🚨 #🇹🇿UhamiajiUpdates #🇹🇿UhamiajiHabari #MjueJiraniYako🇹🇿
UHAMIAJI DODOMA YATOA ELIMU KATIKA SHULE YA SEKONDARI KISASA
Na. Mwandishi Wetu - Dodoma
Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, leo tarehe 18 Februari 2025, imetoa elimu ya masuala ya Uhamiaji katika Shule ya Sekondari Kisasa, ikiwa ni moja ya shule zilizoanzisha Klabu ya Uhamiaji kwa lengo la kupandikiza mbegu ya uzalendo miongoni mwa wanafunzi na kuwaelimisha kuhusu udhibiti wa wahamiaji haramu.
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, Mrakibu wa Uhamiaji Namdula P. Komba, aliwaeleza wanafunzi umuhimu wa elimu ya Uhamiaji kwa jamii, kazi za Idara ya Uhamiaji, vibali vya ukaazi, pasi, viza, pamoja na wahamiaji haramu na madhara yao kwa nchi. Pia, aliwasihi wanafunzi kuwa huru kuuliza maswali yanayohusiana na elimu wanayopewa na Maafisa Uhamiaji wanaofika shuleni hapo.
Kwa upande wake, Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Excel Nziku alitoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa utoaji wa pasipoti, aina za pasipoti, pamoja na mada ya uraia.
Elimu hii imepokelewa vizuri na wanafunzi na walimu, huku Klabu ya Uhamiaji shuleni hapo ikipata idadi kubwa ya wanafunzi kuliko ilivyotarajiwa, ikionyesha mwitikio chanya wa wanafunzi katika kushiriki masuala ya Uhamiaji na uzalendo.
#UhamiajiUsalamaNaMaendeleo🇹🇿 #MjueJiraniYako🇹🇿
🇹🇿#UhamiajiUpDates Uhamiaji Yashiriki Ufunguzi wa Mkutano wa 109 wa Wadau wa Elimu kwa Umma (WASHITIRI 2025) Mbeya.
Na. A/Insp. Amani Mbwaga, Mbeya
Idara ya Uhamiaji Tanzania imeshiriki kikamilifu katika ufunguzi wa Mkutano wa 109 wa Wadau wa Elimu kwa Umma (WASHITIRI 2025), ambapo Mgeni Rasmi, Bw. Methusela Ntonda, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, alifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Palamagamba Kabudi, Mkutano huo umeandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na unafanyika katika Ukumbi wa City Park Garden, Jijini Mbeya.
Katika hotuba yake, Bw. Ntonda aliishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuendeleza ajenda muhimu zinazochangia maendeleo ya Taifa, akieleza kwamba kauli mbiu ya mwaka huu "Tumia Nishati Safi, Tunza Mazingira" inachukua nafasi muhimu katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi, hususan katika kupikia. Aliwahimiza wanahabari kuwa na jukumu kubwa la kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi ya nishati safi na faida zake kwa mazingira na afya za wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayubu Rioba, alieleza kuwa zaidi ya washiriki 250 kutoka taasisi mbalimbali za serikali na mashirika ya umma walihudhuria mkutano huu muhimu. Dkt. Rioba aliendelea kusema kwamba mkutano huu utaleta mafanikio kwa maendeleo ya taifa na kuhakikisha kwamba ajenda ya serikali kuhusu matumizi ya nishati safi inatekelezwa kwa ufanisi.
Idara ya Uhamiaji Tanzania, ikiwa ni miongoni mwa washiriki wa mkutano huu, iliwakilishwa na washiriki wanne kutoka Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Uhamiaji Makao Makuu, wakiongozwa na Mrakibu wa Uhamiaji Juma Dau, Mkaguzi wa Uhamiaji Amani Mbwaga, Konstebo Joseph Katonga, na Konstebo Jafari Mshihiri.
Mkutano wa 109 wa Wadau wa Elimu kwa Umma ni sehemu muhimu ya juhudi za serikali na wadau mbalimbali kuhamasisha matumizi bora ya rasilimali za nishati safi, na wanahabari wana nafasi kubwa katika kuelimisha umma na kutangaza mafanikio ya serikali katika masuala ya nishati, mazingira, na maendeleo.
#🇹🇿Picha na Konstebo Jafari Mshihiri
🇹🇿#UhamiajiUpDates
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania CGI Dkt. Anna Makakala leo tarehe 18 Juni 2024 amekagua Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Uhamiaji linalojengwa Jijini Dodoma, Jengo hilo linajengwa na Kampuni ya Ujenzi ya SUMAJKT.
🌟 Tangazo la Mafunzo 🌟
Salamu kutoka Chuo cha Mafunzo ya uhamiaji cha kikanda Tanzania (TRITA)!
Tunayo furaha kutangaza mpango ujao wa mafunzo kuhusu "usimamizi wa masuala ya kiuhamiaji nchini Tanzania." Mafunzo haya yanakusudia kuwajengea washiriki maarifa
🇹🇿🙏Hongera Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Miaka 03 Chini ya Uongozi wako Idara ya Uhamiaji tumepata Mafanikio Mengi na Makubwa
🇹🇿🙏Hongera Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Miaka 03 Chini ya Uongozi wako Idara ya Uhamiaji tumepata Mafanikio Mengi na Makubwa.
🇹🇿#UhamiajiUpDates
CGI Dkt. Anna Makakala jana tarehe 08 Machi 2024 ikiwa ni Siku ya Wanawake Duniani alishiriki katika Kongamano la nne (04) la The Citizen Rising Woman ambalo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa Mgeni Rasmi.
🇹🇿 #From#India#TBT
40 Immigration Women Officers from Tanzania Mainland and Zanzibar have attended a special Capacity Building Training in Leadership and Development of Gender Equality funded by the Indian Government under the ITEC Programme at Lacknow PRADESH in India.
🇹🇿#Uhamiaji Usalama na Maendeleo Katika Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi 2024.
🇹🇿#Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii
🇹🇿#Uhamiaji Usalama na Maendeleo Katika Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi 2024.
🇹🇿#Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii
🇹🇿#Uhamiaji Usalama na Maendeleo Katika Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi 2024.
🇹🇿#Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii
🇹🇿#Uhamiaji Usalama na Maendeleo Katika Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi 2024.
🇹🇿#Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii
🇹🇿#Uhamiaji Usalama na Maendeleo Katika Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi 2024.
🇹🇿#Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii