5.Unatakiwa udhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii kwasababu yatakufanya uwe mtuma wa mawazo, husababisha huzuni, no rahisi kujilinganisha na kujitoa thamani
6.Unatakiwa ufanye mazoezi kwasababu inasaidia kutuliza akili na kuimarisha mwili
3.Unatakiwa uache ulevi kwasababu itapelekea kupata magonjwa kama shinikizo la damu, saratani ya ini, shida ya figo na hata matatizo ya akili
4.Unatakiwa uachane na kujichua kwasababu inaweza kusababisha uteja wa kihisia, upweke, maumivi ya kiuno na mgongo, mwili kuchoka, mbegu
Wewe ulivyo ni matokeo ya vitu vinavyohusiana na wewe kila siku kama vile
1.Unachokula kila siku
2.Unachowaza kila siku
3.Unachopendelea kufanya mara kwa mara
4.watu unaoshinda nao mara kwa mara
5.Mazingira unayoshinda na kuishi
6.Taarifa unazozipenda kusoma, kuangalia na kusikia
8.Kufanya vitu unavyovipenda hata kama si vya gharama au vinadharauliwa na watu wengi
9.Kutokuigiza maisha au kujilinganisha na watu wengine
10.Kuheshimu watu wote bila ya kujali umri, jinsia, rangi, hali ya kifedha au ya kisiasa
11.Kuwa sababu ya furaha kwa watu wengine
Maisha ya furaha hutengenezwa na wewe mwenyewe kwa vitu vya kawaida kama vile
1.Kujiamini kwa jinsi ulivyo
2.Kuthamini vitu unavyovipenda, unavyovimiliki na unavyofanya
3.Kuwa mwingi wa kushukuru kwa kila kitu kukuhusu wewe na kuthamini mafanikio na hatua unazozipiga kila siku
4.Kuwa mwepesi kusamehe, kuachilia na kusonga mbele
5.Kugusa maisha ya wengine kwa kuwasaidia wenye uhitaji na kufanya mambo mema kila siku
6.Kufanya ibada na kuwa mtu mwema
7.Kuwa na malengo halisi yanayo kuhusu wewe na sio yakuwafurahisha watu au kuwakomoa watu wengine
Hivyo basi katika maisha shukuru makadirio ya mungu kwenye kukupa unachostahili na kukupokonya unachokitaka au kukunyima kabisa unachokihitaji ili akuepushie au akulinde na Shari na maafa ya vitu hivyo ambavyo yeye anavijua zaidi
Katika maisha hakuna kuchelewa ila kuna wakati sahihi na makadirio ya maisha,kwasababu
1.Kuna muda unahitaji kuchelewa kupata unachokihitaji ili ujue thamani yake na gharama ya kukipata ili ukitunze
2.Kuna muda inabidi uchelewe kukipata unachokihitaji ili uepukane na Shari zake
3.Kuna muda inabidi uchelewe kukipata unachokihitaji ili ukipate kikiwa kamilifu, kimetengemaa na kitadumu kwako
4.Kuna muda inabidi ukipate kwa kiasi kidogo ili kukulinda na athari za uwingi wake
5.Kuna muda kukikosa au kuondoka kwa kitu au mtu unaempenda ndio kinga yako
6.Soma vitabu na kuongeza maarifa ili uweze kutengeneza mawazo chanya mara kwa mara
7.Fanya mazoezi kupunguza hamaki mwilini
8.Fanya mazoezi ya kupumua kwa kukutanuka na kusinyaa kwa tumbo, weka mkono tumbo na kifuani kisha ruhusu pumzi iingie ishikilie kidogo kisha itoe taratibu
Unavyoviruhusu vitawale akili yako kwa kiasi kikubwa na kwa muda mwingi ndivyo vitakavyoamua hisia zako ziweje kwa muda huo na baadae
1.Ukijaza vitu hasi akilini mwako utaishia kuona kila kitu kibaya katika maisha yako, utakosa tumaini kwa kila kitu na hautaona mwanga maishani
Fanya hivi
1.Pendelea kujisemesha mambo mazuri
2.Pendelea kujitabiria mambo mazuri
3.Ukiona unaanza kuwaza jiimbishe mf. "Mnakuja kuniharibia mood ila leo hamtaweza"
4.Ukiona unaanza kuwaza tafuta shughuli ya kufanya
5.Fanya mazoezi ya kuyakabili mawazo yako kwa kujiuliza maswali
12.Fanya matendo ya huruma na kusaidia watu itakuongezea amani ya moyo
13. Jijali na jithamini; oga na upendeze,kula vizuri, fanya usafi, pata muda wa kulala vizuri na sehemu safi,jitoe out mara mojamoja
14. Samehe, achilia, shukuru na songa mbele ili uwe huru kihisia na kialili
Ukiona hali ya wasiwasi, hofu na huzuni inazidi kukutawala kila siku basi fanya hivi ili uweze kujiokoa
1.Chukua karatasi na orodhesha changamoto zinazo kukabili kwa kipindi hicho ili ujue mzizi wa tatizo hilo mfn. Changamoto za kiuchumi, afya yako, familia yako au mahusiano yako
"Na kisha kila siku fanya jambo ambalo litakuwa linajibu hayo maswali manne"
11.Kila siku asubuhi na jioni jiambie "Ninajipenda, ninajijali, ninajiamini, ninajithamini na siogopi na wala sikati tamaa" na hata unavyokuwa unajisikia vibaya jiambie hayo maneno