Nimamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema. Aidha Ninamshukuru sana Mhe SSH Rais wa JMT kwa kuniamini nakuniteua kuwa Waziri wa Ardhi, naahidi kufanya kazi kwa weledi mkubwa ktk kumsaidia Mh Rais. Namuomba Mwenyezi Mungu aniongoze ktk utumishi wangu Amen!!
Wale wote wanaojipatia fedha kwakutumia mali za umma 40 zao zimefika. Mtanzania yeyote aliyepanga duka ama kukaa ktk nyumba za NHC lakini hana mkataba na NHC bali amwpangishwa ajitokeze mara moja ofisi za NHC ili atambuliwe kama mpangaji halisi.
Nakushukuru sana Mungu kwa kunipa fursa yakumjulia hali Mkuu wa Majeshi mstaafu General David Msuguli. Mungu ni mwema anaendelea kumlinda akiwa na umri wa miaka 101.
@SumbiziPeter Suala hilo naomba umfikishie Mkurugenzi wa Halmashauri maana mabaraza ya kata yako kwake siyo wizara ya ardhi, hata hivyo nitamwagiza msajiri wa mabaraza ashirikiane na Mkurugenzi kutoa elimu juu kwa wajumbe wa mabaraza ya kata
@wizara_ya_ardhi@kaziiendelee@AngelineMabula Ndugu waziri wa ardhi, naomba umsaidie mama yangu Bi.Kuruthum Issa Abdallah wa Igogo Mwanza , Mama amedhirumiwa Kiwanja chenye nyumba na Tajiri mmoja akishirikiana na mwenyekiti na diwani wa Igogo, mama ni mjane karibia miaka 30 sasa, msaada tafadhali, asante.
Karibu Mwenge wa Uhuru 2021Wilaya ya ILEMELA wenye kauli mbiu "TEHAMA NI MSINGI WA TAIDA ENDELEVU ITUMIE KWA USAHIHI NA UWAJIBIKAJI" Tuko tayari kupokea ujumbe wa MWENGE WA UHURU na kuufanyia kazi
Hongera sana Mhe Janeth Masaburi kwa binti yako kupata mwenza, Mwenyezi Mungu awape ndoa yenye furaha na amani tele siku zote wamche bwana Mungu wao bila kuchoka
Hongera sana Mhe Mwenyekiti wa CCM Taifa Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutuheshimisha Wanawake. Tutaendelea kuchapa kazi kwa bidii ktk Kutekeleza Ilani ya CCM kama tulivyoinadi. Mungu akupe Afya njema siku zote
Nawashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kunichagua kwa kura zote (100%) kuwa Mwenyekiti wa CCM. Nawaahidi utumishi uliotukuka na CCM imara ambayo inaongoza Serikali yetu ya Awamu ya Sita.