"..Mi ndo mwana wa mama aliyenifunza kwamba hakuna maisha bora kwa kijana asiyejitunza, hakuna maisha bora kwa kijina asiyejifunza, kujifunza hakuna maana kwa kijana usiyejituma.." @onetheincredibl - Soga za mzawa
Polisi wanasema 02/05/2026 saa tatu asubuhi eneo la Mburahati, Kinondoni alikamatwa Dammour Massoumbe Nyakairo, @Ninja_Damour na kupelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kihalifu (ambavyo hawajaeleza) na kwamba katika mahojiano ya awali ametoa ushirikiano kwa kueleza mambo mbalimbali (kwa mujibu wa taarifa yao). Hatua za kisheria zinakamillishwa ili afikishwe kwenye mamlaka zingine za kisheria.
Kimsingi, tutampa msaada wa kisheria. #FreeNinja #FreeDamour
WATEKAJI WA NINJA WAMEJULIKANA.
Kwahiyo @tanpol mmekaa na @Ninja_Damour kwa zaidi ya masaa 24, ndugu zake wamezunguka vituo vyote vya Polisi mkakana kwamba sio nyie mliomkamata, saizi ndo mnakubali kwamba mnamshikilia?
Ule ni ukamataji wa aina gani, sheria ipi ambayo inaruhusu maofisa wa Polisi kwenda kukamata mtu huku wakiwa wamevaa musk za kufika sura zao na kutumia gari lenye plate number fake?
Halafu siku hizi watu wote mnaowateka, mnawapeleka kwenye karakana yenu ya kutesea watu hapo Chang’ombe.
Nyie ndo watekaji wenyewe, haya mtuambie na ndugu zetu wengine mliowateka akiwemo Balozi Polepole, @mdudenyagali, @DEUSDEDITHSOKA, @DIONIZKIPANYA25 n.k mmewapeleka wapi..?
#FreeNinjaDamour
Tunaongozwa na mihemko sana na inatufanya tunakosa consistency kwenye maamuzi yetu. Leo naona watu wanawasema wanaopush hashtags tena ila after 2 weeks unawaona kwenye post zao wanajichekesha. No wonder wengi wenu ni WASHENZI NA WAPUMBAVU msiokuwa na akili. #FreeNinja
Brother Popote Ulipo Nakuombea Afya Njema Na Urudi Salama Kuungana Na Familia Yako. MUNGU Ampe Nguvu Na Ujasiri Hasa MAMA Yako(MAMA YETU) Katika Kipindi Hiki. #FreeDamour
Kwa nini tusiache hashtag ya #FreeNinja?
1.Inalinda usalama wa mhanga kwa kuweka macho ya dunia kwake.
2.Inazuia tukio kusahaulika au kuzimwa.
3.Inatuma ujumbe kuwa umma unajua na unafuatilia. Paza sauti, usinyamaze
#FREENINJA
Mama amefarijika kidogo kutuona marafiki zake Ninja ila tunajua moyoni bado ana maumivu makali sana! Tuendelee kuifariji familia na kushinikiza ndugu yetu aachiwe huru maana tunajua hana kosa
Kesho asubuhi tukutane Keko kufuatilia taarifa zake kama yupo mahali hapo #FREENINJA
One evening I bumped into Ninja and bro Imma Mwansasu. Felt like we’d all waited for that exact moment. Ninja is a cool guy. Mtu wa watu. We demand his immediate release. Mtendeeni mshikaji wetu kama mtu. We are pained that muda unaenda na giza linaongezeka. Free Ninja!🤲
Wakuu tusiache kupiga kelele hadi mwenzetu apatikane, leo utaona haikuhusu ukanyamaza, iko siku watafika dirishani kwako, tunahitaji kelele ya kila mmoja wetu mwenetu arudi uraiani @Ninja_Damour#FreeNinja
DAMURU apatikane.
Suala la utekaji na upotezaji wa watu limekuwa doa zito katika jamii, likiacha hofu, majonzi na maswali yasiyo na majibu.
Watu wanaotekwa au kupotea mara nyingi ni wale wasio na hatia, huku familia zao zikibaki katika hali ya sintofahamu na maumivu yasiyopimika.
Kinachoongeza uzito wa tatizo hili ni pale ambapo wale waliokabidhiwa jukumu la kulinda raia wanashindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo na wakihojiwa hutoa maelezo yenye dhihaka.
Inapotokea kwamba vyombo vinavyopaswa kuhakikisha usalama vinageuka kuwa dhaifu, au vinahusishwa moja kwa moja au kwa uzembe na vitendo hivyo, basi hali inakuwa hatari zaidi.
Kukosekana kwa uwajibikaji kunafungua mlango wa mazoea mabaya, ambapo utekaji na mauaji vinaweza kuonekana kama jambo la kawaida lisilo na madhara makubwa kwa wahusika. Hapo ndipo imani ya wananchi kwa mifumo ya ulinzi na sheria huanza kuyeyuka.
Ukiona kwamba anayepaswa kumaliza tatizo anashindwa kulimaliza, basi kuna dalili kuwa chanzo cha tatizo si kile kinachoonekana juu juu. Inaashiria uwepo wa mizizi iliyojificha iwe ni uzembe, maslahi binafsi, au mfumo uliooza.
Katika hali kama hii, suluhisho halipo tu katika kushughulikia matukio ya utekaji, bali katika kubadili au kuondoa kabisa mfumo unaoruhusu vitendo hivyo kuendelea.
Hivyo, wito ni wa wazi na wenye uzito: haki lazima itendeke bila upendeleo. Ikiwa kuna mtu anayehusishwa na vitendo hivi, kama DAMARU, basi arejeshwe mbele ya jamii na Familia yake.
Bila hatua thabiti na za dhati, kivuli cha utekaji na upotezaji wa watu kitaendelea kuitanda jamii kwa muda mrefu zaidi.
HAKI ,UKWELI NA UWAJIBIKAJI Vitaliponya Taifa.
BAK MWABUKUSI.