📍 Morocco
▪️JK AKUTANA NA INIESTA, NYOTA FC BARCELONA, MOROCCO
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Andrés Iniesta, gwiji wa soka wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Spain, walipokutana katika Uwanja wa Ndege wa Casablanca wakijiandaa kuondoka.
Iniesta, ambaye kwa sasa amestaafu soka la ushindani na anaendelea na shughuli za mafunzo na maendeleo ya soka nchini United Arab Emirates (UAE), pia alikuwepo nchini Morocco kushuhudia fainali ya AFCON kati ya Morocco na Senegal.
Kukutana kwao huko kuliakisi mguso wa nadra kati ya historia ya uongozi wa Afrika na urithi wa soka la dunia—kimya, heshima, na mazungumzo mepesi ya wasafiri wa kawaida.
Ninaipongeza timu yetu ya Taifa ya mpira wa miguu, Taifa Stars kwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu.
Heshima hii kubwa kwetu ni matokeo ya maandalizi mazuri na kujituma kwenu katika kila mchezo. Mmeandika historia kubwa kwa Taifa letu na mmeleta furaha kwa Watanzania wote. Hongereni sana.
Ninawatakia kila la kheri katika michezo inayofuata.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa anayewakilisha pia na Morocco @AliMwadini amekutana na Rais wa Chemba ya Bishara, Viwanda na Huduma ya Rabat, nchini Morocco, Bw. Hassan Sakhi, kwenye ofisi za Chemba hiyo Jijini Rabat, Morocco.
Katika mazungumzo yao, wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji katika sekta mbalimbali baina ya Tanzania na Falme ya Morocco.
Wamekubaliana kuandaa mikutano ya kibiashara baina ya wadau wa sekta ya umma na sekta binafsi za pande zote mbili ili kuwezesha pande hizo kunufaika na fursa za ushirikiano zilizopo.
#KitengeUpdates
Nyota ya Kiswahili imeendelea kuangaza Kimataifa baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuridhia Lugha hiyo kuwa moja ya Lugha
zitakazotumika Rasmi katika Mikutano Mikuu ya Shirika hilo.
Kauli hiyo imetolewa katika Mkutano Mkuu wa 43 wa Shirika hilo uliofanyika Samarkand - Uzbekistan kuanzia tarehe 30 Oktoba na unaotarajiwa kuhitimishwa kesho Novemba 13 mwaka huu.
Hatua kubwa iliyotokana na jitihada za Serikali ya Tanzania Kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Kwa kushirikiana na Mabaraza ya Kiswahili Tanzania BAKITA na BAKIZA.
Kufuatia hatua hiyo, tayari Tanzania imepewa fursa ya kuwasilisha hotuba ya nchi baada ya maombi yake kuridhiwa.
Hotuba ambayo imetolewa na Mhe. @AliMwadini , Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa kudumu wa
UNESCO.
#KitengeUpdates
India 🇮🇳 congratulates Tanzania 🇹🇿 for this historic occasion to make Kiswahili an official language of the UNESCO General
Conference. India, as a long-standing partner of our brothers and sisters of Africa, and a champion of
linguistic and cultural pluralism, supports this initiative. ‘India inaunga mkono Afrika’.
@VishalVSharma7
India 🇮🇳 congratulates Tanzania 🇹🇿 for this historic occasion to make Kiswahili an official language of the UNESCO General
Conference. India, as a long-standing partner of our brothers and sisters of Africa, and a champion of
linguistic and cultural pluralism, supports this initiative. ‘India inaunga mkono Afrika’.
@VishalVSharma7
Our most profound and sincere condolences to the leadership and brotherly people of Nigeria, following the passing on of former President Muhammadu Buhari. May God Almighty grant patience and strength to the bereaved family and admit the late President to his mercy.
Nimeishi kijijini Bukumbi. Nimetumia kivuko cha Kigongo Feri kwa miaka kadhaa. Kukamilika kwa daraja hili, kumeweka Sura ya kuvutia sana kwenye KITABU cha Rais Samia. Hongera sana @SuluhuSamia ! Kwa hakika kila zama na Kitabu chake, kitabu chako kinapendeza👏🏾✅
📍Paris, Ufaransa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia Mkutano wa Tatu waUmoja wa Mataifa kuhusu Bahari (UNOC3), unaofanyikaJijini Nice nchini Ufaransa leo tarehe 09 Juni 2025.
