Ukiwa ni Daktari, Askofu, Sheikh, au kwa jina lako lolote, cheo, heshima, umeshuhudia mauaji na ukatili uliosababishwa wakati wa uchaguzi. Halafu ukachagua kukaa kimya, wewe pia ni muuaji. Na utalipwa na Mwenyezi Mungu kama muuaji. Watoto wetu na wajukuu zenu wameuawa wengi sana. Mateso haya yamezidi kipimo cha ubinadamu, na damu isiyo na hatia inamwagika kila siku mbele ya macho ya wale waliopaswa kulinda uhai.
Muuaji mbaya zaidi si yule anayeshika silaha na kuua, bali ni yule anayekaa kimya baada ya kuona mauaji haya. Ukimya ni ushiriki , ukimya ni ridhaa. Kila anayenyamaza wakati wa maovu kama haya, anakuwa sehemu ya maovu hayo. Tusiwe watu wa kukaa kimya tunapoona uovu. Tusiogope kusema ukweli. Ni jukumu letu, kama wanadamu na watoto wa Mungu, kupaza sauti kwa ajili ya haki na maisha ya wasio na hatia.
Spika Ndugai. Tunaokufahamu tunakulilia kwa WEMA WAKO. RIP. Familia. Poleni. Suala la Lissu kufukuzwa Bungeni liliniuma sana. Jioni nikamfuata Spika Ndugai nyumbani kwake Kisasa kumuuliza kulikoni? Mwenzetu wote tunajua yaliyompata?. Utasemaje hujui alipo?
Spika akanieleza kwa utulivu yafuatayo ambayo IN HIS TRIBUTE (kama heshima kwake) ninayaweka wazi. Labda yatasaidia kumuelewa kwa waliokerwa na kauli zake za mizaha (dry humor).
Ndugai aliniambia "Mama ni Maelekezo. MimI nilichofanya kama Spika ni kujaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza Nairobi kutibiwa. Wengine walitaka apelekwe Muhimbili. Hatukuwa na bajeti. CHADEMA hawakuwa na fedha kulipia ndege. Nikamuomba Mbunge wa CCM mhe Turku (RIP) alipie tutamrefund". Akaendelea "Mama Lissu ni mwanasiasa. Akipona atarejea kupambana kadri Mungu atakavyomjalia. Kwa sasa ninakuwa na tahadhari kusurvive katika siasa ngumu za maelekezo huku naongoza muhimili" .
Sikuwa na la kusema zaidi. Nikajua tuna safari ndefu kama taifa. Jamii haitaki kuangalia misingi ya matatizo yetu kimfumo. Tunabaki kulaumu viongozi (personalities) kana kwamba wana freedom kutekeleza majukumu yao. Mfano Utakuta mbunge analaumiwa kwa kutojenga shule, hospitali, barabara. Kwani hiyo si kazi ya Serikali kuu na Halmashauri wanaotoza kodi? Tusimlaumu Ndugai kwa mambo yaliyokuwa ya mfumo. Alipokosea Mungu amsamehe lakini kuna mazuri Mengi alifanya. Apumzike kwa amani.
https://t.co/r6s9OA4SS1
DJ Fete,
Kupitia maumivu ya kusimamishwa kazi kwa sababu ya msimamo wako, najua si rahisi lakini naamini ndani yako kuna kitu kikubwa, msimamo wa kweli, ujasiri na heshima kwa dhamira yako. Walio kusimamisha wana mamlaka ya leo, lakini Mungu ndiye anayeshika kesho.Usiogope. Mara nyingi mlango unapofungwa kwa nguvu, ni ishara kuwa Mungu anafungua mlango mkubwa zaidi , mlango wa heshima, wa uhuru, na wa mafanikio yasiyotegemea mnyororo wa hofu. Endelea kuwa mwaminifu kwa kweli, msimamo, na utu wako maana kesho ni bora kwako kuliko jana.Mbele yako kuna mlango usiofungwa na mkono wa mwanadamu. Much ❤️
NI ZAMU YA VYOMBO VYA HABARI..?
Waandishi wa habari nguli na maarufu wa radio na TV maarufu hapa Jijini Dar es Salaam wamefungiwa na Bodi ya ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) kutangaza au kufanya kazi ya uandishi wa Habari kwa kile kinachoitwa "kushindwa kujisajili katika bodi ya ithibati"
Mpaka naandika habari hii Wahusika na mwaajiri wao wamefanya siri kwa mujibu wa maelekezo waliyopewa na serikali kuwa "wasifanye kazi ya uandishi wa habari na wasiseme lolote kuhusu kuzuiwa kwao"
Kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha sheria ya huduma za habari sura ya 229 kina weka masharti kuwa
"waandishi watakaoshindwa kujisajili hawataruhusiwa kufanya kazi za kihabari"
Waandishi hawa wamewekewa kikwazo hiki baada ya kuwa mwiba katika vipindi vyao na mahojiano yao kwa wakati huu nchi inapoelekea katika uchaguzi Mkuu
Uchunguzi unaonyesha Masoud Kipanya ameingia katika kifungo hiko baada ya kuchora mchoro wa katuni uliowakasirisha watawala uliolenga kutaka media zisitumike kama Toilet Paper
Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Tanzania Balile aliongea na kuonyesha hadharani kukasirishwa na mchoro huo huku akiahidi Masoud Kipanya achunguzwe na mamlaka za nchi.
