EMBE AINA YA RED INDIAN NA HIZI NDIZO SIFA ZAKE.
-Hukomaa Mapema.
-Huzaa Sana.
-Embe Lina ladha Nzuri.
-Embe Lina kokwa dogo.
-Halina kamba kamba.
Miche hii inapatikana makao Makuu ya Wakala wa Mbegu za kilimo "ASA" Mkoani Morogoro.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo Dkt.Sophia Kashenge wa kwanza kulia akitoa Maelezo ya Ujenzi na Uzinduzi wa Duka la Mbegu la Shamba la Msimba Kilosa Mkoani Morogoro kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Mweli wa kwanza kushoto.
Ni siku ya pili Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) Dr.Ashura Kihupi akiongoza Kikao Cha Bodi ya Wakala kinacho jadili na kupitisha Mambo mbalimbali ya wakala.kikao hicho kinafanyika Mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) Dr.Ashura Kihupi ameongoza Kikao Cha Bodi ya Wakala kujadili na kupitisha Mambo mbalimbali ya Wakala Kikao hicho kitakaa kwa siku Mbili Mkoani Morogoro.
Huu ndio ubora wa Mbegu zetu,ndio furaha https://t.co/9finlotnEF Mtama aina ya MACIA unakaribia Kukomaa katika Shamba la Wakala Msimba wilaya ya Kilosa Mkaono Morogoro.
ASA NI CHANZO CHA MBEGU BORA ZA KILIMO TANZANIA.
Naibu waziri wa kilimo Mhe.Antony Mavunde wa nne kutoka kushoto akizindua Mpango wa Africa Connect utakao waunganisha wakulima wa Mpunga kwa kupata Mbolea,Mbegu,Mikopo,Pembe jeo pamoja na uhakika wa Soko.
KAZI INAENDELEA ASA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dr.Ashura Kihupi akiongoza Kikao Cha Bodi ya Wakala kilichofanyika katika ukumbi wa Shamba la Wakala Kilimi Nzega Tabora.
Bodi hiyo itakaa kwa muda wa siku mbili kujadili na kupitia taarifa mbalimbali za.
ASA KAZI INAENDELEA.
MAAGIZO.
Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe ameziagiza Taasisi za TARI,ASA na Kampuni ya Syngementa kufanya utafiti wa maeneo ya Uzalishaji wa Mbegu za Mpunga, Alizeti,Ngano,Soya na Cocoa.
ASA KAZI INAENDELEA.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) Dr.Sophia Kashenge akiongoza Kikao Cha Ushirikiano wa kibiashara kati ya ASA, Kampuni ya Mbolea ya Yara pamoja na Benki ya Equity katika kuunda Kilimo Biashara ili kumrahisishia Mkulima kupata Viuwatilifu.
ASA KAZI INAENDELEA.
MKURUGENZI WA MAZAO WA WAKALA WA MBEGU ZA KILIMO ASA DR.JUSTINE RINGO (KULIA)AKIKAGUA SHAMBA LA NYANYA AINA YA TANYA (KUSHOTO) NI MENEJA WA SHAMBA LA WAKALA TENGERU,BENSONI MINJA.
SHAMBA HILI NI MAALUMU KWA UZALISHAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO ZA MBOGA MBOGA
PONGEZI ZA ASA DAY.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA wakipewa vyeti vya pongezi na Mkurugenzi Mkuu Wa Maendeleo ya Mazao ya kilimo kutoka Wizara ya kilimo Nyasebwa Chimagu kushoto,kulia ni Dr.Sophia Kashenge Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA.
ASA DAY.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dr Sophia Kashenge kulia akiwa anatoa maelezo ya Mbegu ya Mpunga kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ASA Dr,Ashura Kihupi katikati kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya kilimo Nyesebo Nchimagu.