@pastajoshuatz Mwanangu Kama kawaida huyo mtoto anae zungusha nyonga Kama feni bovu anapatikana maana ile package ya Mdinda dinda inabidi imfanyie kazi
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 63
Mhe. Lissu : ulisema hizo video zilikuwepo kwenye mitandao mingine?
George: P ndio alisema.
Mhe. Lissu : Je hukuwa na interest kujua umechapisha kwa mitandao mingine?
George: Sikuwa na interest mimi.
Mhe. Lissu : Waeleze majaji kama umesoma maelezo ya Mahamba.
George: Mimi sikusoma.
Mhe. Lissu : kwahiyo kumbe hukusoma maelezo ya Amin Mahamba?
George: Sikusoma ndio.
Mhe. Lissu : Hizi video clip zilifanyiwa uchunguzi wa kitaalamu cyber forensic analysis?
George: Ni kweli kabisa zilifanyiwa.
Mhe. Lissu : Eribariki Kahaya ndio alifanya kazi hiyo?
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : ni sahihi Kahaya alisema camera iliyotumika ni aina ya Sony
George : Maelezo yake sikusoma na yeye ni shahidi atakuja kutoa.
Mhe. Lissu : Na Kaaya alisema hayo maneno yakiwekwa mtandaoni na Jambo Tv?
George: Mimi sikusoma maelezo yake.
Mhe. Lissu : Waeleze Kama ulisoma maelezo ya Andrew Churu. Yule askari wa Dodoma.
George: Ya Andrew Churu sikusoma, mimi ilisoma ya P.
Mhe. Lissu : maelezo yako uliandikiwa na nani?
George: Niliandika Mwenyewe.
Mhe. Lissu : Je kabla ya kuandika maelezo hayo uliomba ushauri wa kisheria wa mwanasheria yoyote?
George: Sikuomba ushauri kokote.
Mhe. Lissu : Naomba usome kifungu cha 11(4) cha CPA. Ulisema umeandika kifungu cha 11(3)?
George: Ni kweli.
Mhe. Lissu : Ni sahihi hicho kifungu hakiruhusu mtu kujiandikia mwenyewe?
George: Kinaruhusu unaweza kujiandikisha. Kama nilivyoeleza hakuna kifungu kinachozuia na mimi ni Police officer nilijiandika mwenyewe.
Mhe. Lissu : Nani aliyekuonya? Nani aliyekukanya? Section 10(3) of CPA.
George: NI MIMI MWENYEWE NDIO NILIJIKANYA.
Watu wanacheka.ππππ
Mhe. Lissu : Nani alithibitisha pale chini baada ya maelezo yako?
George: Ni Mimi Mwneyewe, nilijiandika, nikajikanya na kujithibitisha mwenyewe.
Mhe. Lissu : ulisema mimi nina kiapo cha JKT nilitoa kinyume na kiapo changu?
George: Ni kweli nilisema hivyo.
Mhe. Lissu : Je wewe umewahi kwenda JKT?
George: MIMI SIJAWAHI KWENDA JKT.
Mhe. Lissu : Nilikwenda JKT kambi gani?
George: Mwaka 1989 ulianzia mafinga iringa na baadae ukaenda Itende Mbeya ukapewa namba fulani anaitaja hapa. Ulifuzu na kupewa cheti.
Mhe. Lissu : Je ulikuwepo mwaka 1989?
George: Sikuwepo.
Mhe. Lissu : Je ulikuwepo Itende?
George: Sikuwepo hata Itende ila wewe umegombea urais taarifa zako zinajulikana.
Mhe. Lissu : ulikiona cheti changu cha Itende?
George: Nimeona copy yako.
Mhe. Lissu : Sasa waeleze Majaji kama hayo uliyosema yapo kwenye maelezo?
George: Hayapo.
Mhe. Lissu : Kama nilienda jeshini miaka 39 mimi ni mwanajeshi?
George: Wewe ni askari wa akiba.
Mhe. Lissu : Soma ibara ya 147(4)
Mnakaa huko mnadanganyana hamjui mambo mnajifanya mnajua.
Jaji anasema Mshitakiwa tafadhali.
George anasoma Katiba sasa Mwanajeshi maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au kudumu katika jeshi la polisi, lawananchi, au la magereza au polisi.
Mhe. Lissu : Sasa waeleze majaji kama mimi nimeajiriwa kwa muda katika mojawapo ya hayo majeshi.
George : Wewe umeajiriwa na JKT.
Mhe. Lissu : Je kwenda JKT mwaka 1989 na 1990 je nilikuwa nimejajiriwa?
George: Hukuwa umeajiriwa.
Mhe. Lissu : nilivyomaliza nilikuwa nimeajiriwa?
George: Hukuwa umeajiriwa.
Mhe. Lissu : Kwenye Katiba kuna maneno askari wa akiba?
George: Hayapo kabisa kwenye Katiba.
Mhe. Lissu : Waeleze kama umewasilisha hati ya kiapo cha utii cha kwangu hapa mahakamani?
George: Sijakiwakilisha mimi, sijaleta hapa.
Mhe. Lissu : Je mtu yeyote aliyepitia JKT anakuwa mwanajeshi milele? Askari wa akiba anatambulika kikatiba?
George: Anatambulika.
Mhe. Lissu : Hawa maaskari wa akiba wana masharti na askari wengine?
George: Ndio.
Mhe. Lissu : Je Kikwete Ruten Kanali ni mwanajeshi alikuwa?
George:Ndio alikuwa mwanajeshi.
Part 64 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 62
Mhe. Lissu : Kifungu cha 39(2)d lengo la uhaini kionekane kwa maandishi in writing, publication or any overt act?
George: Ni sahihi iko hivyo.
Mhe. Lissu : Neno publish maana yake nini soma kifungu cha 3 cha cyber crime act ili tujue maana ya kupublish?
Georgia anasoma hapa kwanza, Publishing means distributing, transmitting, disseminating, printing or offering for sale. Umemaliza?
George: Naendelea kidogo.
Mhe. Lissu : Swali langu sasa shahidi kwa maelezo yako mwenyewe aliyepeleka kwenye mtandao wa Jambo TV ni nani?
George: mfanyakazi wa Jambo Tv.
Mhe. Lissu : Kwa mujibu wa ushahidi wako wewe na P aliyerusha maneno hayo ni P?
George: Hapana, aliyerusha ni wewe Lissu na P.
Mhe. Lissu : kama nilichapisha mimi na P kwanini P hajashitakiwa?
Mhe. Lissu anamwambia George tutafika tu mmezoea kuwasingizia watu kwa makesi ya uongo ila Tutafika tu.
Anatafuta maelezo ya P hapa.
Ameyapata, sasa waonyeshe majaji kuwa P alisema Mh. Lissu alitutoa nje ili tusisikie maneno fulani fulani.
Anaangalia hapa Afande George.
Jibu lake tunasubiri muda huu.
George ametoa macho kama mtu aliyejinyonga kwa kamba.π
Anangalia kwenye maelezo uniambie kama P alisema Lissu alitutoa nje ili kuna maneno tusisikilize.
Anasoma hapa kwamba "walibaki wenyewe Chadema wakatutoa kuzungumza mambo yao"
Mhe. Lissu: Kuna mahali kuna jina la Lissu.
George: Halipo hilo jina, halipo jina la Lissu.
Katuga amesimama ukisoma kifungu cha 170 cha Evidence kama kuna maswali ambayo yanamuonyesha shahidi hafai, anaitwa Nshomile tunaomba haya ya umeiba vyeti haya asiambiwe. Kama kuna tuhuma za kuiba vyeti akafungue kesi.
Mhe. Lissu : basi nitamuita msomi wa polisi.
Mhe. Lissu : Umesema mimi ndie niliyewaalika waandishi wa habari? Ile tar. 03/04.
George : ndio ni wewe ndie uliwaita.
Mhe. Lissu : Je niliwaita kwa njia ya simu?
George: Sijui uliwaita kwa njia ya simu.
Mhe. Lissu: Je barua?
George: Sijui kwa njia gani? Mimi sijui uliwaita kwa njia gani?
Mhe. Lissu : Je nilitangaza magazetini?
George: Sijui mimi ulifanyia wapi?
Mhe. Lissu : Je wewe ni polisi wa aina gani ambae hujui mkutano ulifanyika wapi?
George : HUKUTUALIKA.
Mhe. Lissu : Hujui niliwaalikaje?
George: Sijui njia uliyotumia kuwaalika.
Mhe. Lissu : Je ulimuhoji Katibu Mkuu wa Chadema kuhusu utaratibu wa kualika waandishi?
George: Sikumuhoji.
Mhe. Lissu : Je Amani Gorugwa ulimuhoji?
George: Sikumoji.
Mhe. Lissu ;Ulimhoji Brenda Rupia ulimuhoji kuhusu utaratibu wa kuita waandishi?
George: Nilimuita lakini hakuja.
Mhe. Lissu kwahiyo ulimuhoji?
George: Sikumuhoji.
Mhe. Lissu: Hujui walialikwaje? Hujui nani aliwaalika? Ila unang'ang'ania ni Tundu Lissu ndio alialika.
George: Mimi sijui kwakweli.
Mhe. Lissu : waeleze majaji kama mimi ni mmojawapo wa wakurugenzi wa Jambo TV.
George: sina uhakika na hilo.
Mhe. Lissu : je mimi ni mmoja wa waandishi wa habari wa Jambo Tv
George : sina uhakika na hilo pia.
Mhe. Lissu : Ni kweli au si kweli hizo video zilipatikana kwenye mtandao wa Jambo Tv?
George: Ni kweli zilipatikana huko Jambo TV.
Mhe. Lissu : je unafahamu mimi nina password za mtandao wa Jambo TV uliwaambia hilo majaji?
George: Siwezi kufahamu kama unazo.
Mhe. Lissu : Kama inawezekana kitaalamu kwa mtu asiye na password kuingia na kuweka chochote?
George: Sijui uliingiaje na uliwekaje hizo video.
Kumbukeni jamani kosa lake wanasema alitoa na kusambaza. Hapa anashughulika na kipengele cha kusambaza. ππππ
Part 63 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 60
Mhe. Lissu : wakati unaongoza hiyo timu ulisema, Tar. 06/04 ulimtafuta Mkurugenzi wa Jambo TV John Marwa?
George : siwezi kukutajia ila nilipata namba ya kiongozi wa Jambo TV sikujua jina lake kama ndio Marwa.
Mhe. Lissu : Huyu Kiongozi wa Jambo TV uliyemtafuta ulimuomba akupatie hiyo video clip halisi iliyochukuliwa kwenye mkutano?
George: Ni kweli.
Mhe. Lissu : ni kweli huyo kiongozi alikwambia mfanyakazi yupo Dodoma?
George: Ni kweli, alinipa namba ya simu pia ni kweli ya huyo mfanyakazi wake.
Mhe. Lissu : ni kweli namba hiyo ulimpa DCP Ng'anzi?
George: Ni kweli nilifanya hivyo.
Mhe. Lissu : ni kweli Ng'anzi alimpatia Andrew Churu yule Polisi mwingine?
George: Hilo sijui kwakweli.
Mhe. Lissu : ni kweli tar. 07/04 DCP Ng'anzi alisema amempata huyo aliyerekodi?
George: Ndio ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Na memory card nayo alikwambia imepatikana?
George: Ni kweli aliniambia hivyo.
Mhe. Lissu : Ni kweli DCP Ng'anzi alikwambia kwamba memory card na card reader yake vitaletwa siku hiyo hiyo na Andrew churu ofisini kwako?
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Ni kweli au si kweli kwamba siku ya tar. 07/04 Andrew Churu alisafiri kutoka Dodoma hadi ofisini kwako na kufika usiku?
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Je alikuja na hizo card, na vitu vingine?
George: Ni sahihi alikuja navyo na alikuja pia na hati ya makabidhiano.
Mhe. Lissu : acha kiherehere hiyo hati sijakuuliza.
Mhe. Lissu : je ulisoma maelezo ya P hiyo tarehe 07 ulivyoletewa.
George : ni kweli nilisoma.
Mhe. Lissu : Kwa vile ulisoma, kweli au si kweli huyo P alisema ni yeye ndie alirekodi mkutano na ni yeye alirusha kwenye Jambo TV akaunti?
Anamtafutia maelezo ya huyo P na anamwambia ayasome.
Anasoma George "kuwa mimi nakumbuka mkutano ...β
anasimama Katuga anasema haya maelezo sio yakwake shahidi kwahiyo asiulizwe.
Mhe. Lissu anajibu shahidi mwenyewe ndio kasema kuwa alipelekewa maelezo na huyo P akasoma, na maelezo hayo ndio yanasema nani alichapisha?
Majaji wanasema msomee wewe tafadhali.
Mhe. Lissu anasoma kuwa P anasema ni wao Jambo TV ndio walikuwa wanarusha. Na wao ndio walirekodi.
Mhe. Lissu : Je mimi ndie niliesambaza na kuchapisha?
George : ndio ni wewe uliyechapisha.
Amesimama Katuga Mh. Tunaomba twende kwenye health break tutaendelea.
Mhe. Lissu anasema sawa twende maana huyu shahidi ili nimalizane nae nahitaji siku zingine kama mbili au tatu. Kwahiyo bado tuko nae sana. Siwezi kumuacha haraka.
Majaji wanaandika hapa kidogo.
Sasa twende break tutarudi saa tisa mchana.
Part 61 itaendelea tukitoka break
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 59
Naona George kapewa PGO
Anaisoma hapa kuhusu duties of regional and division crime officers.
Inasema investigators watakuwa responsible kwa maboss wao.
Mhe Lissu : Ni kweli wewe kama kaimu ZCO ulikuwa unawajibika kwa Murilo kama Boss wako?
George: aaah! eeeh unajua
Mhe Lissu : ni kweli au si kweli kama acting ZCO ulikuwa unawajibika maelekezo kutoka kwa ZPC.
George: Ni sahihi nina channel mbili.
Mhe. Lissu : Kwa mujibu wa PGO hii ulikuwa unawajibika kumpa taarifa ZPC ni sahihi?
George: Ni sahihi na alikuwa anapata taarifa na kila hatua alikuwa anapata.
Mhe. Lissu : turudi kwenye maelezo yako ya shahidi yote kuna mahali kokote umemtaja ZPC
George: Kwa maelezo haya hakuna nilipomwandika.
Mhe. Lissu : Je kuna mahali ulisema ulikuwa unampa taarifa, kuna mahali umesema?
George : Kwenye maelezo hakuna hilo jambo, sijasema kwenye hayo maelezo.
Mhe. Lissu :Je kuna mahali ulisema Muliro amekupa maelekezo yoyote hapo?
George: Hakuna mahali nimesema hilo kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu : wambie majaji Mafwele alirudi kazini lini?
George : kama sikosei kati ya tar. 01 au 02 mwezi wa 5 kwahiyo nisingeweza kumtaja. Unajua upelelezi uliendelea
Mhe. lissu anamdakia kwa juu Kaka unajibu maswali yangu acha rongorongo.
Mhe. Lissu : ni kwelI Dcp Ng'anzi alikuletea Boss mpya anayeitwa Amin Mahamba?
George: ni kweli alifanya hivyo.
Amin kama ile ya Idd Amin lissu anasema hivyo π
George : Tar. 08/04 ndio alimleta ACP Amin Mahamba.
Mhe Lissu : Ni sahihi nikisema kuanzia tar. 04 hadi 08 ni sahihi wewe ndio uliongoza hiyo timu? na alipokuja Amin akaanza.
George ni sahihi Mahamba ndio akawa kiongozi.
Mhe. Lissu : Je Amin alilichukua jalada likiwa la uhaini au la uchunguzi?
George ; lilishakuwa la uhaini tayari.
Mhe. Lissu : wewe ndie uliyefanya maamuzi ya kulifanya liwe jalada la uhaini na sio Mahamba Amin.
George : Ni mimi ndie niliyeamua.
Mhe. Lissu nimefurahi sana. Mimi napenda kukamata waongo. Ngoja tumsubiri Amin Mahamba.
Mhe. Lissu : wambie majaji kwamba aliyekwambia kwamba ufungue uhaini ni Kingai?
George: si kweli, nilivyoona element zimekamilika nikaelekeza mimi mwenyewe.
Mhe. Lissu : hizo siku nne ulizochunguza kama ulitoa taarifa ya ofisi ya DPP au hukutoa? Nina maelezo yako kumbuka.
George : Kwamba?
Mimi kama mimi sikutoa hiyo taarifa na sikumwambia ofisi ya DPP.
Mhe. Lissu : Miaka yako 22 ya Upolisi umewahi kufanya uchunguzi wa appendix C makosa ambayo yanashughulikiwa na watu wa ngazi yako.
George: hizo za appendix C.
Mhe. Lissu: usiwe na kimbelembele
Mhe. Lissu : sasa waeleze kama umewahi kufanya uchunguzi wa kesi ya aina hii.
George : publication ya false information ya Dr. Slaa.
Mhe. Lissu : Iliishia wapi?
George Hiyo sikumbuki iliishia wapi,Kesi nyingine ya Lembeli, alikuwa Mbunge
Mhe. Lissu: iliishia wapi?
George : kimya
Mhe. Lissu : waeleze majaji katika miaka yako 22 umewahi kufanya kesi ngapi mtu muhimu kisiasa ni mshitakiwa. Mfano Kama Tundu Lissu? Nataka kujua kama una uzoefu.
George : Kesi ya nne nae iliondolewa ya John Heche Tarime iliondolewa kule Tarime akimuita Rais wa Nchi ana akili ya Tope.
Swali: Je iliishia wapi?
George: Nayo baadae iliondolewa.
Mhe. Lissu : kwahiyo miaka 22 yako ya Upolisi hujachunguza kesi yoyote ya makosa ya aina hii hajapatikana na hatia?
George : ni kweli hakuna ambae aliwahi kukutwa na hatia.
Mhe. Lissu : Kuna yeyote ukiachana na hii ambayo mahakama ilifikia mwisho mahakama ikatoa hukumu?
George: zote hazikufika hatua ya judgement.
Part 60 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 58
Mhe. Lissu : ukaelezea sababu za kumwambia kufungua jalada kwamba ulitaka kujua kama ni halisi au laa?
George: Ni kweli kabisa ilikuwa hivyo.
Mhe. Lissu : hayo maelekezo kwa Michael Gyumi ulitoa tarehe ngapi?
George: Ilikuwa Tar. 04/04/2025.
Mhe. Lissu : waeleze majaji kama hayo maneno kwamba ulimuelekeza Michael Gyumi afungue hilo jalada tar. 04/04.
George : yapo hayo maelezo.
Mhe. Lissu amempa maelezo asome ili kuonesha hayo maelezo. Anayasoma hapa.
Mhe. Lissu: Tafuta sehemu ambayo tar. 04 ulimuelekeza Michael Gyumi afungue hilo jalada. Naona unasoma tu hueleweki hata unasoma nini?