Masoud Kipanya na Ciza Wameshindwa kujisajili kwa sababu ya kukosa sifa ya kusomea taaluma ya uandishi wa Habari kinyume na sheria kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 24 cha sheria ya huduma za habari sura ya 229.
Rungu la namna hii pia linaonekana kumkumba mwanahabari na Mkurugenzi wa Jambo TV, John Marwa ambaye amekuwa mwiba katika mahojiano mbalimbali na kuendesha vipindi vilivyo wakwaza watawala.
Duniani kote watu wenye uzoefu na kazi ya uandishi wa habari kwa zaidi ya miaka 10 kama Masoud Kipanya, SIZA, na John Marwa walipaswa automatically kuwa na sifa za kusajiliwa na bodi ya ithibati ya Waandishi wa Habari kwa kigezo cha uzoefu na muda waliofayia kazi tasnia ya habari.
Hawa ni baadhi ya Waandishi wa Habari wakubwa Duniani ambao hawakusomea taaluma ya uandishi wa Habari Anderson Cooper (CNN na ABC News) Stephen A. Smith (ESPN) na Trevor McDonald (ITN na ITV)
N.B
Kwa upande wa mmoja mtangazaji maaurufu wa radio na Tv kutoka ofisi hiyo hiyo, kwake maarufu kama imekuwa tofauti kidogo. Pamoja na kukidhia sifa zote za Sheria ya Huduma ya Habari na Kujisajili katika Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari
Wenye Mamlaka wamepiga simu kwa mwajiri wake na kumtaka aondolewe katika majukumu yake kwa kile walichokiita "mkosoaji sana"
Boniface Jacob
The voice of the Silenced Majority.
@babbiekabae Kuwa tayari kupoteza kila unachodhania huwezi poteza, Trust less in your circle keep family close and above all Keep God first he will take you places beyond your imagination.
Binafsi, nakubaliana kwa 100% na #noreformsnoelection. MaCCM ni maharamia na hayana huruma katika kulinda maslahi yao. MaCCM hayaoni tatizo kufunga, kuteka, kupoteza, kuua katika uchaguzi. Hivyo, jambo lolote la kuzuia uchaguzi usifanyike kama hakuna ‘reforms’, naliunga mkono.
Ndoa ngumu sana, rafiki yangu ameoa juzi tu hapa, leo ananitext ananiambia, mzee hivi wewe umewezaje?
Mbona mimi inanishinda hii, najiona kabisa natupa taulo!!
Nimeogopa sana, na sio ndoa tu, mahusiano in general ni magumu sana.
Mamlaka ya @tanzaniairports kupitia wafanyakazi wenu na washirika wenu mnawakamata madereva wa Taxi mtandao na kuwanyanyasa kwa kusingizia hawaruhusiwi kufanya kazi hapo na wanalipa kodi @TRATanzania wanalipa vibali vya LATRA
Hii si haki kwa mnachokifanya kwa kushirikiana
Watu wakiona Vijana mtaani wametulia Vijiweni wanahisi hawapambani na hawako serious na maisha, ila kichwani mwa Vijana wengi kuna vita kali zinapigwa kuliko Somalia ama Iraq.
Wanapoamua kutabasamu licha ya matatizo ni kuwa wanathamini baraka ya uhai, wanaamini KESHO ni yao! Kama huwezi kuwapa moyo basi usiwakatishe tamaa.
@JMakamba@ewuratz@TPDCTZ@MsigwaGerson@ikulumawasliano@SuluhuSamia TUNAOMBA SURUHISHO LA KUDUMU JUU YA GAS (CNG) IWEZE PATIKANA LA SIVYO VITENDO VISIVYO VYA KIUNGWANA VITAKUJA TOKEA IWE TOO LATE MAANA WATU ZAIDI YA ELFU 3 KUTEGEMEA KITUO KIMOJA NI UJINGA USIOINGIA AKILINI..
@TPDCTZ@ewuratz@wizarayanishati@MahimbaliK@JMakamba HII NDIO DHAHAMA TUNAYOKUTANA NAYO WATUMIAJI WA NISHATI MBADALA WA GAS (CNG) KATIKA MAGARI YETU, KUMEKUWA NA KERO YA KITUO KIMOJA ILA WAHUSIKA MNAJIFANYA HAMUONA NA MAGARI ZAIDI YA ELFU 3 KUTEGEMEA KITUO KIMOJA @MsigwaGerson
@MsigwaGerson@JMakamba@ikulumawasliano@SuluhuSamia TUNAOMBA TUPATE SURUHISHO LA KUDUMU KATIKA UJAZAJI WA NISHATI MBADALA KATIKA MAGARI YETU MAANA TUMECHOKA NA UNYANYASAJI HUU NA KUTESEKA HUKU MNATUSHAWISHI TUFUNGE MAGARI GAS ALAFU SHIDA INAKUWA HIVI,