"Tuko karibu sana na nyumba ya ibada, mbali sana na Mungu, karibu sana na dini, mbali sana na imani, karibu sana na pesa, mbali sana na utu." ~Togolani Mavura.
"Kila mtu anaweza kuwa tajiri siku moja lakini wachache wanaweza kubakia katika utajiri. Wanaobakia kuwa matajiri ni wale wenye utajiri wa roho, wenye kuinua wengine, wenye utu, wenye nia njema na utajiri wao wa mali na wenye nidhamu ya maisha na hofu ya Mungu."~ Togolani Mavura.
"Katika kurekebisha kwangu kunaweza kusababisha mtikisiko na hata nyufa kwako. Si kwamba nimedhamiria kukutikisa bali ni kwasababu uko karibu sana na mimi. Ungekuwa mbali nisingekufikia. Ndio ilivyo kwenye maisha, ukiona unakereka na mtu huenda tatizo ni wewe umemsogelea sana."