Shahidi anatafuta hapa.
Kimya kidogo.
George: Niliamuru jalada kufunguliwa ila Jina la Insp. Gyumi halipo kiukweli.
Mhe. Lissu : Je nilitaka kujua kama hiyo video halisi au laa?
George: Hayo maneno hayapo kwenye maelezo yangu
Mhe. Lissu : wakati unaangalia sehemu sehemu za video clip ulisema ulikuwa na police notebook na kuandika aliyokuwa anakwambia Kaaya.
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Je hayo maneno kwamba ulikuwa na Police notebook yapo kwenye maelezo yako au hayapo?
George : maneno hayo hayapo kabisa, ningeandika kurasa 200.
Mhe. Lissu: Kweli au si kweli kwamba ASP Gyumi linajitokeza Tar. 08/04 kwa mara ya kwanza?
Anamsomea alichoandika tarehe 08.
George : si kweli alishaonekana nilitaja timu mimi.
Mhe. Lissu : wambie majaji kama umewahi kutaja majina ya hiyo team yako?
George: Hiyo timu sikuwahi kutaja kabisa.
Mhe Lissu : Je ASP Kaaya alikuwa ni mmoja wa hiyo timu?
George : Yeye hakuwepo kwenye hiyo timu alikuwa anapeleleza kivyake.
Mhe. Lissu : Je Andrew Churu alikuwepo au hakuwepo?
George: Huyo nae hakuwepo.
Mhe. Lissu : Je ASP malugala nae alikuwepo kwenye timu uliyounda wewe?
George: Hakuwepo pia.
Mhe. Lissu : Je Elibariki Kaaya?
George: Hakuwepo.
Mhe. Lissu : Katika hati yako ya ushahidi kuna jina la Polisi yeyote ambae uliyeunda wewe lipo kwenye orodha ya hiyo timu yako.?
George : kuna timu mbili hapo,
Alikuwepo ASP Michael Gyumi, ASP Ibrahim, Senior Superitendent Reuben Mwakabonga, ASP Nunu, Detective Koplo Ibrahim, Mimi Mwenyewe, Detective Copro Ramadhani.
Mhe. Lissu : wote uliowataja na hao wengine saba kuna mahali umewataja kama timu ya upelelezi?
George : Kwenye maelezo yangu sijawataja.
Nafikiri hawa ndio wasiojulikana leo tumetajiwa pia.ππππ
Mhe. Lissu : Tar. 07/04/2025 ulisema majira ya mchana nilimuelekeza kupakua na kuitunza kwenye flash disk?
George: Ni kweli kabisa nilimwambia hivyo.
Mhe.Lissu : Naomba uwasomee Majaji maneno yanayoanzia siku ya tar. 07/04/2025 mpaka yanapoanza tarehe 08/04/2025.
Kwenye hayo maelezo hakuna mahali kokote kuwa ulimuagiza apakue hiyo clip, ni kweli au si kweli.
George : hayo yapo.
Mhe. Lissu: haya soma tuone.
George anasoma hapa ila Sauti imekauka anatetemeka.πKumbe na wao kuna mahali huwa wanakuwa wadogo.
Mhe. Lissu : Sasa yote uliyosoma kuna mahali nilimuelekeza Kaaya kuipakua.
George : Kwa haya niliyosoma sasa hivi hayupo huyo mtu anayeitwa Kaaya.
Mhe. Lissu : umemtaja hapa DCP Ramadhani Ng'anzi?
George: Ni kweli nilimtaja
Mhe. Lissu : Na kwenye ushahidi wako jana ulisema kwamba baada ya kufungua jalada ulimpigia DCI Ramadhani Kingai?
George: Ni kweli anaitwa Kingai.
Mhe. Lissu : na ulisema ulimpa taarifa kuhusu jalada hilo la uchunguzi?
George: Ni kweli nilifanya hivyo.
Mhe. Lissu : na alikwambia mawasiliano nae uwe unapitia kwa Ramadhani Ng'anzi ndo alivyokwambia Kingai?
George : ni kweli aliniambia hivyo kwenye jalada hili.
Mhe. Lissu : hata mimi nakuuliza kuhusu jalada hili.
Mhe. Lissu : je unafahamu kuhusu Chain of command?
George: Nafahamu vizuri.
Mhe. Lissu : ni kweli au sio kweli Boss wako ni ZCO wewe kama Deputy wake?
George : Ni kweli.
Mhe. Lissu : ZCO Boss wake ni ZPC?
George: Yes ni kweli Boss wake ni ZPC.
Mhe. Lissu : Nataka unisomee 6(16) PGO.
Part 59 inaendelea post inayofuata,
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 56
Wamemaliza amesimama Lissu kujibu hilo pingamizi.
Kwa vile ni sheria.
Shahidi amesema yeye hana shida maelezo ni yake na yapokelewe.
