Baba Yetu uliye mbinguni. Jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo Mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu. Kama nasi tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi. Lakini utuopoe maovuni, Amina🙏
Tulieni ndugu zangu niwaambie siri moja: Mkimtumainia Mungu mtayashinda yote. Japo magumu ni mengi mtakayokutana nayo, mkimtumainia Mungu mtayashinda yote.
Mtavuka vikwazo vya shetani na magumu yote, mbinu zake shetani na hila hazitawaangusha. Mkimtumaini Mungu mtayashinda yote!
"Uisikie DUA ya mtumwa wako, na ya WATU wako Israeli, WATAKAPOOMBA wakikabili mahali hapa; naam, SIKIA huko MBINGUNI, makao yako; NAWE usikiapo, SAMEHE." {1 Fal 8:30}
@_mike2019 Hatufanani katika mahitaji. Watu wanafanya ambacho wana uhitaji nacho. Wao wameona wanahitaji Kanisa wakajenga. Usiongee kwa niaba ya dunia. Hapo ulipo kama unaona mnahitaji viwanda, shule na hospitali huo ni uhitaji wenu. Jengeni kama wao walivyoona wanahitaji Kanisa wakajenga.
Kanisa Kuu la Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni, Jimbo Katoliki Nnewi - Nigeria. Kanisa hili lilitabarukiwa jana.
Maskani zako Bwana, zapendeza kama nini!
Salamu Maria umejaa neema. Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote. Naye Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu. Utuombee sisi wakosefu. Sasa, na saa ya kufa kwetu, Amina🙏
Baba Yetu uliye mbinguni. Jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo Mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu. Kama nasi tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi. Lakini utuopoe maovuni, Amina🙏
Kumheshimu Mungu
Namtolea roho yangu
Nifanye kazi nipumzike
Amri zake nishike
Wazo, neno, tendo
Namtolea Mungu pote
Roho,mwili, Pendo na uzima wangu
Mungu nitampenda,
Dhambi sitatenda.
Jina lako nasifia
Utakalo hutimia
Kwa utii navumilia
Teso na matata
Nipe bwana Neema zako
Amina
Ee Baba yetu Mungu Mkuu,
Umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo,
Ee Baba Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi nikutii.
Naomba sana Baba wee,
Baraka zako nipokee.
Bikira safi, Ee Maria
Nisipotee nisimamie.
Mlinzi Mkuu Malaika wee,
Kwa Mungu wetu niombee,Amina.