#UNOC2025
📸:O/Makamu wa Rais
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa @AliMwadini akiwa na Mtangazaji wa Wasafi Mzee wa Minyama @mshambuliaji alipoutembelea Ubalozi wa Tanzania Mjini Paris.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. @Alimwadini
amekutana na baadhi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Sayansi ya Siasa (Sciences Po - Reims) na Ecole Normale Supérieure (ENS) vya Ufaransa, ambao pia wanajifunza somo la Kiswahili katika mitaala yao.
📍Paris,Ufaransa
▪️DKT. NCHEMBA NA SHIRIKA LA OECD LA UFARANSA WAZUNGUMZIA SERA ZA KODI NA UWEKEZAJI UFARANSA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), Bw. Mathias Cormann, Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo Jijini Paris nchini Ufaransa, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna Tanzania na Shirika hilo wanavyoweza kushirikiana katika kuimarisha usimamizi wa sera za kodi, usimamizi wa fedha za umma, mageuzi ya taasisi za kifedha na kuimarisha masuala ya uwekezaji nchini Tanzania.
📸:Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha-Paris
- -
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), Bw. Mathias Cormann, Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo Jijini Paris nchini Ufaransa, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna Tanzania na Shirika hilo wanavyoweza kushirikiana katika kuimarisha usimamizi wa sera za kodi, usimamizi wa fedha za umma, mageuzi ya taasisi za kifedha na kuimarisha masuala ya uwekezaji nchini Tanzania.
Mhe. Dkt. Nchemba ilieleza dhamira ya Serikali ya kuimarisha uwezo wa taasisi zake za kifedha kwa kupokea usaidizi wa kitaalamu kutoka OECD katika maeneo hayo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza mapato ya ndani, kuvutia uwekezaji na kuboresha mazingira ya biashara
Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Shirika hilo kwa kupokea utaalam katika kuimarisha vyanzo vya mapato ya ndani, kuimarisha uwekezaji na kukuza uchumi jumuishi utakaochangia kuimarisha mapato yake ya ndani, kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara na hatimaye kukuza uchumi na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania inakubaliana na utozaji wa kodi wenye usawa katika uwekezaji hususani katika uchumi wa kidigitali hivyo Tanzania inaendelea kuliomba Shirika la OECD kutoa mafunzo ya kiufundi katika eneo hilo.
“Tanzania itaweza kuimarisha usimamizi wa fedha za umma, kuongeza uwazi, na kuvutia mitaji ya kimataifa inayohitajika kwa utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya 2030” alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), Bw. Mathias Cormann alisema kuwa Shirika lake liko tayari kushirikiana na Tanzania katika masuala ya usimamizi wa sera za kodi na uwekezaji ili kukuza Uchumi wa nchi kwa kuvutia zaidi mitaji kutoka nje ya nchi.
Ameipongeza Tanzania kwa juhudi zake katika kuhakikisha kunakuwa na kodi zenye usawa hususani katika mazingira yaliyopo sasa ya uchumi wa kidigitali na kuishauri walishauri Tanzania ijiunge na Kituo cha Maendeleo cha OECD, ambacho kwa sasa kina nchi wanachama 12 kutoka Afrika.
Bw. Cormann alizitaja faida za kuwa mwanachama wa kituo hicho ni pamoja na kuchapishwa kwa takwimu za mapato ya kodi (Revenue Statistics), ambazo hutoa uwazi kwa wawekezaji na wadau wa maendeleo, na kusaidia nchi kuonyesha uwezo wake wa kifedha kwa taasisi za fedha za kimataifa na wawekezaji binafsi.
Aidha, aliialika Tanzania kushiriki katika Mkutano wa Jukwaa la Misaada kwa Maendeleo Endelevu, utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu, mkutano ambao utatoa nafasi kwa Tanzania kuwasilisha vipaumbele vyake vya maendeleo, kujifunza kutoka kwa wengine, na kuanzisha ushirikiano mpya katika sekta za mazingira, mabadiliko ya tabianchi na uchumi jumuishi.
@MathiasCormann
Jana nilipata nafasi ya kumkaribisha Mhe. Dkt. Abdulelah Ali S Altokhais, Balozi na Mwakilishi Mpya wa Saudi Arabia kwenye UNESCO na kujadili naye maeneo ya kuimarisha ushirikiano katika masuala yenye manufaa kwa nchi zetu na yenye tija kwa jamii ya kimataifa.
On 20th March 2025, Ambassador @AliMwadini visited Canal+ Headquarters and shared insights with Mr. David Mignot, CEO Africa Canal+ Group and Ms. Cathia Lawson-Hall, Vivendi Group Board Member, on cooperation and potential investment in Tanzania.