki kuwa Taifa moja, imara, lenye amani na mshikamano, misingi uliyotujengea. Tunu hizi muhimu kwa uhai wa Taifa letu daima tutazienzi, tutaziendeleza, tutazisimamia na kuzilinda.
VIDEO:
Rajabu Abdalah (32), mkazi wa Miyuji jijini Dodoma, amekumbwa na maumivu makali kutokana na uvimbe mkubwa wa nyama unaojitokeza shingoni na mgongoni, hali inayomzuia kufanya shughuli zake za kila siku.
Akizungumza na JAMBO TV leo jijini Dodoma, Rajabu amesema amekuwa akihangaika kwa muda mrefu kutafuta matibabu bila mafanikio, huku uvimbe ukiendelea kukua na maumivu yakizidi kila siku.
“Maumivu ni makali sana na uvimbe unaongezeka kila siku. Imekuwa ngumu hata kufanya shughuli ndogondogo kutokana na uzito wa uvimbe huu,” amesema Rajabu kwa uchungu.
Rajabu, ambaye ni baba wa mtoto mmoja na mume wa familia ndogo inayomtegemea, ameomba msaada kutoka kwa Watanzania na serikali ili apate matibabu pamoja na kiti mwendo (wheelchair) kitakachomsaidia katika maisha ya kila siku.
Mama mzazi wa Rajabu, Bi. Hajida Bakari, amesema mtoto wake amezaliwa na afya njema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, lakini walipoanza kugundua uvimbe shingoni tangu akiwa mdogo alipokuwa anaanza kutambaa, uvimbe huo umeendelea kukua na sasa umemuweka katika hali ngumu zaidi.
Kwa yeyote mwenye nia ya kumsaidia Rajabu Abdalah kufanikisha matibabu yake, anapatikana katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Kibaoni jijini Dodoma, au kupitia namba ya simu 0625 658 307.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaomba radhi watumiaji wa mabasi ya mwendokasi kutokana na upungufu wa mabasi, akiwahakikishia kuwa muda wowote tatizo hilo litatatuliwa.
HABARI PICHA:
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza mmoja wa watoto waliofika kumlaki kwenye Viwanja vya Msuya, Mwanga mkoani Kilimanjaro, wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika leo Septemba 30, 2025, siku yake ya kwanza ya kampeni za uchaguzi mkuu mkoani humo.