Mawakili wake hawataki kabisa yapokelewe wanasema kama lengo ni kufanya impeachment sasa kama hana lengo hilo wamejuaje mapema hivi kwamba yasipokelewe kabisa.π Ngoja tuone lakini.
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji nimewasikiliza mawakili wa serikali na jibu langu ni fupi, nakubaliana nao, nakubali kuwa nilikosea kuanzia hatua ya tatu ili nisipoteze muda niko tayari nianze upya kwa utaratibu ambao mahakama ya rufani imemuelekeza.
Anasema siwezi kufanya ilivyo sahihi kwasababu ya Estoppel. Kwasababu I'm estooped.
Kifungu cha 131 cha Evidence Act kinasema ukifanya jambo na upande mwingine ukachukua hatua, Mawakili wa serikali wamepinga wakati nyaraka bado haijapokelewa na mimi nimewakubalia.
Estopel haihusiki hapa hili jambo wao linawaathiri nini kama shahidi ni wakwao na maelezo ni ya kwao.
Hakuna wanachoathirika.
Majaji wanaandika hapa
Anaitwa Katuga kwa ajili ya rejoinder anasema kifungu cha 131 cha Evidence Act kinatuzuia kurudi nyuma anapokuwa amekosea.
Intentionally kinatuzuia, tunamalizia kuwa pingamizi letu liko kishseria na limeletwa kwa ajili ya kulinda integrity.
Lissu anasema hii ya integrity nayo kaitoa wapi? Katuga anasimama anasema basi naomba niitoe.
Watu wanacheka ππππ
Wanaandika majaji kwa muda sasa kama dakika 15 hivi
Wamemaliza na kuanza kujadili kidogo.
Majaji wanasema ni endapo una concede PO mahakama inapaswa kufanya nini?
Mahakama ya rufani imeshatoa maelekezo kwahiyo PO kama itakuwa sustained basi itakuwa sustained na kuidismiss kwasababu upande wa Pili na inareject hiyo nyaraka. Nyaraka haijapokelewa.
Maswali yanaendelea sasa.
Mhe : Elimu yako ulisema jana. Ulisoma kozi ya kwanza Moshi mieizi 6?
George : Ni kweli.
Mhe.Lissu : na baada ya hiyo course ukafuzu na kupata cheti? Jibu: Ni sahihi kabisa.
George : ukaajiliwa kama Polisi Constable?
George : ni sahihi kabisa.
Mhe.Lissu : Baada ya hapo ulienda kusomea Course ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi hapa Dar es Salaam.
George : Ni kweli.
Mhe.Lissu : hayo mafunzo ya mkaguzi msaidizi wa polisi yalichukua miezi mingapi?
George : Miezi 9.
Mhe. Lissu : na baada ya hiyo miezi 9 ulipata cheti?
George: Kweli nilipata cheti.
Mhe. Lissu : Ukapandishwa cheo pia?
George : Kweli nilipandishwa cheo kuwa Assistant Insp. of Police.
Mhe. Lissu : Sasa shahidi baada ya mafunzo hayo ulienda kusoma course ya tatu, Gazette officers course
George : ni sahihi kabisa, nilienda chuo cha Polisi Dar ni kweli.
Mhe. Lissu : na ulisoma kwa miezi 9.
George : kweli kabisa,
Anasema kweli kwa nguvu sana huyu shahidi.π
Mhe. Lissu : Baada ya hapo hujawahi kusoma tena na kupata cheti hadi leo? Kwa mujibu wa ushahidi wako?
George : nimesoma course nyingine ndogondogo.
Mhe. Lissu : Sijakuuliza ndogo ndogo.
George: Nimesoma refresher course kwa mwezi mmoja.
Mhe. Lissu Chuo gani?
George: Mwezi mmoja pale Kidatu. Nikapata cheti.
Mhe. Lissu : na Chuo gani kingine?
George: Mubarak Police Academy kule Egypt miezi miwil kipo Cairo.
Mhe. Lissu : Ukapata shahada gani?
George: Nikapata vyeti viwili pale.
Mhe Lissu: Sasa naomba uwaeleze majaji kama kuna mafunzo mengine uliyohudhuria yaliyokupa kitu kingine zaidi ya Cheti? Nataka kujua mafunzo mengine uliyowahi kupata.
George : nina advance diploma ya uhasibu nilimaliza 2001, Post Graduate Diploma in finance Chuo cha Sauti.
Part 57 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 55
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe Lissu : umeyapata eee?
George : nimeyapata.
Mhe Lissu. Sasa waeleze majaji hivyo ni vitu gani? anza na ya kwanza tafadhali.
George : Ya kwanza ni karatasi ya maelezo yak wangu SSP George.
Mhe. Lissu . Hati ya maelezo yako? Sahihi ni yangu.
George : ya pili pia ni maelezo yangu ya Nyongeza ya tarehe 10.
Mhe.Lissu : je hayo maelezo yana sahihi na wamabie ni za kwako?
George : ni za kwangu sahihi zote.
Mhe. Lissu : Wambie majaji kama ni za kwako kama uko tayari ziingie kama ushahidi wa vielelezo vya utetezi?
George : Hii ya kwanza niliandika
Mhe.Lissu : umeelewa swali langu kweli?
George : niko tayari ziingie mahakamani kama sehemu ya ushahidi.
Mhe. Lissu : Waheshimiwa Majaji naomba hizo nyaraka ziingie kama kielelezo E01.
Anasimama Wakili wa Serikali: Renatus Mkude sijui anataka kusema nini.
Anasema Wah. Majaji naomba Igans semboka aseme. Anasimama Ignas hapa. Waheshimiwa Majaji sisi upande wa Jamhuri mshitakiwa hajazingatia taratibu kwasababu misingi ya kisheria ya maelezo ya shahidi ni kwa ajili ya impeachment purpose na waheshimiwa majaji utaratibu wa kuzingatiwa wa namna ya kuwasilisha maelezo umefafanuliwa na maamuzi lukuki wa mahakama ya rufani ni kifungu cha 154 ambacho kwa sasa ni kifungu cha 163 kwenye R.E 2023. Kinasomwa kwa pamoja na 164 na 173 vya EVIDENCE ACT.
Kimsingi katika vifungu hivi anaweza kuempeach kwa kumuonesha maelezo yake na akitaka kumuonesha lazima afuate utaratibu.
Naomba niwarejeshe katika mashauri matatu.
Shadrack Sospter Mkaruka Mangangari vs Jamhuri Rufaa No. 233/2022 Tanzlii 14/03/2025.
Lilian Jesus vs Jamhuri shauri la rufaa no. 151/2018 Mahakama ya Rufaa.
Shauri la Mahakama ya rufaa ambalo la Ruchere Mwita vs Jamhuri shauri la rufaa no. 348/2013.
Waheshimiwa Majaji mashauri haya yote yalieleza utaratibu wa kuzingatia na naomba ninukuu.
Mhe. Lissu: wanaaongea hizo kesi hawanipatii, wanasema ziko tanzlii mfungwa anafikaje huko.
Jaji: mpatieni tafadhali.
Kumbe hawana. Wameambiwa wakatafute.
Sasa anaendelea.
Mh. Jaji kwenye kesi zote tatu Mahakama ya rufaa ilisema
Jaji huwezi kusema kesi zote tatu, tuambie unasoma kesi gani muda huu.
Wakili: samahani Jaji ni ukurasa wa 26 kesi ya Jesus hii Mahakama ilisema kuhusu hatua za ku impeach shahidi.
Shauri la Jamhuri vs Mnawara hamis Nyanda na wenzake 9 la mwaka 2022. Tanzlii. Jaji Manyanda alisema zipo taratibu 8 za kuzingatia maamuzi ya maelekezo ya mahakama ya rufani.
Hivyo Mh. Jaji tunaona mshitakiwa hajazingatia vigezo.
Anasimama Ajuaye Wakili wa Serikali, Waheshimiwa Majaji lengo la kutumia maelezo ni msimamo wa sheria kwamba yanatumika kwa impeachment peke yake.
Test credibility ya shahidi na yale aliyoyaandika kabla ya kuja mahakamani na ndio maana S.
163 Cap.6 R.E 2023 anakisoma na kukifafanua anavyojua yeye.
Kwahiyo tunaona procedure hazijafuatwa na ombi lake lisikubaliwe.
Anasimama Katuga anasema Waheshimiwa Majaji naunga mkono kilichosemwa na mawakili wenzangu ni msimamo wa sheria kwamba kielelezo kabla hakijapokelewa ni msimamo wa sheria lazima kifuate utaratibu wa kisheria.
Kesi ya Mwanjilisi and 3 others Criminal Appeal no. 154/1994 imesema pia kuhusu utaratibu.
Kifungu cha 163 Cap. 6 kinatoa njia mbili. Kwa kumuonyesha au kutokumuonyesha.
Mashauri waliyosema wenzangu ndio sasa yanaelezea taratibu za kufuatwa.
Naomba maelezo hayo yasipokelewe.
Part 56 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 57
George: Pia nimesoma masters of Bussiness administration nilimalizia Kisii University nchini Kenya.
Nikasoma Masters of Human Resource Management Chuo Kikuu huria cha Tanzania. Nikapata pia cheti. Na sasa nimeanza PHD.
Mhe. Lissu : ni sahihi nikisema kwamba kwa mujibu wa PGO za 2021 wewe ni Professionally qualified member of the Police Officer?
George: NI SAHIHI KABISA ANAJIBU.
Mhe. Lissu : Unatambulika kama ni professionally officer?
George; Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Sasa naomba waeleze kama maelezo haya ya hiki kisomo umeyaweka kwenye hati yako ya maelezo ya mashahidi?
George: Nimeweka elimu yangu ya Kipolisi tu.
Mhe. Lissu: Naomba nikusomee maelezo yako ya Tar. 08/04 umesema hivi kuhusiana na elimu yako. Mimi mtajwa nimeajiriwa na kufanya kazi mikoa mbalimbali...... Anaendelea hapa.
Anamsomea maelezo yake.
Sasa katika niliyosoma kama kuna chochote kinahusiana na vyuo vya Polisi ulivyotaja jana?
George : hakuna kabisa hayo mambo niliyosema jana kuhusu vyuo vya Kipolisi na vyeti nilivyopata.
Mhe. Lissu : ieleze mahakama kama mafunzo yako mengine nje ya upolisi hayo madiploma ya uhasibu na mengine ya sauti kama yapo kwenye hati yako ya maelezo wambie kama yapo?
George : kwenye hiyo hati haipo ila jana nikiwa naulizwa nilisema.
Mhe. Lissu ; Ulitaja au hukutaja jana?
George: Sikutaja haikuwa na umuhimu na jana sikuulizwa ndio maana sikutaja.
Mhe.Lissu : na hizo masters hukutaja pia?
George: Ndio sikutaja kwasababu sikuulizwa ila leo umeniuliza ndio maana nimetaja.
Mhe. Lissu : twende kwenye ushahidi wako wa siku ya tar. 04/04/2025 uliiambia mahakama kwamba uliletewa taarifa za video clip yenye uhaini na ASP John Kaaya.
George : Ni kweli.
Mhe. Lissu : Ulisema pia ASP John kaaya alikwambia aliona video clip kwenye mtandao wa YouTube wa Jambo TV yenye kichwa cha habari uso kwa uso na watanzani ni sahihi?
George : ni kweli heading ilikuwa inasomeka hivyo.
Mhe. Lissu : Sasa wambie majaji kama maneno yako hayo yapo kwenye maelezo yako ya mashahidi?
Mhe. Lissu : Hayo maneno hayapo kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu : ulisema kwamba baada ya kuambiwa hivyo ulimwambia ASP John Kaaya. Akuonyeshe hiyo video clip?
George: Ni kweli ilikuwa hivyo.
Mhe. Lissu : pia jana ulisema kwamba ASP kaaya alikuonyesha sehemu sehemu?
George: Ni kweli alifanya hivyo kwa siku ya tar. 04.
Mhe. Lissu : Waeleze kama haya maneno ya alikuonyesha sehemu sehemu hakukuonyesha yote kama yapo kwenye hati yako ya maelezo.
Yapo au hayapo?
George : Sidhani kama ipo nadhani haitakuwepo. Haipo sawa.
Mhe. Lissu anamsomea na kumuuliza ni kweli au sio kweli.
George : uwa ni kweli.
Mhe. Lissu : Mtu anayetoa maudhui ya uchochezi ni kosa la uhaini. Kweli au si kweli?
George : naomba nitoe maelezo.
Mhe.Lissu : Sitaki maelezo we jibu maudhui ni kosa la uhaini au sio kosa la uhaini.
George : ni kweli ni kosa la uhaini.
Mhe. Lissu : sasa jana ulitaja kifungu cha uhaini ni 39?
George: Ni kweli we anza kusoma kwenye execution..
Mhe. Liissu : unasema??????
George: Samahani ni EXECUTIVE.
Mhe. Lissu ningeshangaa na kisomo chako chote usijue kingereza?
George: Nimekosea hapo.
Anamsomea hicho kifungu cha 39(d).
Mhe. Lissu : Je video uliyoisoma hayo maudhui ya uchochezi yanaingia kwenye 39(2)d?
George: Ndio yanaingia.
George: Naona kama vingine unaruka kwenye hicho kifungu.
Mhe. Lissu : twende taratibu tutamaliza vyote.
Mhe. Lissu : naomba nikusomee maneno nikiyoshitakiwa nayo. Maneno ya uhaini yanasema hivi WANASEMA KITU KIMOJA HAPA WANASEMA HIVI MSIMAMO HUU UNAASHIRIA UASI NI KWELI NI KWELI KWASABBAU TUNASEMA TUNAENDA KUZUIA UCHAGUZI NA TUTAUVURUGA NA TUTAENDA KUKINUKISHA.
Swali langu Je haya niliyosoma yapo kwenye hati ya mashitaka?
George: Hayo uliyosoma hayapo.
Part 58 itaendele kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
Kuna uwezekano mkubwa sana tukashinda dau nono around milioni kumi Jumatatu hii pale Sportybet. Goli moja lipatikane kila mechi, Jumla ya Mechi ni 50.
Mkeka una odds 327+
Stakeπ31K | Payoutπ10.2M
Retweet upewe Code mapema